BIL 860 ZINATUMIKA UJENZI MIRADI YA DHARURA NCHINI -ENG MOHAMED BESTA
habari
MAKUBALIANO YA NM-AIST NA ECSA KUKUZA TEKNOLOJIA BUNIFU ZA KIAFYA
habari
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto) na Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini( ECSA) Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia,) wakisaini hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika Afya leo Oktoba 28,2025.
.....
TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) imesaini hati ya makubaliano na Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA) yenye lengo la kushirikiana katika tafiti, ubunifu na uenezaji wa teknolojia bunifu katika sekta ya afya.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo Oktoba 28,2025, Makamu Mkuu wa Taasisi, Prof. Maulilio Kipanyula, alisema NM-AIST imejikita katika kuzalisha teknolojia bunifu na kufanya tafiti zenye matokeo chanya katika jamii.
Makubaliano hayo yameainisha maeneo kumi ya ushirikiano, yakiwemo tafiti za pamoja, matumizi ya teknolojia za kidijitali katika mifumo ya afya, na kuimarisha ubunifu unaolenga kuzalisha majawabu ya changamoto za kiafya barani Afrika.
“Sisi kama taasisi ya sayansi, teknolojia na ubunifu, tumejidhatiti kuzalisha teknolojia na majawabu yatakayosaidia kuimarisha mifumo ya afya nchini na barani Afrika. ESCAC ipo katika nchi nyingi, hivyo kwa NM-AIST hii ni fursa ya kushirikiana, kujenga mifumo ya afya, na kupeleka majawabu ya kidijitali katika sekta ya afya,” alisema Prof. Kipanyula.
Kwa mujibu wa Prof. Kipanyula, NM-AIST ni taasisi yenye idadi kubwa ya hati miliki (patents) nchini zipatazo 33 ambapo baadhi zinahusiana moja kwa moja na masuala ya afya, ikiwemo teknolojia ya lishe kupitia uji chapchap, mfumo wa kutambua picha za X-ray kwa kutumia akili unde, gauni maalum la theatre, na dripu bunifu inayochanganya mchanganyiko wa dawa kwa wakati mmoja.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa ESCAC, Dkt. Ntuli Kapologwe, alisema makubaliano hayo ni ya kimkakati na yanatarajiwa kuleta matokeo chanya katika muda mfupi, ikiwemo kuanzishwa kwa kituo cha umahiri wa sayansi, teknolojia, ubunifu na utafiti.
“Tumeweka mkazo katika diplomasia ya sayansi na afya, ili nchi wanachama tisa zinufaike na ubunifu wa NM-AIST. Hali ya udumavu katika ukanda wetu ni asilimia 30 hadi 35, hivyo tunahitaji teknolojia za lishe kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema Dkt. Ntuli.
Aliongeza kuwa ushirikiano huo utahusisha pia matumizi ya teknolojia za kidijitali na akili uunde katika utoaji wa huduma za afya, ustawi wa jamii na lishe, sambamba na kuimarisha dhana ya Afya Moja (One Health) kwa nchi zaidi ya 55 barani Afrika.
Kwa sasa, NM-AIST inahudumia wanafunzi kutoka nchi 17 za Afrika, huku ECSA ikijumuisha wanachama kutoka nchi 12, jambo linalotarajiwa kuongeza wigo wa ushirikiano na athari chanya kwa afya ya jamii katika bara zima.
 
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto) na Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini( ECSA) Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia,) wakisaini hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika Afya leo Oktoba 28,2025.

Makamu Mkuu wa NM-AIST, Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto), akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia), ikiwa ishara ya kumbukumbu mara baada ya hafla ya kusaini hati ya makubaliano, Oktoba 28, 2025, Arusha.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto), na Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia), wakionyesha hati ya makubaliano baada ya kuiweka saini, Oktoba 28, 2025, Arusha.
 
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi naTeknolojia ya Nelson Mandela, Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto) akiongea wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano, Oktoba 28, 2025, Arusha.
 
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia), akiongea wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano, Oktoba 28, 2025, Arusha, kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula.
 
Makamu Mkuu wa NM-AIST, Prof. Maulilio Kipanyula (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Jumuiya ya Afya Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Dkt. Ntuli Kapologwe (kulia),pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya NM-AIST na ECSA mara baada ya hafla ya kusaini hati ya makubaliano, Oktoba 28, 2025, Arusha.
Mradi wa WLER wabadilisha mitazamo ya kijamii Kitunda
habariMIAKA 4 YA RAIS SAMIA, BIL 712 ZATEKELEZA MIRADI YA TANROADS MOROGORO-ENG MKUMBO
habariMCHENGERWA AFUNGA KAMPENI KWA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUZINGATIA AMANI
habari

