Kamishna wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora Dkt. Kevin Mandopi akizungumza na wadau
mbalimbali wa masuala ya haki za binadamu katika mkutano wa maadhimisho
ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika
kwenye ofisi za Tume hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali
Bibi. Neema Ringo na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora Bibi. Mary Massay akitoa ufafanuzi kuhusu haki
za watu wenye ualbino katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar
es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Mwakilishi wa UNESCO Bi. Zulmira
Rodrigues akizungumza kwenye mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa
ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino leo jijini Dar es Salaam ambapo
ameishauri Serikali kuweka mikakati ya muda mrefu ili kukomesha ukatili
na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualbino.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi
ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Bibi. Neema Ringo (kushoto)
akitoa rai kwa watanzania kutoa taarifa mapema za vitendo vya ukatili
dhidi ya watu wenye ualbino katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Dkt. Kevin Mandopi na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Bibi. Nkasori Sarakikya.
Baadhi ya waandishi wa habari na
wadau wa masuala ya haki za binadamu wakifuatilia mkutano wa maadhimisho
ya Siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma Kuhusu Ualbino uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Fatma Salum – Maelezo