NAIBU WAZIRI ULEGA AIAMBIA KAMATI YA BUNGE KUWA SERIKALI INA MTAZAMO WA KUIFANYA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI KUWA SEKTA YA UZALISHAJI

March 17, 2018

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Hamis Ulega (Mb) kulia akiongea na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji ilipotembelea chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)  kampasi ya Kigoma jana, wabunge wa kamati hiyo wameambata na maafisa mbali mbali kutoka serikalini.

Kushoto  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Hamis Ulega (Mb) akizunguma katika kikao na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji katika chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)  kampasi ya Kigoma jana, kati kati ni mwenyekiti wa kamati Hiyo Mhe. Mahmoud Hassan  Mgimwa (Mb.) Kalenga na kulia ni Makamu Mwenyekiti Mhe. Christine Gabriel Ishengoma (Mb).




Pichani Mbele ni baadhi wa wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji wakifuatilia mazungumzo katika kikao wakati wa ziara yao katika chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)  kampasi ya Kigoma jana,wengine ni watumishi wa serikali.





NA MWANDISHI MAALUM  - KIGOMA
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdalah Hamis Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ameiambia kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji kuwa, Serikali ina mpango wa kuifanya sekta ya Mifugo na Uvuvi kuwa na mchango mkubwa katika pato la Taifa.
 
Naibu Waziri HamisUlega ameyasema hayo leo Mkoani Kigoma mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji, ilipokuwa katika ziara ya kutembelea  chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)  kampasi ya kigoma jana.
Mhe. Ulega amesema  Wizara yake ina Mkakati  wa kulinda rasilimali za Mifugo na Uvuvi, kwa kuimarisha uvuvi wa bahari kuu na kuitoa sekta hiyo  kwenye kuchangia kiasi na shilingi Bilioni 19 kwa  mwaka katika pato la taifa hadi kufikia kuchangia zaidi ya shilingi Bilioni 50 kwa mwaka.
“Tunaweza kufikia malengo haya kwanza kwa kuimarisha uvuvi wa Bahari kuu kwa kuhakikisha kwanza tasisi yetu ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu inakuwa na nguvu kwa kuweka vizuri sheria na kanuni zetu za uvuvi ikiwa ni pamoja na kufufua shirika letu la TAFICO, Alisema Ulega.”
Sambamba na hilo, Ulega alisema Serikali ina mkakati wa kuwa na Meli ambayo itakuwa na uwezo wa kwenda kuvua na kuchakata mazao ya samaki, jambo ambalo litakwenda sambamba na ufunguaji wa viwanda vya uchakataji wa mazao ya uvuvi.
Naibu Waziri Ulega pia alisema serikali ina lengo la kuhamasisha uwekezaji katika  sekta ya Uvuvi kupitia mafunzo, utafitu na  elimu ya ugani kupitia vyuo vya Feta , ili kuweza  kuwa na wataalam wa kutosha pamoja na kuipa nguvu wakala hiyo ili kuweza  kutoa wataalam  kwani mpaka sasa sekta ya uvuvi  ina uhaba wa wataalam na kuongeza kwa kusema kuwa kwa upande wa utafiti serikalii ina mkakati mkubwa wa kuweza kuiwezesha TAFIRI kwa kuipa kazi maalum za tafiti akitolea mfano wa uelewa mdogo wa baadhi ya wavuvi kuhusiana na zana halali za uvuvi.
Akizungumzia suala la kuingiza samaki aina ya vibua na sato kutoka nje ya nchi, Ulega alisema, “Ukiangalia kwa makini sioni sababu ya kwanini tutoe mathalani kiasi cha shilingi Bilioni 50 kwa mwaka tuwapelekee wavuvi wengine na tuingize tani  elfu 20 na zaidi kuleta hapa ndani za samaki ambao sisi wenyewe tunao.” Alisisitiza Ulega.
“ Ipo Mikakati kwa serikali ya kuwatengenezea wafanya biashara ya samaki mazingira mazuri ili pesa hiyo  iwekezwe hapa nchini.” Alisema.
Awali akitolea mfano wa ulinzi wa rasilimali za uvuvi Ulega alisema “Tumefanya ulinzi wa rasilimali za uvuvi katika ziwa Victoria kwa muda mfupi tu ikiwa ni pamoja na ulinzi wa  utoroshwaji wa Mazao ya Uvuvi nje ya nchi na tumeingiza kiasi kikubwa cha fedha.” Alisema.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka Sekta ya Uvuvi Dkt. Yohana Budeba alisema kuwa njia ya ufugaji wa samaki wa kisasa kupitia chuo cha FETA kitatengeneza wataalam na kuongeza ajira na kupatikana samaki wengi na kupelekea mchango mkubwa wa sekta ya uvuvi katika uchumi wa taifa hili.
WATUMISHI WA AFYA WAJIEPUSHE NA VITENDO VYA RUSHWA SEHEMU ZAO ZA KAZI

