DC MTATURU AZINDUA UHABARISHO WA MAFUNZO YA KUIJENGEA UWEZO JAMII KATIKA KUIBUA NA KUPANGA MIRADI YA MAENDELEO

November 02, 2016
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu aliyesimama akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
 Madiwani, na Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu walengwa wa Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi
 Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Juma Mwanga, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka
 Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu mradi huo
Madiwani,Wakuu wa Idara na Vitengo wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mradi wa kuijengea jamii uwezo katika kuibua na kutekeleza mpango shirikishi

Na Mathias Canal, Singida

Shirika la Health Actions Promotion Association (HAPA) la Mkoani Singida kwa ushirikiano na Shirika la The Foundation For Civil Society la Jijini Dar es salaam linatarajia kuendesha mradi wa miaka mitatu kwa vijiji vyote vya Wilaya ya Ikungi kwa lengo la kuijengea jamii uwezo na mbinu shirikishi kama fursa na vikwazo katika maendeleo.

Mradi huo utaanza na Vijiji 10 vya majaribio (Pilot Villages) kutoka katika kata nne na kila kata itakuwa na Vijiji ama viwili ama Vitatu ambapo uchaguzi wa Vijiji hivyo vya majaribio umezuingatia utayari wa jamii husika katika shughuli za maendeleo pamoja na gharama za uendeshaji wa mradi ili kupata matokeo chanya kwa uendelezaji wa mradi husika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa Uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika kusaidia kutekeleza shughuli za maendeleo, kwani kwa uhabarisho wa mafunzo ya kujenga uwezo wa jamii na Halmashauri yataendelea katika kuimarisha juhudi za Wilaya zinazoendelea kuchukuliwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo pia itakuwa ni fursa kwa jamii kuwa na Uwezo na Nyenzo muhimu katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi.

Amesema kuwa Wilaya ya Ikungi inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kujiletea maendeleo ambapo endapo zitapatiwa upembuzi yakinifu zitapunguza kadhia zinazowakumba wananchi ambapo amezitaja changamoto hizo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati (Kata na Vijiji) ambapo kwa sasa Wilaya ina vituo 39 tu vya kutolea huduma za Afya ambapo upungufu ni Asilimia 60, Ujenzi na Uboreshaji wa miundombinu ya shule za msingi ambapo kuna nyumba za walimu 387 ambapo upungufu ni nyumba 854, Ujenzi na Uboreshaji wa majosho na mifugo kwani kwa sasa yapo majosho 30 huku kati ya hayo majosho 20 ni mabovu.

Dc Mtaturu alisema kuwa Zipo Asasi mbalimbali ambazo zimesajiliwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi lakini zimegeuka na kuwa Asasi zinazofanya kazi za kisiasa tofauti na usajili wao ambapo amesema serikali haitasita kuzichukulia hatua ikiwemo kuzifuta Asasi hizo ili ziache kupotosha wananchi.

Dc Mtaturu alisema kuwa Mradi huo unaotolewa na Shirika la HAPA ni lazima uzingatie matakwa ya kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu kuwa wana nafasi kubwa ya kufanikisha maendeleo yao katika jamii hivyo waache kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa kuwa maendeleo yataletwa na serikali pekee.

Msimamizi wa Mradi wa HAPA Noel Makyao amewataja walengwa wa Mradi huo kuwa ni wananchi wote wa kijiji cha Mradi wa majaribio, Wawakilishi 100 kutoka kila kijiji ambao watachaguliwa ili kuendesha zoezi la kutengeneza bajeti ya mpango wa kila mradi ulioibuliwa na jamii kwa siku tatu mfululizo na watu mashuhuri, wakuu wa madhehebu ya dini na makundi mengine wapatao 20.

Alisema kuwa Jumla ya gharama zote za kutekeleza mradi wa mbinu shirikishi ya kujenga uwezo wa jamii katika kuibua, Kupanga, Kutekeleza na kupima matokeo ya Mradi katika vijiji kumi vya majaribio kwa robo mbili zitakuwa shilingi milioni hamsini (50,000,000/=).

Makyao alisema katika awamu hii ya vijiji kumi vya majaribio jumla ya watu wapatao 25,511 watafikiwa kati ya lengo la watu 25,334 zaidi ya watu 177 ya walengwa wa mradi.

