DEGE ECO - VILLAGE YAFANYA VYEMA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR

July 07, 2015
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village akimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya kununua nyumba.
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village amkimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya kununua nyumba.
 Mmoja ya Afisa Masoko wa Dege Eco - Village
Wafanyakazi wa Dege Eco – Village wakiwa katika picha ya pamoja.
---
Kampuni ya Hifadhi Builders iliyokuwa na mradi mkubwa nchini inayoitwa Dege Eco Village wameweza kushiriki vyema maonyesho ya maonesho 39 ya kimataifa ya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo wa Dege Eco - Village, Bi. Catherine Mhina alisema kwamba Dege Eco Village wanafurahi sana kuweza kuwafikia watanzania wengi ambao walikuwa na shauku ya kujua huduma wanazo zitoa iki ni pamoja na kununua nyumba wanazojenga katika mradi wao.
"Tunashukuru Kila mmoja alikuwa akipita hapa anapenda kujua huduma zetu na pindi unapompa maelezo ya kina hasiti kujaza fomu ili aweze kununua nyumba."
Aliongezea na kusema kwamba mradi huu wa Dege Eco Village iliyopo Ras Dege, Kigamboni itakuwa na huduma za kijamii kama hospitali, shule aina ya chekechea, sekondari, pia kutakuwa supermarket na kadhalika.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

GLOBAL EDUCATION LINK YAVIALIKA CHUO KIKUU CHA SHARDA NA LOVELY PROFESSIONAL VYA INDIA KUSHIRIKI MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR

July 07, 2015
Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel (wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyuo vya nje ya nchi kutoka kushoto ni Meneja Miradi wa Chuo Kikuu cha Lovely Professional cha Nchini India, Bw. Gulshan Sandh na Bw. Sourabh Chaudhary pamoja na Meneja wa Kanda wa Chuo Kikuu cha Sharda cha nchini India, Bw. Deepak Kaushik mara baada ya kuwakaribisha katika ofisi yao iliyopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Global Education Link ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Bw. Abdulmalik Mollel (wa pili toka kulia) akiongea na wageni wake ambao ni viongozi wa vyuo vya nje mara baada ya kuwaalika kushiriki katika maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Principal Academic Officer wa Chuo cha IFM cha jijini Dar es Salaam akisisitiza jambo  la kielimu wakati alipokutana na viongozi wa vyuo vya nje ya nchi ndani ya ndani ya ofisi za GEL zilizopo ndani ya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yanayofanyika viwanja  vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

ZOEZI LA UBORESHWAJI DAFTARI LA WAPIGAKURA LAENDELEA MKOANI PWANI, RAIS JAKAYA KIKWETE AJIANDIKISHA KUPIGA KURA KWA KUTUMIA BVR KIJIJINI MSOGA

July 07, 2015
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.
 Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo leo .
 Bwana SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
 Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais Kikwete akimshukuru Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva baada ya kukabidhiwa kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo. Picha na Freddy Maro.
Rais akuonyesha kitambulisho chake alichopewa mara baada ya kujiandikisha katika daftari daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
---
JUMLA ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa limeingia mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa leo kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.

Bw. Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo.

“Hadi sasa ni mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva.

Aidha alisema kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya kwani kila jambo jipya lina changamoto zake.

“Mfumo huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,” alisema Lubuva.

Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''