RAIS KIKWETE AMLILIA ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA BAKWATA, ALHAJ KUNDYA

July 28, 2014


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Dk. Parseko V. Ole Kone kuomboleza kifo cha aliyepata kuwa Naibu Waziri, Mbunge na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mheshimiwa Alhaji Mahami Rajab Kundya.
Mzee Kundya aliaga dunia jana, Jumapili, Julai 27, 2014 mjini Zanzibar.
Katika salamu zake, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa taifa limempoteza Mzee Kundya katika kipindi ambacho ushauri wake ulikuwa unahitajika sana na kuwa Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa mchango wake katika nafasi zote alizozishikilia za Serikali, za Chama cha Mapinduzi na za kidini.
“Naungana nawe na wana-Singida wote katika kuomboleza kifo cha Mzee Kundya.Tumepoteza kiongozi ambaye mchango wake utaendelea kukumbukwa na sisi sote. Kupitia kwako, natuma pia salamu zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu. Niko nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa na naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Kundya,” amesema Rais Kikwete.

BREAKIN NEWZZZ!!:- SERIKALI YASIMAMISHA UAJIRI WA NAFASI ZA KAZI UHAMIAJI ZILIZOJAZA UWANJA WA TAIFA KAMA MECHI YA YANGA NA SIMBA LIVE!!

July 28, 2014



PINDA AONGOZA MAZISHI YA DK KAPOLI LEO

July 28, 2014

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika mazishi ya Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dk, Irenius  Kapoli, nyubani kwa Marehemu, Mbezi Malamba Mawili jijini Dar es Salaam leo.
 Waomboleaji wakiwa  wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini, Dk, Irenius Joseph Kapoli, katika mazishi  yaliyofanyika nyubani kwa Marehemu,  Mbezi Marambo Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014
 Mwili wa  aliyekuwa Mhadhili wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini,  Dk, Irenius Joseph Kapoli, ukitemswa kaburini katika mazishi  yaliyofanyika  nyubani kwa Marehemu,  Mbezi Marambo Mawili jijini Dar es salaam Julai 28, 2014.
Rais Kikwete akutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki, Amjulia Hali Jaji Lewis Makame

Rais Kikwete akutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki, Amjulia Hali Jaji Lewis Makame

July 28, 2014


D92A2407 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki(IAEA) Dkt.Yukiya Amano ikulu jijini Dar es Salaam leo.D92A2461 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Shirika la kimataifa la Nguvu za Atomiki(IAEA) Dkt. Yukiya Amano ikulu jijini Dar es Salaam leo.
D92A2478 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki(IAEA) Dkt.Yukiya Amano akiuangalia mti kubwa wa Mbuyu katika bustani za ikulu jijini Dar es Salaam huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiomuonesha tunda la ubuyu.
D92A2486 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimuonesha tunda la ubuyu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki(IAEA) Dkt.Yukiya Amano mara baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.
D92A2645 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mwenyekiti mstaafu wa tume ya Uchaguzi JAJI Lewis Makame aliyelazwa katika hospitali ya AMI iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)
MAMA KIKWETE AWATAKA WANAWAKE WENYE UGONJWA WA FISTULA KUJITOKEZA NA KWENDA KUPATA MATIBABU

MAMA KIKWETE AWATAKA WANAWAKE WENYE UGONJWA WA FISTULA KUJITOKEZA NA KWENDA KUPATA MATIBABU

July 28, 2014


Mama-Kikwete
Na Anna Nkinda – Maelezo aliyekuwa Lindi
28/7/2014 Wanawake wenye tatizo la ugonjwa wa Fistula wametakiwa kutokuogopa na kukaa kimya bali wajitokeze  hadharani kwa kwenda Hospitali kupata matibabu  au kuwaambia viongozi wao ili waweze kuwasaidia kwani ugonjwa huo unatibika na matibabu yake ni bure.
Rai hiyo imetolewa  hivi karibuni na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya chama hicho  katika matawi ya Mkoimba, Ng’apang’apa, Mbuyuni B, Mkanga, Mtutu na Rutende.
CRISTIANO RONALDO AMBWAGA TENA LIONEL MESSI, ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA

