Rais wa Zanzibar Dk Shein Ziarani Nchini Djibout

Rais wa Zanzibar Dk Shein Ziarani Nchini Djibout

May 06, 2017
JIBO1
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Viongozi wa Serikali na Wazee wa CCM uwanja wa Ndege wa Kimataifa Zanzibar akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu .(Picha na Ikulu)
JIBO2
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea Nchini Djibout kwa ziara ya kiserikali.(Picha na Ikulu)
JIBO3
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kabla ya kuaza safari yake Nchini Djibout kwa ziara ya kiserikali.(Picha na Ikulu) 

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MKUTANO WA 10 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJJINI DAR ES SALAAM

May 06, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Waziri Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Dkt. Reginald Mengi, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji wa TBNC Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira, na Walemavu Jenista Mhagama.
 Katibu Mkuu Kiongozi na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC), Balozi John Kijazi akitoa utambulisho wa wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza hilo na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwenyekiti Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania(TPSF) Dkt. Reginald Mengi wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri Mkuu na Mjumbe wa Baraza hilo Kassim Majaliwa.
 Rais wa Taasisi ya Wakuu wa Makampuni CEO Round Table Ally Mfuruki akisalimiana na Mwenyetiki wa Taasisi za Kibenki ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu (BOT) Profesa Benno Ndulu wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa Biashara Tanzania (TBNC) uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. 
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakichangia mada wakati wa mkutano huo ulifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakichangia mada wakati wa mkutano huo ulifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) wakichangia mada wakati wa mkutano huo ulifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

VODACOM-TANZANIA YAUNGANA NA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI KUSHEREHEKEA SIKU YA UHURU WA NCHI HIYO JIJINI DAR ES SALAAM

May 06, 2017

Balozi wa Afrika ya  Kusini nchini, Thamsanga Dennis Msekelu akicheza muziki wa asili ya Afrika Kusini Kwaito na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 23 ya Uhuru wa Afrika ya Kusini,Hafla hiyo iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.






Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald(kushoto)akiwa na wageni waalikwa kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 23 ya Uhuru wa Afrika ya Kusini,Hafla hiyo iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC na kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.




Balozi wa Afrika ya  Kusini nchini, Thamsanga Dennis Msekelu akipongezwa na Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald,kuhusiana na sherehe ya maadhimisho ya miaka 23 ya Uhuru wa Afrika ya Kusini iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Sherehe hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC.
TADB, SUA WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

TADB, SUA WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

May 06, 2017


S
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (katikati) akiongoza kikao cha majadiliano juu ya ushirikiano na Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) wakati uongozi wa Chuo hicho walipotembelea Ofisi za TADB. Msafara wa huo wa Chuo cha Kilimo uliongozwa na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Susan Nchimbi-Msolla (wapili kulia) na msaidizi wake Prof. Benard Chove (kulia). Wengine pichani ni wajumbe wa menejimenti ya TADB.
S 1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kushoto) akibadilishana hati za makubaliano na Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Susan Nchimbi-Msolla. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Sheria na Huduma wa TADB, Bibi Neema-Christina John (Kushotot) na Naibu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Benard Chove (kulia). Makubaliano hayo yalisainiwa katika Ofisi za TADB, Dar es Salaam.
S 2
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kushoto) and Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Susan Nchimbi-Msolla wakionesha hati za makubaliano. Makubaliano hayo yanalenga uendelezaji wa masuala ya utafiti na kujengea uwezo wa kitaasisi baina ya pande hizo mbili. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Sheria na Huduma wa TADB, Bibi Neema-Christina John (Kushoto) na Naibu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Benard Chove (kulia).

