LOWASSA NDANI YA DALADALA DAR ES SALAAM LEO

August 24, 2015

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Mh. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya
Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar
es salaam leo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwepo kando ya Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa katikati ya umati wa watu wakati alipotembelea eneo la Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar
es salaam leo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliokuwa kituoni hapo kusubiria usafiri.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es salaam,mapema leo asubuhi.
Mh. Lowassa akishuka kwenye daladala.
Wakazi wa mji wa Mbagala wakiushangilia msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakati walipotembelea Kituo cha Mabasi cha Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam, wakati walipotembelea kituo hicho leo
 
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na Vijana wanaojihusisha na shughuli mbali mbali katika stendi kuu ya
Mabasi yaendayo mikoa ya Lindi na Mtwara, ilipo Mbagala jijini Dar.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia wakazi wa Mbagala.
 

KONGAMANO LA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA NA UWEKEZAJI KUFANYIKA AGOSTI 28-30, 2015 DAR ES SALAAM

August 24, 2015

 Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nuebrand EC, Cathreen Bukuku (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kongamano la wiki ya  huduma za kifedha na uwekezaji litakalofanyika Agosti 28 hadi 30 mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkufunzi na Mratibu wa Mipango wa Kampuni hiyo, Daniel Wadelanga. Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Nuebrand EC.
 Mjumbe wa Timu ya Mauzo wa Benki ya Uba United Bank for Africa, Tesha Filemon (katikati), akizungumza katika mkutano huo  kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
 Meneja wa Tawi la Kariakoo wa Benki ya The Peoples Bank of Zanzibar Ltd, Badru Idd (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu benki hiyo na matawi yake.
 Ofisa Usanifu Bidhaa na Usimamizi wa Sharia Amana Benki, Jaffari Kesowani (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu kazi mbalimbali zinazohusiana na na benki hiyo.
 Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Jubilee Life Insurance, Adam Samson Namuhisa (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Msimamizi wa Masoko wa Kampuni ya Avic Town, Daniel Kure (kulia), akielezea kadhi kadhaa zinazofanywa na kampuni hiyo katika mkutano huo. Kushoto ni maofisa wa kampuni hiyo.
 Meneja Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya  Covenant Bank, Mhina Semwenda (kulia), akizungumzia shughuli zinazofanywa na benki hiyo.
 Wadau mbalimbali kutoka taasisi za kifedha wakiwa 
kwenye mkutano huo.
WAGONJWA 100 WA UGONJWA WA MABUSHA KUFANYIWA UPASUAJI MANISPAA YA MTWARA

WAGONJWA 100 WA UGONJWA WA MABUSHA KUFANYIWA UPASUAJI MANISPAA YA MTWARA

August 24, 2015

X4
Kaimu Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa kambi hiyo ya upasuaji Johansen Bukweri akizungumza kwenye uzinduzi huo, alisema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yamekuwa yakiathiri sehemu kubwa ya jamii katika mkoa wa Mtwara na kuleta mahangaiko mengi kwa wananchi ikiwemo ulemavu, hali ambayo inapunguza uwezo wa wananchi kushiriki katika ujenzi wa Taifa na watoto kutoweza kuhudhuria vizuri katika masomo shuleni
X1
Mratibu wa Taifa wa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira, akielezea majukumu ya mpango huo wakati wa uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye tatizo la ugonjwa wa mabusha Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara,iliyofanyika katika hospitali  ya Mkoa ya Ligula.
X2
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) na Mwenyekiti wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele Afrika Dkt. Mwele Malecela akitoa salamu kwenye uzinduzi wa kambi hiyo, ambapo alisema Matende na mabusha ni magonjwa ambayo yanatakiwa kutokomezwa ifikapo mwaka 2020 nchini Tanzania.
X3 
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ,wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibimayila, akipokea mfano wa hundi toka kwa mwakilishi wa Stat Oil Naomi Makota (kulia) kwa ajili ya upasuaji wa wagonjwa wapatao 100 wa Manispaa ya Mtwara.
X5
Kaimu Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye ugonjwa wa mabusha.
X6
Dkt. Upendo Mwingira akiwafariji wagonjwa waliokwishafanyiwa upasuaji wa mabusha katika hospitali ya mkoa ya Ligula.Upasuaji huo ni wa siku 5.Mkoa wa Mtwara una takribani watu wapatao 2,500 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa mabusha.Kambi hii itafanyika kwa watu waliojiandikisha na itatolewa bila ya malipo.
SHIRIKA LA HABARI LA MAREKANI INERNEWS LAANDAA MAFUNZO YA SIKU TANO KWA WAANDISHI WA HABARI WA ZANZIBAR JUU YA KURIPOTI UCHAGUZI MKUU.

