UN NA EU WAENDELEZA KAMPENI YA UELEWA WA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

November 28, 2016
UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wamejiunga pamoja kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini Tanzania . Aidha kwa pamoja wamezuru miradi iliyofadhiliwa na EU. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Mkwawa kwenye semina iliyoelezea malengo hayo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani. Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.(Picha zote na Zainul Mzige wa Moblog)

Semina katika vyuo hivyo ni sehemu ya mpango madhubuti wa Umoja wa mataifa uliozinduliwa Arusha Mei mwaka huu na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez wenye lengo la kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia. Ujumbe huo wa EU na UN pia ulipata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na EU ukiwamo wa Boma la Kijerumani ambalo lilikarabatiwa kwa ruzuku ya EU kupitia 'fahari yetu – Southern Highlands Culture Solutions'. Boma hilo ni moja ya majengo ya zamani katika mji wa Iringa na lilijengwa na Wajerumani mwaka 1900 kama hospitali ya kijeshi. Baada ya vita ya Kwanza ya Dunia, jengo hilo lilibadilishwa matumizi na watawala wapya, Uingereza, na kulifanya kuwa jengo la utawala. EU imesema inaona fahari kuwa mmoja wa wawekezaji wakubwa katika sekta ya sanaa na urithi wa kitamaduni nchini Tanzania, ikifadhili miradi 10 iliyo chini ya programu ya 10 ya EDF ya kusaidia masuala ya kitamaduni.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (upande wa kushoto katikati) pamoja na Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) alipotembelewa ofisini kwake na ugeni huo. Kulia ni Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever pamoja na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi.

Masuala yanayohusu urithi wa kitamaduni ni muhimu katika kuchagiza ukuaji wa uchumi, ajira na huku ikifuma mahusiano ya kijamii, na kutoa fursa ya kuboresha utalii endelevu mkoani Iringa huku ikileta faida kwa wakazi wa eneo hilo. Bw. Rodriguez, akizungumza katika kampeni hiyo alisema kwamba ajenda 2030 ambayo ni ajenda ya maendeleo endelevu inahitaji ushiriki wa kila mmoja.Aliwapongeza wanachuo hao na wanazuoni kwa kujikita kutambua malengo hayo ya dunia. Aidha aligusia umuhimu wa vijana kushiriki katika masuala ya maendeleo kutokana na ukweli kuwa, kwa taifa kama la Tanzania vijana ni asilimia 60 ya wananchi wote waliopo.Alisema kwamba vijana wanajukumu kubwa la kushiriki katika maendeleo hayo kwa lengo la kuipeleka nchi katika hatua nyingine ya maendeleo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa ameongozana na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Chuo Kikuu cha Iringa.

Hata hivyo alisema kwamba ni wajibu wa kila mtu hasa vijana, kuhakikisha kwamba malengo hayo ya dunia yanafanikiwa . Alisema Umoja wa Mataifa kwa kusaidiwa na wadau wake muhimu kama Umoja wa Ulaya, utaendelea kusaidia Watanzania kuwajibika katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuunga mkono malengo hayo ya dunia. Mmoja wa washiriki alipongeza Umoja na wa Mataifa kwa kuwafikia vijana wa vyuoni na kuwapa semina hiyo. “Ninajisikia mtu mwenye bahati kupata nafasi ya kujifunza maendeleo endelevu kutoka kwa Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini. Nikiwa kama kijana, naona faraja kuona kwamba viongozi wetu wanafuata maelekezo yaliyofafanuliwa kwenye malengo 17 ya maendeleo endelevu; naamini kama tukijitahidi kuyafikia ifikapo 2030, basi Tanzania na duniani kwa ujumla itakuwa eneo jema la kuishi. Na kwa kuwa sasa natambua kuhusu malengo hayo ya dunia, ninaweza kutoa mchango wangu kusaidia kuyafikia -najisikia kuwezeshwa sana.” amesema Mary, mmoja wa washiriki.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akisoma taarifa fupi ya Chuo Kikuu cha Iringa mbele ya ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya wakati semina kuhusu malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.

RAIS DKT.MAGUFULI AMWANDALIA RAIS EDGAR LUNGU DHIFA YA KITAIFA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

November 28, 2016

 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili AlhajAli Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu kwa dhifa hiyo ya kitaifa aliyomwandalia mgeni wake Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.
 Meza kuu ikiwa imesimama kwa Wimbo wa Taifa
 Rais Dkt Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia kusalimiana na viongozi mbalimbali
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akisherehesha hafla hiyo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
 Rais Edgar Lungu wa Zambia akigonganisha glasi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Wimbo wa Taifa 
 Viongozi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Zambia ukipigwa
 Viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na Mkuu wa Itifaki wa Zambia wakiwa wamesimama kwa wimbo wa Taifa 
 Sehemu ya Mawaziri waliohudhuria wakiwa wamesimama
 Viongozi wakiwa wamesimama
 Makatibu wakuu na sehemu ya ujumbe wa Zambia
 Wageni waalikwa na viongozi wa vyama vya siasa
 Baadhi ya mabalozi mbalimbali waliohudhuria
 Wageni mbalimbali

RC SINGIDA AANZA ZIARA KUTEMBELEA KATA 136 ZA MKOANI SINGIDA

November 28, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara Kijijini Doroto
 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe katika ziara yake katika Halmashauri ya Itigi
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Godfrey Mwambe akiongea na wananchi katika ziara ya mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew J. Mtigumwe

Na Mathias Canal

Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii leo ameanza ziara ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Mkoa wa Singida.

