Wenyeviti wa
vijiji wametakiwa kuhakikisha wanawasomea wananchi mapato na matumizi kila
baada ya miezi mitatu na kuhakikisha wanawashirikisha kwenye miradi ya
maendeleo bila kificho wala usiri.
Kauli hiyo imetolewa
na Afisa Tarafwa kata ya Mazingara Hashi Msagati wakati wa kikao cha baraza
la kata WDC kilichofanyika katika kijiji cha mazingara wilayani Handeni hapo
jana alisema ni kwaida ya watendaji kutowasomea wananchi mapato na matumizi ya
kijiji husika.
Alisema nihaki
ya msingi ya mwanakijiji kujua pesa yake inayokusanya kwa ajili ya maendfeleo
ya kijiji inatumika kwa mipango gani ya
maendeleo badala ya kuwafanyia kificho na kutumia fedha kwa malengo yasiyofaa.
“Nawaasa
watendaji wa mitaa,vijiji hadi kata kuhakikisha mnawaeleza wananchi kwa uwazi
bila kificho kiasi cha fedha za ruzuku za maendeleo zilizopatiwa kijiji na pesa
za makusanyo ya ndani huku mkiwashirikisha katika mipango ya maendeleo ya fedha
hizo”alisema Msagati.
Alisema
kunawizi wa kalamu hasa katika maeneo ya
vijiji watendaji wanaandika kuwa wananchi wameidhinisha fedha kumbe sio kweli huku
wahusika wenyewe wakiwa hawajui bali wanaona ujenzi tu unaendelea aidha wa
madarasa au miundombinu yoyote .
Nae Diwani
wa Kata ya Mazingara Kijoli aliwataka watendaji wa kata hiyo kuhamasisha
wananchi kujenga nyumba za kisasa za biashara ili watendaji hao waisha ndani ya
kata hiyo badala ya kuishi nje ya eneo la kazi.
Alisema hali
hiyo imekuwa ikizorotesha shughuli za maendeleo katika kata hiyo kwani
watendaji wengi hawawajibiki ipasavyo kutoka na kuishi mbali na ofisini zao
hivyo huwavigumu kuwapa pale wanapohitajika na wananchi hao.
Mwisho
|
Nasi tunapenda kuwa watangazaji
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Mimi na Mwanafunzi na muandaaji wa kipindi hicho kinachoruka
kituo cha Radio Mwambao Fm kila Jumaamosi saa tatu asubuhi Seleman Kibugo mwenye shati jeusi akiwa na wanafunzi wa shule ya
Shilela Academy iliyopo wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ambao watembelea Kituo Cha
Utangazaji Cha Mwambao Fm Tang leo.
NYUMBA 12 ZA WAVAMIZI WAHIFADHI YA MISITU ZATAKETEZWA KWA MOTO PANGANI
Jumla ya Nyumba 12 zilizokuwa zimejengwa na wahamiaji haramu
jamii ya wafugaji ndani ya hifadhi ya
msitu wa Msububwe wilayani Pangani Mkoani Tanga zimeteketezwa kwa moto na
kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiwa ni katika oparesheni ya
kuondosha wavamizi wa hifadhi hiyo .
Zoezi hilo ambalo linalenga kulinga hifadhi ya msitu huo
dhidi ya wavamizi hao wa kabila la
wamang”ati ambao walikuwa wamevamia hifadhi na kuanza kufanya uharibu wa kuharibu vyanzo vya maji, kukata miti hovyo ya kujengea nyumba , kuni
pamoja na kuchunga mifugo yao.
Akiongea na gazeti hili wakati wa oparesheni hiyo Kaimu
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Pilika Kasanda alisema zoezi hilo litakalo dumu
kwa muda wa siku tano la kuwamisha na
kuharibu makazi ya wavamizi hao ili kulinga
hifadhi hiyo isiendelee kuharibiwa.
“Zoezi hili limeanza leo na litadumu kwa siku tano katika
kukagua na kuwaondosha kwa nguvu wavamizi wote wafugaji walioko ndani ya
hifadhii kwani wameanza uharibu wa vyanzo vya maji ambavyo ndio tegemeo pekee
la wilaya hii”alisema Kasanda.
Alisema wafugaji ho
wamekuwa wakivamia msitu huo mara kwa mara licha ya juhudi mbalimbali
walizozichukuwa za kuwapa elimu kuhusu umuhimu wa hifadhi hiyo na kuwataka
warudi katika makazi yao ya awali lakini imeshindikana.
Hata hivyo Meneja hifadhi msitu huo John Mkenda alisema
kabla ya zoezi hilo walianza kutoa elimu kwa jamii inayozunguka hifadhi kuhusu umuhimu wa
hifadhi hiyo na madhara ya uharibufu unaofanyika ili kuhakikisha wanalinda
hifadhi na viumbe vilivyoko.
