MFUKO wa LSF watoa msaada wa Laptop kwa wasaidizi wa kisheria kwa jamii

MFUKO wa LSF watoa msaada wa Laptop kwa wasaidizi wa kisheria kwa jamii

February 05, 2017
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Kushoto ni Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk akishuhudia. Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya LSF, Joseph Ndunguru akishuhudia.Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Katikatika ni Mjumbe wa Bodi ya LSF, Joseph Ndunguru akishuhudia.Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Katikati akishuhudia ni, Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk. Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Katikati akishuhudia ni, Mjumbe wa Bodi ya LSF, Joseph Ndunguru.Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii. Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamiiMshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii. Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii.Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii. Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii.Baadhi ya laptop zilizotolewa kwa wasaidizi hao wa kisheria kwa jamii. Baadhi ya laptop zilizotolewa kwa wasaidizi hao wa kisheria kwa jamii.Viongozi hao wakiwa katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wakiwa katika hafla hiyo leo jijini Dar es SalaamMkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Mjumbe wa Bodi ya LSF, Joseph Ndunguru (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza.

 MFUKO wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) umekabidhi laptop 170 kwa asasi mbalimbali zinazotoa msaada wa kisheria kwa wananchi wahitaji katika mikoa anuai nchini Tanzania. Akizungumza kabla ya kukabidhi vitendea kazi hivyo kwa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa wa kisheria, Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana aliwataka sema shirika hilo linaamini zitatumika katika kutatua changamoto anuai kwa asasi husika ikiwa ni chachu ya kuongeza ufanisi kwa kazi zao. Laptop hizo 170 zimekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen huku akizitaka asasi hizo muhimu kuendelea kuisaidia jamii inayoitaji msaada wa kisheria popote walipo kwani zipo familia hasa wajane wanaitaji na wanashindwa namna ya kupata. LSF ni mfuko huru wa msaada wa kisheria unaotoa msaada kwa mashirika watoa msaada wa kisheria, kitaasisi na kiufundi ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya sheria chini ya ufadhili wa Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID la Uingereza. Afisa Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Saada Mkangwa (kushoto mbele) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam. Afisa Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Saada Mkangwa (kushoto mbele) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam.Meneja Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Said Chitong (kulia) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam. Meneja Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Said Chitong (kulia) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo. Sehemu ya wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo

NDUGU WAGOMEA MAITI YA MTOTO HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM

February 05, 2017
Mzazi Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini, akiwa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na mwanahabari akidai amebadilishiwa mtoto aliyejifungua.
 Mama mzazi wa Julieth, Veronica Lucas akiwa ameshika shavu kwa masikitiko kufuatia tukio hilo.



 Shangazi yake Julieth, Judith Christopher akielezea tukio hilo 
kwa mwanahabari.
 Julieth Daud (kulia) akiwa na dada yake nje ya wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.

Julieth (aliyekaa kushoto), akiwa na ndugu zake nje ya
wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MZAZI Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake wamegoma kuchukua mwili wa mtoto kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake kutokana na kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala  jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kujifungua.

Akizungumza kwa masikitiko nje ya viwanja vya hospitali hiyo Dar es Salaam jana, Daudi alisema kitendo alichofanyiwa kimemuumiza sana pamoja na ndugu zake wengine.

Alisema alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith Christopher.

"Nilipofika daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya kipimo hicho nilijisia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.

Daudi alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.

Aliongeza kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.

Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa ambapo alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.

Shangazi wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao baina ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.

Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mama yake kuiharibu mimba hiyo kwa nia ya kuitoa na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa mfu.

"Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNN na ili mama wa mtoto aruhusiwe kutoka hospitali inatakiwa ipelekwe barua ya mwenyekiti wa mtaa wake anakoishi" alisema Christopher.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo hakuwa tayari kuzungumza kwa njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.

VIDEO: Sheria Ngowi kuteka soko la fashion nchini...Nini mipango yake?

February 05, 2017

Sio kila unachosoma ndio ndoto yako ya baadae, unaweza ukasoma Udaktari au Sheria lakini pia ukawa na kipaji cha zaidi ya ulichosomea na kujikuta unavutiwa kukitumia kipaji hicho kwa ajili ya jamii inayokuzunguka.

The Beauty TV ilizungumza mambo mengi na Sheria Ngowi na unaweza kumtazama hapa na usisahau ku-subscribe kwa ajili ya taarifa zaidi kutoka The Beauty TV.
-- Zainul A. Mzige, Managing Director, Mzige Media Limited, www.thebeauty.co.tz +255714940992.