CUF MKINGA WAANZA KUJIPANGA NA UCHAGUZI MKUU.2015

July 29, 2013

Na Oscar Assenga,Mkinga.

CHAMA cha Wananchi CUF wilayani Mkinga kimeelezea mikakati yake ya kufanya mikutano ya hadhara katika kata zote zilizopo wilayani humo lengo likiwa kukiimarisha chama hicho pamoja na kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ili kuchukua kata zote.

Akizungumza na BLOG HII,Mwenyekiti wa Chama hicho,Mauya Kileo amesema anaamini lengo lao litafanikiwa kutokana na kukabalika vilivyo na wananchi maeneo mbalimbali wilayani humo kitendo ambacho kiliwawezesha chama hicho kupata kata saba kati ya 21 zilizopo.

Kileo amezitaja kata ambazo zimechukuliwa na chama hicho wilayani humo kuwa ni Mtimbwani, Kwale,Manza ,Boma,Doda,Moa na Duga Sigaya na kueleza mikakati yao ni kuongeza idadi ya kata kwenye uchaguzi huo mkuu kwani hilo linawezekana kutokana na mshikamano walionao.

Aidha aliwataka wanachama wa chama hicho kuendelea kuonyesha mshikamano ili kuweza kufanikisha malengo yao ya siku moja kuongoza halmashauri yaweze kufanikiwa.

JULIO:COASTAL UNION TUTAKUTANA KWENYE LIGI KUU.

July 29, 2013
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
KOCHA Msaidizi timu ya Simba,Jamhuri Kiwelu "Julio"ameipiga vijembe timu ya Coastal Union ya Tanga kwa kusema yenye ni miongoni mwa makocha waliotoa mchango mkubwa kwenye timu hiyo na kuiambia kuwa watakutana kwenye ligi.

Julio alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Blog hii mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Coastal Union,mchezo uliomalizika kwa Simba kukubali kichapo cha bao 1-0 bao ambalo lilifungwa na Chrispian Udula aliyetumia uzembe wa mabeki wa Simba kupachika wavuni bao hilo.

Alisema mchezo huo ulikuwa mzuri na wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kucheza vema lakini pia ushindi huo wa wapinzani wao umewapa hasira ya kutaka kulipiza kisasi kwao kwenye mechi ya ligi kuu kwani huo ndio mpango wao ni kucheza ligi kwa mafanikio msimu ujao.

Kocha huyo alisema walifurahi kucheza mechi hiyo ambayo ilikuwa kipimo cha kuangalia aina ya uchezaji inaoucheza timu yao huku akitolea visingizio kuwa mwamuzi wa mchezo huo,Isihaka Shirikisho kuwa alichangia wao kukosa ushindi kwenye mchezo huo.

Kwa upande wake,Kocha Mkuu wa Coastal Union,Hemed Morroco alisema huo ni mwanzo mzuri kwa timu hiyo kwani malengo yao makubwa ni kuhakikisha wanazifunga timu zote zitakazocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani na ugenini ili kuweza kurudisha heshima ya mwaka 1988 ya kuchukua ubingwa wa ligi hiyo.

Mwisho.
July 29, 2013
KOCHA WA SIMBA JAMHURI KIWELU "JULIO'AKIWA SAMBAMBA NA MAKOCHA WA COASTAL UNION YA TANGA .

BENCHI LA UFUNDI LA COASTAL UNION LIKIWA NA WACHEZAJI WAKE.

WACHEZAJI WASIMBA WAKIUFUATILIA MCHEZO HUO.

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA,OMARI NUNDU AKIIKAGUA TIMU YA SIMBA KABLA YA KUANZA MCHEZO HUO WA JANA.

KIKOSI CHA COASTAL UNION YA TANGA KILICHOISHIKISHA ADABU SIMBA KWA KUIFUNGA BAO 1-0.


MKUU WA KAZI PROMOTA BONGA NAYE PIA ALIKUWEPO KUANGALIA MCHEZO HUO.

