WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI, GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO

September 02, 2017
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mifuko ya Jamii ya PPF na NSSF limeingia ubia katika mradi huo wa uchumi wa viwanda chini ya Kampuni ya MKULAZI.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) akiangalia mbegu za miwa kabla ya kuzipanda katika eneo la Shamba la miwa alipowasili Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.
Shamba la miwa katika mradi wa Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa - MKULAZI katika eneo la Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro likiwa limestawi kama inavyoonekana katika picha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba fupi kwa  Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Morogoro, Watendaji wa Kampuni ya MKULAZI pamoja na Wananchi wanaoishi jirani na Gereza Mbigiri katika ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro Septemba 2, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim(hayupo pichani) namna Jeshi hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa ufufuaji wa Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani Morogoro unakamilika kama ilivyopangwa ambapo matarijio ni kuwa Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka.

SERIKALI KUBORESHA VITUO VYA MALIKALE KUKUZA UTALII WA NDANI NCHINI

September 02, 2017


 Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng Ramo  Makani akisisitiza jambo kwa wabunge wa kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na utalii mara baada ya kuwasili katika mapango ya Amboni Jijini Tanga 



 Wajumbe wa kamati hiyo waakiwa tayari kuingia kwenye mapango hayo
  Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Guide wa Mapango hayo,Athumani Mangula kuingia kwenye mapango hayo
 Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Atashasta Nditiye kulia akiwa na mjumbe wa kamati hiyo,Marry Chatanda ndani ya mapango ya Amboni
 Wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa na wakiangalia maeneo mbalimbali ya utalii kwenye mapango hayo
Wajumbe wakionyeshwa baadhi ya maeneo kwenye mapango hayo
 Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa ndani ya Mapango ya Amboni Jijini Tanga
Muuongoza watalii kwenye Mapango ya Amboni ( Guide) wa Mapango hayo,Athumani Mangula kushoto akimsikiliza kwa umakini mjumbe wa kamati hiyo,Nape Nnauye


 Muuongoza watalii kwenye Mapango ya Amboni ( Guide) wa Mapango hayo,Athumani Mangula akiwaonyesha wajumbe baadhi ya maeneo ndani ya mapango hayo
 Muuongoza watalii kwenye Mapango ya Amboni ( Guide) wa Mapango hayo,Athumani Mangula akisisitiza jambo kwa wajumbe hao
 Wajumbe wa kamati hiyo wakiingia kwenye mapango ya Amboni
Meneja Mawasiliano wa Tanapa ,Pascal Shelutete kushoto akimsikiliza kwa umakini moja kati ya wajumbe wa kamati hiyo wakati wakiwa kwenye mapango ya Amboni
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani amesema serikali ina mpango wa kuboresha vituo vya malikale vilivyopo nchini kwa lengo la kukuza utalii wa ndani ili kuweza kuchangia uchumi.

Aidha pia alieleza mkakati wa kuwapatia njia mbadala wananchi wanaoendesha shughuli za kibinaadamu pembezoni mwa mto zigi eneo la hifadhi ya mapango ya Amboni Jijini hapa ili kunusuru mazingira.

Mhandisi Makani alisema kuwa mpango wa serikali ni kuinua utalii wa ndani pamoja na kutoa kipaumbele katika kuboresha miundombinu kwenye vivutio vya ndani kama hatua ya kuvitangaza.

Akizungumza  na waandishi wa habari eneo la mapango ya Amboni wakati akiwa kwenye ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea hifadhi hiyo ya asili iliyopo nje kidogo mwa Jiji la Tanga.

Mhandisi Makani alizieleza changamoto zilizojitokeza kwenye ziara hiyo kuwa pamoja na uduni wa miundombinu ya barabara, ofisi ya taarifa, kutokuwepo kwa vivutio na huduma muhimu lakini pia shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika eneo hilo zimeonekana kuwa tishio kwenye hifadhi hiyo.

Hata hivyo alisema kuwa serikali ya wilaya na Mkoa kwa upande wake zitalazimika kuchukua hatua ikiwemo kutafuta njia mbadala zitakazofanywa na wananchi hao ili kuacha uharibifu huo huku Wizara yake ikiangalia namna ya kushughulikia changamoto nyingine.

