Waziri Prof. Mghembe awaonya wanaoharibu vyanzo vya maji

March 20, 2015

Mchungaji wa mifugo akinywesha maji mifugo yake kwenye eneo lenye maji ambalo Waizri Prof. Maghembe amepiga marufuku kunywesha kwenye eneo hilo.

Na Hussein Makame-MAELEZO, Musoma

WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amewaonya wananchi wanaoharibu vyanzo vya maji kwamba kufanya hivyo kunahatarisha uhai wa vyanzo hivyo.

Ametoa onyo hilo kwa nyakati tofauti wakati akiwa kwenye shughuli za kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara ambako Maadhimisho ya Wiki ya Maji kitaifa yanafanyika. 

 Akiwa katika kijiji cha Rung’abure, Waziri alishuhudia baadhi ya wafugaji wakinywesha mifugo yao kwenye maeneo ya vyanzo vya maji huku baadhi wakilima karibu na chanzo cha maji.

“Jamani mradi huu ni wa kwenu, lakini nilichokiona pale kwenye chanzo cha maji, nilina ng’ombe kwenye eneo chepechepe” alisema Waziri Prof. Maghembe na kungeza: “Jamani fanyeni juhudi au lolote mnalofanya lakini msiingizi ngombe mule kama mkiingiza basi maisha ya mradi yatakuwa mafupi na hakuna mtu wa kumlaumu kwa sababu ni nyinyi wenyewe mmekuwa kama mtu anayekata tawi la mti alilokalia” Aliongeza kuwa katika eneo la mradi wa Rung’abure kuna mkulima analima kwenye msitu ulioko karibu na chanzo cha maji cha mradi wa kijiji hicho, hivyo anahatarisha chanzo hicho.

“Mtu yule tunamuomba mwaka huu avune mazao yake lakini mwaka kesho asipande pale.Mwenyekiti naomba mumpe shamba lingine kwa sababi akiendelea kulima hakuna maji pale” alisema Waziri Prof. Maghembe.

Alifafanua kuwa suala la kuondoka si hiyari kwani hairuhusiwi kisheria kulima mita 60 kutoka chanzo cha maji, hivyo mkulima huyo ni lazima aondoke mwakani.

“Hili jambo ninalosema si hiari ni suala la kisheria hairuhusiwa kulima kwenye chanzo cha maji kwa umbali wa mita 60 na hilo sio jambo la kumuomba mtu ni jambo la kutekeleza sheria” alisema na kuongeza: “Ninachosema yule aliyelima pale mwaka huu avune mazoa yake mi sina tatizo kabisa baada ya hapo tunamuoba aondoke pale sheria hii sio ya mwaka huu, wala mwaka jana wala mwaka juzi na hilo ni sheria imetungwa mwaka ya 2006” Aliitaka Serikali ya kijiji hicho pia wanasimamia kuhakikisha ng’ombe hawapelekwi kunywa maji kwenye eneo la chanzo cha maji badala yake wakanywe maji kwenye mabirika yaliyojengwa.

Akiwa mjini Mugumu wilayani Serengeti, ambako alitembelea ujenzi wa chujio la maji ya bwawa la Manchira na baada ya ukaguzi huo alizungumza na wananchi wa mji huo. Alisema chujio hilo litachuja maji na kuweka dawa kwenye maji yanayokwenda mjini na kutatua tatizo la uchafu wa maji ambalo linawakabili wananchi wa Mugumu.

“Lakini pia niwaombe sana ndugu zangu mtunze sana mazingira kwani tumeona rasilimali za maji zinapungua sana ninawaomba mtunze sana vyanzo vya maji mtunze na bwawa letu la Manchira” alisema Waziri Prof. Maghembe. Hivyo alisisitiza kuwa ili kuhakikisha bwawa hilo na linaendelea kutumika kwa kipindi kirefu, kitu kikubwa ni kutunza sana mazingira ili kiasi cha rasilimali kilichopo kisiendelee kupungua.

Akiwa katika vijiji vya Ligamba A na Mumagunga vilivyoko wilayani Bunda mkoani Mara, Waziri aliwataka wananchi wapande miti ili kulinda vyanzo vya maji kwenye maeneo yao. Alisema utunzaji wa vyanzo vya maji ni jambo muhimu ili kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji havikauki na kujharibiwa kwani kufanya hivyo kutahatarisha upatiakanaji wa maji.

