RAIS DKT MAGUFULI ATOA POLE NYUMBANI KWA MAREHEMU MZEE ABOUD JUMBE MWINYI, AWEKA SHADA LA MAUA KABURIN

September 03, 2016
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa Bw. Mustapha Aboud Jumbe na Rajabu Aboud Jumbe alipokwenda kutoa mkono wa pole kwa familia ya Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimu wanafamilia  alipokwenda kutoa mkono wa pole nyumbani kwa  Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka sahihi kitabu cha maombolezo  alipokwenda kutoa mkono wa pole nyumbani kwa  Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba  3, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekezwa jambo na Rajabu Aboud Jumbe alipokwenda kutoa mkono wa pole nyumbani kwa  Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016. Nyuma yao ni Mama Janeth Magufuli na wanafamilia wa Mzee Jumbe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kaburini na kutoa heshima zake alipokwenda kutoa mkono wa pole nyumbani kwa  Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi  Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016.

RAIS DKT MAGUFULI AZURU KABURI LA MAREHEMU SHEIKH ABEID AMANI KARUME, AWEKA SHADA LA MAUA

September 03, 2016


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akitoka katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016 baada ya kuweka saini kitabu cha wageni kabla ya kuzuru na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akitoa heshima zake baada ya akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.
 Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli,  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume katika ofisi Kuu ya CCM Makao Kisiwandui mjini Zanzibar leo Agosti 3, 2016.

BALOZI WILSON MASILINGI ATEMBELEA CHUO CHA MTANZANIA WINSTON SALEM, NC.

September 03, 2016



Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akitia saidi kitabu cha wageni katika chuo kinachomilikiwa na Mtanzania Dr. Lucas Shallua kilichopo Winston Salem, North Carolina siku ya Ijumaa Septemba 2, 2016.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akifanya mazungumuzo na mmiliki wa chuo cha Mount Eagle College &University Dr. Lucas Shallua siku ya Ijumaa Septemba 3, 2016 Balozi Wilson Masilingi alipotembelea chuo hicho kilichopo Winston Salem, North Carolina.
 Mazungumuzo yakiendelea, wengine katika kufuatilia mazungumuzo hayo kutoka kushoto ni ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana, Dr. Dorothy Edward Shallua (mke wa Dr. Lucas Shallua), Mke wa Balozi Marystela Masilingi, na mwenyeiki wa Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex.
 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akimsikiliza Dr. Lucas Shallua alipokua akimwonyesha moja ya darasa linalotumia kurekodia masomo ya matandaoni.
 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akimsikiliza Dr. Lucas Shallua (kulia) alipokua amkitembeza na kumwonyesha chuo cha Mount Eagle College & University kilichopo mji wa Winston Salem, North Carolina. Wengine katika picha kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex, Mke wa Balozi Bi. Marystela Masilingi, nyuma ya Balozi asiyeonekana ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana na Mke wa Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua.
 Moja ya madarasa chuoni hapo.
 kutoka kushoto ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex, nyuma ya Mhe. Balozi ni mkewe Marystela Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi, mke wa Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua na Dr. Lucas Shallua ambaye akitoa maelezo kwa Mhe. Balozi wakati akimtembeza na kumwonyesha chuo hicho.

TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 235 KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI MARA

September 03, 2016

Mkuu  wa  Mkoa  wa Mara Dkt. Charles Mlingwa  akiongea na wazazi,walimu na wanafunzi wa shule ya msingiUtegi wilayani Rorya wakati wa hafla ya kukabidhi  madawati   kwa  shule hiyo  jana. Jumla  ya madawati 235 yalitolewa kwa mkoa huo. Pichani kutoka kushoto Meneja waTigo Mkoa wa Mara, Edwin Kisamo,Meneja wa Tigo kanda ya  ziwa, Edgar Mapande ,Mkuu wa wilaya ya  Rorya, Simon Chacha  na   Mwenyekiti wa  Halmashauri  mka Mara, Albert Machiwa

Meneja wa Tigo  Mkoa wa Mara, Edwin Kisamo akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Utegi  wilayani Rorya wakati   wa  hafla ya kukabidhi madawati kwa shule hiyo jana.

Meneja wa  Tigo  kanda ya  ziwa, Edgar Mapande  akiongea na  walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Utegi wilayani Rorya wakati wa hafla ya kukabidhi  madawati kwa shule  hiyo  jana, Wengine  pichani  kushoto  kwake  ni  mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt.Charles  Mlingwana  Mkuu wa wilaya ya   Rorya, Simon Chacha.

