WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI DED WA MBOZI KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI DED WA MBOZI KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA

July 23, 2017
PMO_5114
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa  Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wa wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Vwawa wilayani Mbozi Julai 23, 2017. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa  Wapili  kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Limdi, Erasto Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5127
Cashier wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi  Bahati Chomoka pia amesimamishwa.kazi.
PMO_5129
DT wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Simon Noeli ambaye pia amesimamishwa kazi.
PMO_5133
DED wa Mbozi, Elisey Mgoyi mmoja wa watendaji wa Halmashauri ya  Wilaya ya Mbozi ambao Waziri Mkuu aliagiza wasimashwe kazi na wafanyiwe uchunguzi na TAKUKIURU.
PMO_5191
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe nje kidogo ya mji wa Vwawa mkoani Songwe Julai 23, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5264
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kulia kwake) wakitazama Kimondo wakati walipotembelea Kituo cha Mambo ya Kale cha Mbozi mkoani Songwe Julai 23, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5316
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa wilaya ya Mbozi wakati walipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kyalele wilayani humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5356
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama nguo za batiki  wakati walipotembelea banda la wanawake wajasiriamali wa Mbozi kabla ya  mkutano wa hadahara uliohutubia wa Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nalyelye wilayani Mbozi, Februari 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)
……………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Bw. Eliseyi Mgoyi pamoja na maofisa wengine watatu kwa  tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma.
Pia amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Songwe, Bw. Damian Sutta kuwakamata na kuanza kuwachunguza haraka maofisa hao na kisha ampelekee taarifa ofisini kwake.
Waziri Mkuu amewasimamisha kazi maofisa hao leo (Jumapili, Julai 23, 2017) wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Vwawa, akiwa katika ziara yake ya kikazi.
Maofisa wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Bw. Simon Noel,  Bw. Bahati Chomoka ambaye ni Cashier na Bw. Remmy Haule  ambaye ni Ofisa Ugavi.
Waziri Mkuu amesema Maofisa hao wamekiuka sheria za matengenezo ya magari ya Serikali kwa kwenda kutengeneza katika gereji ambazo hazikusajiliwa na wala hazifanyi shughuli hiyo, jambo ambalo halikubaliki.
Amesema Kampuni ya Umbwila ni moja kati ya Kampuni zinazolipwa fedha nyingi za utengenezaji wa magari ya Halmashauri ya wilaya ya Mbozi huku ikiwa haina sifa za kufanya kazi hiyo ya utengenezaji magari.Kampuni zingine ni Julius Diesel, Kasaba na Mtoni Garage.
“Mfano duka la  Umbwila ambalo linauza vipuri vya magari lakini Halmashauri inalilipa fedha kwa ajili ya utengenezaji wa magari jambo ambalo si sahihi kwa sababu lile ni duka la vipuri na si gereji. Wanamlipa muuza vipuri kama mtengeneza magari”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “hatuwezi kuendesha Serikali kwa namna ambayo haikubaliki kwani watu tuliowapa dhamana ndio wanaongoza kwa vitendo vya rushwa na ufisadi. Wameifanya Halmashauri hii kama shamba la bibi.”
Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu amemtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mheshimiwa Eric Ambakisye kuhakikisha anasimamia vizuri utendaji ndani ya Halmashauri hiyo na kwamba Serikali inataka watu waadilifu na wenye uaminifu na nidhamu.
“Halmashauri inanuka rushwa tunataka iwe safi. Hatuwezi kukubali kuona Halmashauri hii na zingine nchini zikigeuzwa kuwa magenge. Kwa Serikali hii no, hatuhitaji rushwa wala harufu ya ufisadi.”
Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumilia kuona watumishi waliopewa dhamana wakijinufaisha kwa fedha za umma na kuwaacha wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo za maji, afya na elimu, hivyo itaendelea kuwachukulia hatua.
Pia Waziri Mkuu amewataka Madiwani na Wakuu wa Idara katika Halmashauri zote nchini wabadilike na wahakikisha wanashirikiana na kufanya kazi kwa ushirikiano kwani wakigawanyika watashindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA MRADI WA MAJI NGURUKA WILAYA YA UVINZA MKOANI KIGOMA

July 23, 2017
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mapema asubuhi ya leo tarehe 23 Julai 2017 akihutubia wananchi wa kijiji cha LUCHUGI-UVINZA Mkoani Kigoma akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora Kuanza Ziara ya Kiserikali Mkoani Humo 
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mapema asubuhi ya leo tarehe 23 Julai 2017 akihutubia wananchi wa kijiji cha LUCHUGI-UVINZA Mkoani Kigoma akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora Kuanza Ziara ya Kiserikali Mkoani Humo 
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza mwenyekiti wa kijijji cha Uvinza Ndugu Nilisi Noa Ntabai alipokuwa akieleza kero ya maji ya eneo hilo la uvinza ikiwemo kusimama kwa kiwanda cha chumvi Uvinza ambacho kilikuwa tegemeo kwa wananchi wa eneo hilo,ambapo Mhe,Rais amewaahidi wananchi hao kumtuma Waziri wa Viwanda na Biashara kushughulikia tatizo hilo. Julai 23,2017.
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mapema asubuhi ya leo tarehe 23 Julai 2017 akihutubia wananchi wa kijiji cha LUCHUGI-UVINZA Mkoani Kigoma akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora Kuanza Ziara ya Kiserikali Mkoani Humo 
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikagua tanki la akiwa kuhifadhia maji toka mto Maragalasi kabla ya kuweka jiwe la msingi la maradi huo utakao hudumia wananchi wa Nguruka, Uvinza, mkoani Kigoma. Kulia ni  Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge. 
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa ameambatana na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge wakishuka ngazi mara baada ya Mh,Rais Kukagua Ujenzi wa Tanki la Kuhifadhia Maji kwaajili ya Wananchi wa Nguruka kabla ya kuhutubia wananchi. 