WATUMISHI WA AFYA WAJIEPUSHE NA VITENDO VYA RUSHWA SEHEMU ZAO ZA KAZI

March 17, 2018

1
Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akifungua Mkutano Wa Balaza la Wafanyakazi Wa Wizara ya Afya mapema leo Jijini Dar es salaam.
2
Mganga Mkuu Wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(hayupo kwenye picha)
3
Mkurugenzi Wa Mafunzo na Rasilimali watu Dkt.Otilie  Gowelle wakwanza kulia akifuatilia kwa makini maagizo ya Waziri Wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
4
Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu na mganga Mkuu wa Serikali Prof. Kambi wakati wakiimba wimbo wa kuhamasisha umoja na mshikamano kwa Wafanyakazi, pindi wakifanya mkutano wa Baraza la Wafanyakazi, Wakwanza ni Katibu wa Baraza hilo Mary Ntira na wa mwisho ni Afisa Elimu kazi na mratibu wa Jinsia taifa TUGHE Bw. Nsubisi Mwasandende
5
Watumishi wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Dorothy Gwajima wapili kutoka kulia.
6
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu katikati waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi kutoka Wizara ya Afya mara baada ya kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Leo jijini Dar es salaam.
………………….
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
WATUMISHI wa sekta ya Afya nchini wametakiwa kujiepusha na vitendo vya kutaka rushwa kutoka kwa wananchi wanapokuwa sehemu zao za kazi ili kuendana na maadili ya utumishi wa Umma. 
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo jijini  Dar es salaam ili kujadili mustakabari wa utoaji huduma za Afya nchini. 
“Marufuku Watumishi wa sekta ya afya nchini kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na kama wapo naomba waache mara moja kwani atakayebainika anajihusisha na rushwa sheria itafuata mkondo wake mara moja” alisema Waziri Ummy. 
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa watumishi wa sekta ya afya hasa katika sehemu ya kutolea huduma za afya wanatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wananchi pindi wanapotoa huduma sehemu zao za kazi. 
Mbali na hayo Waziri Ummy amewaambia watumishi wa sekta ya afya kuwa kipaumbele katika kutoa elimu juu ya magonjwa yasioambukiza kwani yamekuwa yakiongezeka kila kukicha kutokana na ukosefu  elimu ya kutosha kuhusu magonjwa hayo. 
“Watumishi wa Afya wanatakiwa kuwa mfano hasa katika kufanya mazoezi,  kula lishe bora pamoja na kutoa elimu ya magonjwa mbalimbali ili kuisaidia kuondoa ongezeko la magonjwa yasioambukiza” alisema Waziri Ummy. 
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa ili kufikia adhma ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli la kujenga uchumi wa Viwanda ni lazima kuzingatia utoaji wa huduma bora za afya ili kuwa na wananchi  wenye afya ambao watasukuma gurudumu kufikia lengo hilo. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Taifa wa Balaza la Wafanya kazi TUGHE Bw. Nsubisi Mwasandende amesema kuwa katika kutatua changamoto za magonjwa mbalimbali watendaji wa Wizara ya Afya wanatakiwa kuzingatia hali ya upatikanaji wa chanjo ili kuboresha huduma za afya. 
Aidha Bw.  Mwasandende amesema kuwa watumishi wanatakiwa kulifanyia kazi haraka  agizo la Waziri Ummy Mwalimu la kutokomeza vitendo vya rushwa haraka iwezekanavyo  ikiwa kama moja la adhimio la katiba ya balaza la wafanyakazi.(Chanzo FullshangweBlog)
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KUJADILI MIKAKATI YA JESHI LA MAGEREZA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KUJADILI MIKAKATI YA JESHI LA MAGEREZA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA

March 17, 2018

PIX 1
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa, akisalimiana na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza, Gaston Sanga  mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Nanenane, Mkoani Mororogoro tayari kwa Kikao Maalum cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja leo 17 Machi, 2018 Mkoani Morogoro.
PIX 2
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza kufungua rasmi kikao kazi hicho.
PIX 3
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao Maalum cha kujadili mikakati ya utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula.
PIX 4
Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani).
PIX 5
Washiriki wa Kikao kazi ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifanya maadiliano mbalimbali katika vikundi kama inavyoonekana katika picha.
PIX 6
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza Mikoa yote Tanzania Bara(waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya ufunguzi rasmi wa kikao maalum cha kujadili mikakati ya utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula. Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja leo 17 Machi, 2018 Mkoani Morogoro
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

March 17, 2018

 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Harambee ya kuchangia ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Masaki Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, kwenye Hoteli.



Na Richard Mwaikenda, Dar

HARAMBEE ya uchangiaji wa ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, umevuka malengo baada ya  wadau kuchangia sh. bilioni 1.6 badala la kadirio la awali la sh. Bil. 1.5.

Jumla ya michango hiyo ilitangazwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa harambee iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Masaki Dar es Salaam jana.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alianza kampeni hiyo ya uchangiaji kwa kutoa sh. milioni 10 na sh. mil. 5 zilizotolewa na wanawe pamoja na wajukuu zake.

AAkizungumza wakati wa uzinduzi huo, Samia alitoa wito kwa wadau wote kuendelea kuchangia kwa manufaa ya nchi na ustawi wa jamii kwa ujumla.

"Niwakumbushe kwa mjenga nchi ni mwananchi,na hivyo ujenzi huu ni hatua kubwa na inayofaa kuungwa mkono na sisi kama Serikali, lakini pia na wadau wote wa maendeleo na wanaoitakia mema Tanzania hii," alisema Makamu wa Rais, Samia na kuongeza...

"Tukizungumzia  Tanzania ya Viwanda tunazungumzia  nguvu kazi; hivyo uwepo wa huduma hizi za afya ni muhimu katika kuhakikisha tuna nguvu kazi yenye afya na siha njema katika kuendesha  viwanda hivi pamoja na kujenga Tanzania mpya inayotarajia kufikia uchumi wa kati siku za karibuni."

Samia aliitaka Tamisemi kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuratibu upatikanaji wa vifaa, vifaa tiba na watumishi ili huduma stahiki zianze kutolewa mara tu jengo litakapokamilika.

Mama Samia aliupongeza uongozi na wananchi wa Wilaya ya Muheza, kwa kuamua kujenga hospitali hiyo, ili kuboresha hali ya afya na ustawi wa jamii kwa kusogeza huduma za rufaa ngazi ya wilaya karibu na wananchi badala ya kutegemea huduma hiyo kutoka sehemu nyingine na kwamba jambo hilo ni la kupongezwa sana na ni la kuigwa na wengine.

Hivi sasa wananchi wa wilaya hiyo hupata matibabu katika Hospitali ya Kanisa la Kianglikana na Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo iliyo umbali wa Km 72.

Harambee hiyo iliyowashirikisha wadau mbalimbali wapenda maendeleo, iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo kwa ushirikiano wa uongozi mzima wa wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla.