Rc Mtigumwe ameanza ziara yake hiyo katika Halmashauri ya Itigi, iliyopo katika Wilaya ya Manyoni ambapo atatembelea kata zote za halmashauri hiyo.

Pamoja na kutambua kero za wananchi na mambo mengine pia Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida anatumia mikutano hiyo maalumu kwa ajili ya kufahamiana na wanachi ikiwa ni pamoja kusikiliza kero zao ambazo zimewasua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi.

Mtigumwe akiwa katika Kijiji cha Doroto amehimiza zaidi wananchi kuandaa vyema mashaba yao na kuzingatia kilimo chenye kustahimili ukame kwani kuna mabadiliko makubwa ya tabia nchi jambo ambalo limepelekea kuchelewa kuanza kwa mvua.

Mhe Mtigumwe amewaagiza maafisa kilimo wa Kata na Wilaya zote za Mkoa wa Singida kutokaa ofisini kipindi hiki cha msimu wa kilimo badala yake kwenda mashambani kuwasaidia wananchi mbinu bora za kilimo sambamba na kuwasaidia namna bora ua kuandaa mashamba.

Sambamba na hayo pia amewasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo watakayopatiwa na Maafisa kilimo ili kuwa na uhakika wa kuvuna mazao mengi zaidi kwa kilimo chenye tija.

Katika ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Singida.

NYUMBA YA KISASA INAUZWA IPO JIRANI NA UWANJA WA MPIRA WA AZAM CHAMAZI TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

November 28, 2016






Mwonekano wa Mbele wa nyumba hiyo.


NYUMBA INAUZWA IPO WILAYA YA TEMEKE KATA YA CHAMAZI KARIBU NA UWANJA WA MPIRA WA AZAM NI SEIF CONTAINED NA INA MASTER ROOM NA CHUMBA KIMOJA CHA KULALA, SEBURE, JIKO NA CHOO NA BAFU LA NDANI, BEI NI SHILINGI MILIONI 19 KWA MAWASILIANO PIGA SIMU NAMBA 0687-347676 AU O759-239338. 

MAJALIWA AAGANA RAIS WA CHAD ALIYEONDOKA NCHINI LEO

MAJALIWA AAGANA RAIS WA CHAD ALIYEONDOKA NCHINI LEO

November 28, 2016
mchec3
Rais wa Chad, Idriss Deby akiwapungia wananchi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam wakati alipoondoka nchini Novemba 28, 2016. Kulia ni  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  ambaye alimsindikiza na kushoto ni mke wa Rais wa Chad, Hinda Deby. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mchec4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais wa Chad, Idriss Deby  kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam wakati Rais huyo alipoondoka nchini Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mchec5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Chad, Idriss Deby kwenye uwanja wa ndege wa Julius kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya Rais huyo kuondoka nchini Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mchec6
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Rais wa Chad, Idriss Deby  kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati Rais huyo alpoondoka nchini Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mchec8
Rais wa Chad, Idriss Deby akipokea heshima kwenye uwnja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati alipoondoka nchini Novemb 28, 2016.  Kushoto kwake ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alimsindikiza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RC GAMBO ATOA PIKIPIKI 200 KWA WANDESHA BODA BODA ARUSHA

November 28, 2016


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (aliyesimama) akiongea na madereva wa boda boda kuwaelezea mpango wa Serikali wa kuwapatia Pikipiki 200.

Nteghenjwa Hosseah

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amekutana na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha na kuwajulisha kuhusu mpango wa Serikali wa kuwakwamua kiuchumi kwa kuwawezesha kupata Pikipiki bila Riba wala dhamana.

Rc Gambo amekuja na Mpango huu wa Kuinua uchumi wa Vijana kwa kuwapatia Pikipiki baada ya kukutana na kundi hili la waendesha boda boda kwa mara na kusikiliza malalamiko yao huku miongoni mwa kero yao kubwa ni kutozwa fedha nyingi na wamiliki wa boda boda hizo.

Akiongea na waendesha boda boda Rc Gambo alisema ninaona jinsi mnavyojituma katika kujitafutia riziki lakini hamthaminiki na kazi hii imekua ikidharaulika, sasa muda umefika kwa kazi hii kuwa ya heshima mbele ya Jamii, kila kijana aliyepo katika biashara hii ataweza kumiliki Pikipiki yake na sio kuendesha Pikipiki za watu ambao wamekuwa wakiwanyonya kila siku kwa kuwatoza Fedha nyingi na wao kuzidi kuneemeka wakati ninyi mnazidi kuwa masikini.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Katikati) akiwasili kwenye Kikao na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha.