“Tulianza kutembelea vijiji vinavyozunguka hifadhi ili kutoa
elimu ya mazingira kisha tukawatembelea na wavamizi ambao ni jamii ya wamasai na
kuwashauri watoke kwa amani kabla ya hatua za kisheria kuanza kufuatwa ,tunashukuru
walitii ili wengine walikaidi”alisema Mkenda.
Aliongeza kuwa nyumba nne hawakuzichoma moto kutoka na
kutowakuwa wazazi bali wapo watoto pekee lakini nao wamewapa siku mbili
kuondoka kwa hiari kabla ya kuanza kuchoma moto nyumba hizo pamoja na vitu
vyao.
MWISHO
Mkutano mkuu Coastal Union kufanyika kesho.
Na Oscar Assenga, Tanga.
MKUTANO Mkuu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga unatarajiwa
kufanyika kesho katika makao makuu yake yaliyopo katika barabara ya kumi
na moja jijini Tanga ambapo agenda mbalimbali zitazungumzwa.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Hemed Aurora “Mpiganaji”aliliwaambia waandishi wa habari kuwa agenda kuu itakuwa ni kuwajulisha wanachama wao mafanikio
yaliyopatikana katika msimu wa ligi kuu uliomalizika na malengo yao katika
msimu ujao.
Aurora alisema suala lengine ambalo litazungumza katika
mkutano huo ni Katibu Mkuu wao, Kassim El Siagi kusoma taarifa ya mapato na
matumizi kwa wanachama wao ambao watahudhuria lengo likiwa ni kuwapa ufahamu
kuhusu mambo hayo.
Aliongeza kuwa agenda nyengine ni kuzungumzia maendeleo ya
wachezaji wao pamoja na kuweka mikakati ya ya msimu mpya wa ligi katika mwaka
2013-2014 ambapo lengo lao ni kushiriki ligi hiyo kwa mafanikio makubwa zaidi
ya ligi iliyopita.
Mwenyekiti huyo alisema wachezaji waliosajiliwa na klabu hiyo
wanatarajiwa kuwasili mkoani hapa kuanzia leo na mpaka Julai 3 mwaka huu
wachezaji wote waliosajiliwa watakuwa wamekwisha kuwasili kwa ajili ya
maandalizi ya msimu mpya.
Akizungumzia usajili wao msimu huu, Aurora alisema
walichokifanya ni kuziba mapungufu yaliyijitokeza katika mzunguko wa pili wa
ligi ili kuweza kukiimarisha lengo likiwa kuleta upinzani na mafanikio msimu
ujao.
Mwisho.
WIZARA ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo yapewa changamoto.
Na Oscar Assenga, Tanga.
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imeshauriwa
kuweka utaratibu wa kukaa na makocha wa kigeni wanaofundisha timu za Taifa muda
mrefu ili kuweza kupata mafanikio badala ya kuwabadilisha kila wakati kitendo
ambacho kinadumaza soka badala ya kupiga hatua kwenda mbele.
Ushauri huo ulitolewa na Golikipa wa zamani wa timu ya Coastal Union ya
Tanga, Nyendi Mpangala wakati akizungumza na mwandishi wa blog hii hivi karibuni ambapo alisema kitendo cha ubadilishwaji wa makocha hao
kunawafanya hata wachezaji wenyewe kutokuelewa kile wanachofundishwa kutokana
na kila kocha mpya anakuwa na mbinu zake.
Nyendi aliwahi kuichezea Costal Union ya Tanga kati ya mwaka 2000-2003
alipoamua kuacha kujishughulisha na mambo ya soka hapa nchini na kueleza mpira
wa sasa hivi ni tofauti na zamani kutokana na enzi hizo wachezaji wengi
walikuwa na vipaji vyao binafsi kuliko ilivyokuwa wakati huu .
Alisema ili soka letu hapa nchini liweze kupiga hatua ni lazima serikali
ihakikishe wanahamasisha wadau kuanzisha vituo vya mafunzo ya soka (Academy)
ambazo zitakuwa imara kwa ajili ya maendeleo ya soka hapa nchini ikiwemo
kuvilinda vipaji hivyo pamoja na kulinda viwanja vya michezo vilivyopo maeneno
mbalimbali na kuwapa fuksa wachezaji kucheza.
Akizungumzia nafasi ya mlinda mlango alisema ni ngumu lakini ni rahisi
endapo wachezaji wenyewe wataipenda kutokana na kuwa nafasi ambayo mara moja
unaweza kupata nafasi ya kwenda kucheza kwenye timu nyengine ikiwemo timu ya
Taifa kwa sababu ni mahali ambapo mtu anaonekana.
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)