BOHARI YA DAWA (MSD) YAKARABATI GHALA LA DAWA HOSPITALI YA MIREMBE MKOANI DODOMA

April 18, 2017
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya Mirembe mjini, Dodoma leo lililokarabatiwa na MSD. 

DAWASA YAKAMILISHA KAZI YA UPANUZI WA MTAMBO WA RUVU JUU: SASA WAZALISHA LITA MILIONI 196 ZA MAJI SAFI NA SALAMA

April 18, 2017
Laini ya Umeme unaotoka Chalinze (Sub-Station) na kufika eneo la Mtambo wa Ruvu Juu lililopo Mlandizi Mkoani Pwani.
Laini ya Umeme unaoingia kutoka Chalinze (Sub-Station) na kufika eneo la Mtambo wa Ruvu Juu lililopo Mlandizi Mkoani Pwani ambapo uunganishaji wake sasa umeshakamilika na umeme umewashwa.
Moja ya Transfoma mpya zilizopo katika eneo la Mtambo wa Ruvu Juu ambalo linatumika kutoa umeme unaotumika kwenye mitambo katika eneo hilo.
Moja ya mitambo ya maji katika eneo la Ruvu Juu kama inavyoonekana, mitambo hii ni mipya na kwa sasa ndiyo itasaidia kuongeza uzalishaji wa maji toka lita milioni 82 hadi lita milioni 196 kwa siku.

KIPINDI CHA CLOUDS 360 KILIPORUSHWA MUBASHARA KUTOKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

April 18, 2017
Gari Maalumu la kurusha matangazo ya moja kwa moja la kituo cha Luninga cha Clouds likiwa katika eneo la Serengeti kwa ajili ya kurusha matangao ya moja kwa moja ya kipindi cha Clouds 360.
Watangazaji wa Kipindi cha Clouds 360 ,Sam Sasali na James Tupatupa wakifungua kipindi katika eneo ambalo ni makazi ya Viboko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Watangazaji wa Clouds 360 ,Sam Sasali na James Tupatupa wakiongea na Meneja Mawasilino wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza jambo na watangazaji hao wakati wakifanya mahojiano.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa akizungumza jambo na Mtangazaji Sam Sasali.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema akizungumzia sifa za hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa .
Mwekezaji katika Sekta ya Utalii,Wily Chamburo (wa pili toka kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Ibrahim Musa (aliyevaa koti) pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,Wiliam Mwakilema (kushoto) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA ,Pascal Shelutete.(kulia).
Watangazaji Baby Kabaye na Hassan Noma wakifanya mahojiano na Mwekezaji katika Sekta ya Utalii,Wily Chamburo wakati kipind cha Couds 360 kiliporushwa moja kwa moja kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Watangazaji Baby Kabaye na Hasan Ngoma wakifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa wakati kipindi cha Clouds 360 kiliporushwa moja kwa moja kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mtangazaji wa Sport 360 katika kipindi cha Clouds 360 ,James Tupatupa akifanya mahojiano na Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete wakati akizungumzia Utalii wa kimichezo pamoja na namna TANAPA inavyoshiriki katika kukuza Michezo mbalimbali nchini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitoa neno la Shukrani wakati kipindi cha Clouds 360 kilipokuwa kikihitimisha ziara yake katika Hifadhi ya Taifa za Serengeti.
Wadau waliokuwepo katika shughuli nzima ya urushwaji wa kipindi cha Clouds 360 wakifuatilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea.
Watangazaji wa Kipindi cha Clouds 360 wakiwa katika picha ya pamoja na Wadau mara baada ya kuhitimisha ziara ya urushwaji wa kipindi hicho katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MKURUGENZI WA JIJI ARUSHA ATOA SEMINA KWA WATENDAJI WAKE

April 18, 2017
 Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athumani Juma Kihamia

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg Athumani Juma Kihamia amefanya kikao na watumishi wa serikali katika Kata ya Muriety na Terati na kuzungumza mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha utendaji kazi wao.

Kihamia amesema kuwa lengo hasa la kuonana na watumishi hao ni muendelezo wa ziara yake ya kutembela kila Kata na kuwakumbusha watumishi hao jinsi ya kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Raisi John Magufuli.