ZIARA YA BULEMBO KUKAGUA MCHAKATO WA UCHAGUZI CCM MKOA WA DAR ES SALAAM

May 06, 2017
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na viongozi wa CCM na Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, katika Ofisi ya CCM mkoa huo, mwanzoni mwa ziara yake, kukagua uhai wa chama na mwenendo wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa CCM. Waliokaa kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa  huo, Lugano Mwafongo
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaji Abdallah Bulembo akiwasili katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Jumuia hiyo leo. Anayemkaribusha ni Mjumbe wa NEC, Ramesh Patel.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akisalimia baadhi ya wanachama wa CCM nje ya Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala baada ya kuwasili kweye ofisi hiyo, leo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaji Abdallah Bulembo akipokea saluti ya Kijana wa CCM alipowasili ofisi ya CCM wilaya ya Ilala jana akiwa katika ziara hiyo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akivishwa skafu na kijana wa CCM alipowasili Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala kufanya ziara hiyo
Mwenyekiti wa Jumuia  ya Wazazi alhaj Abdallah Bulembo akisalimia wana CCM
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Buulembo akimsalimia Mbunge wa zamani wa Ukonga, Paul Rupia nje ya Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala alipowasili kwenye ofisi hiyo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya CCM wilaya ya Ilala, baada ya kuwasili kuanza ziara hiyo. Kulia ni Mjumbe wa NEC Ramesh Patel Baadhi ya viongozi wa CCM kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi waliofuatana na Bulembo kwenye ziara hiyo
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj abdallah Bulembo akisalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye ukumbi kilikofanyika kikao cha viongozi wa Jumuia hiyo, Tabata jana.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akiingia ukumbini, Tabata
Ukumbi ukilipuka kwa nyimbo za mapokezi Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo alipingia ukumbini
Mwenyekiti wa Jumuiaya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili meza kuu tayari kuendesha kikao. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe na kulia ni Mjumbe wa NEC, Ramesh Patel ambaye anajiita Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala

BURIANI MWANAHABARI REVOCATUS BULIZYA

May 06, 2017
Marehemu Revocatus Bulizya enzi za uhai wake
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Revocatus Bulizya wakati ukiingizwa katika Kanisa la Katoliki Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya ibada ya kuuaga kabla ya kwenda kwenye mazishi yaliyofanyika Mwandege Kongowe Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.

SINGIDA INAZALISHA NUSU YA ASALI YOTE INAYOZALISHWA NCHINI; WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AELEZA.

May 06, 2017

 
 Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akizindua kikundi cha wazalishaji nyuki cha Kisaki katika manispaa ya Singida.

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akiwa anatazama asali inayozalishwa na kikundi cha wazalishaji nyuki Kisaki, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kikundi hicho Philemon Kiemi. 


Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akimpongeza Jacob Edward Mashimba kwa kuhitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kabla ya kumtunuku cheti cha mafunzo hayo.
Eneo la kikundi cha wafugaji nyuki kibiashara likiwa na mizinga ya nyuki ya kutosha katika kijiji cha Kisaki, Manispaa ya Singida. Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akipata maelezo ya ukamuaji na upakiaji wa asali kisasa kutoka kwa Mkurugenzi wa kikundi cha uzalishaji nyuki Philemon Kiemi.

……………………………………………………………………………….

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda Mkoa wa Singida kwa kuzalisha nusu ya asali yote inayopatikana nchini Tanzania.

Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ametoa pongezi hizo wakati akifunga mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara wa kikundi cha wafugaji nyuki wa kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida ambapo aliwatunuku vijana 23 vyeti vya mafunzo hayo.

Amesema Singida imekuwa ikizalisha tani elfu 17 kwa mwaka huku uzalishaji kwa nchi nzima ukiwa ni tani elfu 34 kwa mwaka hivyo basi wananchi watumie fursa ya hiyo kuzalisha asali bora ili ipate soko la kimataifa.

Mheshimiwa Pinda amesema asali ina faida kubwa kwakuwa imekuwa ikitumika kama chakulana pia dawa huku akiongeza kuwa baadhi ya wazalishaji wameweza kutumia nta kuzalisha mshumaa na gundi ijapokuwa bado si kwa kiwango cha kutoshelesha hata soko la ndani.

Ameongeza kuwa kuwa wananchi watumie fursa ya nchi ya Tanzania kuwa na misitu hekta milioni 35 kufuga nyuki kwa wingi ili misitu hiyo iwezwe kutunzwa huku ikiwafaidisha kwa kuvuna asali na mazao yake.

