MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi jana jioni amekarimu
wageni wafanyabiashara wa Ufaransa waliopo katika wiki ya Ufaransa
nchini. Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika katika
hoteli ya Serena, wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa hamsini ya
Ufaransa wakiongozwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula
huku wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Zoro. Akizungumza
kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hicho, Dk. Mengi alisema
katika hoteli ya Serana ikiwa ni njia mojawapo ya kuonesha shukurani
kwa wafanyabiashara hao kuamua kuja nchini kuwekeza. Alisema jioni hii
ya leo hana maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya kuwakarimu wageni hao
ambao ni muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya uchumi na taifa kwa
ujumla.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi (katikati) akibadilishana mawazo
na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hafla maalum
ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili ya ugeni huo katika hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Balozi wa
Ufaransa nchini, Malika Berak.(Picha zote na Thebeautytz.com)
“Ujio wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia hii ndiyo tunayoita win win situation”
alisema Dk Mengi na kuongeza kuwa ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa
teknolojia wa taifa hili. Aidha alisema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni
mwa mataifa yenye msuli wa kiuchumi kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia
Watanzania kuwa na rafiki mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia.
Alisema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa
sasa utaendelezwa zaidi. Aliwatakia wageni wake chakula chema.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiwakaribisha wafanyabiashara
kutoka nchini Ufaransa kwenye halfa ya chakula cha jioni aliyoiandaa
maalum kwa wafanyabiashara hao katika hoteli ya Serena jijini Dae es
Salaam.
Mgeni rasmi ambaye alikuwa Balozi wa Ufaransa
nchini, Malika Berak alisema kwamba amefurahishwa sana na ukarimu wa Dk
Mengi na kusema kwamba yeye anaamini biashara na urafiki ni kitu muhimu
katika kuimarisha mahusiano.
“ …Business and friendship goes Together..”
alisema balozi huyo kwa lugha ya kiingereza na kuongeza kwamba kutokana
na chakula hicho anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na
Tanzania si wa kubahatisha unakua. Katika chakula hicho miongoni mwa wa
kampuni zilizofika ni Airbus, Siemens, General electrical na kadhalika.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi na Mgeni rasmi Balozi wa
Ufaransa nchini, Malika Berak (kulia) wakiendelea kupokea wageni
mbalimbali kwenye hafla ya chakula cha jioni aliyoandaa kwa
wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akitoa neno la ukaribisho kwenye
‘cocktail’ kabla ya kushiriki chakula cha jioni na wafanyabiashara
kutoka nchini Ufaransa.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Eng. Raymond Mbilinyi
(kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika halfa
ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Dk.Mengi kwa wafanyabiashara
kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce Mhaville (katikati) wakifurahi jambo
na Mkurugenzi wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga
katika hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini
Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
wa Masoko wa IPP Ltd, Bi. Joyce Luhanga (kushoto) akielezea jinsi
‘Application’ ya ITV Tanzania inavyofanya kazi kupitia simu za viganjani
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga
(kulia) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka
Ufaransa iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar
es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One Joyce
Mhaville.
‘Meet
and Greet’ ikiendelea kwa wenyeji na wafanyabiashara kutoka makampuni
makubwa nchini Ufaransa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa
na Dk.Mengi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji
mkongwe nchini Mzee Zahir Ally Zoro akitumbuiza kwenye hafla ya chakula
cha jioni kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyoandaliwa na
Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meza
kuu kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi wa
ufaransa Bi. Beatrice Alperte, mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini,
Malika Berak, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi pamoja
na Mshehereshaji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta
Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye
akisherehesha wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wafanyabiashara
kutoka Ufaransa iliyoandaliwa na Dk Mengi kwenye hoteli Serena jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiteta jambo na mgeni rasmi
Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak wakati wa hafla ya chakula cha
usiku kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa iliyofanyika usiku wa
kuamkia leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akizungumza na wafanyabiashara
kutoka nchini Ufaransa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha
juu na chini ni wafanyabiashara kutoka makampuni makubwa nchini
Ufaransa wakijumuika na wenyeji wao katika hafla ya chakula cha jioni
iliyoandaliwa na Dk.Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.