MASHINDANO YA OLIMPIKI 2020 NCHINI JAPAN KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA - DK. KIGWANGALLA

April 22, 2018




Na Hamza Temba-Ngorongoro, Arusha

Mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika nchini Japan mwaka 2020 yatatumika kunadi vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia timu ya Taifa ya riadha na banda la maonesho ya utalii.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kukamilika kwa mashindano ya riadha ya Ngorongoro Marathon 2018 katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana.

Dkt. Kigwangalla alitoa kauli hiyo wakati akijibu ombi la Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka ambaye aliiomba wizara yake kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kusaidia maandalizi ya timu ya Taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo.

Mtaka pia aliomba Mamlaka hiyo itumie timu ya Taifa ya riadha Tanzania kama mabalozi wao wa kutangaza vivutio vya utalii vya hifadhi hiyo ya Ngorongoro ndani na nje ya nchi.

Akijibu maombi hayo, Dk. Kigwangalla alisema kitaundwa kikosi kazi cha pamoja kati ya wizara yake kupitia taasisi zake hususan Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Chama cha Riadha Tanzania ili kuainisha mahitaji ya mashindano hayo na kuweka makubaliano yatakayonufaisha pande zote.

"Kama tunaweza kupata jukwaa la nchi zaidi ya 50 au 100 kwa kufadhili wanariadha 200 kwenda kushiriki, manake hilo jukwaa linatulipa, kwa sababu tunawekeza kidogo tunaonekana kwa kiasi kikubwa.

"Mwaka 2020 kwenye Olimpiki lazima tuwekeze, na sisi Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zetu tutapenda tuunde kikosi kazi cha pamoja ili tuangalie gharama zinazohusika, maandalizi yanayohitajika ili na sisi kama Wizara kupitia taasisi zetu kama Ngorongoro tuweze kuona nini mchango wetu, lakini sisi tutataka tujue faida yetu hasa itakuwa ni nini" alisema Dk. Kigwangalla.

Alisema mashindano hayo yatatoa fursa pana kwa Taifa kutangaza vivutio vyake mbali na juhudi zinazofanywa hivi sasa kupitia maonesho ya kimataifa. "Kupitia mashindano hayo tutapeleka pia maombi kwenye ofisi ya balozi wetu nchini Japan ili tupewe banda la kunadi vivutio vyetu vya utalii" alisema.

Dk. Kigwangalla pia aliitaka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kukubali ombi la Chama cha Riadha Tanzania la kuanzisha kituo cha mafunzo ya riadha mjini Karatu ili kuimarisha mchezo huo na timu ya riadha Tanzania sambamba na kutumia kituo hicho kama fursa ya kutangaza utalii wa hifadhi hiyo.

Alisema kituo hicho pia kijengwe sanamu za wanariadha mashuhuri waliowahi kuiletea sifa Tanzania na kuweka rekodi mbalimbali ili kutoa motisha kwa wanariadha wengine wanaochipukia.

Alisema mbali na kuanzisha kituo hicho, timu hiyo ya Riadha Tanzania inaweza pia kupewa jina la Ngorongoro ili kuitangaza hifadhi hiyo yenye vivutio vya kipekee duniani ambavyo vimeifanya itambulike kama sehemu ya urithi wa dunia.

Mashindano ya Ngorongoro Marathon kwa mwaka huu 2018 yamehusisha washikiri kutoka Tanzania na Kenya ambapo washindi wa kwanza wa mbio hizo za kilomita 21 upande wanaume na wanawake wametoka nchini Kenya. Kaulimbiu ya mashindano hayo imelenga kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimsalimia Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dkt. Fredy Manongi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Waziri Kigwangalla akiwa tayari kuzindua mashindano hayo katika umbali wa kilomita 21.

