RAIS KAGAME KUFUNGUA MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM-2016

June 23, 2016
Ofisa Mawasiliano Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Theresa Chilambo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu maonesho  ya 40 ya biashara ya kimataifa yatakayoanza rasmi Juni 28, 2016 hadi Julai 8, 2016 katika viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Biashara, Anna Bulondo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka (katikati), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho hayo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

RAIS Paul Kagame wa Rwanda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayotarajiwa kuanza Juni 28,2016 hadi Julai 8,2016 ambayo yatafunguliwa rasmi Julai 1,2016 na Rais huyo akiambatana na mwenyeji wake Rais Dk.John Magufuli.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka alisema maonesho hayo yatatoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi pamoja na taasisi mbalimbali kutangaza biashara na huduma wanazotoa, kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani kujifunza mambo ya biashara na uzalishaji bora wa bidhaa kulingana na soko la kimataifa, kutengeneza jukwaa la kibishara ambap hutoa fursa kwa wafanyabiashara kutengeneza mitandao ya mawasiliano baina yao inayowasaidia kukuza biashara na kufikia malengo waliyojiwekea na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa zao.

Rutageruka alisema nchi 30 zitashiriki maonesho hayo huku makampuni yakiwa  650.

Alitaja viingilio katika maonesho hayo kuwa kwa watoto itakuwa ni sh.1000 na wakubwa sh.3000 hiyo ni kuanzia Juni 28n hadi Julai 8,2016 lakini katika siku ya Julai 7,  2016 kwa wakubwa itakuwa ni sh.4000.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kutembelea kwenye maonesho hayo ili kujifunza mambo ya biashara.

WAZIRI WA AFYA , MAENDELEO YA JAMII , JINSIA, WAZEE NA WATOTO ATEMBELEA VIJIJI VILIVYOKUMBWA NA MLIPUKO WA UGONJWA USIOJULIKANA WILAYANI KONDOA

June 23, 2016

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana  katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa.
 
Katika ziara hilyo ameambatana na wataalam mbalimbali ambao wameweka kambi kwenye vijiji hivyo ili kufuatilia wagonjwa majumbani.vile vile ametembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya kondoa.
Mbunge wa Kondoa Mhe. Juma Nkamia akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kondoa.Mhe.Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana  katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa.

PATA VICHWA VYA HABARI KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO ALHAMISI JUNI 23

June 23, 2016







 Mkurugenzi Muhimbili Akutana na Madaktari, Aongeza Posho

Mkurugenzi Muhimbili Akutana na Madaktari, Aongeza Posho

June 23, 2016
MSE1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru LEO amekutana na madaktari bingwa wa hospitali hiyo kwa ajili ya kuwasikiliza na kujibu kero mbalimbali. MSE2 
Baadhi ya madaktari bingwa wakimsikiliza Profesa Museru baada ya kukutana nao LEO kwenye ukumbi wa CPL katika hospitali hiyo. MSE3 
Dk Saidia Primos wa hospitali hiyo akiuliza swali kwenye mkutano huo. MSE4Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Kimambo (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario kwenye mkutano huo LEO.
………………………………………………………………………………………………………….
Na Neema Mwangomo, Dar es salaam          
                                                                                                                                                                             
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH), Profesa  Lawrence Museru leo amekutana na Madaktari  wa MNH  ikiwa ni mkakati wa kukutana na watumishi kwa lengo la kuwasikiliza na kujibu kero zao.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru amewapongeza  madaktari hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuimarisha utoaji huduma kwa wagonjwa na kwamba hali hiyo imechangia MNH kuongeza mapato yake.
Amesema kuongezeka kwa mapato ya Hospitali  na kufikia Shingili Bilioni 4. 5 kwa mwezi kumetokana na kila mmoja kutimiza wajibu wake.
Amesema kutokana na mafanikio hayo,  MNH imewaongezea madaktari  wake posho mbalimbali  ili kuongeza tija katika utendaji, lakini pia hospitali  imeamua  kutenga Shilingi Milioni 800 kwa mwaka ili kuwapa mkono wa heri wastaafu wake  jambo ambalo awali halikuwapo.
Hata hivyo amesema mbali na hatua hiyo, pia  MNH imefanikiwa kulipa malimbikizo mbalimbali ya stahiki  za wafanyakazi wake ikiwamo  pesa za likizo kwa madaktari pamoja na watumishi wengine kwa ujumla.
“ Awali changamoto kubwa ilikuwa ni ucheleweshaji wa stahiki za wafanyakazi kwa Madaktari na watumishi wengine, lakini katika hilo tumefanikiwa kwani tunaenda nalo vizuri na tumelipa malimbikizo hayo “ amesema Profesa Museru.
Akielezea mipango ya MNH  Profesa Museru amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina mipango mbalimbali ya kuendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vitanda vya Chumba ya wagonjwa Mahututi-ICU-, kuongeza ICU ya watoto pamoja na kina Mama wajawazito.
Kaimu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH kesho Juni 23, 2016 atakutana na Wauguzi pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii.
PROF. MAKAME MBARAWA AZINDUA BODI YA TPA

PROF. MAKAME MBARAWA AZINDUA BODI YA TPA

June 23, 2016

TPA1Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu MKuu wa WIzara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho.
TPA2 
Wajumbe wa Bodi mpya ya Bandari Nchini (TPA), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.
TPA3Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, vitendea kazi baada ya kuizindua rasmi bodi hiyo.
TPA4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga alipokagua eneo la kupakulia makontena bandarini hapo.
TPA5 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Eng. Aloyce Matei (wa kwanza kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), alipokagua miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam.
TPA6 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kushoto), wakati alipokagua eneo la kuhifadhia  magari katika bandari ya Dar es Salaam.
Habari Picha na Benjamini Sawe-Maelezo.