TAMASHA KUBWA LA CASTLE LITE UNLOCKS LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

July 23, 2017

Msanii Vanessa Mdee akiwa jukwaani akiwakonga mashabiki.

Dk. Kigwangalla aweka jiwe la msingi la ujenzi wa bweni la makazi ya wazee ya Kolandoto, Shinganga

July 23, 2017
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akipongezwa na Mwakilishi wa Wazee wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa zoezi hilo la kuweka jiwe la Msingi la jengo la makazi ya Wazee Kolandoto.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akipata maelezo namna jengo hilo litakavyokuwa wakati alipotembelea kwa ajili ya kuweka jiwe la Msingi la jengo la makazi ya Wazee Kolandoto.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo linapojengwa jengo la Wazee Kolandoto.  ambapo aliwela jiwe la Msingi la jengo la makazi ya Wazee Kolandoto.

Na Mwandishi Wetu Shinyanga

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), itaendelea kusimamia haki za wananchi wake kuanzia watoto, Vijana na Wazee ilikulinda haki na hutu wao hapa nchini.

Dk. Kigwangalla amesema hayo Julai 22,2017, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bweni la makazi ya Wazee ya Kolandoto, yaliyopo umbali wa zaidi ya  KM 10, kutoka Shinyanga Mjini, mkoani Shinyanga.

 Ambapo mabli na kuweka jiwe hilo la msingi la ujenzi wa bweni hilo, pia alifungua rasmi jiko maalum la gesi ambalo litakuwa likitumika kwa ajili ya chakula cha wazee hao pamoja na kukabidhi Bajaji ya miguu mitatu itakayorahisisha usafiri kwa wazee hao kwenye makazi yao hayo.

Makazi ya wazee ya Kolandoto ni ya muda mrefu, ambapo kwa uanzishwaji wa ujenzi wa bweni hilo litakuwa faraja kwa wazee wanaoishi hapo kwani litakuwa na uwezo wa kuchukua wazee zaidi ya 20.
“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imeweka msisitizo kuendelea kuwaenzi wazee kwa michango yao katika kulijenga taifa letu. Serikali ina jukumu la kuwatambua wazee na kuwapatia huduma za matibabu bila malipo na kuhakikisha wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji. Katika kutekeleza haya, Serikali ya Awamu ya tano imeunda Wizara inayosimamia masuala ya wazee ili kuhakikisha haki zao zinalindwa.  Katika kufanikisha azma hiyo, serikali inahudumia makazi hayo 17 ya  wazee wasiojiweza hapa nchini” alieleza Dk. Kigwangalla

Mpaka likikamilika litatosha kuwahudumia wazee wasiojiweza 20. Hivi sasa kuna wazee 16, kituoni hapa. Majengo ya zamani ni ya udongo na yamekaa zaidi ya miaka 50 bila ukarabati.

Kimsingi hayafai tena kwa matumizi ya binadamu (yapo condemned). Tumeyakarabati ili yaweze kutumika wakati tukijenga jengo hili jipya la kisasa” alieleza Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla aliongeza kuwa, Pamoja na ujenzi wa jengo hilo kwenye makazi ya wazee wasiojiweza, Wizara yake imefanya maboresho makubwa na muhimu sana kwenye makazi hayo ikiwemo kuweka majiko ya kisasa ya gesi, vyombo vya kupikia na kulia chakula, huduma ya maji, vifaa vya huduma ya kwanza, vifaa vya chumba cha kulala na vyombo vya usafiri (Bajaj)na huduma muhimu kwa wazee hao.

Hata hivyo, Dk. Kigwangalla ameeleza pamoja na ufinyu wa bajeti wanayopewa  kwa ajili ya idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, amewapongeza wataalamu wa idara hiyo wakiongozwa na Katibu Mkuu, Ndg. Sihaba Nkinga, kwa ubunifu uliowezesha kufanyika bila kupokea pesa ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Wataalamu wanapaswa kutumia ujuzi wao kuleta tija na ufanisi kwenye utekelezaji wa majukumu tuliyopewa. Nawapongeza sana kwa kufanya jambo hili kubwa na la umuhimu” alimalizia Dk. Kigwnagalla.