Mheshimiwa Pinda amewaasa vijana waliohitimu mafunzo ya ufugaji nyuki kibiashara kuhakikisha wanaisambaza elimu waliyoipata kwa wenzao pamoja na wao kuwa wagujai nyuki wa mfano katika maeneo yao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Singda Elias Tarimo amesema Manispaa ya Singida ina vikundi 16 vya uufugaji nyuki na wafugaji nyuki wengi wakiwa katika kata za Uhamaka, Mungumaji, Mtamaa, Mwankonko na Kisaki.

Tarimo amesema wataendelea kuhamasisha vijana na wakazi wengi kufuga nyuki kisasa na kusisitiza ufugaji nyuki kibiashara ndio wenye tija na manufaa kwa mfugaji.

Mmoja wa wahitimu Jacob Edward Mashimba amesema mafunzo ni mazuri na yatawasaidia katika kutunza mazingira kutokana na jamii imekuwa ikikata miti kwa wingi.

Mashimba amesema katika jamii anayotoka ya kihadzabe ambayo bado inategemea asali kama chakula kikuu elimu ya ufugaji nyuki kibiashara itasaidia licha ya upungufu wa baadhi ya vifaa vya kisasa vya ufugaji nyuki.
SAFARI ZA ATCL MKOANI TABORA ZAZINDULIWA RASMI

SAFARI ZA ATCL MKOANI TABORA ZAZINDULIWA RASMI

May 06, 2017
JJ1
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, wakiwa ndani ya ndege kuelekea katika uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani Tabora.
JJ2
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akihutubia wananchi wa Tabora (hawapo pichani), waliohudhuria uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani humo.
JJ3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani Tabora.
JJ4
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri, wakati wa uzinduzi wa safari za Ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani humo.
JJ5
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri, wakikata keki kama ishara ya kuzindua rasmi safari za Ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), mkoani humo.
JJ6
Baadhi ya viongozi na wabunge wakiingia kwenye ndege aina ya Bombardier Dash 8 Q400 ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), iliyotua kwa mara ya kwanza mkoani Tabora katika uzinduzi wa safari za ndege mkoani humo.
Dr. Ntuyabaliwe Foundation yahimiza wanafunzi kusoma vitabu

Dr. Ntuyabaliwe Foundation yahimiza wanafunzi kusoma vitabu

May 06, 2017
Wananafunzi wa Shule za Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada na ziada, ili waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi, alipozungumza na wanafunzi, walimu na wajumbe ya Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho, wakati akizindua maktaba iliyokarabatiwa na mfuko huo. Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya msingi Makumbusho jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz) 
 Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo, alitoa shukrani kwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation kwa mchango wake wa vitabu kwa ajili ya maktaba hiyo, na kuomba kupatiwa mtaalam wa kutunza maktaba, ikiwezekana mwalimu mmoja akasomeshwe taaluma hiyo. Naye Afisa Taaluma Fatma Mwiru akimwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka waalimu kuwasaidia wanafunzi kupata vitabu mbalimbali, kwa kuwashirikisha wadau wa elimu, wachapishaji vitabu pamoja na wahisani. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akizungumza alipokuwa akimkaribisha Mama Jacqueline Mengi.[/caption] Aidha Mama Jaqueline Mengi amesema Dr. Ntuyabaliwe Foundation ilianzishwa mwaka jana ikiwa na lengo la kuchangia katika sekta ya elimu, ambapo iligundua shule nyingi za msingi zinakabiliwa na uhaba wa maktaba na vitabu. Shule ya Msingi Makumbusho inakuwa ya shule ya pili katika wilaya ya Kinondoni na ya kwanza katika kata ya Makumbusho, kusaidiwa ujenzi wa maktaba na msaada wa vitabu na Dr. Ntuyabaliwe Foundation, ikitanguliwa na Shule ya Msingi Hananasifu.  
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi alipowasili katika shule ya msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi. Katikati ni Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni katika uzinduzi huo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyekwamilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni. Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule msingi Makumbusho kabla ya uzinduzi huo. Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimwongoza Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi kuelekea eneo la uzinduzi wa maktaba hiyo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la maktaba hiyo. Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akisoma moja ya vitabu vya hadithi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho waliowakilisha wenzao katika uzinduzi huo.