WACHAMBUZI WA SIASA NA DIPLOMASIA WATOA WITO KWA VIJANA NA WANANCHI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMIU KWA UZALENDO NA BUSARA
habari
Na Rahel Pallangyo
Wachambuzi wa masuala ya siasa, diplomasia, na maendeleo wametoa wito kwa vijana na wananchi kwa ujumla kutumia mitandao ya kijamii kwa busara na uzalendo, huku wakisisitiza umuhimu wa kufanya tathmini ya kina kuhusu ukweli wa taarifa wanazopokea na kusambaza, hususan katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi.
Wito huo umetolewa Oktoba 26, 2025, jijini Dar es Salaam, wakati wa mdahalo wa 'Wajibu wa Kidijitali kwa Amani ya Nchi Kabla, Wakati na Baada ya Uchaguzi” uliofanyika katika Ukumbi wa American Corner, Makumbusho ya Taifa
Mchambuzi wa masuala ya diplomasia na siasa, Abdulkarim Atik, amewataka vijana nchini kufanya tathmini ya kina kuhusu ukweli wa taarifa wanazopokea na kusambaza kupitia majukwaa ya kidijitali. Amesema lengo ni kuepusha taharuki na migawanyiko katika jamii inayosababishwa na habari za uwongo na propaganda zenye lengo baya.
"Ikiwa vijana watatambua ukweli wa taarifa wanazopata, itawasaidia kufanya maamuzi sahihi na kuchangia katika kulinda amani ya nchi hususan kipindi cha uchaguzi," alisisitiza Atik.
Naye Mwandishi wa habari wa Crown Televisheni, Imani Luvanga, amesisitiza kuwa mitandao ya kidijitali ni nyenzo muhimu ya mawasiliano na taarifa, na kwamba siyo mibaya kama inavyodhaniwa. Alifafanua kuwa changamoto kubwa ipo kwa watumiaji, ambao mara nyingi hueneza taarifa zisizo sahihi na zenye kuchochea migogoro.
Luvanga alieleza kuwa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii yanaweza kuleta mabadiliko chanya, yakiwemo maendeleo ya kiuchumi. Alisisitiza umuhimu wa watu kujitambua wanapotumia mitandao hiyo, kwa kuelewa sababu za kuitumia, aina ya taarifa wanazohitaji, na faida wanazotarajia kunufaika nazo.
Kwa upande wake, mdau wa siasa na maendeleo, Reeves Ngalemwa, alisisitiza umuhimu wa kuweka msingi imara wa uzalendo tangu utotoni.
"Ni muhimu kuweka mazingira ya kuwaandaa watoto kujifunza uzalendo tangu wakiwa shule za msingi ili wakue wakiwa na mapenzi ya kweli kwa nchi yao," alisema Ngalemwa.
Aliongeza kuwa lengo la kuanza kuwajenga watoto katika hatua za awali ni kuandaa kizazi chenye uelewa mpana wa masuala ya kitaifa, kinachotambua lipi ni sahihi na lipi si sahihi, hususan katika zama hizi za kidijitali. Ngalemwa alihitimisha kwa kusema kuwa msingi huu imara utasaidia kujenga Taifa lenye vijana wanaopenda na kulinda maslahi ya nchi yao.
Mchambuzi wa masuala ya vyombo vya habari na mpiga picha maarufu, Isa Michuzi, amesisitiza kwamba wananchi wanatakiwa kujua na kuyachunguza kwa kina mambo mengi yaliyomo katiukja mitandao kwani mengine ni propaganda za chuki.
"Watu wanastahili kuangalia kwa umakini sana. Propaganda inaweza kuwa nzuri au mbaya. Tumefika hapa si kwa bahati mbaya, ni matokeo ya kuruka hatua. Kila mtu awe mlinzi wa taifa," alieleza Michuzi.
Alionya kuwa kutokuwa na uangalifu katika kusambaza taarifa hufanya jamii iingie katika migogoro isiyo ya lazima.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TBN , Beda Msimbe alizungumzia haja ya vijana wa sasa kuwa na ndoto zilizojengwa imara katika muktadha wa kitaifa na uzalendo huku wakiangalia mambo katika upana wake na si kuchukua tukio moja tu.
Alisema vijana wanahitaji msingi imara ili maamuzi yao yawe ya kusonga mbele badala ya kuumiza taifa. Lengo ni kuweka maslahi ya Taifa mbele katika matumizi yao ya mitandao ya kijamii na katika kufanya maamuzi ya kisiasa.
Mdahalo huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti Jukwaa la Wachambuzi, Magid Mjengwa ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wahariri wa mawasiliano ya kidijitali, wanabloga kutoka Taasisi ya Tanzania Bloggers Network (TBN), wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia, wadau wa amani, na waandishi wa habari.
REA YAWASHA UMEME KWENYE SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI MTWARA
habari
TANZANIA YAING’ARA KIKANDA MASHINDANO YA UANDISHI WA INSHA ZA EAC NA SADC
habari 
 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Hussein Omar,akikabidhi vyeti mbalimbali kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2023 na 2024 hafla iliyofanyika leo Oktoba 26,2025 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa tuzo kwa wanafunzi ambao ni washindi wa uandishi wa insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2023 na 2024 huku ikiwasisitiza kutumia uwezo wao binafsi katika kuandika insha badala ya kutegemea matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba.
Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo hizo leo Oktoba 26,2025 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Hussein Omar amesema kuwa uandishi wa insha ni sehemu ya mafunzo na inawajengea wigo mpana wa kujifunza masuala muhimu yanayohusu jumuiya hizo.