WANAWAKE MKOANI MWANZA WATAKIWA KUHUDHURIA KONGAMANO LA SAUTI YA MWANAMKE.

November 02, 2016
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Wanawake mkoani Mwanza wamehimizwa kuhudhuria Kongamano la Sauti ya Mwanamke litakalowakutanisha baadhi ya wanawake waliofanikiwa kiuchumi nchini, ili kujifunza na kuhamasika katika kujikwamua kiuchumi.

Mwandaaji wa Kongamano hilo, Mboni Masimba ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha runinga cha The Mboni Show, amesema kongamano hilo limelenga kuwahamasisha wanawake kufanya kazi kwa bidii na kwa kujiamini zaidi bila kuongopa vikwazo vya kibiashara.

“Njoo ujifunze nguvu ya mwanamke katika biashara, kushinda vikwazo, kujiamini, kufanya kazi kwa bidii, kutoogopa hatari za kibiashara pamoja na kuwa na malengo ya muda mrefu ambapo wahamasishaji na wafundaji mbalimbali watakuwepo”. Amesema Masimba na kuongeza kwamba pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa Isha Mashauzi na Zarry Edosha pamoja na vichekesho kutoka kwa Katarina Wa Karatu.

Aidha Masimba amesema tayari tiketi za kongamano hilo litakalofanyika tarehe sita mwezi huu kwenye ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza zimeanza kuuzwa kwa shilingi elfu arobaini katika maeneo mbalimbali ikiwemo Gold Crest Hotel, TSN Super Market Rock City Mall, Flora Salon, Kayvies Beaty Parlour Magnum Hotel Ghana, Idda Garments Ghana, Diamond Bar Kona ya Bwiru pamoja Bladict Classic Wear mtaa wa Uhuru Dampo.
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi.
TEKNOLOJIA INAVYOBADILI MIENDENDO YA WASAFIRI

TEKNOLOJIA INAVYOBADILI MIENDENDO YA WASAFIRI

November 02, 2016


Na Jumia Travel Tanzania

Miaka kadhaa iliyopita kabla ya matumizi ya tekinolojia kuingia na kushika kasi mtu ulikuwa ukitaka kusafiri itakubidi kuulizia kwa watu ambao tayari wameshawahi kuwepo kwenye eneo unalolitarajia kwenda.

Baadae kidogo simu zilivyoanza kuingia zilirahisisha mambo watu wakawa wanapigiana simu na kuulizana hali na mazingira kwa ujumla ya eneo wanalotaka kwenda ili kujiandaa vema.

Lakini sasa hivi kwa msaada wa tekinolojia ni wewe tu aidha na simu au kompyuta yako iliyounganishwa vizuri na mtandao wa intaneti ambapo unaweza kupata taarifa lukuki bila ya kumuhusisha mtu yeyote yule. 

Kadiri ya maendeleo ya tekinolojia yanavyokua sehemu mbalimbali duniani na ndivyo huduma mbalimbali zinavyosogezwa na kurahisishwa zaidi kumzunguka binadamu.

Leo hii mtu huna haja ya kupata shida ya kuanza kusumbuka kutembea umbali mrefu au kumuuliza jirani, ndugu au jamaa kuhusu huduma kama vile za usafiri, malazi, bidhaa, na bei zake kwani kila kitu kimo na kinaweza kupatikana kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Vivyo hivyo kwa upande wa huduma za usafiri na utalii zilivyorahisishwa na mitandao ya huduma za hoteli kama vile Jumia Travel, Expedia, Airbnb, TripAdvisor, Booking.com na kadhalika.

Wasafiri na watalii wengi wa siku hizi kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi wanapenda kupata huduma wazitakazo kwa urahisi zaidi na uhakika wakiwa mahali popote.

Wanataka kwamba wakiingia kwenye mtandao aweze kupata taarifa zote juu ya sehemu anayotaka kwenda kama vile atafika kwa njia gani pamoja na sehemu atakayofikia.

Kwa upande wa malazi mitandao iliyotajwa hapo juu imekuwa na nafasi kubwa sana katika kuhakikisha msafiri anapata sehemu ya uhakika anayoihitaji, gharama na hadhi yake.

