TOSAMAGANGA ALUMNI ASSOCIATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA ZAIDI YA SH MILION MOJA LAKI SITA KATIKA HOSPITALI YA TOSAMAGANGA

October 16, 2017
 Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwa wanajadili kitu walipokuwa kwenye ziara ya kuitembelea shule waliyosoma
 Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Tosamaganga mkoani Iringa
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwa katika hospital ya Tosamaganga.

 Na Fredy Mgunda,Iringa

Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wametoa msaada wa mashuka sabini na tano na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 1,672,500 katika hospitali ya Tosamaganga iliyopo katika katta ya kalenga mkoani Iringa kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya afya ikizingatiwa kuwa wengi wao waliwahi kutibiwa hapo wakati wanasoma.

akizungumza wakati wa hafla ya kukadhi msaada huo mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi alisema kuwa walijipanga kuja kutoa msaada huu kwa kuwa wangi wao walikuwa wanatibiwa katika hospital hiyo wakati wakiwa masomoni miaka mingi iliyopita.

“Leo hii tunaafya njema kwa ajili tulitibiwa vizuri kipindi tulivyokuwa tunaumwa na ilitusaidia kufanya vizuri masomo yetu na ndio maana leo hii tupo hapa bila kupata huduma iliyobora nafikiri wengi wetu tusinge kuwa hapa” alisema Mbilinyi

Mbilinyi alisema kuwa wamechangisha kidogo walichopata wameamua kununua vifaa hivyo ambavyo wanafikiri vitakuwa na msaada kwa wagonjwa waliopo hospitalini hapo.
“Hiki kidogo tu lakini tunajua kwa namna moja au nyingine vinaweza kuwasaidia wagonjwa na kuwapunguzia mzigo uongozi wa hospitali yetu pendwa ambayo imekuwa ikitutibu kwa muda mrefu sana kipindi tukiwa masomoni katika sekondari ya Tosamaganga” alisema Mbilinyi

Dr Steven Biginagwa ni daktari bingwa wa magonjwa ya watoto na mtafiti wa ugonjwa wa malaria alisema kuwa hospital hiyo iliokoa maisha yake kwa kupata huduma bora kwani alikuwa na ugonjwa wa utumbo kujifunga  lakini madaktari waliokoa maisha yangu hadi hii leo.

“Mimi nililazwa hapa mwezi wa kwaza na mwezi wa pili wa masomo nilipata matatizo ya huo ugonjwa lakini nashukuru mungu kuwawezesha wahudumu wote wa hii hospital kunitibu na kuokoa maisha yangu hadi leo nipo na afya yangu njema na mfanyakazi niliajiliwa hivyo bila kuwepo kwa hospital hii sijui leo hii ningekuwa wapi” alisema Dr Biginagwa

Dr Biginagwa alisema kuwa licha ya kumaliza masomo yake lakini mitihani mine ya mwisho alifanyia hodini akiwa amelazwa kutokana na ugonjwa aliokuwa nao na madaktari walimsaidia kupata huduma bora ndio maana alifanya vizuri mitihani kwenye mitihani na kufaulu vizuri.

“Kwa miaka yangu vyote miwili nimekuwa nikishinda sana hapa hospitalini lakini mungu alisaidia nikamaliza masomo yangu na nafikiri kutokana na hudumu nilikuwa napewa hapa ndio iliyonipelekea kwenda kusomea udaktari na ndio maana hadi leo hii mimi ni daktari bingwa wa magonjwa ya watoto” alisema Dr Biginagwa

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa TASAF Ladslausi Mwamanga aliwaomba wananchi popote walipo hapa nchi kukumbuka kutoa msaada waote katika hospital ili kuendelea kuboresha sekta ya afya kwa kuwa serikali bila wadau haiwezi kukamilisha kila kitu yenyewe.

“Unajua kuwa serikali inamambo mengi ambayo inayaofanya hivyo kukamilisha kila kitu kwa wakati ni vigumu sana hivyo sasa sisi wadau tuendelee kuisaidia serikali kwa kile tuchokipata kutoa msaada kwenye sekta hii ya afya ambayo inachangamoto nyingi sana” alisema Mwamanga

Naye diwani wa kata ya Kalenga Thobias Kangalawe aliwashukuru wanafunzi hao waliosoma shule ya Tosamaganga miaka iliyopita kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya Tosamaganga,alisema kuwa ni nadra sana kuona watu wanakumbuka walikopatia mafanikio na kutoa msaada kama wenu.