Waziri Prof. Maghembe anaendelea na ziara ya kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji katika vijiji mbalimbali vya wilaya za mkoa wa Mara ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa.

Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD (TDL),yachangia kiasi cha sh.milioni 10 kwenye Mfuko wa Imetosha Foundation

March 20, 2015

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD,David Mgwassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa Imetosha Foundation.Kushoto ni Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu na kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi.
Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es salaam leo,wakati wa kutangaza matembezi ya hisani yatakayofanyika Machi 29 kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam na kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Mathius Chikawe.Wengine pichani toka kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi,Katibu wa Harakati ya Imetosha,Salome Gregory pamoja na Mwanamuziki Mkongwe nchini,Jhiko Manyika “Jhikoman”.
Sehemu ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha waliofika kwenye Mkutano na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es salaam,wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Picha na Othman Michuzi
……………………………………………
Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD (TDL),imechangia kiasi cha sh.milioni 10 kwa harakati ya Imetosha inayopiga vita mauaji ya watu wenye Ualbino,ambayo itafanya matembezi ya hisani machi 29 mwaka huu yatakayofanyika kuanzia katika viwanja vya Biafra na kuishia katika Viwanja vya Leaders Klabu,Kinondoni jijjni Dar es Salaam.
Akizunguma na waandishi wa habari wakati kutangaza kutoa mchango huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,David Mgwassa amesema kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu ni jukumu la kila mtanzania,hivyo TDL kama watanzania wameona umuhimu kuchangia harakati hizo,kwani hata sifa mbaya zinazopatikana nje ya nchi hazilengi mtu mmoja au kundi fulani. 
Amesema watu wengine wajitokeze kuunga mkono harakati hizo ili kuwa sehemu ya watu ambao wanaguswa na suala la mauji ya watu wenye ualbino.
Matembezi hayo yataongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe ambapo ujumbe wa serikali utatolewa katika harakati zinazoendelea za kukomesha mauaji ya watu hao wenye Ualbino.
Akizungumzia Matembezi hayo,Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu amesema matembezi hayo hayalengi kukusanya fedha wanachohitaji ni watu washiriki matembezi hayo.
mdimu amesema kuwa harakati hiyo ni ya kutoa elimu katika mikoa ambayo mauji ya watu wenye ualbino ili kuweza kubadilisha hali hiyo na isiendelee kuwepo.
“Hatulengi masuala ya fedha tunachotaka wananchi wafikishiwe elimu na watu wanaofanya hivyo washindwe kufanya kutokana na elimu iliyotolewa kuanzia katika familia”amesma Mdimu.
Amesema harakati hizo zimetokana na nguvu ya wadau ambao wamejitolea nguvu zao katika kuweza kukomesha mauaji ya watu wenye Ualbino hapa nchini.
Wahariri, Tamwa wakutana kufanya tathmini ukatili unaosababishwa na pombe

Wahariri, Tamwa wakutana kufanya tathmini ukatili unaosababishwa na pombe

March 20, 2015

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo (katikati) akionesha ripoti ya utafiti juu ya matumizi ya pombe na inavyochangia unyanyasaji wa kijinsia kwa Wilaya ya Kinondoni. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la IOGT ambalo ndio wawezeshaji wa utafiti huo. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la IOGT. Ripoti hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo (katikati) akionesha ripoti ya utafiti juu ya matumizi ya pombe na inavyochangia unyanyasaji wa kijinsia kwa Wilaya ya Kinondoni. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la IOGT ambalo ndio wawezeshaji wa utafiti huo. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la IOGT. Ripoti hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la IOGT nchini Tanzania (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi wa ripoti ya matumizi ya pombe na athari katika vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Mwakilishi wa Shirika la IOGT nchini Tanzania (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi wa ripoti ya matumizi ya pombe na athari katika vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Kiongozi Mkuu wa Utafiti juu ya matumizi ya pombe uliofanyika Wilaya ya Kinondoni, Dk. Severine Kessy (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna utafiti ulivyoendeshwa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo. Utafiti huo uliendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT.
Kiongozi Mkuu wa Utafiti juu ya matumizi ya pombe uliofanyika Wilaya ya Kinondoni, Dk. Severine Kessy (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna utafiti ulivyoendeshwa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gladness Munuo. Utafiti huo uliendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT.
Kiongozi Mkuu wa Utafiti juu ya matumizi ya pombe uliofanyika Wilaya ya Kinondoni, Dk. Severine Kessy akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna utafiti ulivyoendeshwa. Utafiti huo uliendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT.
Kiongozi Mkuu wa Utafiti juu ya matumizi ya pombe uliofanyika Wilaya ya Kinondoni, Dk. Severine Kessy akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna utafiti ulivyoendeshwa. Utafiti huo uliendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo wakifuatilia matukio na ufafanuzi juu ya ripoti hiyo.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo wakifuatilia matukio na ufafanuzi juu ya ripoti hiyo.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo wakifuatilia matukio na ufafanuzi juu ya ripoti hiyo.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo wakifuatilia matukio na ufafanuzi juu ya ripoti hiyo.
KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA

March 20, 2015

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kugonga kokoto pamoja na akina mama wajasiriamali katika kata ya Elerai mjini Arusha  wakati alipowatembelea  na kukagua shughuli zao,  ambapo aliwaambia “Asiwasumbue mtu wala kuwaambieni muondoke kwani ninawafahamu kwa muda mrefu toka nikiwa Mbunge wa jimbo hili  la Arusha mjini miaka ya nyuma”, aliwaagiza viongozi wa CCM wa kata hiyo kutojiingiza hata kidogo na kuleta mgogoro na wananchi hao ambao wanajitafutia rizki katika kazi yao hiyo.
Ameongeza kuwa CCM ni chama kinachotakiwa kuwasemea na kuwatetea wanyonge na siyo kuwakandamiza na kuwaonea  “Lazima viongozi na watendaji wa serikali na chama wawajibike kwa wananchi ambao ndiyo walioingia mkataba na CCM ambayo iliunda serikali inayotekeleza ilani yake” amesema .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mkoa wa Arusha akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, inayotekelezwa na serikali ya CCM huku akihimiza uhai wa Chama hicho akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ARUSHA)2 
Kada wa CCM Viola naye akimwaga maneno ya sumu wakati wa mkutano wa katibu Mkuu wa Ndugu Abdulrahman Kinana na wafanya biashara wa soko la Kilombero jijini Arusha. 13 
Nape Nnauye akizungumza na umati wa wafanyabiashara na baadhi ya wananchi mbele ya jengo la Soko la Kilombero jijini Arusha. 14 
Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wakiwa katika mkutano huo. 15 
Kiongozi wa wafanyabiashara wa soko la Kilombero jijini Arusha akisoma risala kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana huku Nape Nnauye akiwa amemshikia kipaza sauti. 10 
Serikali inahitaji wamafundi sanifu 10,000 wa maabara (Laboratory Technicians) mpya zionazojengwa nchini.

Serikali inahitaji wamafundi sanifu 10,000 wa maabara (Laboratory Technicians) mpya zionazojengwa nchini.

March 20, 2015

001
Waziri wa TAMISEMI Mhe.Hawa Ghasia akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais na Menejimenti ya Utumishi wa Umma lililoulizwa na Mhe. Yahya Issa (Mb )wa Chwaka tarehe 20.03.2015.Mjini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO,Dodoma.
Serikali imesema inauhitaji wamafundi sanifu 10,000 wa maabara(Laboratory Technicians) mpya zionazojengwa nchini.
Hayo yameyasema na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bungeni Mjini Dodoma, Mhe.Hawa Ghasia alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa (CUF).
Katika swali lake Issa alitaka kujua kwa nini Serikali huwapa mikatabawatumishi waliostaafu wakati wapo vijana wengi ambao hawana kazi.
Waziri Ghasia alisema Serikali hutoa mikataba kwa baadhi ya kada ambazo bado hazijitoshelezi kutokana na kuwa na wataalamu wachache.