Mitandao hii inatoa uwanja mpana wa kuweza kupata huduma zote sehemu moja, za uhakika tena ndani ya muda anaoutaka msafiri.

Tofauti na kipindi cha nyuma kidogo ambapo ilimbidi mtu afanye taratibu za malazi kwa sehemu anayokwenda mpaka atakapofika.

Kwa namna moja ama nyingine mitandao hii ya huduma za hoteli kwa mtandao na tekinolojia kwa ujumla imeleta msaada mkubwa na mapinduzi ya hali ya juu kwa watoa huduma nchini na sehemu zingine duniani.

Licha ya maendeleo hayo na madhumuni mazuri ya tekinolojia katika kuboresha maisha ya binadamu lakini bado kuna changamoto kubwa kwa watumiaji hususani wasafiri kuiamini na kuitumia mara kwa mara lakini pia hata kwa wenye hoteli na sehemu zingine zinazotoa huduma za malazi kwa ujumla.

Bado wasafiri wengi wanaamini kuwa huduma za kweli na uhakika utazipata mara utakapofika eneo husika licha ya kuwa kwenye mitandao hii kuna picha, huduma, gharama na mawasiliano ya wahusika.

Na kwa upande wa wamiliki wa sehemu za malazi kama vile hoteli bado nao hawana imani kubwa na wamiliki wa hii mitandao. Wao wanadhani kwamba wanaweza kutumia hoteli zao kuwatapeli wateja na kunufaika wao binafsi, dhana ambayo si kweli.

Ukweli wa mambo ni kwamba kwa watumiaji wa huduma hizi, wateja na wamiliki wa hoteli ambao huitumia mara kwa mara wamethibitisha imekuwa na msaada mkubwa sana.

Kwa mfano, hoteli nyingi hutegemea umaarufu wa sehemu husika ndio mteja aende na kutumia huduma zao kitu ambacho kwa dunia tuliyopo na tunayokwenda nayo kinapitwa na wakati.

Kupitia mitandao hii wamiliki wa hoteli na sehemu zingine za malazi wana wigo mpana wa kuwapata wateja kutoka maeneo mbalimbali kwani huduma zao zinakuwa tayari kwenye mitandao hiyo.

Jumia Travel ni miongoni mwa mitandao hiyo ambayo inayo orodha ndefu ya hoteli takribani 1,500 za nchini Tanzania bara na visiwani ambazo zinaweza kufikiwa na watu wa ndani na nje ya nchi.

Hii ni fursa kwa wamiliki wa hoteli kuweza kutambua wateja wao ni watu wa aina gani na wanatarajia vitu gani kutoka kwao. Wateja wa sasa wanategemea kwa kiasi kikubwa kukuta taarifa zote kuhusu huduma za hoteli husika kuwepo kwenye mtandao na kupatikana mara moja pale wanapozihitaji.

Kwa bahati mbaya si hoteli na sehemu za malazi zote ambazo taarifa zake unaweza kuzikuta mtandaoni na hapo ndipo mitandao hii inapokuja kuziba hilo pengo.

Mitandao ya huduma za hoteli imekuja kuziba pengo lililokuwepo kwa muda mrefu baina ya watoa huduma hizo na wateja ambapo athari zilikuwa kwa pande zote mbili.

Wamiliki kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakikosa wateja wengi ambao wangeweza kuwafikia kwa njia ya mtandao kwa kutegemea ambao wanakwenda moja kwa moja na hivyo kupoteza mapato mengi. Na pia kwa wateja ambao walikuwa na shauku ya kujua sehemu husika kabla ya kwenda walikuwa wanakosa fursa hiyo kwa sababu hakukuwa na mbadala wa huduma hiyo. 

Kuhusu Jumia Travel
Jumia Travel (travel.jumia.com) ni mtandao nambari moja unaongoza wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao wenye orodha ya hoteli zaidi ya 25,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya hoteli 200,000 duniani kote.

Dhumuni letu ni kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.

Hapa Jumia Travel, tunao mamia ya wataalamu katika masuala ya utalii ambao huwasiliana na wateja wetu. Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi zifuatazo Lagos (Naijeria), Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan (Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar Es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto (Ureno) na Paris (Ufaransa).

