KUTANA NA 'TYRESE' WA TANZANIA AITWAYE BANYE

July 20, 2017


Elias Banyenza nduo jina alilopewa na wazazi wake, lakini unafahamika na wengi kwa jina la Banye. Anapenda kuimba na RnB ndio muziki ana unaoupenda zaidi. Banye alianza kuimba akiwa Sunday Schools na Talent Shows lakini alivutiwa zaidi na Mwanamziki Tyrese tangu alipomuona mara ya kwanza kwenye Tangazo la Coca-Cola la mwaka 1986 na kujaribu kumfuatisha jinsi alivyoimba kila mara lile Tangazo lilipopita. 
Watu wengi wakimuona kwa mara ya kwanza huwa wanahisi kama waliwahi kumuona sehemu nahisi hii ni kwasababu waliwahi kuomuona kwenye sehemu zifuatazo:- Mwaka 2014/2015 alikuwa miongoni mwa wawashiriki 6 (Damian Soul,Grace Matata,Eli Daddy, Rogers Lucas, Myra) waliowakilisha Tanzania kwenye shindano la kuimba la Maisha Superstar nchini Kenya, kipindi hicho cha Tv kilirushwa na Maisha Magic ambapo walienda kushindana na washiriki wengine 12 kutoka nchi tofauti tofauti za Africa Mashariki, walisimamiwa na Shaa, AY(Tanzania), Jose Chameleon, Maurice Kirya (Uganda),Nameless, King Kaka(Kenya) na Music Director alikuwa Eric Wanaina. 
Mwaka 2015/2016, alikuwa kati ya washiriki 5 (Nandy, Jeff, Kechu na Zouccu) waliochagulia kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano makubwa zaidi ya Karaoke kuwahi kutokea Africa, Tecno Own The Stage Lagos nchini Nigeria, kipindi hicho kilirushwa na Africa Magic Showcase ambapo pia alishindana na waimbaji wengine 14 kutoka sehemu mbalimbali za bara la Afrika. Kwenye shindano hili walikuwa chini ya usimamizi wa Yemi Alade, MI, ID Cabasa (Nigeria), Bien Soul/Saut Sol, Anto Neosoul(Kenya) and AY (Tanzania) 
Ndoto yake kubwa alitamani atoke kimuziki kupitia Mashindano ya kuimba, lakini hakuweza kufanya vizuri huko kwa sababu alikuwa anafanya multitasking…ikiwemo Shule,Kazi na Muziki kwa wakati mmoja hivyo kumpelekea kufanya maandalizi ya zima moto.
Ukiachana na Muziki Banye amesoma Masters of Business Administration in Marketing na Bachelor in Mass Communication na kaspecilize kwenye Public Relations and Marketing. Na sasa kaamua kuingia studio na wimbo wake wa kwanza ni huo Brown Colour.

SHAKA ATAKA VIJANA KUJIUNGA NA UJASILIAMALI

July 20, 2017





Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Umoja wa Viijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM ) umesema vijana wanaoendelea  kulalamika bila kufanya kazi, kujituma na kutoa jasho la uchapakazi watakawia sana kufikia malengo chanya na kujikwamua hatimaye  maisha.

Hayo yameelezwa jana kaimu katibu mkuu shaka Hamdu Shaka alipotembelea kikundi cha ujasiriamali katika kata ya Mwandiga wilaya ya Kigoma vijijini Mkoani hapa .

Shaka alisema hakuna njia mbadala na ya mkato ya kujikwamua kimaisha na hali ngumu yoyote ya umasikini bila kijana mwenyewe kuamua kujishughulisha na kuzalisha mali hatimaye kujitegemea.

Aliwasifu wana kikundi hicho kwa kujikusanya, kupanga mipango na mikakati ya  mradi wa kufyatua matofali, kuzalisha sabuni na kuwa na kikundi cha Vicoba kwa mtimdo wa kuweka na kukopa pia kununu hisa.

"Vijana wengi huwa wanawaza, wanapanga na kutaka kutenda  hawatendi, kikundi hiki ni makini na kimeamua kuonyesha kwa vitendo jinsi kilivyopania kujikwamua na umasikini wa vipato hatimaye kujijenga kiuchumi "Alisema Shaka .

Shaka aliwahimiza watendaji wa halmashauri ya Kigoma vijijini kuona haja ya kukipa umuhimu kikundi hicho kwa kuwapatia wataalam, mitaji na vyanzo vya fedha.

"Vijana mnakawia, jiungeni ili kushiriki katika shughuli za ujasiriamli kwa lengo la kuacha utegemezi badala yake mjiajiri na kujitegemea kiuchumi kama kikundi cha "Alisema

TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF)

July 20, 2017
TAARIFA YA KAMATI YA UCHAGUZI TAFCA

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA), Ramadhani Mambosasa ametangaza majina manane ya wagombea waliopitishwa katika usaili katika mchakato uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 10, mwaka huu mjini Dodoma.

Waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi - ngazi ya taifa ni pamoja na Kidao Wilfred, Lisiter Manyara, Michael Bundala, Dismas Haonga, Jamhuri Kihwelo, George Komba, Samuel Moja na Mwalwasi.

Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

WAGANDA KUWACHEZESHA RWANDA, TANZANIA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limewateua waamuzi wa Uganda kuchezesha mchezo wa marudiano kati ya Amavubi ya Rwanda na Taifa Stars ya Tanzania. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Nyamirambo, Jumamosi saa 10.00 jioni kwa saa za Rwanda sawa na saa 9.00 alasiri kwa saa za Tanzania, utachezeshwa na Brian Nsubuga Miiro ambaye atakuwa na jukumu la kupiliza kipenga.

Waamuzi wasaidizi watakuwa Ronald Katenya (Line 1) na Dick Okello (Line 2) wakati Mwamuzi wa akiba atakuwa Chelanget Ali Sabila huku Kamishna wa mchezo atakuwa Ali Mohamed Ahmed kutoka Somalia.

Mchezo huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN). Timu hiyo kwa mwaka huu imecheza mechi 10 za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare minne na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa.
MH RAIS WA JAMUHURI YA BURUNDI AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI NA KUPOKELEWA NA MWENYEJI WAKE MH RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI – NGARA MKOANI KAGERA JULAI 20,2017

MH RAIS WA JAMUHURI YA BURUNDI AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI NA KUPOKELEWA NA MWENYEJI WAKE MH RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI – NGARA MKOANI KAGERA JULAI 20,2017

July 20, 2017
Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza Akihutubia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 julai 2017
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Rais wa Burundi kuwahutubia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyikakatika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 julai 2017
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017
Umati wa ananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini Ngara kusikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa posta mjini Ngara julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwapungia wananchi alipowasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017
Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akikagua graride la lililoandaliwa na jeshi la ulinzi la Tanzania JWTZ katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Kumpokea katika Uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye uwanja wa Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA MUWEKEZAJI WA MKONGE MKOANI TANGA.

WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA MUWEKEZAJI WA MKONGE MKOANI TANGA.

July 20, 2017

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa kata ya Mnazi wilaya ya Lushoto mkoni Tanga waliozuia msafara wake na kumpa malalamiko kuhusu mashamba matatu yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua mashamba ya katani yanayomilikiwa na kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited yaliyopo kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua miundombinu na mazingira ya kazi ya mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997. 
Mazingira ya shamba yaliyotelekezwa na mmiliki wake wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini Bwana Leo Komba kuhusu hatua zilizochukuliwa na ofisi yake hadi sasa kwa mmiliki ambae ameshindwa kuwa na sifa za umiliki na hajalipa kodi ya ardhi tangu mwaka 2004 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga kuhusu shamba hilo linalostahili kufutwa kama ilivyopendekezwa na ofisi ya Mkoa wa Tanga na ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini kwa kuwa mmiliki. 
Baadhi ya mitambo iliyochakaa ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937. 
Baadhi ya mitambo iliyochakaa ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA MKOA WA SONGWE

July 20, 2017

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kulia ni mkewe Mary.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songwe, Elias Nawela  baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. 
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimia wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  (kulia) alipozungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini  kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha  Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 20117. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini wa mkoa wa Songwe kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 2017. Kushoto ni Mkewe Mary na Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.

Baadhi ya watumishi wa umma na viongozi wa dini wa mkoa wa Songwe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipowahutubia kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MBUNGE JUMAA HAMIDU AWESSO AFANIKISHA NDOTO ZA VIJANA PANGANI

July 20, 2017
 Mbunge wa Pangani Jumaa Hamidu Awesso aliyevaa shati la bluu akiwa na baadhi ya viongozi wa simba mapema leo wakati alipowatembelea vijana wake wanaofanyiwa majaribio na klabu hiyo
 Kijana Abdallah Hamisi Abeid  maarufu kam Jr kutokea Pangani aliyechaguliwa kujiunga na klabu ya Simba B
Kijana Abdallah Hamisi Abeid akiwa na wenzake waliofanyiwa majaribio na Simba B 

 Na Mohammed Hammie

Mbunge wa jimbo la Pangani Jumaa Hamidu Awesso hatimae amefanikisha ndoto za kijana Abdallah Hamisi Abeid  maarufu kama Jr kutokea Pangani Mjini kwa kuchaguliwa kuchezea klabu ya Simba B baada ya kupenya katika mchujo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mheshimiwa Awesso amesema kuwa, kufanikiwa kwa kijana huyo ndio mwanzo wa kuibua vijana wengine wenye vipaji vya soka katika jimbo lake la Pangani.