“”Siyo kwamba watumishi wangu wa Halmashauri hawafanyi kazi Bali ni kuwakumbusha majukumu yao katika kutumikia wananchi hasa katika kasi ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu ambayo inatutaka tuwe karibu zaidi na wananchi wetu na Mimi kama Mtendaji mkuu lazima nisimamie kikamilifu “” Alisema Mkurugenzi Kihamia

Vile vile amesema kuwa watendaji wa serikali wanatakiwa wajitume kwa nguvu zote wasisubiri mpaka viongozi wa juu wafike kwenye maeneo yao na wananchi walalmike wakati kuna kiongozi katika eneo hilo ambaye analipwa na serikali ili kusaidia wananchi.

“” Hatutaki Mwananchi atoke kwenye Kata mpaka kwa mkuu wa Mkoa au mkuu wa Wilaya wakati kwenda kumlalamikia masuala madogo madogo wakati kuna kiongozi ambaye tumemuweka ili atatue kero akitokea Mtumishi wa hivyo ajue kwamba hatoshi kuongoza wananchi “”Alisema Kihamia

Ameongeza kuwa kwasasa anahakikisha Huduma zinaboreshwa katika jiji la Arusha kwa kumjengea Mtumishi uzoefu wa kufanya kazi bila kuogopa changamoto zilizopo na kuwa jasiri wakati anaongoza wananchi kwenye maeneo yao.

Hata hivyo amewagiza watumishi hao wa serikali wakiwemo watendaji kutekeleza kwa muda uliowekwa mambo muhimu kama vikundi vya vijana na Wanawake, kuainisha maeneo ya biashara na idadi yake ikiwemo mabango Na maduka yote,majengo na miradi viporo pamoja na kuainisha Yale maeneo yote ya wazi.

MWIMBAJI JIMMY GOSPIAN ASHINDA TUZO YA ZABURI AWARDS 2016/17 KANDA YA ZIWA

April 18, 2017
Mwimbaji chipukizi wa muziki wa Injili Jijini Mwanza, Jimmy Gospian (kushoto), ameibuka mshindi kwenye Tuzo za ZABURI AWARDS 2016/17 zilizotolewa jana kwa waimbaji wa Injili Kanda ya Ziwa na Kampuni ya Famara Entertainment, Uwanja wa CCM Kirumba.

Gospian kutoka ngome ya BMG, aliibuka mshindi katika kipengere cha Mwimbaji Bora Chipukizi wa Kiume ambapo washindi wa tuzo hizo walipatikana kwa wingi wa kura za mashabiki.

Washindi wengine kwenye tuzo hizo ni; Kwaya Bora-Mwanza Singers, Albamu Bora-Pokea Sifa ya Rebeka Pius, Mwimbaji Bora wa Kike-Betty Lucas, Mwimbaji Bora wa Kiume-Derick Ndonge, Mwimbaji Bora Chipukizi wa Kike-Julieth Busagi, Kundi Bora-Kihayile Group na Tuzo ya Heshima-AIC Chang'ombe Vijana Choir.

Mbali na utoaji wa tuzo hizo, pia kulikuwa na uzinduzi wa Albamu ya PAZIA LA HEKALU iliyoimbwa na kwaya ya AIC Chang'ombe Vijana Choir
Jimmy Gospian akipokea tuzo yake, Mwimbaji Bora Chipukizi wa Kiume
Jimmy Gospian anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo wimbo uliomtambulisha vyema uitwao, Nakujua Bwana
Jimmy Gospian (kushoto) akipokea pongezi kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Famara Entertainment
Baadhi ya waimbaji wa Kwaya ya AIC Chang'ombe Vijana Choir

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye utoaji wa tuzo hizo
JACQUELINE NTUYABALIWE ANYAKUA TUZO ZA A-PRIME DESIGN

JACQUELINE NTUYABALIWE ANYAKUA TUZO ZA A-PRIME DESIGN

April 18, 2017
Mrembo wa Tanzania mwenye tamaa ya kuwa na himaya ya samani za kimataifa kupitia kampuni yake, kama alivyowahi kuelezwa na jarida la Forbes hivi karibuni, Jacqueline Ntuyabaliwe ametwaa tuzo mbili za ubunifu kupitia kampuni ya Molocaho by Amorette. Ushindi wake huo unamuingiza katika kundi la watu wenye ubunifu mkubwa wa bidhaa za majumbani na katika maofisi, muda mfupi tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. Molocaho by Amorette kampuni ya kubuni na kutengeneza samani ilizinduliwa Septemba 2016. Miezi michache tu tangu kuundwa kwake inaonesha kukimbia na kufanikisha tuzo tatu za kimataifa. Katika tuzo zenye ushindani mkali na heshima kubwa kwenye ubunifu za kimataifa zijulikanzo kama A-Prime Design (A'Design) zilizofanyika mjini Roma mwishoni mwa wiki Jacqueline amepata tuzo katika kategori mbalimbali na kuwa wa
pili kategori nyingine.
  
Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi. 
 Bidhaa zilizompatia tuzo ni samani na pia za mwanga. Ngorongoro Settee ilimpatia medali ya shaba kwa upande wa samani na katika bidhaa za mwanga Sayari Lamp pia ilimpatia tuzo ya shaba. Nafasi ya pili ilipatikana katika kiti cha Flamingo. Taarifa zilizofikia thebeauty zinasema kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016 na kiti cha Ngorongoro na kategori ya Lighting Products and Lighting Projects Design Category ya mwaka 2016 ilikuwa na Sayari lamp. Na Kiti cha Flamingo kilimpatia nafasi ya pili katika kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016. Muonekano wa kiti cha Ngorongoro Settee uliompatia tuzo Jacqueline Mengi kupitia kampuni yake ya Molocaho by Amorette.[/caption] A-Prime Design Shindano aliloshiriki Jacqueline Mengi akiwa na kampuni yake ya Molocaho by Amorette la A’Design hushirikisha wabunifu, wagunduzi na makampuni yanayotengeneza bidhaa mbalimbali za ubunifu wa ndani. Shindano la A' Design limeanzishwa kwa lengo la kuhakikisha kwamba wabunifu wanakuja na bidhaa bora kabisa zenye ushindani mkali katika soko la kimataifa. Kwa kawaida tuzo zake hutolewa katika kusanyiko kubwa la wabunifu linalofanyika Roma, Italia kwa kuratibiwa na OMC Design Studios SRL . Jacqueline, Miss Tanzania (2000) hivi karibuni alishiriki tuzo za rais za CTI na ana mafunzo ya Interior Design kutoka Rhodec International. Kampuni ya Molocaho by Amorette, kampuni ya Tanzania inajishughulisha na utengenezaji wa samani bora kwa namna mteja anavyohitaji, nyuzi, taa, urembaji, samani za nje na kwenye bustani. Sayari Lamp iliyompatia tuzo katika kategori ya Lighting Products and Lighting Projects Design Category ya mwaka 2016.[/caption] Molocaho inatengeneza samani zenye mahadhi ya kiafrika ikichanganya utamaduni wa Tanzania katika mazingira ya kisasa na kumalizia na ubunifu wa kimataifa. Molocaho, moja ya makampuni ya Afrika Mashariki ya samani yanayokua kwa kasi, imejipatia nafasi kubwa ya heshima kwa kuhakikisha kwamba inatumia mali ghafi na mbao njema pekee za Tanzania kutengeneza samani zenye kwenda kimataifa. Katika mahojiano na jarida maarufu la Forbes alishawahi kusema kwamba anawania soko la kimataifa kutokana na ukweli kuwa bidhaa anazotengeneza zimejipambanua kwa wateja. Muonekano wa kiti cha Flamingo kilimpatia nafasi ya pili katika kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016.[/caption] Jacqueline Ntuyabaliwe, pamoja na kuwa na ratiba yenye changamoto sana (Yeye ni balozi wa WildAid na yumo ndani ya bodi kadhaa; mama wa watoto pacha wavulana; mke kwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na akiendesha taasisi ya hisani ya elimu), huhakikisha anakagua kila samani inayozalishwa kiwandani kwake kabla ya kuuzwa au kusafirishwa. Mume wake, Reginald Mengi, ni tajiri mwenye mafanikio makubwa nchini Tanzania ambaye ameujenga utajiri wake kwa kufanya karibu kila kitu kuanzia uzalishaji wa kinywaji cha Coca-Cola hadi uchimbaji wa madini na kumiliki vituo vya televisheni na magazeti. Kwa tuzo hizo Amorette, inajidhihirisha kuwa chata yenye mafanikio makubwa nchini Tanzania na huku ikipanda kwa kasi kimataifa.