Kabla ya mwezi Juni mwaka 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa mwaka 2013 na Jumia ambayo inaendeshwa kwa kushirikiana na MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axas kama washirika wao katika masuala ya kifedha. 

Sherehe za familia za Bayport Kibaha zamfurahisha mama Anna Mkapa

November 02, 2016
Afisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akizungumza jambo katika sherehe za Siku ya Familia ya wana Bayport waliosherekea pamoja na watoto wao pamoja na watoto wanaolelewa na kituo cha Kibaha Children Village Centre (KCVC), mwishoni mwa wiki iliyopita.

Watoto walivyojiachia kwenye ‘party’ ya Bayport Kibaha

Na Mwandishi Wetu, Kibaha
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, iliwaacha watoto hoi mwishoni mwa wiki baada ya kuandaa sherehe maalum kwa ajili ya wafanyakazi wa tasisi hiyo pamoja na watoto wao kufurahia pamoja na watoto wenzao wanaolelewa na kituo cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

Sherehe hizo zilianza asubuhi na kumalizika jioni ambapo tukio hilo liliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bayport, John Mbaga, pamoja na mlezi wa Kituo hicho ambaye ni mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa.
Baadhi ya watoto wakipata chakula cha mchana katika party hiyo ya Bayport Kibaha.
Baadhi ya michezo waliyocheza watoto hao ni kubembea, kucheza muziki, kupewa burudani ya mazingaombwe sanjari na nyinginezo nyingi zilizowaburudisha na kuwafurahisha.

Akizungumza katika salamu za ukaribisho kwenye kituo hicho, mlezi wa KCVC, Mama Anna Mkapa, alisema amefurahishwa na ujio wa Bayport na watoto wao kwenda kufanya sherehe maalum ya kuonyesha upendo na ukarimu kwa watoto wanaoishi na kulelewa na kituo hicho.

“Siwezi kusema mengi kutokana na ujio wenu badala yake niwakaribishe tu nyie na watoto wenu ili wote tufarahi pamoja hususan watoto ambao ndio msingi madhubuti wa kutukutanisha hapa,” alisema Mama Anna Mkapa.

Zilikuwa ni shangwe kutwa nzima kutoka kwa wafanyakazi wa Bayport na watoto.
Katika wakati wote wa burudani hizo, watoto hao walionekana kufurahia zaidi uandaaji wa tukio hilo lililotanguliwa na wimbo wa ukaribisho ulioimbwa na watoto hao mara baada ya wageni kutoka jijini Dar es Salaam kuanza kuingia katika maeneo ya kituo hicho.

Mlezi wa kituo cha KCVC, Mama Anna Mkapa, akisalimia wafanyakazi na watoto katika sherehe za familia zilizofanyika mwishoni mwa wiki.

Akizungumzia sherehe hizo mwishoni mwa wiki, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, alisema wamejisikia faraja kubwa kufurahi pamoja na watoto wote waliokuwapo kwenye sherehe za wana familia wa Bayport, wakiamini kuwa wametumia wakati huo kubadilishana mawazo na kuwapa watoto haki ya kupendwa.

“Nimefurahishwa sana na jinsi tulivyoshiriki katika sherehe hizi za familia, zaidi kuona watoto wetu wana furaha kubwa nikiamini kwamba utaratibu huu utatumiwa na watu wote kutenga muda mahususi kwa ajili ya kukutana na kujumuika pamoja na watoto wao pamoja na wale wanaoishi katika vituo kama hivi kwa sababu wote wana haki ya kupendwa.

“Si mimi tu, bali nina uhakika wafanyakazi wote wa Bayport tumefarijika kwa kufurahia pamoja siku ya familia ya wana Bayport kufurahia siku nzima na watoto wetu wanaolelewa na kituo hiki cha KCVC kwa sababu nao kama tulivyowaona wamefurahishwa pia,” alisema.

Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema ni jambo la kujivunia mno kupata nafasi ya kuburudika na watoto, akiamini kuwa taasisi yao ina kila sababu ya kuishi karibu na jamii kutokana na kuungwa mkono na Watanzania wote.