Nyinyi watu wa kipekee kabisa toka nimekuwa kiongozi siajwahi kuona kundi kubwa lenye kujali wapi walikotoa na kuendelea kutafuta njia mbdala za kusiadia kutatua changamoto kama nyinyi hivyo hongeni na namuomba mungu awaongezee pale mlipo punguza” alisema kangalawe

TMA yatoa semina kwa wanahabari juu utabiri mpya msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili 2018

TMA yatoa semina kwa wanahabari juu utabiri mpya msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili 2018

October 16, 2017
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kulia) akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa wanahabari juu utabiri mpya msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili 2018, wakati akifunga rasmi semina Sehemu ya wanahabari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)kwa wanahabari juu utabiri mpya msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili 2018, unaotarajiwa kutolewa na mamlaka hiyo Oktoba 17, 2017 jijini Dar es Salaam. Utabiri wa msimu wa mvua za Novemba mwaka huu hadi Aprili 2018, kwa maeneo ya kusini mwa Tanzania unatolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2017. 
Baadhi ya washiriki katika semina hiyo wakiwasilisha kazi za makundi kwenye semina hiyo iliyofanyika Ofisi za TMA jijini Da 
Baadhi ya washiriki katika semina hiyo wakiwasilisha kazi za makundi kwenye semina hiyo iliyofanyika Ofisi za TMA jijini Dar es Salaam. 
Mmoja wa washiriki katika semina hiyo akichangia mada. 
Meza kuu ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (wa kwanza kulia) ikifuatilia kwa makini uwasilishaji wa kazi za makundi katika semina hiyo iliyofanyika Ofisi za TMA jijini Dar es Salaam. 
Picha ya pamoja kwa washiriki katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)kwa wanahabari juu utabiri mpya msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili 2018, unaotarajiwa kutolewa na mamlaka hiyo Oktoba 17, 2017 jijini Dar es Salaam 
Picha ya pamoja kwa washiriki katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)kwa wanahabari juu utabiri mpya msimu wa mvua za Novemba hadi Aprili 2018, unaotarajiwa kutolewa na mamlaka hiyo Oktoba 17, 2017 jijini Dar es Salaam.

Mwanza watakiwa kuchangamkia fursa Maendeleo Bank

October 16, 2017
Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akizungumza hii leo Jijini Mwanza, nje ya ukumbi wa mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo nchini TCCIA pamoja na Best Dialogue (Mpango wa kuboresha mazingira ya biashara Tanzania).

Binagi Media Group
Wananchi mkoani Mwanza wametakiwa kuchangamkia fursa ya ununuaji wa hisa za Maendeleo Bank ambazo zimeanza kuuzwa tangu Septemba 18 hadi Novemba 03 mwaka huu.

Mkurugenzi wa benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba ametoa rai hiyo hii leo Jijini Mwanza kwenye mafunzo ya mjadala baina ya sekta ya umma na sekta binafsi yaliyoandaliwa na Chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA pamoja na pamoja na Best Dialogue (Mpango wa kuboresha mazingira ya biashara Tanzania).

Mwangalaba amesema hisa za benki hiyo zinauzwa kwa thamani ya shilingi 600 na kwamba kiwango cha chini ya ununuzi ni hisa 100 zenye thamani ya shilingi 60,000 hivyo wananchi wakiwemo wachangamkie fursa hiyo.

“Tunauza hisa katika soko la hisa na hisa hizi zinauzwa kwenye matawi yote ya benki ya CRDB ambapo tunaunga mkono juhudi za Rais wetu anayesema uchumi wa Tanzania umilikiwe na watanzania wenyewe na njia mojawapo ya kuwajumuisha watanzania wengi ni uuzaji wa hisa sokoni”. Amesisitiza Mwangalaba na kuongeza kwamba hisa hizo pia zinapatikana ofisi za TCCIA.

Naye Mshauri wa Hisa, Richard Manamba amesema ununuzi wa hisa una faida nyingi ikiwemo wanunuzi kupata gawio la faida ambalo benki hulipata na kwamba hisa hizo huongezeka thamani kulingana na nguvu ya soko.