Miongoni mwa shughuli zinazo elezwa  kufanywa na wananchi kwenye maeneo hayo ni ugongaji kokoto na kilimo kazi zilizodaiwa kusababisha mmomonyoko wa ardhi nyakati za mvua na kutishia uwepo wa mapango hayo.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo, Injinia Atashasta Nditiye alisema kamati hiyo itaishawishi serikali kuwa na mpango wa kuwaendeleza watumishi wa Idara hiyo ili kuwapa utaalamu wa kutosha na hivyo kuleta ufanisi zaidi.

Nditiye alisema kuwa kamati yake pia itahakikisha kuwa vivutio vyote vya asili vinatangazwa na kwamba itawashawishi viongozi wakuu wa nchi kuvitembelea vivutio hivyo na kujionea changamoto zilizopo ili kurahisisha utatuzi wake.

Naye Mkurugenzi msaidizi wa Mambo ya Kale, Digna Tillya alieleza kuwa kituo cha Amboni ambacho kinasimamiwa na Mambo ya Kale kilianzishwa mwaka 1937  na wakoloni waingereza na kwamba vivutio vingine  kwa Mkoa wa Tanga  vilivyoibuliwa  karne ya 16 ni mji mkongwe
Tongoni.

Tillya alieleza changamoto wanazokabiliana nazo sambamba na shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo kuwa  ni uchakavu wa miundombinu ya barabara na kukosekana kwa ofisi kwa ajili ya kutolea taarifa za kituo.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII,BI.SIHABA NKINGA AFUNGUA MKUTANO WA REPSSI JIJINI ARUSHA

September 02, 2017


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi Sihaba Nkinga akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa watoto ulioandaliwa na taasisi ya REPSSI yenye makao yake nchini Afrika Kusini kutoka mataifa zaidi ya 30 barani Afrika unaofanyika jijini Arusha,mkutano huo pamoja na mambo mengine unalenga kuwawezesha  watoto sauti zao kusikika na kuwajenga kisaikolojia.

Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya REPSSI,Noreen Huni ambaye ni raia wa Zimbabwe akizungumza katika mkutano huo wa kimataifa jijini Arusha leo.

Watoto kutoka mataifa mbalimbali wakifatilia mada kwenye mkutano huo.

Watoto kutoka mataifa mbalimbali wakiwa kwenye mkutano  ambao unawapa fursa ya kuwasilisha taarifa za matukio ambayo ni changamoto kwao.

Watoto wakiwa kwenye mkutano ambao unawapa fursa ya kuwasilisha taarifa za matukio ambayo ni changamoto kwa mamlaka husika na kutafutiwa ufumbuzi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi Sihaba Nkinga(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa baraza la watoto nchini,Joel Festo(kushoto) na Mwenyekiti wa baraza la watoto nchini Kenya,Brian Musyoka  katika mkutano wa kimataifa wa watoto ulioandaliwa na taasisi ya REPSSI yenye makao yake nchini Afrika Kusini .

Mmoja wa washiriki akifatilia kwa makini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto,Bi Sihaba Nkinga(katikati)akiagana na viongozi wa watoto mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Arusha.
MAADHIMISHO YA KIFO CHA MWANGOSI 2017, WANAHABARI WALILIA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.

MAADHIMISHO YA KIFO CHA MWANGOSI 2017, WANAHABARI WALILIA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.

September 02, 2017
Waandishi wa habari nchini Tanzania wameendelea kulaani mazingira magumu ya utendaji kazi wanayokumbana nayo ikiwemo kukabiliana na sheria zinazohatarisha uhuru wa habari kwa ujumla. 

Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakary Karsan ameyasema hayo hii leo Jijini Mwanza, kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya mwanahabari Daud Mwangosi, aliyeuawa na polisi mwaka 2012 akiwa kazini katika Kijiji cha Nyololo mkoani Iringa. 

Karsan amesema mbali na waandishi wa habari kukumbana na sheria hatarishi zinazominya uhuru wa habari, pia wanakabiliana na maslahi duni kutokana na serikali kuweka mazingira magumu ya biashara za matangazo kwenye vyombo vya habari wanavyofanyia kazi. 

 Amesema ni wakati mwafaka sasa waandishi wa habari pamoja na wananchi kwa ujumla kupaza sauti zao kudai mazingira huru kwa wanahabari, akisema serikali inayominya uhuru wa habari ni serikali inayowatesa wananchi wake. 