Washiriki wa mbio hizo kutoka Tanzania na Kenya wakitimua mbio kuanza mashindano hayo ya Ngorongoro Marathon 2018 umbali wa Kilomita 21 mjini Karatu mkoani Arusha. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Baadhi ya watalii nao walitumia fursa hiyo kusaka medali.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wakiwa katika harakati za kusaka medali.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihitimisha mbio za kilomita 21 za mashindano ya Ngorongoro Marathon 2018 yaliyofanyika katika mji wa Karatu mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Haikuwa kazi rahisi, washiriki wengine walilazimika kuvua viatu na kuvaa kandambili ili kurahisiha kazi yao ya kutafuta medali.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akionesha medali aliyopewa pamoja na washiriki wengine wa mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 yaliyofanyika mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki nchini Tanzania, Filbert Bayi akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akitoa salamu zake katika hagla hiyo ambapo ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kufadhili mashindano hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mfaume Taka akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Karatu.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha mashindano hayo mjini Karatu.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi cheti cha shukurani Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dkt. Fredy Manongi kwa kufanikisha mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 zilizofanyika katika mji wa Karatu mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi milioni moja mshindi wa kwanza wa kilomita 21 kwa wanawake, Monica Chemko kutoka Kenya katika mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 zilizofanyika katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi milioni moja mshindi wa kwanza wa kilomita 21 kwa wananume, Joseph Patha kutoka Kenya katika mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 zilizofanyika katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wengine wa mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 yaliyifanyika mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21.

BAADA YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA KUKAMILIKA (NFRA) ITAKUWA NA UWEZO WA KUHIFADHI TANI 501,000

April 22, 2018


Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akitoa taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi huo Mtaa wa Relini-Kizota Mjini Dodoma, Jana 21 Aprili 2018. Picha Na Mathias Canal-NRFA

Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma.

Hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini inazidi kuimarika huku serikali kupitia wizara ya kilimo ikiwa imejipanga kukabiliana na changamoto ya uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao mbalimbali hususani mahindi.

Katika taarifa ya Bi Vumilia L. Zikankuba Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula katika hafla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa vihenge na maghala ya kisasa katika Mtaa wa Relini-Kizota Mjini Dodoma aliyoitoa mbele ya mgeni rasmi-Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) jana tarehe 21 aprili, 2018 alieleza kuwa mradi huo pindi utakapokamilika utafungua fursa kubwa kwa wakulima nchini.

Alisema kuwa Baada ya Mradi huu kukamilika uwezo wa kuhifadhi wa Wakala wa Taifa wa Kuhifadhi Chakula utakuwa mara mbili ya uwezo wa sasa yaani kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000 huku ikitarajiwa kufikia Tani 700,000 kufikia mwaka 2025.

Bi Vumilia alieleza kuwa Mikataba ya mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula, ilisainiwa na kuanza kazi tarehe 09 Desemba 2017 kati ya (NFRA) na makampuni mawili toka nchini Poland ambayo ni Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o. Aidha, mradi huo utatekelezwa kwa gharama ya Dola za kimarekani milioni 55 na unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi kumi na nane (18) kuanzia mwezi Mei 2018.

Maandalizi ya awali ya mradi huo yalifanywa na kampuni kutoka nchini Poland iliyofanya upembuzi yakinifu wa awali na kupendekeza gharama za mradi kuwa dola za kimarekani millioni 55 ambazo zingetosheleza kujenga vihenge vyenye uwezo wa Tani 150,000 na maghala yenye uwezo wa Tani 50,000, hivyo kufanya uwezo wa jumla wa mradi kuwa Tani 200,000.

Alisema, ili kujiridhisha zaidi Wakala kupitia Wizara mama, iliunda timu ambayo ilifanya upya tathmini ya mradi na kupata thamani halisi ya mradi (value for money) ili kuleta ushindani katika utekelezaji wa mradi kwa kushirikisha timu ya Wataalamu wa ndani.

Timu hiyo iliundwa na Wahandisi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandisi na Wataalamu wa mazingira kutoka TBA pamoja na Mhandisi toka Wizara ya Kilimo. Hivyo timu hiyo ilifanya upya kazi ya usanifu wa msingi, kuandaa makadirio ya gharama za mradi, na kuandaa makabrasha ya zabuni ili kutimiza azma mbili nilizotangulia kuzitaja hapo awali.

Matokeo ya jumla ya kazi hiyo, yalibainisha kuwa kiasi cha fedha Dola milioni 55 kinatosheleza ujenzi wa vihenge vya kisasa vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 190,000, na maghala Tani 60,000 hivyo kufanya ongezeko la hifadhi ya Tani 50,000.

Aidha, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula unamiliki maghala ya kuhifadhi nafaka 34 yenye uwezo wa jumla ya Tani 251,000. Uwezo huu wa sasa wa maghala hautoshelezi mahitaji ya dharula ya chakula kwa mfululizo wa miezi mitatu kwa akiba isiyo pungua Tani 700,000, hivyo kupelekea uhitaji wa kuongeza uwezo wa uhifadhi.