RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA KAGOMA-BIHARAMULO-LUSAHUNGA YENYE UREFU WA KILOMETA 154

July 19, 2017
 Rais Dkt John pombe Magufuli mapema leo amefungua barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda
 Rais Dkt John pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya akina Mama waliofika kushuhudia hafla fupi ya ufunguzi wa barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda. Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akipungia vikundi vya kwaya,ngoma na Burudani alipowasili kwenye viwanja vya stendi ya Biharamulo tayari kwa kuzindua Barabara ya Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Baadhi ya waananchi waliohudhuria uzinduzi wa Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,wakimsikiliza kwa makini Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, wakati akiwahutubia 19 Julai 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mustafa kijuu akisoma taarifa ya mkoa wake mbela ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,wakati wa ufunguzi wa Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akihutubia wananchi wa Biharamulo wakati wa ufunguzi wa Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.

NAIBU WAZIRI MANYANYA :AWATA WAZAZI KUFUATILIA MAENDELEO YA WATOTO WAO .

July 19, 2017
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya wa pili kutoka kulia akitembelea shule ya Msingi Bagamoyo wakati wa ziara yake wilayani Korogwe kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel na anayefuatia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akiwasili katika shule ya Msingi Matondoo wakati ewa ziara yake ya kukagua maendeleo ya sekta hiyo wilayani Korogwe
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akisalimiana na walimu wa shule ya msingi Matondoo wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya wa pili kutoka klushoto akimsikiliza Afisa Tarafa ya Korogwe mjini,Michael John kuhusu ujenzi wa baadhi ya madarasa kwenye shule hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Mji,Jumanne Shauri anayefuatia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel wakati wa ziara yake wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akiwa ameshika mtoto wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Jumanne Shauri
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Bagamoyo iliyopo wilayani Korogwe ambapo aliwataka kusoma kwa bidii ili waweze kupata mafanikio

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Jumanne Shauri akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Matondoo wakati wa ziara hiyo ambapo aliwataka kutilia mkazo masomo ya sayansi
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akisalimia na wananchi wa Jimbo lake wakati wa ziara hiyo ya
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe ,Jumanne Shauri akizungumza katika ziara ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanyawa tatu kutoka kulia
Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza katika halfa hiyo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akimuonyesha kitu Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati waliojiwekea kuhakikisha wanapiga hatu kubwa kielimu
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya ambaye hayupo pichani

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya katika akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mhandisi Robert Gabriel kushoto wakati wa ziara yake alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa maktaba ya wilaya hiyo ambao umeshindwa kuendea kwa muda mrefu ambapo aliagiza uendelezwe kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Mji Jumanne Shauri na
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia,
Mhandisi Stella Manyanya akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi matondoo

SPORTPESA YATOA SHUKRANI KWA WANAHABARI, SERIKALI, VYOMBO VYA DOLA NA WANANCHI KUFANIKISHA ZIARA YA EVERTON

July 19, 2017
 Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sportpesa, Tarimba Abbas akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo,  ambapo alitoa shukrani kwa wanahabari, vyombo vya dola, serikali na watanzania kwa kufanikisha ziara ya timu ya Everton ya Uingereza hapa nchini. PICHA , HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Tarimba alisema kuwa ziara ya Everton nchini imekuwa ni ya mafanikio makubwa kimichezo, kiuchumi, kijamii na hasa kuutangaza vilivyo utalii wa Tanzania Duniani.

Tarimba hakusita pia kuishukuru Ikulu kwa kuwapa sapoti kubwa kufanikisha ziara ya Everton hasa katika masuala ya kumpata mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na kuruhusu  vyombo vya dola kwa ajili ya usalama wa timu hiyo.

"Kwa niaba ya SportPesa ambao ndiyo wadhamini wakuu wa timu hiyo, tutakuwa wachoyo wa fadhila kama tutashindwa kuwashukuru wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine walituunga mkono  katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya ziara hii yanafanikiwa." Alisema Tarimba na kuongeza kuwa...

Napenda Kumshukuru Rais  John Magufuli kwa kutoa baraka zake, lakini pia nipende kumshukuru  Makamu wake Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa utayari wa kuwapokea wageni wetu ."

Alimshukuru pia Waziri wa Habari, Utamadjuni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe  kwa niaba ya wizara hiyo kwa kuwa bega kwabega  katika jukumu hilo hizo. Pia hakusita kutoa pole kwa waziri huyo kwa kufiwa na mkewe.
 Tarimba akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya kampuni hiyo, Oysterbay Dar es Salaam.

