WIKI YA AIBU KWA WAPINZANI NA UTEUZI WA RAIS WA WAKUU WAPYA WA WILAYA HUYU NAYE WAMECHAFUA BILA SABABU UZUSHI MTUPU!!

February 21, 2015


Wiki nzima hii toka Rais ateue Wakuu wapya wa Wilaya Wapinzani wamekuwa kwenye kazi kubwa sana ya kumchafua Mkuu mpya wa Wilaya ya Mufindi pichani ambaye pia ni Makamu wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mh. Mboni Mhita na wamekuwa wakitumia picha za chini kujaribu kuonyesha kwamba hizi picha ni za Mboni Mhita ukweli huu hapa kwamba ni watu wawili tofauti na infact Mheshimiwa Mboni aliwahi kupiga picha na huyo mtu hapo chini wanayemtumia picha zake kama Mboni ambaye ni mke wa mtu tayari tofauti na huyu dada kwenye picha aliyevaa kofia ya CCM. Wapinzani wameishangaza sana Dunia na hizi mbinu chafu za kutaka kumachafua Rais wa Jamhuri kwamba kila Mwanamke anayemteua uongozi wa juu ni hawara yake ni uongo na uzushi wa kitoto sana ukweli ni kwamba ni wao Viongozi wa upinzani ndio wanao ongoza kwa kuwatia mimba wabunge wao wa viti maalum na hata kuwaingiza bungeni vimada vyao, wananchi ni muhimu sana tukawaangalia Wapinzani kwa macho yetu yote mawili nini nia na madhumuni hasa kuwachafua kina mama wanaopewa uongozi wa juu na hasa kumchafua Rais bila sababu!! - Le Mutuz


DKT. SHEIN AFUNGUA MSIKITI WA MAKUNDUCHI,ZANZIBAR

February 21, 2015

Msikiti mpya wa Kijiji cha Kiongoni Makunduchi wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja ambao leo umefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa Msikiti Mpya wa Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja (kulia) Mkuu wa Mkoa Kusini Dk.Idriss Muslim Hijja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuufungua Msikiti Mpya wa Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja na kuanza rasmi shuhuli za Ibada (kulia) Mkuu wa Mkoa Kusini Dk.Idriss Muslim Hijja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kushoto) pamoja na Mashekhe na Viongozi na Waislamu mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada ya Swala ya Dhuhuri iliyoongozwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) baada ya ufunguzi wa Msikiti Mpya katika Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa kulia) pamoja na Mashekhe na Viongozi na Waislamu mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada ya Swala ya Dhuhuri iliyoongozwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji (hayupo pichani) baada ya ufunguzi wa Msikiti Mpya katika Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Zanzibar Dr.Sheikh Muhidin Siasa akitoa mawaidha baada ya ufunguzi wa Msikiti mpya wa Kijiji cha Kiongoni Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji (kulia) alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein azungumze na waislamu baada ya ufunguzi wa Msikiti Mpya katika Kijiji cha Kiongoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Waislamu wa Kijiji cha Kiongoni Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kuufungua Msikiti mpya kijijini hapo leo uliojengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe, Haroun Ali Suleiman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waislamu wa Kijiji cha Kiongoni Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kuufungua Msikiti mpya kijijini hapo leo uliojengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe, Haroun Ali Suleiman.[Picha na Ikulu.]

WASANII WA BONGO FLAVA WAMKUMBUKA MEZ B KWENYE BONANZA LA PSPF

February 21, 2015

Msanii wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flava, Shilole na wacheza show wake, wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka msanii mwenzao wa Bongo Flava, Mez B, mzaliwa wa Dodoma, wakati wa bonanza lililoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Februari 20, 2015. Bonanza hilo lilipambwa na michezo mbalimbali kama vile, soka, netibole, voliboli na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto wa Mjomba band. Wasanii wengine ni pamoja na Chege na Temba na Mr. Blue. Mez B, ni mzaliwa wa mkoa wa Dodoma, ambaye alifariki leo saa tano kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma, alikokuwa akipatiwa matibabu. Anatarajiwa kuzikwa Jumatatu ijayo Februari 23.
Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiburudisha wanachuo na watu wengine waluohudhuria bonanza hilo 
Chege(kulia) na Temba
Wanachuo na watu wengine wakipagawishwa na muziki uliokuwa ukiungurumishwa kwenye bonanza hilo
Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (wapili kulia) akiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, wakwanza kulia, wakati akitoa nasaha kwa timu mbili za soka kutoka vyuo vikuu mkoani Dodoma
Maafisa wa juu wa PSPF, wakipasha misuli. Hata hivyo hawakuingian uwanjani kusakata kabumbu kutokana na muda kuwa mchache
DJ Tass, akitoa saluti kuashiria kumkumbuka Mez B
Mchezaji wa timu ya Nertiboli ya chuo cha fedha CBE mkoani Dodoma, akiruka juu kumzuia mchezaji mwenzake kutoka UDOM 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kulia), akikabidhi jezi kwa mwakilishi wa moja ya timu za vyuo viklivyoshiriki bonanza hilo  