Hata hivyo, Dk. Kigwangalla amesema kuwa, Serikali itaendelea kuimalisha makazi ya wazee hao kwani inatambua thamani yao hivyo ni jukumu la kuwasaidia huku pia akitoa rai kwa Jamii kuweza kukaa nao wazee hao kwani Uzee unapitiwa na jamii yote na haukwepi.

RIPOTI: HOTELI ZA NYOTA MBILI NA TATU HUPENDELEWA ZAIDI NA WATEJA

July 23, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Je ushawahi kupanga kwamba unataka kwenda kulala kwenye hoteli ya nyota ngapi? Ni vigezo gani ambavyo huwa unavitumia kutambua kwamba hoteli hiyo hadhi yake ni nyota fulani? Ni vigezo gani huja kwanza akilini pindi unapofanya uchaguzi wa hoteli hiyo? Ni maswali magumu ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyajibu labda awe anajihusisha au kufanya kazi kwenye sekta ya hoteli au mtu anayesafiri mara kwa mara.

UBALOZI WA JAPAN NCHINI WAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI MBALIMBALI YA KIMAENDELEO MKOANI IRINGA

July 23, 2017
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi wa pili kulia na wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni Shule ya Idodi sekondari leo
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi wa pili kulia na wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni Shule ya Idodi sekondari leo 
Vitanda vilivyopo katika bweni hilo 
Hili ndilo bweni la kisasa lililojengwa na ubalozi wa Japan nchini 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkaribisha balozi wa Japan nchini 
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akizungumza na wananchi na wanafunzi wa sekondari ya Idodi 
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akikabidhi taa za mionzi ya jua kwa mkuu wa shule ya sekondari Idodi kulia kwake ni mbunge wa Isiman Wiliam Lukuvi na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na katibu wa CCM Iringa vijijini Dodo Sambo 
Balozi wa Japan nchini akimkabidhi taa hizo mbunge wa Isimani wiliam Lukuvi 

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA LEO

July 23, 2017
TFF YAMPONGEZA TENGA

Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace John Karia amempongeza Leodegar Chilla Tenga - Rais wa Heshima wa TFF kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Leodegar Chilla Tenga aliteuliwa Ijumaa iliyopita katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mjini Rabat nchini Morocco ambako katika kamati hiyo muhimu, Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya.

“Hii ni sifa kwa nchi. Na ni sifa kwa Mheshimiwa Tenga. Tunajisikia fahari Tanzania kung’ara katika medani za uteuzi katika vyombo vya kimataifa kama CAF. Uteuzi wake ni kwamba anafungua njia kwa nchi na wengine ili kufanya vema,” anasema.

Karia amesema ana imani na Tenga na Bwalya katika kamati yao kwa sababu ni wachezaji na manahodha wa zamani wa timu za taifa. Itakumbukwa kwamba Tenga alikuwa akicheza kama mlinzi Bwalya alikuwa mshambuliaji. “Wote ni wataalamu. wanajua, tutafanikiwa.”

Katika mkutano huo mbali na kuteua akina Tenga na kuunda kamati nyingine, pia ulifanya marekebisho ya muundo wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na sasa yatakuwa yakifanyika katikati ya mwaka badala ya mwanzoni mwa mwaka. 

Kwa miaka ya nyuma hadi mwaka huu ambako michuano hiyo ilifanyika Gabon, ilikuwa ikifanyika kuanzia katikati ya Januari hadi Februari. Mbali na kuzitoa Fainali za AFCON katikati ya mwaka hadi mwanzoni, pia idadi ya timu za kushiriki zimeongezwa kutoka 16 hadi 24 ambako sasa utakuwa na timu washindwa 10 badala ya mbili kama ilivyokuwa awali.

“Watanzania wasikate tamaa, hata kama kwa mfumo wa sasa unaofutwa au tuseme kubadilishwa, bado tuna malengo yetu yalikuwa ni kufuzu, Tunajipanga kwa hali ya sasa na hatujaanza vibaya na Lesotho. Bado tuna nafasi,” amesema Karia.

Michuano hiyo kuhamishwa kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon.

Hii si mara ya kwanza kwa Tenga aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), bali amekuwa akiteuliwa mara kwa mara kuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF. Hongera sana Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Chilla Tenga.


BAHATI HAIKUWA UPANDE WETU - KOCHA

Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Fulgence Novatus, amesema kwamba Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti  ya SBL haikuwa na bahati katika mchezo dhidi ya Amavubi ya Rwanda uliofanyika Uwanja wa Kigali ulioko kata ya Nyamirambo.

“Tumecheza vema, tulitafuta nafasi za kutosha. Tumeshambulia sana na kumiliki mpira. Lakini kila tulipojaribu kufunga, bahati haikuwa kwetu,” amesema Novatus mara baada ya mchezo huo.

Matokeo ya sare tasa ya jana yanawapa nafasi ya kusonga mbele Rwanda baada ya sare ya 1-1 katika mchezo uliofanyika Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mchezo huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) na sasa Rwanda itacheza na Uganda mwezi ujao.

Pamoja na kushindwa kusonge mbele, Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi baada ya kucheza mechi 11 za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare mitano na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa.