January 23, 2014

RATIBA NA MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA RAUNDI YA PILI, KAGERA SUGAR vs MBEYA CITY KUCHEZWA KAITABA STADIUM JUMAMOSI, YANGA VS ASHANTI UNITE TAIFA


Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza Jumamosi kwa mechi tano katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam, Tanga wakati mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting inahamishiwa uwanja mwingine.

Ashanti United itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union itacheza na Oljoro JKT katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar.
Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Mgambo Shooting itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex wakati Simba na Rhino Rangers zitaumana kwenye Uwanja wa Taifa.

Mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine inahamishiwa uwanja mwingine kwa vile huo bado nyasi zake ambazo zimepandwa hivi karibuni hazijawa tayari kuhimili mechi hiyo.

Hivyo Tanzania Prisons inatakiwa kutafuta uwanja mwingine unaokidhi viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mechi hiyo, na nyingine dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Januari 29 mwaka huu.

Pia matumizi ya tiketi za elektroniki yanaanza katika mzunguko huu kwa vile viwanja nane ambavyo tayari vimefungwa vifaa vya tiketi hizo. Vilevile tunakumbusha washabiki wa mpira wa miguu kuwa tiketi za elektroniki haziuzwi viwanjani.
Viongozi wa Kagera Sugar(kulia) ni Kocha mkuu
SIMBA SC 2, KAGERA SUGAR 2 walipotoshana nguvu msimu uliopita na Simba

Wachezaji wakisalimiana.

Kikosi cha Mbeya City kilichopambana na Azam FC katika msimu wa kwanza

MSIMAMO ULIVYO KWA SASA:
NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Young Africans
13
8
4
1
31
11
20
28
2
Azam FC
13
7
6
0
23
10
13
27
3
Mbeya City
13
7
6
0
20
11
9
27
4
Simba SC
13
6
6
1
26
13
13
24
5
Kagera Sugar
13
5
5
3
15
10
3
20
6
Mtibwa Sugar
13
5
5
3
19
17
2
20
7
Ruvu Shootings
13
4
5
4
15
15
0
17
8
Coastal Union
13
3
7
3
10
7
3
16
9
JKT Ruvu
13
5
0
8
10
16
-6
15
10
Rhino Rangers
12
2
4
6
9
16
-7
10
11
JKT Oljoro
13
2
4
7
9
19
-10
10
12
Ashanti United
13
2
4
7
12
24
-12
10
13
Tanzania Prisons
12
1
5
6
6
16
-10
8
14
Mgambo JKT
13
1
3
9
3
23
-20
6
RATIBA
RAUNDI YA PILI
25 Januari 2014
Ashanti United vs Yanga
Azam FC vs Mtibwa Sugar
Coastal Union vs JKT Oljoro
Kagera Sugar vs Mbeya City
Tanzania Prisons vs Ruvu Shootings
JKT Ruvu vs Mgambo JKT

Jumapili, 26 Januari 2014
JKT Ruvu vs Mgambo JKT
Simba vs Rhino Rangers
Tanzania Prisons vs Ruvu Shootings [Imeahirishwa, Sababu ya Uwanja]
January 23, 2014

HALMASHAURI YA SIHA IMEPITISHA BAJETI YA SH. BILIONI 19.3

Na Omary Mlekwa, Siha

HALMASHAURI ya wilaya Siha mkoani Kilimanjaro imesema imeshindwa kukamilisha  kwa miradi ya kimaendeleo kwa wakati kutokana na kuchelewa kupokea fedha za miradi kutoka hazina  pamoja na uchache wa vyanzo vya mapato ya ndani pamoja na mabadiliko ya tabia nchini.

Akizungumza katika kikao maalumu  cha baraza la madiwani kujadili bajeti ya mwaka wa fedha wa 2014/2015, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Rashidi Kitambulio alisema uchelewashaji umesababisha miradi ya kielimu, afya miundombinu kukwama. Mkurugenzi huyo alisema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri uzalishaji   wa mazao na kuathiri mapato yatokanayo na mazao mashambani ambapo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 walikusudiwa kukusanya kiasi milioni 239,500,000 badala yake walishindwa kufikia lengo hilo.

Awali akitoa taarifa ya rasmi ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka fedha 2014/2015 mkurugenzi wa huyo alisema kuwa wanatazamia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 19.320,034,512 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ruzuku toka serikali kuu na mapato ya ndani.


Kitambulio alifafanua kuwa kiasi hicho  ni sawa na ongezeko la shilingi bilioni 2,297,943,008 ikilinganishwa fedha  zilizoidhinishwa katika  bajeti ya shilingi bilioni 17,022,091,594 ya mwaka wa fedha 2012/2013



Alisema katika bajeti hiyo wanakusudia kukusanya shilingi bilioni 1, 935,247,550kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani  ikiwemo ushuru wa masoko, ushuru wa vituo vya mabasi , ushuru wa mazao na vyanzo vingine vilivyopo katika halmashauri hiyo.
January 23, 2014

Thursday, January 23, 2014

YANGA YAWATOA SHAKA MASHABIKI JUU YA MCHEZAJI OKWI

Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wake kutokuwa na wasiwasi juu ya mchezaji Okwi ambaye amepigwa stop na TFF kucheza yanga hadi wapate uthibitisho wa uhalali wake kucheza Yanga.

Katibu mkuu wa Yanga Beno Njovu amesema mashabiki watulie kwani Okwi ni mchezaji halali wa yanga hakuna wa kumzuia kucheza mpira kwani kila kitu kilikamilia na kinachosubiriwa na FIFA kuweka ukweli wa mchezaji huyo

Awali Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana leo (Januari 22 mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.

Okwi ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.

Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.

Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.

MECHI ZA TANZANIA PRISONS YAZASOGEZWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mechi za raundi ya 14 na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari 25 na 29 mwaka huu.

Awali Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechi hizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.

Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.
January 23, 2014

FREDERICK SUMAYE ATUA CLOUDS MEDIA GROUP



Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipowasili mapema leo kwenye makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar,pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kwenye moja ya Ofisi za kampuni hiyo,alipofanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.

TAFCA MOROGORO WAANDAA SEMINA YA KOZI KWA MAKOCHA

January 23, 2014
Na Daudi Julian, Morogoro
CHAMA  cha makocha wa mpira wa miguu Tanzania (TAFCA) mkoa wa Morogoro kimeandaa kozi ya kati kwa makocha wa mchezo huo inayotarajiwa kuanza kufanyika Februari 26, mwaka huu, mkoani hapa.

Akizungumza na mtandao huu, katibu  mkuu wa chama hicho, Hemed Mumba alisema maandalizi kwa ajili ya kozi hiyo itakayochukua siku kumi yanakwenda vizuri na kwamba tayari baadhi ya makocha wameshajiandikisha.

Mumba alisema lengo la kozi hiyo ni kuwaendeleza makocha wa mpira wa miguu mkoani Morogoro na mikoa mingine ili kuhakikisha mchezo wa soka unapiga hatua kubwa.

Alisema ada ya ushiriki katika kozi hiyo ni Sh.60,000 na mwisho wa kulipa ada hiyo ni Februari 16.

RAIS MALINZI MGENI RASMI TUZO ZA MAKOCHA BORA MACHI 8 DAR ES SALAAM.

January 23, 2014
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam.
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya tuzo ya makocha wa mpira wa miguu Tanzania inayotarajia kufanyika Machi 8, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao huu jijini Dar, Afisa Mtendaji wa tuzo hiyo, Fredrick Luunga alisema kamati ya maandalizi ya tuzo iliyokutana hivi karibuni ndiyo iliyopitisha jina la Malinzi kuwa mgeni rasmi siku hiyo.

Luunga alisema lengo la kumwalika kiongozi huyo wa juu wa soka ni kuthamini mchango wake katika kuendeleza mchezo huo hapa nchini na pia kumpa fursa ya kukutana na kuzungumza na makocha wa mpira wa miguu Tanzania na wadau wengine kupitia hafla hiyo.

DC SIHA AWATAKA WATAALAMU WA HALMASHAUTI KUIMARISHA UKUSANYAJI WA USHURU.

January 23, 2014
Na Omary Mlekwa,Hai.MKUU wa wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Dkt Charles Mlingwa amewataka wataalumu wa halamashauri hiyo kuimarisha hali ya ukusanyaji wa ushuru wa aina  mbalimbali bila kubugudhi wananchi ili kuongeza mapato ya ndani

Pia aliwataka wataalamu hao kuwa na  takwimu sahihi za walapi kodi
wakubwa na wadogo ili kuweza kuweka makisio ya mapato na matumizi yanayoendana na utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo

Akizungumza na wajumbe wa baraza pamoja na wananchi waliohudhuria
kikao maalumu cha baraza la madiwani cha kujadili na kupisha bajeti ya mwaka wa fedha wa mwaka 2014/2015 alisema wataalamu wakiimarisha ukusanyaji itasaidia kupunguza utegemezi  wa kutoka serikalini

Kauli hiyo aliitoa baada ya baadhi ya madiwani kupinga bajeti ya

ushuru wa mazao kwa madai kuwa inawaumiza wakulima wa mazao mbalimbali

TINDU LISU ANGURUMA TANGA.

January 23, 2014
Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, aliwataka Watanzania, hususan wanachama wa chama hicho kutopoteza muda kujadili suala la baadhi ya wanachama wa chama hicho waliopatikana na makosa ya usaliti na utovu wa maadili ndani ya chama hicho.

Ingawa hakuwataja wanachama hao aliowaita wasaliti, ni wazi alikuwa akiwalenga, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba. Tayari chama hicho kilikuwa kimeshawapokonya uanachama, Dk. Kitila na Mwigamba, huku Zitto akiendelea kubakia ndani ya chama hicho baada ya Mahakama Kuu kuizuia Chadema kumjadili.

Akifafanua, Lissu alisema, wanachama wa Chadema wanapaswa wajikite zaidi kukiimarisha chama hicho kila mahali na kujadili masuala yanayowahusu.

Lissu, ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Taifa, (BAVICHA), John Heche, alisema taifa linakabiliwa na masuala mengi ambayo yanahitaji umakini wa kila mwanachama wa chama hicho, akitolea mfano wa kujadili maudhui ya Rasimu ya Pili ya Katiba mpya, ili taifa lipate Katiba mpya na bora.

Aliwaambia wananchi wa maeneo hayo kwamba kutokana na uongozi mbovu, rasilimali za Tanzania zimeendelea kutafunwa na watu wachache kwa kupitia sera za ubinafsishaji ambazo zimetumiwa na watawala kama mianya ya kujigawia mali kwa mgongo wa uwekezaji, huku wazawa wengi wakiwa hawana la kufanya.

MATUKIO YA MKUTANO WA CHADEMA JANA MKOANI TANGA.TINDU LISU,JOHN HECHE WAUTEKA MKUTANO HUO

January 23, 2014


Tundu Lisu kulia akisalimiana na Ofisa wa Polisi Mkoani Tanga ambaye alikuwa kwenye mkutano huo

Tundu Lisu kushoto akimnadi Mgombea Udiwani kata ya Kiomoni Mwanaisha Omari jana

Mwanasheria Mkuu wa Chadema,Tundu Lisu akiwahutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Lwande Kata ya Kiomoni.






Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini,Amani Golugwa akiwahutubia wananchi wa Kijiji hicho jana.

Tindu Lisu katika akilakiwa na viongozi wa Chadema mara baada ya kutua katika viwanja vya Kijiji cha Lwande kata ya Kiomoni


JENGO LA SHIRIKA LA BIMA YA TAIFA (NIC) KILIMANJARO LAWAKA MOTO.

January 23, 2014

JENGO la Shirika la Bima la Taifa, mkoani Kilimanjaro (NIC), juzi  lilinusurika kuteketea kwa moto baada ya moto mkubwa kuibuka katika  moja ya Vyumba vya ofisi zake na kuteketeza baadhi ya nyaraka muhimu kabla ya zima moto kufika na kuuzima kabla haujasababisha madhara  makubwa.


Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa mashuhuda wakiwemo baadhi ya  wafanyakazi wa shirika hilo, lililoko katika Jengo namba 2021, mtaa wa  TRA, Manispaa ya Moshi, mkoani hapa, moto huo ulianzia katika moja ya  vyumba vinavyotumika kuhifadhia nyaraka za Bima.
Baadhi ya maeneo ya ofisi katika Jengo hilo yaliyoathirika na moto huo
TAIFA LETU.com ilifika katika eneo la tukio na kukuta sehemu kubwa ya  moto huo ukiwa umeshazimwa kutokana na juhudi za pamoja ya wafanyakazi  wa Shirika hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha zimamoto, ambao tofauti ilivyozoeleka walifanikiwa kuwahi kufika  katika eneo la tukio.

Polisi wakikagua Baadhi ya maeneo ya ofisi katika Jengo hilo yaliyoathirika na moto huo

Akizungumza na gazeti hili kuhusu chanzo cha moto huo, Meneja wa  shirika hilo mkoani Kilimanjaro, John Mdenye alisema chanzo cha moto  huo haujafahamika bado na kuongeza kuwa alipata taarifa kutoka kwa katibu wake kuhusu kuonekana kwa Moshi ikitokea katika moja ya Stoo za  Shirika hilo.

Meneja wa NIC mkoani Kilimanjaro, John Mdenye akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu chanzo cha moto huo
“Nilikuwa Ofisini tangu saa mbili asubuhi, majira ya saa sita hivi,  Principle wangu alikuja na kunieleza kuwa kuna moshi katika stoo yetu  ya kuhifadhia faili za bima, baada ya kama dakika 10 kuliibuka moto mkubwa kutokea maeneo hayo, haraka niliwasiliana na zima moto ambao  walikuja kutoa msaada,” alisema Mdenye.

Mmoja wa Wafanyakazi akizungumza na Waaandishi wa Habari
Aidha Meneja huyo alisema mpaka sasa haijafamika moto huo utakuwa  umesababishwa na nini japo wanahisi huenda moto huo utakuwa umeanzia  katika ngazi za kupanda juu ambako kuna nyumba ya mpangaji mmoja  ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Gari la zimamoto likiondoka katika eneo la Jengo la Shirika la Bima ya Taifa, lililowaka moto
Alisema hisia hizo hata hivyo hazitoi uthibitisho wa moto kuanzia  katika nyumba ya mpangaji huyo kwani kilichoonekana mpaka sasa ni  kuwepo kwa mtungi wa gesi katika sehemu ya chini ya ngazi hizo hivyo kutoa wasiwasi huenda mpangaji huyo alikuwa anapikia hapo kutokana na sheria katika mkataba kutomruhusu kupika katika nyumba yake iliyoko  ghorofani kwa usalama wa ofisi za bima zilizoko chini.


 
Mpaka sasa haijafahamika kiasi cha thamani ya mali iliyoharibiwa  kutokana na moto huo japo hadi mwandishi wa gazeti hili anaondoka katika eneo la tukio, mali iliyoripotiwa kuharibika ni faili zote za bima zilizoteketea katika moto huo, kompyuta mbili moja ikiwa ni kompyuta mpakato ya Meneja huyo.

chanzo:www.kijiwechetu.blogspot.com