Awali mbunge huyo kijana aliandaa vijana wanne kwa ajili kuwapeleka kwenye klabu hiyo kongwe kwa ajili ya kufanyiwa majaribio, kwa lengo la kufanikisha ndoto zao za kuchezea klabu kubwa hapa nchini.

"Nilichukua vijana wanne na kuwaleta hapa Dar es salaam kwenye klabu ya Simba ambao ni Abdallah Hamisi aliyepata nafasi, wengine ni Bakari Mohammed, Gasper Anthony na Sueli Salum ambao kwa sasa naendelea kuwafanyia mpango wa kufanya majaribio kwenye klabu nyengine" amesema Mheshimiwa Awesso.

Kijana Abdallah Hamisi au Jr ambaye wengi humfananisha na Mbwana Samatta, anatokea katika klabu ya Blackburn ya Pangani Mjini ambayo imekuwa na mashabiki wengi kutokana na kujaa vijana wengi wenye vipaji vya kusukuma kabumbu.

"Kabla sijajiunga na Black Burn nilitokea klabu nyengine ya Pangani United, kwa hiyo sina uzoefu mkubwa sana lakini nina uwezo wa kipekee na ndio maana nimechaguliwa kujiunga na Simba B" anasema Jr.

"Pia namshukuru sana Mbunge wangu Jumaa Awesso kwa jitihada zake za kutukusanya sisi vijana wenye vipaji na kuhakikisha tunafikia ndoto zake, kwa kweli ni mbunge pekee ambaye anaonyesha mapenzi ya dhati kwa wananchi wake, sio tu katika soka hata katika mambo mengine ya kimaendeleo" amesema Jr.

Jr amewataka pia vijana wengine wilayani Pangani na Tanzania kwa ujumla kuwa na uthubutu na kujiamini pindi wanapopatiwa fursa ya kuonyesha vipaji vyao mahala ambapo pana uwezekano wa kutoka kimaisha.

Pia amewataka vijana wenzake ambao hawakupata nafasi hiyo, kutokata tamaa na badala yake waendelee kufanya majaribio kwenye vilabu vyengine vikubwa hapa nchini.

Mbunge Jumaa Awesso ameahidi kuendelea kuibua vijana wengine wenye vipaji kutokea Pangani pasipo kujali itikadi, ili vijana hao wawe chachu ya kuitangaza wilaya hiyo na kuiletea heshima hata ikibidi katika anga za kimataifa.
Mohammed Hammie Rajab
PR Manager/Radio Editor
Uzikwasa/Pangani Fm Radio
P.o Box 1, Pangani
E-mail: ankomo25@yahoo.com
Phone: +255678900424
              +255719000010  

NAIBU WAZIRI MPINA AFANYA ZIARA USIKUKUBAINI UHARIBIFU WA MAZINGIRA UTOKANAO NA UCHIMBAJI WA MCHANGA.

July 20, 2017


Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiwa na mchanga mkononi akiwasikiliza maafisa wataalam katikati Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye pia ni katibu wake Bw. Daniel Sagata, na kulia ni Afisa kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenge akieleza kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi kati kati ya mto Mpigi katika eneo la Mpaka wa Bagamoyo na Dar es Salaam, ambapo uharibifu huo Umeharibu eneo ambapo limepita Bomba kubwa la maji safi (halipo pichani) linalo safirisha maji kutoka Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini na kuhudunia seheu ya mkoa mkoa wa Pwani na Jiji la Dar es Salaam, Bomba ambalo lipo hatarini kuharibika.

Afisa Mtaalam kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenje (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri Mpina Sehemu ya mto Mpigi ( haipo Pichani, iliyoharibiwa vibaya kutokana na shughuli za uchimbaji wa mchanga. (Picha na Evelyn Mkokoi)



NA; EVELYN MKOKOI
Katika hali isiyoya kawaida, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amefanya ziara ya Oparesheni maalum kwa kushirikiana na jeshi la Police kitengo cha FFU ili kuweza kubaini uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa uchimbani na uchotaji wa mchanga katika vyanzo vya maji na maeneo mengine.
Akiwa katikati ya Mto Mpigi uliopo katika mpaka wa Dar es salaam na Bagamoyo usiku wa kuamkia leo, naibu Waziri Mpina alisema kuwa watu wanaochimba na kuchota mchanga kiholelea watachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria, kutaifishwa kwa magari yao na hata kufikishwa mahakamani.
“kama mnavyoona hapa na kama tulivyosikia kutoka kwa mtu wa DAWASA haya mabomba ya maji yanayopita katika mito yanaharibika kutokana na shughuli hizi na serikali inaweza kuingia gharama kubwa sana kurekebisha mabomba haya kama bomba hili Mtaalam amesema hapa itagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80 kutengeneza bomba hili.” Alisema Mpina.

