RAIS MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA WAHITIMU CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI

January 23, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili  katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo Peter Massao. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa jeshi kwa cheo cha Luteni Usu.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika viwanja vya Chuo hicho.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia gwaride lililokuwa likipita mbele yake  kutoa heshima.
 Gwaride la Wahitimu likipita kutoa heshima mbele ya mgeni rasmi  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli .
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Meja Generali Paulo Peter Massao. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi aliyefanya vizuri  O/Cdt. Mmang’anda katika Mafunzo hayo. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wapya hawapo pichani .
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma jarida  la Ngome baada ya kukamilika zoezi la kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wapya aliowatunuku Kamisheni pamoja na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Wananchi. 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na watoto waliofika kushuhudia tukio hilo la kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wapya wa Jeshi. Picha na IKULU


WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA MNADA WA NYAMA CHOMA DODOMA

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA MNADA WA NYAMA CHOMA DODOMA

January 23, 2016
IMG-20160123-WA0051
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wafanyabiashara wa eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ikiwa ni moja ya ziara zake kufatilia hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya nchi, akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa (mwenye skafu shingoni) pamoja na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Alek Barakena (mwenye suti nyeusi).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ikiwa ni moja ya ziara zake kufatilia hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Baada ya kutembelea mnada huo, Mhe. Ummy aliwataka wananchi wa eneo hilo kutambua kuwa bado ugonjwa wa kipindupindu upo na unaendelea kusambaa maeneo mbalimbali ya nchi hivyo ni wajibu wao kama wananchi kuweka mazingira yao katika hali ya usafi ili kutokomeza uonjwa huo.
Aidha ili kuzidi kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu, Waziri Ummy ameagiza kuendelea kutekelezwa kwa agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa ambaye aliagiza kusimamishwa kwa shughuli za kuuza nyama nyoma katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.
“Kipindupindu kimesambaa sehemu nyingi nchini ikiwepo hapa Dodoma na hivyo naagiza katazo la Mkuu wa Wilaya, Dkt Jasmine Tiisekwa liendelee kuwepo hadi ugonjwa wa kipindupindu uishe Dodoma na niwajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kipindupindu kinakwisha,” alisema Waziri Mhe. Ummy.
Pamoja na hayo pia Waziri huyo wa Afya ameutaka uongozi wa Manispaa ya Dodoma kufanya kikao cha pamoja na wafanyabiashara hao wa nyama choma ili kuona ni jinsi gani wanaweza kuendelea na biashara zao huku wakizingatia kanuni za usafi wa afya na mazingira bila kusababisha kuzidi kusambaa kwa kipindupindu.
IMG-20160123-WA0050
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.
IMG-20160123-WA0045
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maagizo ya wafanyabiashara hao kusitisha shughuli zao mara moja katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.
IMG-20160123-WA0043 IMG-20160123-WA0044
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa (wa tatu kulia) na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Alek Barakena (kushoto) wakisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo (hayupo pichani).
IMG-20160123-WA0046
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ambaye jina lake halikupatikana alipofanya ziara ya katika eneo hilo.

TOTO AFRICANS WAWANG'OA MAJIRANI ZAO PAMBA KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO.

January 23, 2016
Wachezaji wa Toto Africans (Jezi za Njano) wakisalimiana na wachezaji wa Pamba, kabla ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza hii leo. Katika Mchezo huo Toto wamewatupa nje ya michuano hiyo majirani zao Pamba kwa jumla ya magori 4-1.

Magoli ya Toto yamefungwa na Miraji Athuman Madenga aliefunga magoli mawili, Eddo Christopher pamoja na Waziri Junior Shentembo huku bao la Pamba likifungwa na James Sungura.
Kwa matokeo hayo, Pamba wametupwa nje ya Michuano hiyo na Toto wameweza kusonga mbele na kutinga hatua ya 16 bora.
Kamisaa wa mchezo akiwa katika picha ya pamoja na Waamuzi pamoja na Makeptaini wa timu za Pamba na Toto.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mwanza (Katikati) akiwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia mchezo kati ya Toto na Pamba
Shambulizi langoni mwa Timu ya Pamba
Wachezaji wa Toto Africans wakishangilia ushindi wao dhidi ya timu ya Pamba katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Bado kuna mwitikio mdogo wa mashabiki wa soka kufika uwanjani Jijini Mwanza. Hapo ni jukwaa kuu.
Wanahabari
Kushoto ni Gervas Mbaya ambae ni Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya Pamba akiteta jambo na bwana Cathbert ambae ni Msemaji wa Timu ya Toto Africans. Katikati ni Mwanahabari Moses Methew.
Kushoto ni Hashim Kibode ambae ni Team Manager wa Timu ya Pamba, katikati ni Kocha Msaidizi wa Timu hiyo Yangoo Mamboleo na Kulia ni Afisa Habari na Mahusiano Gervas Mbaya wakiteta jambo baada ya kutolewa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho na Timu ya Toto kwa kutundikwa bao 4-1.
Dominik Glawogger ambae ni Kocha Mkuu wa Timu ya Toto (Katikati) akizungumza na wanahabari baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya timu ya Pamba.
Mdau wa Michezo akiwa katika mahojiano
Kutoka Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Mimi ni GB Pazzo, Mzee wa Ekotitee wa Binagi Media Group.
WAZIRI KITWANGA: KAMATAKAMATA INAYOENDELEA KWA RAIA WA KIGENI NCHINI, HAITAGUSA WENYE VIBALI HALALI