Katika harambee hiyo iliyohanikizwa na Bendi ya Mwanamuziki Mkongwe King Kiki, shairi maalumu na kwaya ya wasanii wa wilaya hiyo pamoja na kuwepo msosi ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Wapo Wadau waliotoa fedha taslimu na wengine kuahidi kutoa fedha, saruji, mabati, mchanga, kokoto, samani, mbao, ujenzi wa barabara pamoja na ujenzi wa baadhi ya wodi, ofisi na mochari.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Tumbo  alisema kuwa kila mwana Muheza ameahidi kuchangia sh. 2,000 na zaidi na baadhi yao wanatumia nguvu zao kusaidia ujenzi wa Hospitali hiyo.

Mhandisi Tumbo, alisema kuwa hospitali hiyo itakayogharimu zaidi ya bil 11 itakapokamilika,imeanza kujengwa kwenye eneo la heka 100 katika Kijiji cha Tanganyika, Kata ya Lusanga, wilayani humo na inatarajiwa kukamilika mwaka 2020.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella, Mbunge wa Jimbo la Muheza, Adadi Rajab, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu, IGP Mstaafu, Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu. IMENDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG;0715264202,0689425467,0754264203




 Baadhi ya wadau wakiwa katika hafla hiyo
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Muheza, Desderia Haule akiwa na baadhi ya wadau
 Mwanamuziki Mkongwe, King Kikii akiwa na  mjumbe wa Kamati ya Harambee hiyo,
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (katikati), akiwa na Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama wakati wa harambee hiyo. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Mkikita, Neema Ngowi.
 Kwaya ikitumbuiza
 Sehemu ya waalikwa wachangiaji wa harambee hiyo
 Wasanii wakiimba wimbo wa kutoa shukrani kwa Mama Samia kukubali kuwa mgeni rasmi  wa harambee hiyo
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella akitoa pongezi kwa wadau walihudhuria hafla hiyo
 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akielezea mikakati ya kuboresha sekta ya afya nchini ikiwemo ujenzi wa hospitali hiyo ya Wilaya ya Muheza.
 Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo akizungumza katika harambee hiyo ambapo alihakikisha kuunga mkono kwa nguvu zote ujenzi wa hospitali hiyo.

 Mama Samia akibonyeza kitufe kuzindua harambee hiyo
 Shamrashamra za uzinduzi huo
 Mama Samia akifurahia zawadi aliyozawadiwa na uongozi wa wilaya hiyo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akijaza fomu kuchangia ujenzi wa hospitali hiyo.
 IGP Mstaafu, Said Mwema  akiahidi kuchangia ujenzi wa hospitali hiyo
 Mdau akiahidi kuchangia
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), akipewa mkono wa shukrani na Makamu wa Rais, Mama Samia pamoja na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu baada ya kuahidi kuchangia sh. mil. 1 za kusaidia ujenzi wa hospitali hiyo.
 Rais wa TFF,  Karia akiahidi kuchangia harambee hiyo ambapo aliahidi mapato ya mchezo wa Ngao ya Hisani yataelekezwa kwenye ujenzi wa Hospitali hiyo.
 Wachangiaji wakipongezwa na Viongozi akiwemo Makamu wa Rais, Samia
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ambayo pia kuandaa matamasha ya Pasaka na Chrismas, Alex Msama akipongezwa na Makamu wa Rais, Samia baada ya kuahidi kutoka mchango kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo. Pia aliahidi kutoa mchango kutoka kwenye sehemu ya mapato ya Tamasha la Pasaka.
 Ofisa Uhusiano wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Neema Ngowi akipongezwa na  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuahidi kutoa sh. mil. 1 zitakazochangwa na wanachama wa matandao huo.
 Msreheshaji wa Harambee hiyo, Charles Mwakipesile akipewa mkono wa shukrani na Makamu wa Rais, Mama Samia baada ya kuahidi kutoa sh. mil 1 za ujenzi wa hospitali hiyo.
 Sasa ni wakati wa msosi

 Viongozi wa Mkikita, CEO Adam Ngamange na  PRO Neema Ngowi wakipata msosi


Makamu wa Rais, Mama Samia akikabidhiwa zawadi ikiwa ni shukrani kwa kufanikisha harambee hiyo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Tumbo.