“Bayport imeanzishwa nchini Tanzania tangu mwaka 2006 na imekuwa ikiungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Watanzania, hivyo tutaendelea kuwa karibu na jamii kwa kushiriki mambo mbalimbali yenye tija na yenye kujenga ushirikiano sahihi kwa watu wote,” Alisema Cheyo na kusema kuwa wana matawi 83 katika wilaya na mikoa ya Tanzania Bara.


Mbali na mikopo ya fedha isiyokuwa na amana wala dhamana inayotolewa na taasisi hiyo, pia wana huduma ya mikopo ya viwanja katika maeneo mbalimbali kama vile Msakasa (Kilwa), Tundi Songani (Kigamboni), Boko Timiza (Kibaha) na Kimara Ng’ombe (Bagamoyo).

MKUTANO MKUU NA KONGAMANO LA WAPIMAJI ARDHI LAFUNGULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

November 02, 2016
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akifungua mkutano mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi linalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia leo Novemva 2-3, 2016.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa moja ya vifaa vinavyotumika katika upimaji wa Ardhi mapema leo katika Mkutano mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akipewa maelezo jinsi mambo yalivyobadirika katika mfumo wa Kidigitali.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiwa amebeba moja ya kifaa kinachotumika katika upimaji.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa kifaa cha kisasa kinachotumika katika upimaji.
Wapimaji wa Ardhi wakiwa katika mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi.
Wapimaji wa Ardhi wakiwa katika mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akitoa cheti cha shukrani kwa makampuni yaliweza kusaidia kufanikisha mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi. Pembeni kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Bw. Justo Lyamuya.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

BI.FATMA KUWAFUNDA WANAWAKE KWENYE KONGAMANO LA SAUTI YA MWANAMKE JIJINI MWANZA.

November 02, 2016
Mbali na kupata burudani, chakula pamoja na vinywaji, mfundaji mashuhuri nchini Bi.Fatma atakuwa mfundaji kwenye Kongamano la Sauti ya Mwanamke Jijini Mwanza, tarehe 06.11.2016 Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Ni kuanzia saa kumi alasiri kwa kiingilio cha shilingi elfu arobaini tu.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi
UN NA EU ZATOA EURO LAKI NANE KUSAIDIA WATOTO WA KIKE

UN NA EU ZATOA EURO LAKI NANE KUSAIDIA WATOTO WA KIKE

November 02, 2016
Shirika la Umoja wa Mataifa la UN kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wametoa Euro laki nane kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu na wahanga wa mimba za utotoni waishio kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit .

Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi Anna Muro amesema kuwa msaada huo utasaidia kuwawezesha wanawake Waweze kushiriki kwenye maendeleo ya jamii .

Akizungumza katika kituo hicho kinacholelea watoto 30 wenye watoto ambao walipata mimba katika umri mdogo na kushindwa kuendelea na masomo ambapo wanasaidiwa na kituo hicho kupata elimu ya ufundi wa ushonaji na mapishi ili kupata stadi zitakaowasaidia kujikwamua kimaisha.
Mwasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara akitoa maelezo kwa Maafisa wa UN na EU wakati walipotembelea kituo shirika hilo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama, Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kulia) pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia).(Picha na Ferdinand Shayo).

Anna amesema kuwa watoto wengi wanakabiliwa na changamoto ya usafirishaji wa binadamu jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu na haki za watoto hivyo amewataka Jamii na serikali kupiga vita usafirishwaji wa watoto.

Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama amewataka watoto wanaoishi katika kituo hicho kutumia fursa ya mafunzo wanayoyapata kujiendeleza kielimu na kukua kiuchumi ili kutokomeza umasikini na mimba za utotoni kwa watoto wa kike.