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mwanza (MPC), Osoro Nyawangah amewasihi waandishi wa habari kuiambia serikali kwa uwazi pale inapoenenda kinyume huku akiisihi serikali kuwaacha waandishi wa habari kufanya kazi kwa mjibu wa taratibu za uandishi, akitolea mfano onyo lililotolewa na serikali kwa baadhi ya magazeti baada ya kuripoti suala la bomoa bomoa Jijini Dar es salaam. Nashon Kenedy ambaye ni mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria maadhimisho hayo amewataka waandishi wenzake nchini kuungana pamoja kama zilivyo taasisi nyingine ili kutetea haki na maslahi yao jambo ambalo litasaidia kuondokana na sheria zinazolalamikiwa kwamba ni kandamizi huku akiwaonya wale wasiotambua umuhimu wa wanahabari kuacha kununua magazeti, kusikiliza redio na kutazama luninga kwani vyombo hivyo ni matokeo ya uwepo wa wanahabari.

 Enzi za uhai wake, Daudi Mwangosi alikuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten na pia Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Iringa ambapo aliuawa na polisi Septemba 02,2012 akiwa kazini katika Kijiji cha Nyololo mkoani Iringa akiripoti habari za mkutano wa kisiasa. 

Julai mwaka jana askari huyo mwenye nambari G.2573 Pacificius Cleophace Simon akiwa na miaka 27, alihukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kutumikia kifungo cha miaka 15 gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Tazama video na picha hapo chini
[embed]https://youtu.be/Cjm9BP0YIS8[/embed] Pia Mkurugenzi wa UTPC, Abubakary Karsan amesema Tuzo ya Daudi Mwangosi itatolewa Septemba 17 mwaka huu kwenye Mkutano Mkuu wa UTPC utakaofanyika mkoani Tanga. Mara ya kwanza mwaka 2013 tuzo hiyo ilichukuliwa na Absalom Kibanda ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 ambapo tangu mwaka huo tuzo hiyo haijawahi kutolewa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa mshindi wake. Baadhi ya sifa za mshindi wa tuzo hiyo ni Mwandishi awe amepigwa, kuumizwa ama kuuawa akiwa kazini ambapo vigezo hivyo vimekuwa changamoto kwa miaka kadhaa katika kumpata mshindi wa tuzo ya Daudi Mwangosi. Mwenyekiti wa MPC, Osoro Nyawangah akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mwanahabari Pius Rugonzibwa akitoa maoni yake kwenye maadhimisho hayo
Mmoja wa wageni washiriki akichangia maoni yake kwenye maadhimisho hayo Baadhi ya wahudhuriaji wa maadhimisho hayo. Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima kutazama maadhimisho yaliyopita.

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WASALI KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO LA MAGOMENI JIJI DAR ES SALAAM

September 02, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amepiga magoti pamoja na  mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakiombewa sala  na Maaskofu wa Kanisa hilo la Waadventista Wasabato, Sala iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Marc Walwa Malekana(wa kwanza kushoto)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakikabidhi mifuko 400 ya Saruji itakayotumika katika ujenzi wa Kanisa hilo la Wasabato la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Navana Cable aliyeambatana na mtoto  wake Rebecca Cable ambao familia yao imeahidi kumalizia ujenzi wa Kanisa hilo la Waadventista la Wasabato mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kuendesha Harambee ya Papo kwa papo Kanisani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhariri Mtendaji waMagazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz mara baada ya kuahidi kuchangia katika kanisa hilo.

Waziri Mstaafu katika awamu iliyopita Steven Wasira naye akichangia katika Harambee hiyo Kanisani hapo.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Ndugu Dkt. Edward Hosea mara baada ya kuchangia katika ujenzi wa kanisa hilo la Wasabato lililopo Magomeni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshika mkono mtoto ambaye alikua anamsalimia wakati akitoka ibadani katika kanisa hilo la Magomeni.
Waumini mbalimbali wa Kanisa hilo wakiwa ibadani kama wanavyoonekana pichani. PICHA NA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amepiga magoti na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai katika Ibada ya Jumamosi kanisani hapo  jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na   mkewe Mama Janeth Magufuli wakiimba nyimbo katika ibada hiyo ya Jumamosi katika Kanisa la Waadventista Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na   mkewe Mama Janeth Magufuli wakisikiliza neno katika Ibada hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisoma neno pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli kanisani hapo wakati wa Ibada ya jumamosi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista la Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai  kabla ya kuendesha Harambee ya Ujenzi wa kanisa hilo ambapo zaidi ya Sh. 25milioni ziliahidiwa kukusanywa.

SHAKA AZUNGUMZIA MAENDELEO YA UCHAGUZI WA NDANI WA UVCCM

September 02, 2017

Ndugu Waandishi wa habari;
Kwa mara nyingine tena tunawakaribisha kwa mikono miwili katika mkutano huu muhimu. Karibuni sana huku nikiwaomba  mjione mko huru na mko nyumbani .

Dhana ya Demokrasia ni jambo muhimu linalohitaji kuheshimiwa na kuenziwa ndani ya Chama na  Jumuiya zake. Kiongozi wa UVCCM mahali popote pale huchaguliwa kwa kufanyika uchaguzi huru na wa  haki unaozingatia Kanuni na Taratibu za Uchaguzi kama zilivyoagizwa na vikao husika bila ya kukiuka, kupuuzwa au kuvunjwa.

Nia ya UVCCM ni kujenga na kudumisha haiba  njema ya kuendelea kuheshimu misingi ya demorasia ya kweli , yenye kuchunga  adabu na kufuata nidhamu, miiko na maadili kwa kila mwanachama anayetaka kutumia haki ya kuchagua au kuchaguliwa.

April Mwaka 2017 Chama Cha Mapinduzi kilianza mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama na Jumuiya zake. Kufuatia mabadiliko ya Kanuni ya UVCCM yaliyofanyika mwezi Machi, 2017 tulianza Uchaguzi katika ngazi za Matawi ambapo hadi leo jumla ya Matawi 23,529  sawa na Asilimia 99.4% kati ya Matawi  23,670 sawa na Asilimia 0.59% yamekamilisha uchaguzi.

Ngazi za   Kata  3,913 sawa na Asilimia 96.59% kati ya Kata 4,051 sawa na asilimia 3.4% zimekamilisha uchaguzi .Kwa upande wa majimbo ya  Zanzibar majimbo 54 sawa na Asilimia 100%, wamekamilisha uchaguzi.  

Ngazi ya Wilaya na Mkoa  mchakato wa uchujaji wa  majina kwa Vijana waliomba nafasi mbali mbali ndani ya Jumuiya yetu , umeanza na  unaendelea vizuri huku jumla ya Vijana 7,606 wamejitokeza kuchuka fomu za kugombea nafasi mbali mbali katka Jumuiya yetu, hali inayoonyesha kumekupo kwa mabadiliko  na msisimko wa kisiasa ukilinganisha na chaguzi zilizopita.

Kwa upande wa ngazi ya Taifa Vijana 350 wamejitokeza kuomba nafasi za uongozi ndani ya UVCCM kama ifuatavyo:-

(i)
Nafasi ya Mwenyekiti
113
Walioomba
(ii)
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa
24
Walioomba
(iii)
Nafasi 5 za Wajumbe wa H/Kuu
103
Walioomba
(iv)
Nafasi  5 za Wajumbe wa B/Kuu Taifa
81
Walioomba
(v)
Nafasi 1 Wawakilishi UWT
14
Walioomba
(vi)
Nafasi 1 Wawakilishi Wazazi
15
Walioomba

Maandalizi kwa ajili ya Mikutano Mikuu ya Wilaya hadi Taifa yanaendelea vyema ambapo chaguzi zote ndani ya UVCCM zinategemewa kukamilika Novemba 2017.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunaendelea kusisitiza kuwa sifa na wasifu wa kila mgombea aliyeomba kuteuliwa kwa kadri alivyojaza kwenye fomu yake, utaandaliwa na kuandikwa vizuri katika kitabu maalum cha wagombea wote ambacho watapatiwa wajumbe wa Mkutano siku ya uchaguzi husika.
Kila mgombea atapata nafasi ya kujieleza na kutoa wasifu wake, kutaja dhamira na malengo yake mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu husika baada ya taratibu za vikao vya uteuzi kukamilika si kinyume na hivyo.

Tunaendelea kuwakumbusha kuwa ni mwiko kwa mgombea kuanza kampeni mapema  au wapambe wake kufanya ushabiki wa kisiasa kumnadi, kumpigia debe, au kujipitisha na kuelezea nafasi anayogombea. Ukiukaji huo wa Kanuni na taratibu utampotezea sifa za kuteuliwa.