“Kundi hili limekuwa likitumiwa kwa maslahi ya watu wachache kwa kuwa wamekuwa wakipewa Pikipiki hizo kwa faidi kubwa na mmiliki anapokea Fedha zaidi yya mara mbili ya bei ya kununulia Pikipiki hiyo ndipo aamue kummilikisha kijana pikipiki hiyo au aamue kuendelea kupokea Fedha kwa kipindi chote wakati ninyi mnapata tabu barabarani huko na mnaambulia Fedha kidogo kiasi ambacho hamuwezi fikia hatua ya kumiliki Pikipiki zenu” Alisema Gambo.

Aliongeza kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imeona ni vyema ikawajengea uwezo vijana waliopo katika kazi hii kwa kuwapa mafunzo na kuwapatia Pikipiki ambazo mtatakiwa kurejesha kiasi cha Fedha halali iliyonunuliwa Pikipiki hiyo kisha kumilikishwa chombo bila ya riba yeyote wala dhamana.
Lucas Malusu ni dereva wa boda boda Kutoka Kata ya Elerai (aliyesimama katikati) akitoa maoni yake katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Bayport yatoa msaada wa kompyuta za Sh Milioni 500 kwa Serikali

November 28, 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga akikabidhi moja ya kompyuta zilizokabidhiwa na Taasisi yake kwa ajili ya serikali. Anayepokea ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo imeipatia serikali msaada wa kompyuta 205 zenye thamani ya Sh Milioni 500 kwa ajili ya matumizi yao ya kiofisi, kwa kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga wa pili kutoka kushoto waliosimama, akipeana mkono na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala, Mheshimiwa Angellah Kairuki baada ya kukabidhiwa kompyuta 205 na Taasisi ya Bayport, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Laurean Ndumbaro na Kaimu Katibu Mkuu Bi Susan Mlawi.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam, ambapo kompyuta 125 zitabaki Makao Makuu ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kompyuta 80 zilizosalia zitagawanywa na Wizara yenyewe kwa kuangalia mahitaji ya ofisi zao.
Baadhi ya Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia halfa ya makabidhiano ya kompyuta kutoka kwa Taasisi ya Bayport Financial Services.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, alisema msaada wa kompyuta hizo zinatokana na kiu yao kubwa ya kushirikiana na serikali kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa ajili ya kufanikisha huduma bora kwa Watanzania.

Alisema taasisi yao ilipanga wamalize mwaka kwa kukabidhi kompyuta kwa ofisi za serikali, ikiwa ni mwendelezo wa kusherehekea miaka 10 ya huduma zao tangu Bayport ilipoanzishwa mwaka 2006 nchini Tanzania.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki katikati akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa kompyuta kutoka kwa Bayport Financial Services leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Dk Laurean Ndumbaro na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bayport, John Mbaga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala, Mheshimiwa Angellah Kairuki wa pili waliosimama mstari wa mbele, akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi Susan Mlawi pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Laurean Ndumbaro kulia kwa waziri wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Bayport na baadhi ya wakuu wa Idara wa Ofisi ya Rais.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki, akizungumza katika halfa ya makabidhiano kompyuta 205 za aina mbalimbali kutoka kwa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa ofisi za serikali nchini Tanzania. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Bayport, John Mbaga.

“Tunakabidhi kompyuta hizi 240 kwa serikali huku tukijipa moyo kuwa zitatumiwa ipasavyo na watumishi wetu wa umma wanaotuhudumia katika majukumu yao na kuongeza ufanisi, hivyo Bayport itaendelea kushirikiana na serikali kwa nguvu zote.

“Sisi jukumu letu ni kushirikiana na serikali sambamba na kujitolea kwenye jamii kwa kusaidia mambo mbalimbali kwa ajili ya kuwakwamua wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kwa kupitia sekta ya mikopo,” Alisema.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki, aliishukuru Bayport kwa kutekeleza ahadi yao ya msaada wa kompyuta kwenye wizara yao.

Alisema wamevutiwa na kompyuta hizo zilizotolewa kwa wakati muafaka, huku akisema zitarahisisha utoaji wa huduma bora kwa watumishi wa umma katika ofisi watakazopokea baada ya kufikishwa kwao.

“Tulipata taarifa kuwa wenzetu wa Bayport wanatuletea msaada huu ambao kwa hakika ni mkubwa na umekuja wakati muafaka na utawawezesha watumishi wetu kufanya kazi vizuri kwa kupata hivi vitendea kazi,” alisema.

Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo ya fedha kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, huku pia ikitoa huduma za mikopo ya viwanja katika miradi yake ya Bagamoyo, Kigamboni, Kibaha na Kilwa.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA ZAMBIA EDGAR CHAGWA LUNGU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

November 28, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu wakipita katikati ya Gadi ya Mapokezi iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.