SHIRIKA LA HABARI LA MAREKANI INERNEWS LAANDAA MAFUNZO YA SIKU TANO KWA WAANDISHI WA HABARI WA ZANZIBAR JUU YA KURIPOTI UCHAGUZI MKUU.

August 24, 2015

1
Mkufunzi  na Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim akitoa  mada katika mafunzo  ya  siku tano  juu ya kuandika Habari za Uchaguzi Mkuu yaliyoandaliwa na Shirika  la Habari la Marekani  Internews  kwa waandishi wa Habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
2
Mhadhiri wa Sheria, Kitivo cha Sheria Zanzibar University, Ali Uki akionyesha kitabu cha Sheria cha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kitabu  cha Sheria cha Tanzania na cha Zanzibar  ambavyo  vinawapasa waandishi wa habari kuvisoma na kuzitumia sheria  hizo katika kuandika habari za Uchaguzi Mkuu kwa usahihi.
8
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Zanzibar Leo Hafsa Golo akiwasilisha mada ya grop lake katika mafunzo ya kuandika Habari za Uchaguzi Mkuu yaliyoandaliwa na Shirika la Habari la Ineternews la Marekani katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
5
Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan akiwasilisha mada ya wajibu wa vyombo vya habari katika kuripoti Uchaguzi Mkuu katika mafunzo ya waandishi wa Habari yanayofanyika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar
4 
Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo juu ya kuripoti Habari za Uchaguzi kutoka vyombo mbali mbali vya Serikali na binafasi wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwakilishwa.
6
Mtayarishaji na Mtangazaji wa vipindi wa Redio Zenj FM Mustapha Mussa akitoa mchango katika mafunzo hayo yanayofanyika Ukumbi wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Zanzibar.
7
Washiriki wa mafunzo ya kuripoti Uchaguzi Mkuu wakiwa katika kazi za vikundi wakijadiliana katika kufanikisha mafunzo hayo.

UFAFANUZI KWA KUHUSU KASORO ZA BVR NA UWEKAJI WAZI WA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

August 24, 2015
Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) ulikamilika tarehe 04/08/2015 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
 