TANZANIA YA UCHUMI WA VIWANDA ITAFANIKIWA KWA KUFUATA KILIMO CHA KITAFITI NA TAFITI

July 20, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Geofrey Ngupula akizungumza na maofisa ugani na waandishi wa habari wilayani humo leo,  wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya maofisa ugani yalioandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknojia (OFAB),  yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi lishe katika kuelekea serikali ya viwanda. Kulia ni Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) wa wilaya hiyo, Arafa Njechele na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Kiwele Michael.

SHAKA APONGEZA WAGANGA NA WAUGUZI

July 20, 2017
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema serikali ya awamu ya tano itaendelea kuwajali na kuwahudumia wagonjwa kwa kupeleka idadi ya waganga, wauguzi, dawa na utoaji wa vifaa tiba katika zahanati vituo vya afya na hospitali za wilaya nchini .

Pia Serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha katika kila Kata na Wilaya kunajengwa zahanati na vituo vya afya ili kunusuru pia kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano .

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipotembelea katika kituo cha Afya cha kijiji cha Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma katika siku ya pili ya ziara yake kuona utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm katika maendeleo ya kisekta . 

Shaka alisema serikali ya Chama Cha Mapinduzi zina wajibu wa kufuatilia kwa karibu na kujua kama yale yote yalioahidiwa katika ilani , yanayotimizwa na iwapo yanawafikia na kuwahudumia wananchi kama inavyokusudiwa na serikali Kuu kwa wananchi wake. 
Alisema pamoja na kukabiliwa na upungufu wa idadi ya Waganga na Wauguzi katika Kituo cha Afya Nguruka, waliopo wamekuwa wakijituma bila kuchoka  huku  wakitoa huduma kwa njia makini na sahihi ili kunusuru na kutibu  wagonjwa . 

"Serikali ya CCM  katu haitapuuzia dhamana waliopewa na wananchi kwa  kuiweka madarakani kidemokrasia , maeneo yote ya kisekta yataendelea kupata huduma bora kwa wakati stahili hususan eneo la Afya kwa upelekaji vifaa tiba, dawa, Waganga na Wauguzi " Alisema Shaka .

Alisema katika kuonyesha serikali kujali matatizo ya wagonjwa hivi karibuni Rais John Magufuli amepeleka shilingi milioni kumi katika kituo cha Afya Nguruka kwa ajili ya kufanyika upanuzi wa wodi ya wazazi  huku kanisa la shalom likijenga wodi hiyo. 

"Rais wetu  hapati usingizi kwa raha kutokana na kufikiria wanachi wake, kila wakati amwkuwa akiwahimiza wataalam wa huduma za afya na watendaji dhamana wa serikali watimize wajibu wao bila kuchoka. Huuu ndiyo uungwana alionao kiongozi wetu na kila mmoja wetu sasa lazima awajibike 'Alisema Shaka mara baada ya kutazama  wodi hiyo.
Aidha Kaimu huyo Katibu Mkuu wa UVCCM aliwataka watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza kujiongeza katika mikakati ya ubunifu, utendaji unaoonekana na kujali maisha ya watu, matumizi bora ya fedha za ruzuku ya umma toka serikali kuu na kuhakikisha wanawatibia wagonjwa kwa wema. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu Msaidizi wa Kituo cha Afya Nguruka Dk Beatrice Mtasigwa alimueleza Shaka licha kukabiliwa na upungufu wa Waganga na Wauguzi, wamekuwa wakiwahudumia wagonjwa mbalimbali toka vijiji vyote wanaofika kituoni kati 80 hadi 120 kwa siku. 

Dk Mtasigwa alisema hatua ya ujenzi na upanuzi wa wodi ya wazazi , uwepo wa badhi ya vifaa tiba vya kisasa utasaidia kwa kiasi kikubwa kunusuru  maisha ya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano. 

Naye Mbunge wa Vijana Mkoa Kigoma Zainab Katimba alitoa shilingi laki mbili na kumkabidhi Mganga Mkuu Msaidizi wa Kituo hicho cha Afya kusaidia kununulia shuka ambazo zitatumika katika wodi ya wazazi.

Katimba alisema bila kina mama hakutakuwa na Taifa kwasbabau nchi na mataifa yote yanajazwa na nguvu za kina mama ambazo ndiyo wazazi wanaoleta neema ya kupatikana  watoto duniani , wataalam wa fani mbalimbali, viongozi, wabunge na wanasiasa.
Shaka anaendelea na ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Kigoma Mjini kabla ya kuelekea Kibondo, kasulu, Buhigwe, Kakonko na Kigoma vijijini mkoani hapa.