Maendeleo Bank yenye mtaji wa shilingi bilioni 10 sokoni inaendelea kuongeza mtaji wake hadi kufikia shilingi bilioni 17 ambapo inatarajiwa kufungua matawi yake katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza.
Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akielezea umuhimu wa kununua hisa za benki hiyo hii leo Jijini Mwanza ambapo mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yanafanyika.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba wakati akielezea umuhimu wa kununua hisa za benki hiyo.
Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Elibariki Mmari akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Mkurugenzi wa "Maendeleo Bank", Ibrahim Mwangalaba (kulia), wakifutahia mada kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Mkurugenzi wa "Maendeleo Bank", Ibrahim Mwangalaba (kulia), wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye majadiliano ya makundi
Majadiliano yakiendelea
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye majadiliano ya makundi
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye majadiliano ya makundi
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo (wa tatu) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo (wa tatu) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.

TATIZO LA UMEME MTWARA NA LINDI KUPATIWA UFUMBUZI KATIKA KIPINJDI CHA SIKU 10: WAZIRI DKT.KALEMANI

October 16, 2017



Waziri wa Nishati Dkt. Medardi Kalemani, akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Mtawara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea kazi inayofanywa na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) kurekebisha mashine 8 kati ya tisa zilizoharibika. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, na kulia ni Kamu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.

 NA K-VIS BLOG/Mtwara
Serikali imewaomba wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuwa na subira, katika kipind hiki ambapo upatikanaji wa umeme kwenye mikoa hiyo umeathirika baada ya mashine 5 kati ya 9 za kufua umeme (turbines) kuharibika.

Hata hivyo Mafundui wa TANESCO wamekuwa katika juhudi kubwa za kuzifanyia matengenezo mashine hizo, zilizofungwa miaka 10 iliyopita.

"tayari tumeagiza vipuri kwa ajili ya kutengeneza mashine hizo ambazo kwa ujumla wake huzalisha Megawati 18 za umeme, ambazo zitawasili ndani ya siku 7 ili kuweza kuondoa tatizo la kuzimika umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara." Alisema Dkt. Kalemani.

Alisema, baada ya kwasili kwa vipuri hivyo, kazi ya kuzifanyia matengenezo itaendelea na amememuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, kuleta wataalamu wote wa TANESCO popote walipo nchini, wafika Mtwara na kuungana na wataalamu waliopo ili kazi ya kuzitengeneza mashine hizo iende kwa kasi.

Kati ya mshine 9 ni mashine nne tu zinazotoa Megawati 8 ndio zinafanya kazi, hali inayosababisha kuwepo kwa mgao wa umeme unaofikia hadi masaa 8 kwa siku.

 Dkt. Kalemani ambaye amewasili mkoani Mtwara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea juhudi za Mafundi wa TANESCO  za kurejesha upatikanaji wa umeme katika hali yake ya kawaida amesema vipuri hivyo vifungwe kwa muda wa siku tatu badala ya wiki 3na kwamba ndani ya siku 10 umeme utakuwa katika hali yake ya kawaida.

Mkoa wa Mtawara na Lindi unategemea mashine hizo zinazozalisha umeme unaotumia gesi asilia.
Ukiachilia mbali kuharibika kwa mashine hizo, miundombinu mingine ya umeme kwenye mikoa hiyo iko salama na katika ubora wa hali ya juu ambapo vituo vipya vya kupoza na kusambaza umeme wa 132kV hapo hapo mkoani Mtwara na kingine huko Mahumbika mkoani Lindi vinafanya kazi pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme (transmission lines), nao uko katika hali bora.

 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Evod Mmanda, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt,. Tito Mwinuka, wakitembelea kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara leo Oktoba 16, 2017.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medardi Kalemani, akizungumza baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme mkoani Mtawara leo Oktoba 16, 2017 ili kujionea kazi inayofanywa na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) kurekebisha mashine 8 kati ya tisa zilizoharibika
 Fundi wa TANESCO, akitengeneza moja ya mashine zilizoharibika kwenye kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara.
  Fundi wa TANESCO, akitengeneza moja ya mashine zilizoharibika kwenye kituo cha kufua umeme mkoani Mtwara.
 Fundi wa TANESCO, akichukua spana ili kuendelea na kazi.
 Hii ni moja kati ya mashine zizlizoharibika.