“Kwa mfano kwa sasa Serikali ina mahitaji makubwa wa mafundi sanifu wa maabara kwa ajili ya kusimamia maabara zetu zinazojengwa walipo kwasasa hawafiki 1,000 wakati mahitaji ni 10,0000,” alisema Ghasia.
Awali akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo, Ghasia alisema sio seraya Serikali kuwaajiri wastaafu isipokuwa pale tu inapoonekana ni kwamanufaa ya umma kutokana na mahitaji makubwa katika sekta husika.
Alisema vijana na wasomi waliohitimu vyuo mbalimbali hapa nchini hupatiwa ajira kulingana na mahitaji ya bajeti iliyopo.
Waziri Ghasia alisema Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Pensheni kwa Watumishi wa Umma sura namba 371, mtumishi wa umma anayo hiari ya kustaafu kwa hiyari akifikisha umri wa miaka 55.
003
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wakiwa wamesimama ndani ya Bunge mara baada ya kutambulishwa kwa uwepo wao,Mjini Dodoma tarehe 20.03.2015.
MAMA SALMA KIWETE AKABIDHI GARI LA WAGONJWA KWENYE HOSPITALI YA MKOMAINDO HUKO MASASI.

MAMA SALMA KIWETE AKABIDHI GARI LA WAGONJWA KWENYE HOSPITALI YA MKOMAINDO HUKO MASASI.

March 20, 2015

1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na mmoja wa wauguzi katika hospitali ya Wilaya ya Masasi, Mkomaindo, mara baada ya kuwasili hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatembelea wagonjwa tarehe 19.3.2015.
9
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Masasi waliohudhuria sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa (ambulance) kwenye Hospitali ya Mkomaindo huko Masasi tarehe 19.3.2015.
7
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa kwenye hospitali ya Mkomaindo huko Masasi tarehe 19.3.2015.
2
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwelekeza Bibi Zauda Amuli,18, mkazi wa Mtaa wa Moroco namna ya kumnyonyesha mtoto wake mchanga aliyezaliwa tarehe 17.3.2015 katika hospitali ya Mkomaindo huko Masasi tarehe 19.3.2015.
3
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimchukua mtoto mchanga kutoka kwa mama yake Bibi Malisela Amandus, 24, anayeishi mtaa wa Silabu huko Masasi wakati Mama Salma alipotembelea hopitalini hapo kuwajulia hali wagonjwa tarehe 19.3.2015.
4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Halima Dendegu (kushoto) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkomaindo Dkt. Musa Rashid (kulia) wakitembelea maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
5
Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais akiwasalimia wazee wa Mji wa Masasi wakati alipowasili kwenye eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi kwa ajili ya kukabidhi gari la wagonjwa kwenye hospitali ya Wilaya, Mkomaindo, tarehe 19.3.2015.
6
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasslimia wanafunzi waliofika kwenye sherehe ya kukabidhi gari la wagonjwa (ambulance) kwenye Hospitali ya Wilaya ya Masasi, Mkomaindo, tarehe 19.3.2015.
10
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi kadi ya gari la wagonjwa (ambulance) kwa Meya wa Mji wa Masasi Mheshimiwa Andrew Mtumsha kwenye sherehe iliyofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi tarehe 19.3.2015. Aliyesimama kulia kwa Mama Salma ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ni Ndugu Halima Dendegu.
11
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na serikali kuangalia sehemu ya ndani ya gari la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa kwenye hospitali ya Mkomaindo.
12
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na wananchi mbalimbali kwa kuwapungia mikono baada ya kukamilisha zoezi la kukabidhi gari la wagonjwa kwenye hospitali ya Mkomaindo huko Masasi tarehe 19.3.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
PINDA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA AJI WA BUNDA

PINDA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA AJI WA BUNDA

March 20, 2015

1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua eneo la chanzo cha maji cha mradi wa maji wa Bunda katika  katika ziwa Victoria kwenye kijiji cha Nyabehu mkoani Mara  ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya maji, Machi 20, 2015. Kulia kwake ni Mbunge wa Bunda na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephene Wasira.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
3
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Bunda katika  kijiji cha Nyabehu mkoani Mara ,Machi 20, 2015 ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya Maji. . Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kushoto ni Mbunge wa Mwibara, Kange Lugora.  Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephene Wasirra.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
5
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua   moja kati ya mashine tisa za kusukuma  maji katika mradi wa Maji wa Bunda  uliopo kwenye ziwa Victoria katika kijiji cha Nyabihu  wilayani Bunda ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya maji Machi 20, 2015. Kulia kwake ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.
Mama Kikwete aitaka jamii kuhamasisha kinamama wajawazito kujifungua katika vituo vya afya

Mama Kikwete aitaka jamii kuhamasisha kinamama wajawazito kujifungua katika vituo vya afya