CRISTIANO RONALDO AMBWAGA TENA LIONEL MESSI, ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA

July 28, 2014


Cristiano Ronaldo wins Goal 50
Imechapishwa Julai 28, 2014, saa 10:34 jioni

CRISTIANO Ronaldo ameshinda tuzo ya Goal 50 ya mchezaji bora wa dunia baada ya kuwa na msimu mzuri wa 2013-14.
Mshambuliaji huyo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu kama sehemu ya kuheshimu kazi aliyoifanyia Real Madrid kutwaa taji la 10 la ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Nyota huyo mwenye miaka 29, pia alishinda kombe la mfalme (Copa del Rey) na kufunga magoli 51 katika mashindano yote ya klabu na taifa lake.
WALIOSHINDA TUZO YA Goal 50 mpaka sasa:
2008- Cristiano Ronaldo
2009 -Lionel Messi
2010- Wesley Sneijder
2011-Lionel Messi
2012- Cristiano Ronaldo
2013 -Lionel Messi
2014 -Cristiano Ronaldo.
Ronaldo alishinda kiatu cha dhahabu sambamba na Luis Suarez na mapema mwaka huu alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia na kushinda tuzo ya 2013 FIFA Ballon d`Or.
Baada ya kupokea tuzo hiyo, Ronaldo alisema: “Ni heshima kubwa kwangu kuchaguliwa kuwa mchezaji bora. Kiukweli nimefurahi sana”.
“Nashawishika kusema nisingeweza kutwaa tuzo hii bila sapoti kutoka watu wa Real Madrid”.
Goal 50 ni moja ya tuzo za heshima kwenye mchezo wa soka kwasababu wanaochagua wanatoka katika mitandao mikubwa ya soka duniani.
Kura zinapigwa baada ya kumalizika kwa misimu ya ligi za ndani na mashindano ya kimataifa na wanaopiga kura wanatoka mataifa mbalimbali.
Zaidi ya waandishi wa habari 600 kutoka katika machapisho 35 wanachagua wachezaji 50 wa juu kwenye tuzo hiyo.
Ronaldo ameongoza mwaka huu akifuatiwa na Arjen Robben, aliyeifanyia makubwa Uholanzi katika fainali za kombe la dunia na kuisaidia klabu yake ya Bayern kutwaa makombe manne msimu wa 2013-14.


Mshindi wa mwaka jana, Lionel Messi alishika nafasi ya tatu baada ya msimu mbaya katika klabu yake ya Barcelona na kushindwa kutwaa kombe la dunia nchini Brazil.

DANADANA YA RATIBA YAVURUGA MIPANGO KABAMBE YA MBEYA CITY FC

July 28, 2014

Na Baraka Mpenja, Mbeya


DHAHIRI Mbeya City fc imeharibiwa mpango wake wa kucheza mechi za kirafiki katika nchi za Zambia na Malawi kufuatia shirikisho la soka Tanzania, TFF, kupiga teke ratiba ya ligi kuu mpaka septemba 20 mwaka huu.
Kocha mkuu wa klabu hiyo Juma Mwambusi anakiri wazi kuwa kusogeza mbele ligi kuu kumeathiri mipango mingi ya maandalizi ikiwemo ratiba ya kucheza mechi za kirafiki nchi jirani.
Awali Mwambusi alikuwa na mpango ya kucheza mechi mbili nchini Zambia, halafu baadaye mbili Malawi, lakini sasa imekuwa ngumu kwasababu hata wapinzani wao katika nchi hizo watakuwa na ratiba nyingine.
“Kusogezwa mbele ligi kuu kumetuharibia mipango yetu mingi ya maandalizi, kuhusu mechi za kimataifa za kirafiki, sasa itategemeana na nafasi  yao kama tunataka kuwaomba tena kucheza,” alisema Mwambusi.
Mwambusi aliongeza kuwa bajeti ya timu kuwa ndogo kumemfanya avunje kambi ya maandalizi na kuwapa likizo wachezaji wake.
Mbeya City fc ni moja ya timu zilizofanya vizuri msimu uliopita kwa kushika nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia pointi 49.
City ilishinda mechi 13, ilitoka sare mechi 10 na kufungwa mechi 3.  Ilifunga mabao 33 na kufungwa mabao 20, hivyo wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa kuwa 13.
Mbeya City ilifanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza bila kufungwa mechi yoyote, lakini mzunguko wa pili ilifungwa mechi tatu dhidi ya Yanga, Coastal Union na Azam fc.
Timu zilizoshika nafasi ya kwanza mpaka ya nne kwa maana ya Azam, Yanga, na Simba, ni mabingwa Azam pekee waliweza kutoka na pointi tatu katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Simba na Yanga ziliambulia pointi moja tu, lakini Mnyama alishindwa kushinda hata Dar es salaam na kutoka sare ya 2-2, wakati Yanga walishinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.
Azam waliifunga Mbeya City mabao 2-1 uwanja wa Sokoine, wakati Coastal Union wao waliwafunga mabao 2-0 katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Msimu ujao, Mbeya City fc wanatazamiwa kuwa washindani wa ubingwa kutokana na wachezaji wake wa kikosi cha kwanza kubakia na kuongeza nguvu kidogo ikiwemo kumsajili mshambuliaji wa Kagera Sugar, Them Felix `Mnyama

WABUNGE VIJANA ,JOSHUA NASSARI NA STEPHEN MASELE KUKUTANA NA RAIS OBAMA LEO.

July 28, 2014


Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari  akizungumza wakati wa tafrija ya chakula cha jioni baada ya maafali ya kuhitimu mafunzo ya wiki tisa kwa viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika yaliyokuwa yakifanyika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani ,
Hotuba ya Mh,Nassari ilionekana kuwagusa wageni mbalimbali katika tafrija hiyo na wengine kushindwa kujizuia na kuanza kutokwa na machozi.

