TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA TFF.

December 28, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

DESEMBA 28, 2017

RELEASE NAMBA 438,439,440,441 NA 442



LIGI KUU BARA MZUNGUKO WA 12 KUENDELEA KESHO



Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) mzunguko wa 12 katika msimu wa 2017/2018 inaendelea wikiendi hii baada ya kusimama kwa wiki tatu kupisha michuano ya CECAFA huko Kenya na mechi za raundi ya pili ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).



VPL ambayo wadhamini wenza ni Kituo cha Televisheni cha Azam (Azam Tv) na KCB - Benki inayotoa huduma zake kisasa, itaanza kesho Ijumaa Desemba 29, 2017 kwa mchezo kati ya Azam FC na Stand United kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku.



Jumamosi Desemba 30, kutakuwa na michezo mitatu - Lipuli na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa kuanzia saa 8:00 mchana; Mtibwa Sugar na Majimaji ya Songea katika dimba la Manungu, Turiani mkoani Morogoro ilihali Ndanda itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona - Mtwara. Mechi hizo mbili zitachezwa kuanzia saa 10:00 jioni.



Jumapili, mabingwa watetezi wa VPL, Young Africans watakuwa wageni wa Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuanzia saa 10:00 jioni huku Njombe Mji FC na Singida United wakitangulia kwa mchezo utakaoanza 8:00 mchana Uwanja wa Saba Saba, Njombe.



VPL itakamilisha mechi za mzunguko wa 12 katika mechi zitakazopigwa mwakani, Januari mosi  ambako Mbeya City wakiikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya  na Mwadui wakiikaribisha Ruvu Shooting zote kuanzia saa 10:00 jioni.



Baada ya mechi hizo, Ligi Kuu itasimama tena kupisha mechi za Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar na raundi ya tatu ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayochezwa kati ya Januari 5 na 7 mwakani kabla ya kuingia kwenye mzunguko wa 13 wa ligi kuanzia Januari 13 na 17, 2018.





TFF KURASIMISHA MASHINDANO YASIYO RASMI



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lipo kwenye mkakati madhubuti wa kuyarasimisha mashindano yasiyo rasmi ili kuweza kutambuliwa.



Kumekuwa na upotoshaji unaofanywa kwa makusudi kuwa Rais wa TFF Wallace Karia amefuta mashindano yote ya aina hiyo taarifa ambazo sio sahihi alichokisema Rais Karia wakati akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ni kuwa TFF inaandaa kanuni ili mashindano yote ya aina hiyo yachezwe kwa kukidhi vigezo katika utaratibu mzuri na watapata vibali kupitia FA wilaya na mikoa baada ya kutimiza vigezo vitakavyowekwa wakati yale yenye sura ya kitaifa yatapata kibali kutoka TFF.



Nia ya TFF ni njema yenye lengo ya kuufanya Mpira wa Tanzania kuwa katika muelekeo mmoja wenye kufuata utaratibu wenye tija na wenye kuchochea maendeleo ya mchezo wa soka hapa nchini.



WATANZANIA WAENDELEA KUJITOKEZA KUNUNUA TIKETI ZA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA ZA RUSSIA.



Watanzania wameendelea kujitokeza kununua tiketi za Kombe la Dunia zitakazochezwa mwakani nchini Russia.



Mpaka sasa kati ya tiketi 290 zilizotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) tiketi za Fainali tayari zimemalizika zikiwa zimebakia tiketi za nusu fainali na hatua ya makundi.



Hatua ya makundi ya fainali hizo za Kombe la Dunia ndio yenye tiketi nyingi zaidi zikiwa zimetolewa tiketi 250.



Yeyote mwenye nia ya kununua tiketi awasiliane na Idara ya mashindano ya TFF mwisho Januari 15, 2018.



KADI MAALUMU ZA KUINGILIA UWANJANI KWA WAANDISHI



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea kusisitiza utaratibu kwa Waandishi wa Habari za Michezo wa namna ya kuingia kuripoti mechi za fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika Russia mwakani.



Mwandishi anayehitaji kuripoti fainali hizo awasiliane moja kwa moja na Idara ya Habari na Mawasiliano TFF ili kuweza kupata kadi hizo maalumu (Accreditation) ambazo zinapatikana kupitia link maalumu inayosimamiwa na   idara hiyo.



Mwisho wa kuomba kadi hizo maalumu kwa waandishi ili kuweza kuthibitishwa FIFA ni Januari 15, 2017.



TFF, OFISI YA MKUU WA MKOA KUWANOA MAKOCHA



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kesho anatarajia kuzindua rasmi kozi ya ukocha kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari iliyoanza leo Desemba 28, 2017.



Kozi hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa TFF na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam itakayochukuwa muda wa siku 10 itafanyika kwenye vituo viwili vya Makao Makuu ya TFF, Karume – Ilala na Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.



……………………………………………………………………..……………..……

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA



RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWASILISHA FOMU ZAKE ZA TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI KWA VIONGOZI WA UMMA KATIKA OFISI ZA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAM

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWASILISHA FOMU ZAKE ZA TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI KWA VIONGOZI WA UMMA KATIKA OFISI ZA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAM

December 28, 2017

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma kwa ajili ya  kuwasilisha Fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kuwasili katika Makao makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma kwa Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katika Makao makuu ya ofisi hizo yaliyopo katika Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliokuwepo katika jengo la Sukari House wakati akitoka katika katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati akitoka katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya  Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika jengo la Sukari House jijini Dar es Salaam.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi walio simama kando ya barabara inayopita mtaa wa Ohio wakati akitoka katika Ofisi za za Sekretarieti ya  Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

ARUSHA WAIOMBA KAMPUNI YA ABACUS PHARMA (A) LTD KUWAPELEKEA BIDHAA ZA SUGAR FREE

December 28, 2017
Muonekano wa jiji la Arusha katika picha

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa jijini Arusha wameiomba Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD kuwapelekea bidhaa za Sugar Free ambazo zinasaidia kupunguza  matumizi makubwa ya sukari.


Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo mkoani humo kusherehekea Sikukuu ya Krisimasi walisema bidhaa hizo ni mkombozi kwao.

"Binafsi napenda kusema bidhaa hizi za Sugar Free kwa hapa Arusha zitapata soko kubwa kutokana na watu wengi kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari" alisema Mzee Mollel mkazi wa Njiro.

Mollel alisema watu wengi jijini humo wananchi kwa masharti ya ulaji na unywaji wa vitu visivyo na sukari jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa karibu familia nyingi.

Alisema wakazi wa jiji hilo wamezipokea kwa mikono miwili bidhaa hizo ambapo wameiomba kampuni hizo kufungua tawi mjini humo ili bidhaa hizo ziweze kupatika wakati wote.

"Tunaomba bidhaa hizi ziuzwe na maofisa mauzo wa kampuni hiyo wasiwape wenye maduka itakuwa changamoto kupata maelezo ya kina ya matumizi yake na tunahofu wakiachiwa wafanyabiashara wengine wanaweza kutupandishia bei" alisema mkazi mwingine wa jiji hilo aliyejitambulisha kwa jina la Laizer.

Laizer alisema humo kumekuwa na unywaji na ulaji wa vyakula vyenye sukari lakini kuingia kwa bidhaa hizo zitasaidia sana wananchi hasa baada ya kupata maelekezo ya utumiaji wake.

Akizungumza bidhaa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 


Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.



"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.


Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.

Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.


Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika. 

Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.


Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.

Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.

Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.