Shilole na kundi lake 


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (kulia), akiteta jambo na Meneja Masoko na mawasiliano wa PSPF, Constatina Martin

Nahodha wa timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM-DIPLOMA, Abdallah Shaaban, (kushoto, akipokea kombe la ubingwa wa soka, kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, baada ya kuibuka washindi kwa upande wa soka kwenye tamasha hilo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu

Nasaha kwa wachezaji wa Netiboli

Katika bonanza hilo, Meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari, Mwanjaa Seme, (kushoto), aliitumia vizuri fursa ya mkusanyiko mkubwa wa watu kusaka wanachama ambapo dereva huyu wa bodaboda alikuwa miongoni mwa waliojiunga na mpango huo

MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KWENYE SHEREHE YA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) HUKO WETE-PEMBA

February 21, 2015


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume huko Pemba na kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Ndugu Mwanajuma Majid Abdalla tarehe 20.2.2015. Mama Salma alialikwa Pemba kama Mgeni Rasmi kwenye sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) iliyoandaliwa na Al-Madrasat Jabal- Hiraa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Karume huko Pemba kwa ziara ya kikazi ya siku moja kisiwani humo tarehe 20.2.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi kwa kuvishwa shada na wasichana wa Almadrsat Jabal-Hiraa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Shule ya Utaani huko Wete Pemba ilikofanyika sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambapo Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi tarehe 20.2.2015.
Mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) kwenye Shule ya Utaani huko Wete Pemba wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) aliyokuwa akitoa wa viongozi na wananchi waliohudhuria sherehe hizo tarehe 20.2.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa nasaha zake kwenye Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) iliyofanyika kwenye Shule ya Utaani huko Wete katika Mkoa wa Kaskazini Pemba huku mamia ya watu wakimsikiliza. Mama Salma alikuwa Mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo iliyofanyika tarehe 20.2.2015. PICHA NA JOHN LUKUWI

FAINALI DARAJA LA KWANZA KUCHEZWA CHAMAZI .

February 21, 2015

Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), inatarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Awali mchezo huo wa fainali ulikuwa umepangwa kufanyika kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TTF imepelekea mchezo huo kuhamishiwa Chamazi.

Mchezo huo wa fainali utaanza saa 10 kamili jioni, na utaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV ili kuwapa nafasi wapenzi na wadau wa soka waliopo mbali na hasa mikoani kuweza kushuhudia mchezo huo.

Bingwa wa Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza atazawadiwa Kombe pamoja na medali, huku mshindi wa pili akipata kikombe na medali pia.

Viingilio vya mchezo huo ni tsh.5,000 kwa jukwaa kuu na tsh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.

Wakati huo huo, Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea leo (Jumamosi)  katika viwanja vitatu tofauti, Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Ndanda FC ya Mtwara watawakaribisha Wagosi wa Kaya timu ya Coastal Union kutoka jijini Tanga katika mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Ngwanda Sijaona.

Huku wakata miwa wa Kagera Sugar wanaoutimia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakiwakaribisha Maafande wa Jeshi la Polisi kutoka mjini Morogoro timu ya Polisi.

Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea tena kesho jumapili katika viwanja vitatu   tofauti, Uwanja wa Chamazi wenyeji Azam FC wataikaribisha timu ya maafande wa Jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons, mchezo utakaonza majira ya saa 2 kamili usiku.

Mjini Shinyanga wenyeji timu ya Stand United wataikaribisha Simba SC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, timu ya Mbeya City wakicheza na timu ya Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania  
 

LOGA AULA AFC LEOPARDS YA KENYA

February 21, 2015

KOCHA wa zamani wa Simba SC, Zdravko Logarusic ameteuliwa kuifundisha, AFC Leopards ya Kenya na tayari ameshatua kuanza kibarua hicho.