WATANGAZAJI WA RADI BREEZE FM WATEMBELEA COASTAL UNION LEO

July 28, 2014
MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKISISITIZA JAMBO KWENYE MAZUNGUMZO NA WAANDISHI WA HABARI WA RADIO BREEZE WALIOITEMBELEA KLABU HIYO LEO ALIYEVAA KOTI JEUSI NI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI SALIM BAWAZIRI NA KULIA NI MTANGAZAJI WA RADIO NA MHARIRI WA MICHEZO ALLEN MAKUNDI.

KUSHOTO MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKISISITIZA JAMBO NA WAANDISHI WA HABARI WA RADIO BREEZE YA TANGA WALIOITEMBELEA KLABU HIYO LEO


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA TZ NCHINI URUSI, NA WA UJERUMAN NCHINI TZ NA KUMKARIBISHA MPYA WA UJERUMAN

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA TZ NCHINI URUSI, NA WA UJERUMAN NCHINI TZ NA KUMKARIBISHA MPYA WA UJERUMAN

July 28, 2014

01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon Kochanke, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kujitambulisha kuanza kazi. Kushoto ni aliyekuwa Kaimu Balozi wa Ujeruman Tanzania, aliyemaliza muda wake. Hans Koeppel. Picha na OMR
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi, Luteni Generali Wyjones Matthew Kisamba, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kumuaga akielekea kuanza kazi. Picha na OMR
02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na  Balozi mpya wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon Kochanke, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kujitambulisha kuanza kazi.
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi, Luteni Generali Wyjones Matthew Kisamba, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
03
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na aliyekuwa Kaimu Balozi wa Ujeruman Tanzania, aliyemaliza muda wake, Hans Koeppel  wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake. Kushoto ni Balozi mpya wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke, aliyefika kujitambulisha kuanza kazi. Picha na OMR

Rais Kikwete aandaa futari kwa yatima, walemavu wa ngozi na watoto waishio kwenye mazingira magumu ikulu Dar es salaam

July 28, 2014

Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu  na viongozi wa vituo mbalimbali vya yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari  aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Vijana kutoka Chama cha Albino Wilaya ya Kinondoni wakimshukuru Mama Salma Kikwete kwa futari 
Vijana kutoka Chama cha Albino Wilaya ya Kinondoni wakipata picha ya pamoja na Mama Salma Kikwete baada ya  futari waliyoandaliwa na Rais Kikwete

Rais Kikwete akipita meza moja baada ya ingine kuwasalimia yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Kikwete akipita meza moja baada ya ingine kuwasalimia yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Kikwete akipita meza moja baada ya ingine kuwasalimia yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru kwa kuja viongozi wa vituo mbalimbali vya yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu katika futari  aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Mama Salma Kikwete akitoa neno la shukurani kwa waalikwa kwenye futari hiyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mtoto Khaitham Jumbe Jumbe ambaye alimuandalia zawadi
Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka kwa mtoto Khaitham Jumbe Jumbe mwenye umri wa miaka saba na mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi ya Yemen iliyoko Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka kwa mtoto Khaitham Jumbe Jumbe mwenye umri wa miaka saba na mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi ya Yemen iliyoko Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Aliyeketi kushoto ni Bi. Mwajuma Hassan wa Chama cha Albino Wilaya ya Kinondoni.

Wageni waalikwa wakifurahia zawadi walizopewa kwenye futari hiyo
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Kikwete akipakua futari  Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakiswali swala ya Magharibi wakati wa  futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni.
PICHA NA IKULU

KASSIM MGANGA KUACHIA VIDEO YA MOTOMOTO.

July 28, 2014
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
MSANII wa Mziki wa Bongo Fleva Kassim Mganga “Tajiri wa Mahaba” amesema mipango ya kutoa video ya wimbo wake mpya wa “Motomoto” imekamilika wa asilimia kubwa na hivyo muda wowote huenda ikaachiwa kwa mashabiki wake kwa ajili ya kuiona.

Wimbo huo wa Moto Moto umetayarishwa na Banny Record chini ya Sheby Cleverly na Video yake imefanywa na Ogopa yenye makazi yake nchini Nairobi Kenya kwa kiwango cha hali ya juu.

Akizungumza jana , Kassim alisema wimbo huo wenye asili ya ngoma za kitanzania na mchanyakio aliuachia wiki mbili zilizopita hivyo anaamani utakuwa tishio kwenye tasnia ya mziki huo hapa nchini.

Akizngumzia mziki huo hapa nchini, Kassim alisema umekuwa sana kwa sababu wanamuziki wanajulikana na kupata mafanikio makubwa ikiwemo kusaidia jamii zao na kujikwamua kimaisha hivyo wasanii wanapaswa kuuheshima.

Hata msanii huyo aliiomba serikali kuweka ulinzi wa kazi za wasanii ili waweze kunufaika na kazi zao ipasavyo hali itakayochangia kuongeza pato lao na Taifa kwa ujumla katika harakati za kuwapa maendeleo.

     “Tunaiomba serikali iweke mkono wake katika kuwasaidia wasanii wa mziki huo ili waweze kufaidika na kazi hizo kwa kuweka mazingira mazuri yanatayowawezesha kupata mafanikio “Alisema Kassim.

Aidha pia alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuweka mipango mizuri ambayo imewapa mafanikio wasanii wa mziki huu hapa nchini “Alisema Kassim.