Baada ya kukamilika kwa zoezi la Uboreshaji Tume imekuwa ikichakata (processing) taarifa za Wapiga Kura ili kuweza kuandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura, katika maandalizi hayo mifumo imeweza kugundua kasoro mbali mbali ambazo baadhi zimefanyiwa kazi na zingine zinaendelea kufanyiwa kazi, kasoro hizo ni pamoja na Wapiga Kura Kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Mfumo wa BVR unao mfumo mdogo wa “Mini AFIS” unaoweza kubaini Mpiga Kura anayataka kujiandikisha zaidi ya mara moja katika kituo husika, mfumo huo ulikuwa umeandaliwa ili kuweza kubaini Wapiga Kura wanaotaka kujiandikisha zaidi ya mara moja na kuzuia Uandikishaji huo katika BVR Kit yoyote. Hii ingewekana iwapo Mfumo wa mawasiliano ungekuwa na nguvu katika vituo vyote na kuweza kuwasiliana na mifumo iliyoko katika kituo kikuu cha maandalizi ya Daftari(Data Processing Center) kwani katika kituo hicho imewekwa mifumo ya hali ya juu inayoongoza kimataifa katika kulinganisha alama za vidole na kubaini waliojiandikisha zaidi ya mara moja.
Kwa kutokuwa na mawasiliano yenye nguvu kutoka katika kila kituo Tume ilianza kulinganisha taarifa za Wapiga Kura mara tu baada ya taarifa kufikishwa katika kituo cha maandalizi ya Daftari hivyo kwa mitambo iliyopo Tume imebaini Wapiga Kura wote waliojiandikisha Zaidi ya mara moja ambao taarifa zao zimeisha chakatwa ambao kwa sasa imefikia 52,062 Idadi hii inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na uchakataji wa taarifa.
Baadhi ya vituo kutokuwa na Wapiga kura.
Tatizo hili linasababishwa na maombi ya kuanzishwa kwa vituo wakati zoezi la Uandikishaji limeanza, baadhi ya vituo hivyo havikutumika wakati wa Uandikishaji kama ilivyokusudiwa kwa sasa Tume inafanyika kazi ya kuhamisha Wapiga Kura na kuwapeleka katika vituo hivyo ili kuwapunguzia umbali mrefu kutoka kwenye vituo walivyojiandikisha wakati wa zoezi la Uandikishaji, kazi hii Tume inaendelea kuifanya kwa kushirikiana na watendaji wa Kata katika Halmashauri husika.
Baadhi ya Vituo kuwa na Wapiga Kura wachache au Wengi katika Vituo vya Uandikishaji.
Tatizo hili pia lilisababishwa na vituo kuongezwa wakati zoezi la Uandikishaji limeanza. Kabla ya kuongezwa vituo katika BVR kutokana na hamasa ya Wapiga Kura Kujiandikisha Wapiga Kura hao walianza kujiandikisha katika vituo vingine na baada ya kuongeza vituo katika BVR vituo vilivyoongezwa viliendelea kufanya Uandikishaji kwa siku mbili au tatu za mwisho hivyo kuonekana kama vina Wapiga Kura wachache, kasoro hiyo inarekebishwa pia kwa kusaidiana na watendaji wa Kata husika ili kuwahamisha Wapiga Kura waliojiandikisha katika vituo kabla ya kuongeza kwenye BVR vituo vilivyoombwa kuongezwa na kupelekwa kwenye vituo karibu na maeneo wanayoishi.
Wapiga kura kuandikishiwa katika Mfumo wa Mafunzo.
Katika taarifa zilizochakatwa imebainika kuwa baadhi ya Wapiga Kura waliandikishwa kwa kutumia mfumo wa mafunzo uliowekwa katika katika BVR kit iliyotakiwa kutumika wakati wa mafunzo tu, Usahihi wa taarifa za Biometric za Wapiga Kura hao kuwa sahihi lakini baadhi ya taarifa nyingine kuhitaji marekebisho kutoka katika fomu za Uandikishaji zilikizojazwa. Kazi hiyo inaendelea kufanyika katika kitu cha maandalizi ya Daftari kwa kuwa fomu zote za uandikishaji zimeishafika. Marekebisho hayo yalichelewesha kidogo baadhi ya taarifa katika madaftari yaliyowekwa wazi. Kazi ya Kurekebisha kasoro hizo zimeendelea kurekebishjwa na kabla ya tarehe 05/09/2015 kasoro zote zitakuwa zimerekebishwa.
Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura kutochukuliwa taarifa zao katika BVR Kit.