March 20, 2015

download 
Na Anna Nkinda – Maelezo, Masasi
…………………………………
 Jamii imehimizwa kuhamasisha kinamama wajawazito kujifungua katika vituo vya afya ambako watasaidiwa  na wakunga wenye ujuzi  kwa kufanya hivyo vifo vya kinamama na watoto wachanga vinavyotokana na tatizo la uzazi vitapungua.
Mwito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wananchi waliohudhuria hafla  ya makabidhiano ya gari la wagonjwa la Hospitali ya mji wa Masasi  ilijulikanayo kwa jina la Mkomaindo iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo.
Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema mtoto wa kike akibeba mimba katika  umri mdogo, mama mjamzito asipohudhuria kliniki mapema  na kwa muda uliopangwa  na kutojifungua katika vituo vya afya mama anaweza kupata  matatizo ikiwa ni pamoja na kupotea maisha wakati wa kujifungua.
“Wanaume mnapaswa kuunga mkono juhudi hizi katika kipindi cha ujauzito kina mama waondolewe majukumu ya kazi nzito muwe nao karibu, wahurumieni na kujiepusha na aina yoyote ya unyanyasaji. Wawezesheni wake zenu  kuhudhuria  kliniki na kupima ujauzito kipindi chote cha ujauzito na ifikapo tarehe ya kujifungua wasindikize katika  vituo vya afya.
“Pale watakapogundulika kuwa na matatizo ya kujifungua wapeni ushirikiano wa kutosha ikiwemo rasilimali fedha kwa ajili ya huduma yoyote ya rufaa itakayohitajika”, Mama Kikwete alihimiza.
Kwa upande wa vifo vya watoto alisema hutokana na kutokuwa na uwezo kama vile fedha za kumpeleka mama mjamzito aliyeshindwa kujifungua, kumuwahisha mtoto Hospitali mara apatapo matatizo kama vile ya kupumua, homa, na kuharisha.
Mama Kikwete alisema , “Huduma ya gari la dharula la wagonjwa ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya watu. Taarifa za kila siku zinaonyesha ni jinsi gani kina mama wajawazito wanapoteza maisha  kutokana na kucheleweshwa kufika katika vituo vya afya”.
Aidha Mwenyekiti huyo wa WAMA aliupongeza uongozi wa wilaya hiyo na watumishi wa sekta ya afya  kwa kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU kutoka asilimia 5.07 hadi kufikia 2.13 kwa mwaka 2014 ukilinganisha na mwaka 2013 ambapo kasi ya maambukizi ilikuwa asilimia 7.13.
Akisoma taarifa ya Idara ya afya Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya mji wa Masasi Dkt. Albano Nditi alisema katika mji huo kuna  vituo nane vinavyotoa huduma ya afya ya uzazi na mtoto ambazo ni upimaji wa kina mama wajawazito na watoto, kuzalisha na ufuatiliaji wa makuzi ya watoto.
Dkt.  Nditi alisema idadi ya wasichana wanaobeba mimba wakiwa na umri wa chini ya miaka 20 ni kubwa hali hiyo  inatokana na uelewa mdogo wa jamii juu ya athari za kubeba mimba katika umri mdogo. Pia asilimia 55 ya wanawake wajawazito wanaoanza kliniki hawakamilishi mahudhurio yote manne kwani waliowengi huanza kliniki wakiwa wamechelewa.
Alifafanua, “Kwa mwaka 2014 kina mama waliojifungua katika vituo vya  kutolea huduma ni  ni 4,762  kati ya hao wenye umri wa chini ya miaka 20 ni 1541  na zaidi ya miaka 20 ni 3,221. Waliojifungulia majumbani na kwa wakunga wa jadi ni 278 kati ya hao wenye umri wa chini ya miaka 20 ni 68 na zaidi ya miaka 20 ni 210”.
Vifo vilivyotokana na uzazi kwa mwaka jana vilikuwa 22, tatizo la vifo vya uzazi bado ni kubwa hii inatokana ana uhaba wa watumishi wenye ujuzi, mahudhurio duni ya kina mama Kliniki, kuchelewa kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya wakati wa kujifungua na uhaba wa vifaa kwenye wodi ya wazazi”.
Alizitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni upungufu wa madaktari, wauguzi wenye ujuzi, maafisa afya mazingira na madereva, upungufu wa magari ya kubebea wagonjwa, upungufu na uchakavu  wa majengo, uhaba wa vitanda na mashuka  katika wodi za wagonjwa  na ukosefu wa vituo vya kutolea huduma za afya katika baadhi ya maeneo hasa yaliyo pembezoni mwa mji.
Kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Dkt. Nditi alisema jumla ya kaya  274 kati ya 28,875 zilizopo katika mji huo zimejiunga na mfuko hali hiyo inatokana na mwitikio na uelewa mdogo kutoka kwa wananchi juu ya kujiunga na huduma hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi  Andrew Mtumusha alimshukuru Mama Kikwete kwa msaada wa gari alilowapatia na kusema kuwa litaokoa vifo vingi vya wakinamama wajawazito, watoto na wanaume  ambavyo vinatokea pale ambapo mgonjwa anacheleweshwa  kufikishwa Hospitali kubwa kutokana na tatizo la usafiri.
“Ninakupongeza  kwa moyo wa huruma na upendo ulionao, nakuomba uendelee kutukumbuka zaidi na zaidi kwenye mambo mbalimbali. Nina kuahidi  gari hili litatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa ya usafirishaji wagonjwa bila upendeleo wowote”, Mtumusha alishukuru.
Taasisi ya WAMA iliamua kukabidhi gari hilo liliopatikana kwa kushirikiana na Shirika la Sayeed  Corporation katika Hospitali ya Mkomaindo kutokana na wakina mama wengi kuhitaji huduma ya usafiri ili waweze kufika Hospitali kwa wakati na uwepo wa huduma ya mama na mtoto ambayo inatolewa mahali hapo.
WAZIRI LUKUVI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WILAYA ZA ARUMERU NA JIJI LA ARUSHA,ATAKA UTARATIBU WA KUMBUKUMBU ZA MASJALA UFUATWE