WAZIRI KITWANGA: KAMATAKAMATA INAYOENDELEA KWA RAIA WA KIGENI NCHINI, HAITAGUSA WENYE VIBALI HALALI

January 23, 2016

C1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na raia wa China wanaoishi nchini, katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
C2
Kaimu Balozi wa China nchini, Zhang Biao akizungumza katika sherehe ya raia wa China wanaoishi nchini ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) kuja kuzungumza na mamia ya wachina hao waliohudhuria sherehe hiyo. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri, wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
C3
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), kwa kutoa hotuba nzuri iliyowafafanulia wachina waishio nchini kuwa Serikali ya Tanzania inawajali na inatambua umuhimu wa ushirikiano wao uliodumu kwa kipindi cha miaka mingi, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Wachina waishio nchini jana walifanya sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na mamia ya wachina hao. Kulia ni Kaimu Balozi wa China nchini, Zhang Biao.
C4
Raia wa China wanaoishi nchini wakishindana kula Tunda aina ya Tikiti wakati wa Sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika Sherehe hiyo ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) alikuwa mgeni rasmi ilihudhuria na mamia ya raia hao wa China. Hata hivyo, Waziri Kitwanga alisema raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
C5
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwapongeza raia wa China walioshinda mchezo wa bahati nasibu walioucheza katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
C6
Kikundi cha Karate kinachoongozwa na raia wa China wanaoishi nchini kikitoa burudani katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
C7
Sehemu ya raia wa China wanaoishi nchini, wakimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kwa Wachina hao katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam jana. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NAPE ATEMBELEA KITUO CHA UTAMADUNI BUJORA PAMOJA NA CHUO CHA MAENDELEO YA MICHEZO MALYA MKOANI MWANZA

January 23, 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akikaribishwa kwenye kituo cha utamaduni wa Kisukuma Bujora na Mlezi na Mshauri wa kituo cha utamaduni pamoja na machifu wa Kisukuma Jaji Mstaafu Mark Bomani
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (katikati) akizungumza na Machifu wa kisukuma kwenye kituo cha Utamaduni Bujora, kulia pichani ni Jaji Mstaafu Mark Bomani na kushoto ni Chifu Charles Kafipa wa Bukumbi mkoani Mwanza
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo juu ya nyumba za asili za wasukuma kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha Utamaduni wa Kisukuma Padri Fabian Mhoja.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia hesabu za kisukuma kwenye kituo cha Bujora mkoani Mwanza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo juu ya utamaduni wa kucheza bao kwenye kituo cha Utamaduni wa kisukuma Bujora.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia zana mbali mbali za kiasili kwenye nyumba ya utamaduni Bujora.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo namna machifu walivyokuwa mashujaa na viongozi hodari.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo juu ya chuo cha Bujora
Wapiga ngoma wakipiga kwa ufahari ngoma mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
Baadhi ya wageni wakiangalia ngoma mbali mbali zikichezwa kwenye kituo cha Bujora mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye kituo cha utamaduni wa kisukuma Bujora ambapo aliwapongeza kituo hicho kwa kudumisha utamaduni na kuahidi serikali itaendelea kukisaidia.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia amepewa jina la Chifu Sangeja( aliyeshika usinga) akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii kutoka nchini Denmark ambao wanajifunza utamaduni wa Kisukuma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia uwanja wa ndani wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya.
Sehemu ya jukwaa la kukalia la uwanja wa ndai wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza.
Wanafunzi  wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya wilayani Kwimba wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifurahia jambo wakati akizungumza na wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya michezo, Malya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ambapo aliahidi kutatua changamoto mapema.
wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo- Malya wakionyesha uwezo wao wa kimichezo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya mkoani Mwanza.