Tatizo hili lilisababisha baadhi Wapiga kura kutoonekana katika vituo walivyojiandikisha, zipo baadhi ya BVR Kit ziliibiwa na zikafanyika jitihada za kung’oa baadhi ya vifaa katika BVR kama vile Laptop na vifaa vingine. Zipo BVR mbili (2) kati ya BVR Kit 8000 ziliibiwa na walioiba walifanya jitihada za kuiba baadhi ya vifaa katika BVR kit hizo, BVR Kit hizo zilipatikana lakini zikiwa katika hali mbaya ya Uaribifu hivyo kushidwa kuondoa taarifa za Wapiga Kura mara moja, kwa kuwa Tume iliweka vifaa mahususi inapojitokeza changamoto kama hiyo kutopoteza taarifa za Wapiga Kura, chombo hicho kinachohifadhi taarifa za Wapiga Kura mara inapotokea uaribifu mbukbwa hususan wa kompyuta kuweza kupata taarifa za Wapiga Kura bila tatizo, Tume tayari imekwisha pata vifaa vilivyokuwa vimeifadhi taarifa za Wapiga kura na tayari taarifa hizo zinaingizwa katika mfumo wa kuchakata taarifa za Wapiga Kura.
Kata Mpya.
Kwa mujibu wa sheria OWM ­ TAMISEMI ndiyo yenye hadhi ya kupandisha na kugawa maeneo ya kiutawala ili kuchochea maendeleo ya haraka kwa wananchi wake. Mabadiliko hayo ya mipaka ya kiutawala yanahitaji kuhuishwa na Tume katika Mifumo yake ili kuwezesha chaguzi kufanyika na hasa chaguzi za madiwani, hivyo yanafanyika marekebisho ya kuhamisha kuweka vituo na Wapiga Kura katika maeneo mapya ya kiutawala yaliyoanzishwa, ikiwa ni pamoja na:­ Vitongoji, Mitaa,Vijiji, Kata na Halmashauri.
Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura taarifa zao kukosewa na BVR Kit Opereta wakati wa Uandikishaji.
Baadhi ya Wapiga kura taarifa zao zilikosewa na BVR Opereta wakati wa Uandikishaji hivyo kuhitaji marekesho na kupatiwa kadi mpya. Tume ilipeleka BVR Kit katika Halmashauri zote wakati wa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura, ili kufanya marekebisho ya taarifa za Wapiga kura pale panapohitajika. Marekebisho yamefanyika Tume inategemea Taarifa hizo zitafika na kuingizwa katika mifumo ili kupata taarifa sahihi.
Wapiga Kura Kujiandikishia katika maeneo tofauti na maneo wanayoishi.
Baadhi ya Wapiga Kura walijiandikisha katika maeneo tafauti na maeneo wanyaoishi, hivyo kuhitaji kuhamisha taarifa zao, tatizo hili limebainika katika maeneo mengi ya mjini, hasa kwa Wapiga Kura kutaka kuwahi kupata kadi za Mpiga kura, kasoro hii imeendelea kurekebishwa wakati wa zoezi la kuweka wazi Daftari.
Uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.
Uwekaji wazi wa Daftari la awali la Wapiga Kura ni takwa la kisheria, kifungu cha 11a cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 kinaitaka Tume kuweka wazi Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uhakiki wa Taarifa na kurekebisha kasoro zozote zinalizojitokeza.
Ili kuhakiki taarifa katika Daftari la Awali la Wapiga Kura wananchi wanatakiwa kufika katika Ofisi za kata ili kuweza kuangalia kama majina yao yapo katika Daftari, na ikiwa Taarifa zao ni sahihi mfano Jina, Jinsia, Tarehe ya kuzaliwa na Kituo chake cha kujiandikishia, Aidha, kwa Wapiga kura waliohama kata au jimbo moja kwenda kata au jimbo lingine wanatakiwa kuhamisha taarifa zao.
Zoezi hili la uhakiki lilianza rasmi tarehe 07/08/2015 katika Mikoa mbali mbali na limekuwa likiendelea hadi sasa ili kuhakikisha kila Mpiga kura aliyeandikishwa kupiga kura anaweza kupiga kura bila usumbufu wowote.
Katika zoezi hili Tume imeweka utaratibu wa kuwaondoa watu wote waliojiandikisha katika Daftari ambao siyo raia wa Tanzania, ambapo mchakato huo unaishia katika mahakama ya wilaya. Ili kasoro hii iweze kuondolewa Tume inahitaji kwa kiasi kikubwa Ushirikiano na wananchi wanaoishi nao ili kuwawekea pingamizi na waweze kuondolewa katika Daftari, ni ukweli kwamba iwapo wananchi watawaficha na kutowawekea pingamizi tatizo hili litakuwa gumu kwa Tume kulitatua.
Kasoro mbalimbali zilizobainika wakati wa Uandikishaji Tume itahakikisha inazirekebisha ili kuhakikisha kuwa Tume inakuwa na Daftari sahihi na la kuhaminika.
Imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''
WANANCHI WAMZUIA MGOMBEA MWENZA WA CCM BARABARANI MWANGA