WAZIRI LUKUVI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WILAYA ZA ARUMERU NA JIJI LA ARUSHA,ATAKA UTARATIBU WA KUMBUKUMBU ZA MASJALA UFUATWE

March 20, 2015

004
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi(kulia)akiwasili kwenye makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Arusha,iliyopo wilayani Arumeru katika ziara yake ya siku tatu na ujumbe wake.
007
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi akizungumza na wakazi wa wilaya ya Arumeru kwenye viwanja vya halmashauri ya Arusha eneo la Sekei,alipata fursa ya kusikiliza kero za mashamba ambayo aliahidi kuifanyia kazi,kulia ni Mpima Ramani mkoa wa Arusha,Hamduni Mansoor na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Agatha Msuya.
002
Mzee Alfred Lekshon mkazi wa wilaya ya Arumeru akimweleza Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi jinsi alivyonyang’anywa shamba lake lenye ukubwa hekari 25.
001
Mkazi wa Olosiva ,wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha,ambaye  ni mjane Mwanahamisi Almasi akisimulia kero anazozipata kutoka kwa mtu anayetaka kumnyang’anya nyumba na kiwanja chake na kuwa amekua akisumbuliwa na kutishiwa .
003
Mwekezaji ambaye kutoka nchini Denmark,Finn Petersen ambaye kutokana na migogoro ya ardhi ameshindwa kuendelea na uwekezaji wake eneo la Oljoro baada ya eneo lake kuvamiwa na wananchi.
005
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Juma Idd(katikati)akifafanua jambo  wakati akieleza mpango wa kutekeleza  mradi wa kuliweka Jiji la Arusha  katika hadhi ya kimaita utakaotekelezwa hivi karibuni,kulia ni Mpima Ramani wa mkoa wa Arusha,Hamduni Mansoor.
006
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi(kushoto)akipata ufafanuzi  wa mojawapo wa majalada kwenye ofisi ya Masjala ya Ardhi kutoka Afisa Ardhi Mteule wa halmashauri ya wilaya ya Arusha,Rehema Mdee .
008
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Arusha,Agatha Msuya akizungumza kwenye mkutano wa wananchi kueleza kero za mashamba na viwanja kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
009
Meya wa Jiji la Arusha,Gaudence Lyimo akizungumza na wananchi kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa wakati wa mkutano wa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi kusikiliza kero za wananchi.Picha zote na Muungano Saguya.