PICHA ZA MATUKIO YA WARSHA YA SIKU MBILI ILIYOHUSU HUDUMA ZA WAZEE KWENYE MAENEO YAO YA UTENDAJI

July 29, 2013
WASHIRIKI WA WARSHA HIYO WAKIIFUATILIA

WASHIRIKI WAKIWA MAINI KUFUATILIA MIJADALA KWENYE WARSHA HIYO.






Na Oscar Assenga,Tanga.
WATENDAJI wa Serikali wametakiwa kuwa na huruma kwa wazee hasa katika utoaji huduma mbalimbali ikiwemo za matibabu,malazi na mahitaji yao muhimu kwani wengi wao hushindwa kupewa kipaumbele wanapohitaji huduma hizo kutokana aina ya maisha waliyonayo kwenye jamii zinazowazunguka.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na washiriki kwenye warsha ya siku mbili iliyokuwa ikihusu huduma za wazee kwenye maeneo ya watendaji zinapewa kipaumbele iliyoratibiwa na asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Old Nguvumali Women Centre (Ongwece) yenye makazi yake nguvumali jijini Tanga ambapo ilihusisha watendaji wa kata kutoka halmashauri ya jiji la Tanga na wakuu wa idara.

Akizungumza katika warsha hiyo,Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mabokweni,Hamza Omari alisema  serikali haina budi kuhakikisha inawasaidia wazee wa aina zote hapa nchini kwa kutenga bajeti maalumu ambayo itawahudumia kwenye mahitaji yao muhimu kutokana na wazee wengine kutopata msaada kwenye jamii zao.

Masoud alisema wazee wengi hawana utambulisho wa matibabu na kusema endapo watafanikiwa kuwekewa utaratibu wa kuwa na vitambulisho itasaidia kuondokana na adha ambazo wamekuwa wakikutana nazo mara kwa mara wanapokuwa wakihitaji huduma hiyo muhimu

Aidha aliongeza kuwa wakati umefika kwa jamii kubadilika na kuwathamini wazee ikiwemo kuacha kusema wazee wamepitwa wakati kwani hata nao watakuja kuwa miongoni mwao siku zijazo na huenda wakakutana na hali kama hizo endapo watashindwa kuwajali na kuwaheshimu wakati huu.

Naye Hanafi Masoud ambaye ni Ofisa Mtendaji kata ya Chumbageni alisema tatizo kubwa lililopo kwenye jamii nyingi hapa nchini ni kupotoka kimaadili na kushindwa kuwaheshimu na kuwapa kipaumbele wazee kama ilivyokuwa  hapo zamani.

Aidha aliiomba asasi zisizo za kiserikali ziendelee kuhamasisha jamii ili kuweza kuona umuhimu wa wazee kutokana na wengi wao kuwa na mchango mkubwa sana lakini pia akiitaka serikali kuhakikisha inawahudumia wazee wasiojiweza kwa asilimia mia moja.

Kwa upande wake,Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Kassim Sengasu alishauri jamii kuangalia mfumo gani ambayo unaweza kutumika kuwaangalie wazee baada ya kustaafu kwa kushirikiana na taasisi za kidini kwani zikiwekwa pembeni hao wazee watakuwa kwenye hali ngumu sana.

Hata hivyo,Mwezeshaji wa Warsha hiyo,Lucas Munako alisema dhana ya uzee ipo rasmi kwenye mfumo wa serikali na imejikita katika umri kwa mujibu wa miongozo iliyopo kuanzia miaka sitini na kutaka wazee wangewekewa utaratibu mzuri wa kuwawezesha ili kuweza kujikimu katika maisha yao.

Awali akizungumza ,Mratibu wa Asasi hiyo,Devina Kibaja alisema lengo la warsha hiyo kwa watendaji hao ni kuweza kuwapa uelewa wa juu ya umuhimu wa wazee katika maeneo yao ya kiutendaji wanayoyaongoza katika sehemu zao wanazotoka.

Mwisho.