WANANCHI WAMZUIA MGOMBEA MWENZA WA CCM BARABARANI MWANGA

August 24, 2015
Bi. Samia Othuman Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo. Bi. Samia Othuman Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo.Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo. Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.Mjumbe Mkuu wa Baraza Kuu la Wanawake na Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Same, Anjela Kailuki akizungumza alipokuwa anamnadi Bi. Samia Suluhu, BAADHI ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya kuendelea na safari yake.

 Bi. Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi hao kusogea zaidi barabarani wakati akipita huku wakinyoosha mikono ya kumuomba asimame ili azungumze nao eneo la kilometa chache kabla ya kuingia njia panda. Wananchi hao wengi wakiwa wakinamama walimsimamisha kwa kuingia pembezoni mwa barabara alipokuwa akipita na hivyo kulazimika kusimama kwa dakika chache na kuzungumza nao. 

 Akizungumza aliwaambia amefarijika na kuwaona na mapenzi makubwa na chama chao hivyo kuwaeleza kuwa yeye ni mwanamke pia na anajua kwa karibu kero ambazo wanakabiliana nazo akinamama sehemu mbalimbali na kuahidi endapo watapata ridhaa pamoja na Dk. John Magufuli atahakikisha anasimamia vizuri utaratibu wa kuwawezesha akinamama kupitia vikundi vya kijamii ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao. 

Alisema yeye ni mwanamke mzazi anatambua shida wanazokumbana nazo akinamama hasa kwenye wodi za wazazi hivyo akifanikiwa kuingia madarakani atahakikisha anasimamia ipasavyo ilani ya chama ambayo imeeleza vizuri juu ya uboreshaji huduma za afya ikiwemo wodi za akinamama na hali ya upatikanaji madawa. 

"...Matatizo ya wanawake nayafahamu vizuri wala sisimuliwi maana na mimi ni mzazi nimeingia wodi ya wazazi mkitupa ridhaa na mwenzangu (mgombea urais, Dk. Magufuli) nitahakikisha nayasimamia haya vizuri," alisema Bi. 

Suluhu akizungumza muda mfupi na wananchi waliomzuia barabarani wakiomba awasalimu. Alisema kero ya maji imekuwa inawatesa akinamama kwa kutumia muda mwingi kutafuta maji na kushindwa kuzalisha uchumi wa familia ipasavyo, hivyo Serikali ya CCM imeanza mradi wa kutoa maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu na kuyaingiza katika vijiji vyenye shida ya maji.

 Aidha akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara Mwanga ameisikia kero ya uhaba wa mabweni kwa wanafunzi wa kike suala ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa mabinti hao kutiwa mimba na kukatisha masomo eneo hilo na kudai suala hilo lipo katika ilani ya CCM mwaka huu na litashughulikiwa vizuri endapo watapewa ridhaa na wananchi, ikiwa ni pamoja na suala zima la kupambana na kuongeza fursa za vijana ili kukabiliana na uhaba wa ajira. 

Alisema Serikali iliyopita imejitahidi kuongeza huduma za umeme katika vijiji ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi lakini katika awamu hii CCM ikipewa ridhaa itahakikisha vijiji vilivyobaki kwa baadhi ya maeneo vinawekewa umeme.

 Alisema anawapa akinamama kazi kuhakikisha Dk. Magufuli na wagombea wa CCM eneo hilo wanashinda kwa asilimia 80 kwani wao ndio wenye ushawishi mkubwa katika familia. Vivyo hivyo kuwataka madiwani wanaogombea kuhakikisha mgombea uraisi na wengine wanapata kura za kutosha ili kushinda uchaguzi. 

