KONGAMANO LA VIONGOZI WASTAAFU AFRIKA (African Leadership Forum 2016) LAMALIZIKA JIJINI DAR ES SALAAM

KONGAMANO LA VIONGOZI WASTAAFU AFRIKA (African Leadership Forum 2016) LAMALIZIKA JIJINI DAR ES SALAAM

July 30, 2016


1 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati akifunga  wa Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza jana na kumalizika leo  jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2 
Rais Mstaafu wa Namibia Mh. Hifikepunye Pohamba akifuatilia mada katika kongamano hilo Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza jana na kumalizika leo jijini Dar es salaam
3 
Viongozi mbalimbali na washiriki wakiwa katika kongamano hilo lililomalizika leo.
4 
Viongozi na washiriki pa oja na waalikwa wakiendelea na kongamano hilo le kabla ya kumalizika na kufungwa rasmi leo.
5 
Rais Mstaafu wa Tanzania Mh Benjamin William Mkapa katikati akiwa na Ali Mufuruki mmoja wa washiriki wa kongamano hilo pamoja na Dk. Elsie Kanza wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
6 
Rais Mstaafu wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza kulia  ni miongoni mwa marais wastaafu waliohudhuria katika kongamano hilo.
7
8 
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mh. Thabo Mbeki akizungumza na kutoa mchango wake kuhusu masuala ya kiuchumi katika kongamano hilo.
9
MAJALIWA MJULIA HALI SPIKA

MAJALIWA MJULIA HALI SPIKA

July 30, 2016

ND1 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai  wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika  jijini Dar es salaam kumsalimia  Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Bunge)
ND2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai  wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika  jijini Dar es salaam kumsalimia  Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Bunge)

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA MKOANI MWANZA AANZA ZIARA ZA KUKAGUA MIUNDOMBINU JIMBONI HUMO.

July 30, 2016
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula (katikati), jana amefanya ziara ya kukagua Ukarabati wa Miundombinu ya barabara, mitaro na madaraja katika Kata ya Kirumba Jimboni humo ikiwa ni mwanzo wa ziara zake katika Kata zote za Manispaa ya Ilemela ili kujionea namna ukarabati wa mbiundombinu ya barabara unavyoendelea.

Kulia ni Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu katika Kata ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi Milioni 195 zimetengwa kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake ambazo ziliharibika kutokana na mvua ambapo miongoni mwa barabara zinazokarabatiwa katika Kata ya Kirumba ni barabara ya Villa, Kabuhoro, CWT-Sabatho.
Na BMG
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (wa nne kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.
Mitaro katika barabara ya Villa inaendelea kukarabatiwa ili kuondoa adha ambayo huwa inajitokeza wakati wa mvua na kusababisha adha kubwa kwa wananchi.
Hii ni barabara ya CWT-Sabatho, awali ilikuwa haitamaniki kwani ilikuwa ni mashimo tupu. Lakini sasa inapitika vyema na kilichosalia ni ukarabati wa mitaro ili mvua ikinyesha isiweze kusababisha uharibifu wa ukarabati huu.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (wa tatu kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.
Namna miundombinu ya barabara na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Ukaguzi wa miundombinu ya barabara na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Pia kuna ujenzi wa daraja katika barabara ya Kabuhoro Ziwani ambapo kulikuwa na adha kubwa kwa wananchi ambapo ukarabati huu unaleta ahueni kwa wakazi wa eneo hio pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

Aliagiza ukarabati wa mbiundombinu ya barabara kukamilika haraka kabla msimu wa mvua haujaanza na kwamba Manispaa ya Ilemela imetenga Shilingi Milioni 625 ikiwa ni fedha za mfuko wa dharura na shilingi Milioni 146 ambazo ni fedha za mfuko wa barabara, fedha zote ikiwa ni kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (mwenye miwani) akiteta kidogo na wakazi wa Kata ya Kirumba alipotembelea Kata hiyo ili kujionea ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Kata hiyo.
Katibu wa Mbunge, Heri James (mwenye kofia) ambapo alisema ofisi ya mbunge itahakikisha ahadi zilizotolewa na mbunge wakati wa kampeni zinatekelezwa ikiwemo suala la upatikanaji wa maji na ukarabati wa miundombinu.
Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu katika Kata ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi Milioni 195 zimetengwa kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake ambazo ziliharibika kutokana na mvua.
Diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, ambapo alibainisha kwamba barabara za Kata hiyo zilikuwa zimeharibika sana kutokana na mvua zilizonyesha mwishoni mwanza mwaka jana. 

Alishukuru ushirikiano baina yake na wananchi wa Kata yake, ofisi ya mbunge pamoja na halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kwamba juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kuwafikishia wananchi maendeleo zimepokelewa vyema na wananchi huku akiwasihi kuitunza vyema miundombinu hiyo.
Mmoja wa wakazi wa Kirumba akieleza adha waliyokuwa wakiipata wakazi wa Kata hiyo kabla ukarabati haujafanyika ambapo aliongeza kwamba ni vyema ukarabati huo ukaendelea kufanyika hususani katika ujenzi wa mitaro ili kuondoa adha ambayo huwa inajitokeza wakati wa mvua ikwemo kuharibu miundombinu ya barabara kutokana na kukosekana kwa mitaro.
Mkazi wa Kirumba akitoa shukurani zake kwa ukarabati unaofanyika katika barabara za Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imeanza ukarabati wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha changarawe pamoja na mikakati ya ujenzi wa baadhi ya barabara kwa kiwango cha lami.

Akikagua zoezi la ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Kata ya kirumba, Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula, ametaka ukarabati wa miundombinu hiyo ikiwemo mitaro, kukamilika mapema kabla msimu wa mvua haujaanza ili kuepukana na athari za mvua.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano, hali ya miundo mbinu ya barabara katika jimbo hilo itakuwa katika hali nzuri na hivyo kupunguza kero ya ubovu wa miundombinu ambayo imekuwepo kwa muda mrefu katika Manispaa ya Ilemela.

Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, amesema Manispaa hiyo imetenga shilingi Milioni 625 zilizotokana na fedha za mfuko wa dharura na barabara kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara katika manispaa hiyo japo amebainisha kwamba bado fedha hizo hazitoshi hivyo ni vyema serikali ikaendelea kutenga fedha zaidi kwa ajili ya kutekeleza ukarabari huo.

Wakati ukarabati huo ukiendelea, diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, amewataka wananchi kutunza vyema mbiundombinu ya barabara inayoendelea kukarabatiwa ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mitaro.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kirumba, wamepongeza juhudi za ukarabati wa miundombinu ya barabara zinazofanyika katika Manispaa ya Ilemela na kuongeza kwamba ni vyema juhudi hizo zikandelea ili kumaliza kero zilizokuwepo awali.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela, yuko katika mwendelezo wa ziara katika Kata zote 19 za Manispaa ya Ilemela ili kujionea ukarabati wa Miundombinu ya barabara ambayo ni pamoja na ujenzi wa mitaro na madaraja ambao unaelezwa kuleta ahueni kwa wananchi wa Manispaa hiy ikizingatiwa kwamba awali hali ya miundombinu ya barabara awali haikuwa ya kuridhisha.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play Hapo Chini.

KIWANDA MAARUFU CHA DANGOTE CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 15 KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA.

July 30, 2016
Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ( katikati) Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Khatib Kizinga (kushoto) wakipata maelezo toka kwa Bw. Sultani Pwaga wa kiwanda cha Gas cha Madiba Mjini Mtwara  wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mpina kiwandani hapo.


Eneo ya fukwe ya Mnazibay Mjini Mtwara inavyooneka kuathirika na athari za mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababisha sunami mwaka 2015 february..Naibu Waziri Mpina Alitembelea eneo hilo kujionea athari za mabadiliko ya tabia nchi. (Picha na Evelyn Mkokoi)

EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
29/7/2016

Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limekitoza faini ya shilingi milioni 15, Kiwanda maarufu cha kutengeneza simenti cha Dagonte Industry limited kilichopo  mjini Mtwara kusini mwa Tanzania,  kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Katika siku ya Pili ya Ziara ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara .

Imebainika kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze kazi ya kutengenza siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani hapo, kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva na makondakta wanao chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na kusafirisha kwenda sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafia sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji wa eneo hilo.
Kwa Mujibu wa Naibu waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo pamoja na kuhamsha uongozi wa kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka kiwanda hicho kuajiri afisa mazingira ataeshughulia changamoto hizo.
Kwa upande wake Meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho Bw. James Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa baadhi ya miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa baadhi ya vibali kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria ya mazingira.
Naibu waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha Madiba na kukisifu kwa  utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya serikali, kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.
Ziara ya Mhe. Mpina pia ilihisisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua korosho cha micro mix cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi pamoja na fukwe ya mnazi bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

SKY SPORTS YAUNGANA NA STARTIMES KUONYESHA LIGI YA CHINA

July 30, 2016


Na Dotto Mwaibale

Kituo cha matangazo ya luninga cha Sky Sports cha nchini Uingereza katikati ya wiki hii kilisaini mkataba mnono wa kuonyesha moja kwa moja ligi kuu ya China kwa misimu mitatu ijayo ambayo pia kwa Tanzania inaonekana kupitia visimbuzi vya StarTimes.

Sky Sports wameamua kuanza kuionyesha ligi hiyo baada ya kuvutiwa na jitihada kubwa zinazofanywa na China katika kukuza soka la nchini mwao hususani kupambana sambamba na vilabu vikubwa vya barani Ulaya katika kusajili wachezaji nyota kutokea ligi hiyo.

Ligi hiyo imeanza kujizolea umaarufu na kuvuta hisia za watu baada ya kuona majina ya wachezaji wakubwa yakielekea huko kama vile Ramires aliyetokea Chelsea, Gervinho aliyewahi kuchezea Arsenal, Obafemi Martins aliyechezea Newcastle United na hivi karibuni nyota wa Italia Graziano Pelle aliyetokea Southampton na kujiunga na Shandong Luneng.

Akizungumzia juu ya taarifa hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania,  Lanfang Liao ameelezea kuwa hiyo ni habari njema kwetu sisi pia kwani mapema mwaka huu tuliingia makubaliano ya kuitangaza ligi hiyo pia baada ya kuona mbali kuwa itakuja kuwa maarufu na hilo linaanza kujidhihirisha.

“Ukiwa unazungumzia ligi ambazo zinakua kwa kasi duniani kwa sasa hutoacha kuizungumzia ligi kuu ya nchini China au maarufu kama ‘Chinese Super Cup’. Na hii ni kutokana na ushindani uliopo hivi sasa unaopelekwa na wachezaji pamoja na makocha wazuri katika soka ukiachilia mbali malipo makubwa wanayoyapokea ambayo yanakwenda sambasamba na vilabu vikubwa vya barani Ulaya. Mashabiki wa soka hivi sasa wanaweza kutazama mechi za ligi hiyo na kuziona sura ambazo awali walikwishaziona barani Ulaya kama vile Graziano Pelle, Ramires, Gervinho, Hulk, Asamoah Gyan, Jackson Martinez, Ezequiel Lavezzi na wengineo wengi.” Alifafanua  Liao

“StarTimes kadiri siku zinavyokwenda mbele ndivyo tunazidi kuboresha zaidi huduma zetu hususani ligi mbalimbali za soka kwani tunatambua watanzania ni wapenzi wakubwa. Na kwa kuwa na wigo mpana wa mashindano mbalimbali kunawafanya waweze kufurahia zaidi huduma zetu. Ligi ya China kwa sasa ni ligi kubwa duniani na ndiyo maana Sky Sports wameamua kuinonesha barani Ulaya huku kwa sisi Tanzania na Afrika kwa ujumla ni kupitia visimbuzi vyetu pekee unaweza kutazama mechi zote moja kwa moja.” Alihitisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo ya matangazo ya dijitali nchini

Baada ya kusaini makubaliano hayo kwa mara ya kwanza kabisa Sky Sports wataingia mzigoni kuanza kuonyesha mechi za ligi hiyo siku ya Jumamosi ya Julai 30, 2016 ambapo timu za Shanghai Greenland Shenhua itakuwa kiburuani kuwakabili Jiangsu Suning FC (saa 8:35 mchana) na siku ya Jumapili, Julai 31 timu ya Guangzhou R&F inayonolewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Sven Goran Eriksson kumenyana na Shanghai SIPG (saa 8:35 mchana).

Mechi hizo zote kwa hapa nchini Tanzania zitaonekana moja kwa moja kwenye visimbuzi vya StarTimes kupitia chaneli za Sports Focus na World Football.

WAKURUGENZI MKOANI SIMIYU WAAGIZWA KUTENGA BAJETI ZA MAAFISA KILIMO

July 30, 2016
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo wa mkoa huo(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (katikati) akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo wa mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kikiwa na lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah na (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
Viongozi na Maafisa kilimo wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu.


         Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa kilimo wa Vijiji,Kata na Wilaya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ambacho kilihudhuriwa na Wakuu wa wilaya,Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi na Makatibu Tawala Wilaya kutoka  katika wilaya zote tano za mkoa huo.

Mtaka amesema Maafisa Kilimo wanapaswa kuwezeshwa kwa kupewa vyombo vya usafiri kama pikipiki na magari pamoja na mafuta, ili waweze kuwafikia wakulima katika maeneo yao kwa ajili ya kuwapa ushauri wa kitaalam kila wanapowahitaji katika kuendeleza kilimo bora na chenye tija.

“Mwaka huu kilimo kwa mkoa wetu ni  kipaumbele cha pili na Halmashauri za Mkoa huu zinategemea kilimo kwa takribani asilimia 90 ya mapato yake ya ndani, ipo haja  kuwawezesha maafisa kilimo kwa kuwa wana mchango kubwa katika mapato ya Halmashauri. Ningependa kuona mwaka 2016/2017 hadhi ya Maafisa Kilimo inapanda, Wakurugenzi muwathamini hawa wataalam ndiyo wanaowasaidia kupata hayo mapato katika pamba, choroko, dengu, mpunga na mazao mengine”, alisema Mtaka.

Aidha, kufuatia makubaliano kati ya Serikali ya  Tanzania na India yaliyofanywa hivi karibuni kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa India juu ya biashara ya mazao ya jamii ya mikunde kama choroko, dengu na mbaazi takribani tani milioni sita, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unayo fursa kubwa ya  kuzalisha mazao haya kwa takribani asilimia 60 kama ilivyo katika zao la pamba, kwa kuwa kuna ardhi yenye rutuba na wananchi wanalima mazao hayo. 

Katika kufikia azma hiyo, Mtaka amewataka Maafisa kilimo kutumia muda huu kufanya tafiti katika vituo mbalimbali vya utafiti  juu ya mbegu bora, kabla ya msimu wa mazao ya mikunde haujaanza ili wakati utakapofika uzalishaji wa mazao hayo ufanyike kitaalam na kuongeza uzalishaji kuliko ilivyo sasa.

Wakati huo huo Mtaka amewaagiza viongozi na Maafisa Kilimo kutoka katika wilaya zote kuwa na mashamba ya mifano ambayo yatatumika kama mashamba darasa kwa wananchi ili wananchi wajifunze kutoka kwao kwa kuwaonesha kuwa maelezo wanayoyatoa yanatekelezeka. 

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Uchumi na Uzalishaji katika Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Bw. Joseph Nandrie ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Simiyu kulima mazao yanayostahimili ukame kama mihogo na mtama ili kukabiliana na baa la njaa.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo