Nchi yetu. Nyumba zetu. Mustakabali wetu.
Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo - hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa.
Mchango wa mabadiliko ya mazingira katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote.
Idadi kubwa ya 'wakimbizi wa mazingira' sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa.
Na hili hii inategemewa kundelea kuongezeka.
Kufikia 2030, Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa imeonya kuwa, kufikia mwaka 2030 watu wapatao milioni 135 wako katika hatari ya kuhama makazi yao kwa sababu ya kuenea kwa jangwa, na watu milioni 60 wanatarajiwa kuhama kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Afrika ya Kaskazini na Ulaya.
Utabiri huu unaonyesha kuwa sehemu zilizo kame na zile zilizo kame zaidi huathirika zaidi na kuenea kwa jangwa na kuhama kwa watu.