Muasisi wa kituo hicho Martina Simon Siara ameshukuru ugeni kutoka UN na EU uliofika kituoni hapo kwa ajili ya kutazama shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho pamoja na kuwaunga mkono ili waweze kuongeza tija katika kuisaidia jamii.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (wa pili kulia) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Muasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara (kulia) walipotembelea shirika hilo lililopo jijini Arusha.
Wawakilishi kutoka EU na UN wakitazama shughuli za mikono zinazofanywa na watoto wanaoishi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipotembelea kituo hicho hivi karibuni kilichopo jijini Arusha.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro wakishirikiana kuingiza shanga ambazo hutumika kushona mavazi ya utamaduni yanayoshonwa na watoto wa kike wanaoshi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit (katikati) ni mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Rosemary Innocent.
Binti mwenye ulemavu wa ngozi, Rosemary Innocent na wenzake wakiendelea na darasa la kutengeneza vitu mbalimbali kituoni hapo.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (kushoto) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro katika picha ya pamoja na binti aliyeshona vazi la kuvutia la kimasai lililonakshiwa na shanga walipotembelea kituo hicho.
Wawakilishi wa UN na EU wakitazama kitengo cha elimu ya mapishi katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
wanafunzi wanaojifunza ushonaji katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama akitazama mabinti wanaojifunza ushonaji nguo kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akifafanua jambo kwa vijana na watoto wanaoishi katika kituo hicho walipokitembelea jijini Arusha.
Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro akizungumza na wale, vijana pamoja na watoto wanaoishi kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Wawakilishi wa UN na EU katika picha ya pamoja na walezi na watoto wanaoishi kwenye kituo hicho.

WATUMISHI WAWILI WA SERIKALINI WAFUKUZWA KAZI NA DED WA ILEJE

November 02, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi akiongea wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la madiwani Wilaya ya Ileje. 

na fredy mgunda,Ileje

BARAZA la Madiwani Wilayani Ileje limebariki kufutwa kazi kwa watumishi wawili wa Halmashauri hiyo kutokanana makosa ya wizi wa mamillioni ya fedha za wafadhili za mradi wa UKIMWI wa water reed
Akizungumza wakati wa kufungwa kwa Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ubatizo Songa amesema kuwa, wameamua kuchukua uamuzi huo mara baada ya kuridhishwa na uchunguzi uliofanywa na
kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Ras wa Songwe na kubaini kuwa, Mganga Daraja la pili Josephat Yisuya na Grace Kibona wameweza kuingizia Halamashauri hasara ya zaidi Milioni 84.

“Josephati aliweza kujipatia kiasi cha fedha shilingi milioni 36254200 /-wakati Grace Kibona Mhasibu Daraja la kwanza aliweza kujipatia Kiasi cha shilingi milioni 48742500/-fedha za mradi wa Water Aid zilizofika katika Halmashauri ya wilaya ya Ileje”alisema Songa

Mwenyekiti huyo ameagiza watu hao kurudisha kiasi hicho chote cha Fedha katika Akaunti ya Halmashauri hili ziweze kufanya kazi zingine.
 
kwa mtumishi mwengine Anna mwakipesile kesi yake bado inaendelea na uchunguzi wakati huo watumishi 2 baada ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa na ras songwe waliachiwa huru na kurudishwa kazini baada ya tume kuridhika na utetezi wao


Wakati huo huo Mkurugenzi mtendaji Bw Haji Mnasi amewavua vyeo wakuu wa shule wawili ambao ni Henry Musomba wa sekondari Ibaba na Emecka Minga wa sekondari Ngulugulu kwa makosa mabalimbali yakiwemo utoro,uzembe ,lugha chafu na matumizi mabaya ralislimali

Aidha Mnasi alisema kuwa ni wakati wa kila mfanyakazi wa serikalini kujitathimni kwa kile alichofanya kwani waliotuhumiwa ni wengi lakini bado uchunguzi unaendelea hivyo hawajaishia hapo kwani kila mmoja atakayebainika kufanya ubadhilifu sheria itafata mkondo wake.

Ametoa onyo kwa watumishi kuacha kujihusiha na mambo yaliyo kinyume na maadili ya utumishi wa kwa kujiingiza katika masuala ya kifisadi serikali aitamfumbiamcaho kwani hu ni wakatii wa kuwahudumia wananchi wa nyonge kwa maslahii ya Taifa.

“Mimi sipo tayari kufukuzwa kazi kwa uzembe wa watumishi wazembe nitafuatili utendaji wa watumishi wote wa Ileje ili tuweze kuwatumikia wananchi kama inavyopaswa na kuidumisha kauli ya hapa kazi tu iliyotelwa na rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli” alisema Mnasi