Kwa upande wake Asumta Mshana aliyekuwa mbunge wa CCM na uchaguzi huu aligombea na kura hazikutosha alisema anawashangaa wanachama ambao waligombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi na waliposhindwa wakaamua kuondoka ndani ya chama hicho. Alihoji kwani walipokuwa wakiomba nafasi hizo hawakutambua kuna kushindwa na kushinda? 

Aliwafananisha wanaofanya hivyo ni sawa na akinababa wanaoamua kukimbia familia zao jambo ambalo ni aibu. "Nawashauri wababi ndani ya chama na kukijenga chama ili kiweze kufanya vizuri, kama kura hazikutosha safari hii usikimbie chama kwani mlikuwa hamjui kuna kushinda na kushindwa unapoomba uongozi," alisema. 

Naye Mwenyekiti wa CCM, Mkoa Idd Juma Mohamed alimshukuru Bi. Samia kwa kuamua kuanza kampeni katika mkoa wake na kumuhakikishia watahimiza wapiga kura kwani Kilimanjaro bado ni ngome ya CCm na watahakikisha wanatwaa majimbo yote, viti vya udiwani.

MAGUFULI AITIKISA KATAVI,WAZIRI MKUU PINDA AMNADI KWA KISHINDO.

August 24, 2015
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli akihutubia wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Azimio mjini Mpanda, mkoani Katavi.

Copy the BEST Traders and Make Money (One Click) : http://ow.ly/KNICZ

 Waziri Mkuu MizengO Pinda akimtambulisha Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli mbele ya umati wa watu waliofurika jioni ya leo kwenye uwanja wa Azimio mjini MPanda mkoani Katavi wakati wa muendelezo wa kampeni za chama hicho mkoani humo leo.Chama cha CCM kimezindua kampeni zake jana katika viwanja vya Jangwani jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama na wakereketwa wa chama hicho cha CCM
 Wananchi wakishangilia wakati  Waziri Mkuu Pinda alipokuwa akimnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli  wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa  Azimio mjini Mpanda, mkoani Katavi
 Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wamefurika leo katika uwanja wa Azimio mjini MPanda wakimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jonh Pombe Magufuli kupitia chama cha CCM,mkoani Katavi.
Wananchi wa kata ya Katumba wilayani Nsimbo wakiwa wamekusanyika kwa wingi kumsikiliza Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata hiyo, wilayani Nsimbo mkoani Katavi 
Waziri Mkuu Pinda akimuelekeza jambo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokwenda kuwahutubia wananchi wa Mpanda mjini kwenye kutano wa kampeni  mkoani Katavi.
   Sehemu ya umati wa Wananchi wa kata ya Mishamo,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 



  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimtambulisha Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni  katika kata ya  Mishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi.
 Mmoja wa wananchi akimshangilia Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika kijiji cha Mpandandogo,mkoani Katavi
 Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakisubiri kumisikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni  katika kata ya Mishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
  Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakishangilia wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni kwenye kata yaMishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni kwenye kata ya Mishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi.

   Sehemu ya umati wa Wananchi wa kata ya Mishamo,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Kata ya Mishamo mapema leo mchana wakati wa mkutano wa kampeni  wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
  Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakishangilia wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni kwenye kata yaMishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
  Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakishangilia wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni kwenye kata yaMishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi. 
 Sehemu ya Wananchi wa kata ya Mishamo,wakisubiri kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni  katika kata ya Mishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda pichani kushoto akiwa na baadhi ya wanachama cha CCM,ndani ya wilaya ya jimbo la Nsimbo wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokwenda kuwahutubia wananchi hao kwenye kutano wa kampeni  mkoani Katavi.
Wafuasi na wanachama cha CCM wakifurahia mkutano wa kampeni wa mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli jioni ya leo katika uwanja wa Azimio mjini Mpanda mkoani Katavi.

PICHA NA MICHUZI JR-KATAVI
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.