“Nawaomba wanafunzi kujiepusha na matumizi ya Akili Mnemba katika kuandika insha zenu kwa sababu kwanza itakuwa sio uhalisia wa uandishi wenu, lakini pia ni aina ya udanganyifu ambao utawatoa kwenye kinyang’anyiro cha ushindani,” amesema Dkt.Omar
Aidha, amewataka wanafunzi kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kwa ufasaha katika kufanya tafiti ili kuongeza maarifa kuhusu shughuli, malengo na mipango ya jumuiya hizo mbili.
Aidha amesema kuwa ushindi huo ni ishara ya ubora wa elimu nchini na juhudi za pamoja za walimu, wakuu wa shule, na wizara husika katika kuandaa wanafunzi wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kujenga hoja.
“Ninafarijika kuona wanafunzi wetu wanaongoza katika ngazi za kikanda, jambo linaloonyesha kuwa Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika kukuza elimu bora na ubunifu kwa vijana wake,” amesema
Pia ametoa wito kwa wakuu wa shule na waratibu wa insha kuhakikisha wanafunzi wote wanashiriki kikamilifu katika mashindano hayo kwa kufuata miongozo iliyowekwa, huku akisisitiza umuhimu wa kuhamasisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu kushiriki.
“Wakuu wa shule ni wasimamizi wakuu wa mashindano hayo, hivyo wanapaswa kuhakikisha wanafunzi wanashiriki kikamilifu na kufuata taratibu za uandishi ili kuepuka kuondolewa katika hatua za usahihishaji,” ameongeza Dkt.Omar
Kwa upande wake Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa,amesema mashindano hayo yamekuwa kichocheo kikubwa cha kukuza umahiri wa wanafunzi katika uandishi, utafiti, na ufahamu mpana wa masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa katika jumuiya hizo mbili za kikanda.
“Mashindano hayo yamekuwa chachu kwa vijana kufanya utafiti, kujifunza na kuelewa vyema hatua za uimarishaji mahusiano baina ya nchi wanachama na umuhimu wa muunganiko huu wa kikanda,” amesema Dkt. Mtahabwa.
Dkt. Mtahabwa amewapongeza washindi wote wa kitaifa na kikanda, akiwemo Hollo Alice Kadala kutoka Shule ya Sekondari Msalato, aliyeshika nafasi ya tatu kitaifa na ya tatu kikanda katika mashindano ya SADC mwaka 2023, pamoja na Blandina Kabalemesa wa Shule ya Sekondari Anwarite, aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa na ya nne kikanda katika mashindano ya EAC mwaka 2024.
“Hawa wanafunzi ni mfano bora wa kuigwa. Ushindi wao unaonyesha juhudi na ubora wa elimu yetu. Tunawapongeza walimu, wazazi na waratibu wote kwa malezi bora na mwongozo uliowezesha mafanikio haya,” amesema
Awali, Mratibu wa Insha kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Bi.Matuha Masati,ameipongeza Sekretarieti ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Nchi za SADC Kwa kuendesha Mashindano ya Uandishi wa Insha kwani yamekuwa chachu Kwa vijana kufanya utafiti,kujifunza na kufahamu vizuri mchakato na hatua mbalimbali za uimarishaji Kwa nchi wanachama.
Amesema kuwa mashindano hayo husimamiwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) kwa insha za nchi za Afrika Mashariki (EAC) na za SADC husimamiwa na Wizara ya Elimu kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar.
Amesema kuwa jumla ya wanafunzi 1,096 walishiriki katika mashindano ya uandishi wa insha za EAC na SADC mwaka 2023, wakiwemo wanafunzi 557 wa EAC na 539 wa SADC, huku mwaka 2024 ukishirikisha wanafunzi 892, kati yao 243 wa SADC na 649 wa EAC.
“Kwa sasa, Wizara inatoa tuzo kwa washindi 10 bora wa kitaifa kwa kila shindano, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walipewa tu washindi watatu wa juu. Hatua hii imeongeza hamasa kubwa kwa wanafunzi kushiriki,” amesema

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Hussein Omar,akizungumza wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2023 na 2024 hafla iliyofanyika leo Oktoba 26,2025 jijini Dodoma.
 
Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene M. Mtahabwa,akizungumza wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2023 na 2024 hafla iliyofanyika leo Oktoba 26,2025 jijini Dodoma.
 
Mratibu wa Insha wa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi. Matuha Massati, akitoa maelezo wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2023 na 2024 hafla iliyofanyika leo Oktoba 26,2025 jijini Dodoma.

Hollo Alice Kadala kutoka Shule ya Sekondari Msalato, aliyeshika nafasi ya tatu kitaifa na ya tatu kikanda katika mashindano ya SADC mwaka 2023,akizungumza wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2023 na 2024 hafla iliyofanyika leo Oktoba 26,2025 jijini Dodoma.
  
Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Hussein Omar, (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2023 na 2024 hafla iliyofanyika leo Oktoba 26,2025 jijini Dodoma.