COASTAL UNION YAIKALISHA MBEYA CITY.YAIPIGA MABAO 2-0

February 22, 2014


NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

MABAO mawili yaliyofungwa na Mohamed Mtindi yalitosha kuipa ushindi timu ya Coastal Union kwenye mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Mbeya City mchezo uliochezwa leo kwenye dimba la CCM Mkwakwani.


Bao hizo zilifungwa kwenye dakika za 82 na 89 ziliweza kuinua shangwe na nderemo kwa wapenzi na mashabiki wa soka mkoani Tanga ambao walijitokeza kushuhudia mchezo huo.



Mchezo huo ambao ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu ambapo mpaka timu zote zinakwenda mnapumziko hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzie.



Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kuingia uwanjani hapo zikiwa zimefanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake ambapo kwa upande wa Coastal Union waliwatoa Ally Iddy,Crispian Odulla na Ayoub Yahaya ambao nafasi zao zilichukuliwa na Suleimani Selembe,Mohamed Mtindi,Yayo Lutimba na Keneth Masumbuko.



Kwa upande wa Mbeya City waliwatoa Mwegane Yeya,Jeremia John nafasi zao zilichukuliwa na Fransisi Casto na Richard Peter ambao waliweza kucheza vema licha ya kushindwa kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo.



Vikosi vilivyozeshwa leo kwa upande wa Coastal Union iliwachezesha Shabani Kado,mbwana hamisi,abdi banda,juma nyoso,yusuph chuma,jerry santo,Daniel lyanga,ally iddi,haruna moshi,crispian odulla na ayoub yahya.



Kwa upande wa Mbeya City iliwachezesha Davidi buruani,azizi sibo,hasan mwasapili,deogratis Julius,yusuph abdallah,Anthony matogolo,mwagane yeya,steven mazand,paul nonga,jeremia john na peter mapunda.

Picha na matukio mengine ya mechi hii yatakujia muda sio mrefu.