 Tarimba akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na vyombo vya habari.
Wanahabari wakisilkiliza majibu ya maswali yao waliyomuuliza Tarimba

Tigo kuungana na wabia wengine kuongeza kasi katika upatikanaji wa Mtandao wa simu kwa wananchi 70,000 katika maeneo ya vijijini Tanzania

July 19, 2017
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Tigo Simon Karikari (wa kwanza kulia) akchangia mada wakati wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknolojia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu ulioandaliwa na GSMA360 Afrika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

MAOFISA UGANI WA WILAYA YA BUKOMBE WATAKIWA KUWA NA KUMBUKUMBU ZA KILIMO

July 19, 2017



 Mkuu wa wilaya ya Bukombe,. Joseph Maganga (kulia), akizungumza na maofisa Ugani wa Wilaya hiyo kwenye mafunzo ya kilimo cha mazao ya Mihogo,Pambana Viazi lishe yaliyoandaliwa na Tume yaTaifa yaSayansi na Teknolojia(COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia OFAB. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya hiyo, Zacharia Bwile na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Baraka Maganga.

WAZIRI JAFFO AONYA WATAKAOKWAMISHA JITIHADA ZA GREEN VOICES KUPAMBANA NA MAZINGIRA

July 19, 2017
Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) akisikiliza maelezo kutoka kwa mama Abia Magembe kuhusu bidhaa zinazotokana na zao la muhogo. Kushoto kabisa ni Mratibu wa Mradi wa Green Voices kutoka Hispania, Alicia Cebada na kulia ni Mratibu wa mradi huo nchini Tanzania, Secelela Balisidya.

NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo, amesema halmashauri zinawajibu wa kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

JUMIA TRAVEL YAZINDUA YAUNGANISHA MFUMO WA HUDUMA KWA WATEJA NA FACEBOOK MESSENGER

July 19, 2017


Kampuni inayoongoza kwa uwakala wa huduma za kusafiri mtandaoni Afrika, Jumia Travel imezindua mfumo mpya wa huduma kwa wateja kupitia ‘Facebook Messenger’ kwa kushirikiana na Salesforce (Kampuni kinara kwenye Usimamizi wa Huduma kwa Wateja)

WILAYA YA GEITA KUTENGA MILIONI 50 KWA AJILI YA MAFUNZO YA KUBORESHA KILIMO

July 19, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi akizungumza wakati akifungua  mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani  wa wilayani yake wilayani humo jana yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),  yenye lengo  la kuwakumbusha wataalamu hao wa kilimo nafasi yao pamoja na kuwapatia mbinu mpya za kisasa katika kulima mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi vitamu katika kuelekea serikali ya viwanda. 

Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma yatumia Tehama kuboresha utoaji wa huduma kwa umma

July 19, 2017

Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katika Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Usikose kuangalia kipindi hiki uone jinsi ambavyo TEHAMA inasaidia kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katrina taasisi hiyo



HAPPY BIRTHDAY MWANALIBENEKE KRANTZ MWANTEPELE

July 19, 2017


Leo tarehe 19 July ni siku ya kuzaliwa Mwanalibeneke la blogu  Krantz Mwantepele ambaye ni Mkurungezi Mtendaji  wa KONCEPT , Mkurungezi Mtendaji wa ROGECH ANIMATIONS & VFX na pia katibu wa Tanzania Blogers Network  kwa  niaba ya wasomaji  wetu tunapenda kukutakutakia maisha marefu na yenye baraka na fanaka tele.


Mungu akupe maisha marefu na kukupa mwongozo sahihi kwa ndoto zako za kuweza kutengeneza ajira kwa vijana wenye nia na ari ya kujiajiri .

Mnaweza kutembelea blog zinazomilikiwa na  KONCEPT

Mwanaharakati Mzalendo Blog link www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com


Mzalendo Times link www.mzalendotimes.blogspot.com


Na hivi karibuni kutazinduliwa KONCEPT TV (ONLINE TV)

Pia unaweza kumfuata Krantz katika mitandao ya kijamii kama
 Facebook kwa jina la Mwanaharakati mzalendo  https://www.facebook.com/MWANTEPELE

Instagram/ twitter  @ mzalendo89


 "   HAPPY BIRTHDAY KRANTZ "