Logarusic ambaye ni raia wa Crotia ametua Kenya, juzi jioni saa 12:30 kwa madaha kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta huku akiwa mawani mazito ya jua.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya mtandao wa kijamii wa facebook, Zdravko Logarusic alisema amekwenda Kenya baada ya mapumziko baada ya Simba ya Dar es Salaam kumtupia virago 

“Nafurahi kurejea Kenya kwani naamini kazi niliyoifanya nikiwa na Gor-Mahia wengi walivutiwa nayo naamini hata Tanzania kipindi nilichokuwa na Simba mashabiki walivutiwa na kiwango changu cha ufundishaji ila siasa za mpira ndo zinafanya kocha waondoke kwenye vilabu na kujikuta wanakurudi tena”, alisema Loga

Logarusic kocha mwenye kujiamini alipokelewa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Allan Kasavuli na Katibu msaidizi, Asava Kadima na ameshajiunga na timu kambini Mumias, magharibi mwa Kenya ambapo ilikuwa na kocha msaidizi, Yusuf Chippo

Logarusic anakuwa na kibarua cha kwanza leo baada ya AFC Leopards itakapokuwa  ikicheza dhidi ya Chemelil Sugar  nyumbani kwao, ambapo pazia la Ligi Kuu ya Kenya litakuwa likifunguliwa rasmi licha ya mgogoro unaoendelea na Shirikisho la Soka Kenya, FKF, kuhusu idadi ya timu zitakazoshiriki ligi hiyo.

 ‘Loga’,  ambaye amewahi kuzifundisha klabu za Ashanti Gold na King Faisal FC za Ghana pamoja Gor Mahia ambao wapinzani wa Leopards ya Kenya na Simba ya Dar es Salaam amefurahi kurejea Kenya ujio ambao mashabiki wameupokea kwa furaha

DIAMOND PLUTNUMZ AWAJIBU JOKATE NA WEMA KWA BOOONGE LA DOOOOOONGOOOOO A.K.A DI DI DISS

February 21, 2015

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RASMI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

February 21, 2015

Tanzania inaunga mkono kwa dhati Ushirikiano wa Kikanda na
muumini mkubwa wa Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC). 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo  jijini
Nairobi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya ambaye amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi
cha mwaka mmoja uliopita
 “Tunaamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki
iliyogawanyika, haitaweza kuchukua nafasi yake kamili na heshima
katika familia ya Mataifa ya Afrika na dunia kwa ujumla” Rais amesema
na kuongeza kuwa Tanzania inakua kuwa masoko yaliyogawanyika,
miundombinu hafifu baina ya nchi, havina nafasi katika dunia ya leo
wala ya baadaye. 
 
Rais
Kikwete amesema na kumpongeza Rais Kenyatta kwa kusimamia
utekelezwaji wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa
kipindi chake cha uenyekiti na kuahidi kuwa Tanzania haitawaangusha
wana Afrika Mashariki katika kutekeleza azma yao ya pamoja ya
kuendeleza Jumuiya ambayo inaundwa na nchi za Burundi, Kenya, Rwanda,
Tanzania na Uganda. 
 
Rais
Kikwete amesema katika utekelezaji wa ajenda ya EAC, biashara
imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba nchi zote wanachama zinayaona
matunda hayo.
Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 biashara katika nchi za EAC
imeongezeka kutoka dola za kimarekani 3, 722.9 hadi dola 5,805.6
ambapo kati ya mwaka 2012 hadi 2013 kumekua na ongezeko la asilimia
6. 
“Kama biashara isiyo rasmi ingerasimishwa, kwa hakika,
ongezeko hili la biashara lingekua juu zaidi ya hapa, hivyo imefikia
wakati muafaka kurasimisha biashara isiyo rasmi katika ushirikiano
wetu” Rais amesema na kuongeza kuwa ” kwa njia hii serikali
zitakusanya kodi na hivyo kuna umuhimu wa kuelekeza nguvu katika
kusaidia biashara ndogo ndogo na zile zisizo rasmi kwa kuziwekea
mazingira mazuri”. 
Rais
Kikwete amerejea nyumbani mara baada ya mkutano huo ambao umehudhuriwa
na Marais wa nchi zote tano za Jumuiya na Rais Salva Kiir wa Sudan
Kusini ambaye amehudhuria kama mualikwa maalum katika kipindi hiki
ambapo mazungumzo ya awali ya kuijadili nchi yake kama inaweza kupata
uanachama katika EAC yanaendelea.
  Rais Jakaya
Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na
Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais
Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia
kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International
Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida
wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari
20, 2015
 Rais Jakaya
Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na
Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya
katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20,
2015
 Rais Jakaya
Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa
wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya
wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20,
2015
 Kutoka kushoto ni
mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais wa
Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho
Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni
(Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa
mikutano kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za
Afrika Mashariki 
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa
Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi
Uenyekiti wa  EAC  kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo Ijumaa Februari 20,
2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi. Picha na IKULU