Mkuu wa Mkoa  wa Mara Dkt. Charles Mlingwa  akipokea  madawati 235 kwa  mkoa   wa Mara toka  kwa  Meneja  wa Tigo kanda ya  ziwa, Edgar Mapande  kwenye hafla  iliyofanyika  shule  ya  msingi   Utegi  wilayani   Rorya    jana


Mkuu wa mkoa  wa Mara Dkt. Charles Mlingwa  na  Meneja  wa   Tigo  kanda  ya  ziwa, Edgar Mapande  wakinyanyua mikono   juu   mara  baada  ya  makabidhiano  ya  madawati 135 kwa  wilaya ya Rorya na jumla ya   madawati 235 kwa  mkoa  wa Mara, hafla  iliyofanyika  shule yamsingi  Utegi wilayani  Rorya  jana

  


Wanafunzi wa  shule  ya   msingi   Utegi   wakiwa  wameketi kwenye madawati waliopewa na kampuni ya simu za mkononi Tigo    jana.


DIANA EDWARD NDIYE LETE RAHA MISS KINONDONI 2016

September 03, 2016
 Malkia wa Kinondoni 2016 Diana Edward ndiye huyu hapa.
 Lete Raha Miss Kinondoni 2016, Diana Edward (katikati), akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa mshindi Dar es Salaam jana. Kulia ni  mshindi wa pili Regina Ndimbo na kushoto ni mshindi wa tatu, Sia Pius.
 Warembo hao wakiserebuka wakati wakijitambulisha.
 Wadau wakifuatilia kwa karibu shindano hilo. 
 Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika vazi la ubunifu. Kutoka kushoto ni Catherine Liston, Hafsa Mahamoud na Mariana Charles.

 Washiriki hao waliofanikiwa kuingia 10 bora.
 Washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora. Kutoka kulia ni Hafsa Mahamoud, Diana Edward ambaye ndiye Miss Kinondoni 2016. Regina Ndimbo, Sia Pius na Jackline Kimambo.

Majaji wa shindano hilo wakiwa kazini.

Mgeni rasmi wa shindano hilo, Gift Msuya (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo.

 Hapa ni sebene kwa kwenda mbele.
 Wakina mama wakimtuza mwanamuziki Christian Bella wakati akiimba wimbo wa Nani kama mama.

Mgeni rasmi wa shindano hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya (katikati), akikabidhi zawadi.

Na Dotto Mwaibale

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Lete Raha Miss Kinondoni  2016 imemtangaza Diana Edward  kuwa mlimbwende wa wilaya hiyo baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana.

Edward aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake 20 waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Regina Ndimbo huku ya tatu ikichukuliwa na Sia Pius ambapo Happyness Munisi akishinda nafasi ya utanashati.

Akizungumza wakati wa mchakato wa kutoa zawadi Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George alisema asilimia 10 ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo yatakwenda Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure katika mazingira bora.

Katika shindano hilo washindi waliofanikiwa kuingia tano bora wataingia moja kwa moja katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia bia ya Windhoek Lager na Draught pamoja na Gazeti la Lete Raha na wadhamini wengine.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift  Msuya alisema Serikali itaendelea kuunga mkono mashindano hayo ambayo yamekuwa yakitoa ajira na kuibua vipaji vya watoto wa kike.

Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa dansi Christian Bella na kundi la sanaa la Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd.



JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI JIJNI MWANZA.

September 03, 2016
Taasisi mbalimbali zikiwemo za Serikali na binafsi kutoka ndani na nje ya nchi zimeshiriki Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki, yanayofanyika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza. Maonesho hayo huandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini, TCCIA.

Taasisi mbalimbali za Wajasiriamali, Wafanyabiashara na Viwanda hutumia Maonesho hayo kukutana na wateja wapya, kutangaza na hata kuuza bidhaa zake. Mbali na hilo taasisi mbalimbali hutumia fursa hiyo kukutana na wananchi na kufikisha elimu husika.

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kujumuisha vitengo vyake ikiwemo Kikosi cha Usalama barabarani na dawati la jinsia, limetumia maonesho hayo kufikisha elimu mbalimbali kwa wananchi na hata kupokea maoni kutoka kwa wananchi.
Na BMG
Banda la Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Kitengo cha dawati la jinsia
Banda la Jeshi la polisi mkoani Mwanza, kitengo cha Usalama barabarani
Maonesho hayo yalianza Agosti 26,2016 na ufungi rasmi kufanyika Agosti 30,2016 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela alifungua Maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kama picha inavyoonekana mgeni rasmi akiwa kwenye banda la jeshi la polisi mkoani Mwanza.
Endelea kutazama picha, Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, akikagua mabanda ya washiriki mbalimbali
Soma zaidi HAPA