Waziri Lukuvi ahitimisha ziara ya siku mbili kushuhudia utendaji wa NHC

April 01, 2015

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Nyumba za gharama nafuu za NHC Mwongozo, Kigamboni Dar es Salaam zinavyoonekana leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo ya Injinia wa NHC, Elisante Ulomi anayesimamia Mradi wa Mwongozo Housing Estate mchana wa leo. Mojawapo ya Nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada, Kigamboni Dar es Salaam inavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea. Nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada, Kigamboni Dar es Salaam zinavyoonekana leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea. Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea. Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea. Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri alipozitembelea. Nyumba ya mfano itakayojengwa katika kitalu nambari 300 kona ya kuelekea kwenye Hospitali ya Mikocheni jijini, Dar es Salaam leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya Nyumba ya mfano itakayojengwa katika kitalu nambari 300 kona ya kuelekea kwenye Hospitali ya Mikocheni jijini, Dar es Salaam leo. Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria kutoka kwa Mkurugeni wa Ubunifu wa NHC, Issack Peter alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Mmojawapo wa mafundi wajenzi wanaojenga nyumba hizo za Victoria akiwa kazini wakati wa ziara ya Waziri.
BUNGE LAPITISHA SHERIA YA KUANZISHWA BARAZA LA VIJANA

BUNGE LAPITISHA SHERIA YA KUANZISHWA BARAZA LA VIJANA

April 01, 2015

unnamed999 
Na Anitha Jonas – MAELEZO,Dodoma.
…………………………………………………….
Serikali inatarajia kuanzisha Baraza la Vijana litakalo kuwa chombo cha vijana kitakacho waunganisha Kitaifa bila kujali itikadi zao za Kisiasa,Imani zao za Kidini wala tofauti zao za Rangi,hayo yamesemwa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Fenella Mukangara alipokuwa akisoma Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania Bungeni Mjini Dodoma.
Mheshimiwa Mukangara aliendelea kusema Baraza hilo litaisaidia Serikali kuweza kuwafikia vijana kwa urahisi na kusikiliza shida zao pamoja na kutoa ufumbuzi wa hoja mbalimbali za vijana.Hata hivyo chimbuko la Muswada huo ni katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya 2007,Ibara ya 3 Sehemu ndogo ya 11 inayosema kwa uwazi Serikali itawezesha kuundwa kwa Baraza Baraza la Vijana na kuanzisha mfumo wa kisheria ili kuliwezesha kufanya kazi.
“Madhumuni ya Muswada huu ni Kutunga Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania(The Youth Council of Tanzania 2015) ili kuwa na chombo cha Kitaifa cha kuwewezesha vijana kujadili masuala yao,kutambua majukumu yao,kukuza maadili mema,kukuza moyo wa umoja ,uzalendo,uwajibikaji na kujitolea kwa malengo chanya miongoni mwao katika nchi yetu,”alisema Mhe.Mukangara.
Mbali na hayo katika sehemu ya pili kifungu cha 4-15 cha Muswada huo unaeleza juu ya masharti mbalimbali kuhusu Uanzishwaji,Uanachama,Muundo na kazi za Baraza.Pia sehemu hii imefafanua Mamlaka ya Baraza na vyombo vya utendaji katika ngazi ya Taifa,Mkoa na Wilaya.
Aidha,kwa upande wa maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii yaliyosomwa na Mwenyekiti wake Said Mtanda aliishauri Serikali katika kifungu cha 4(3)Kisomeke Uanachama utakuwa na uwazi na hiari kwa kijana yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 15 mpaka 35.Pia kifungu cha 4(4) imeeleza kuwa baraza halitakuwa kisiasa liongezwe neno halitakuwa na Itikadi za Kidini.
Katika kipindi cha majadiliao ya Muswada huo naye Mhe.Kuluthum Mchuchuri (Mb) Viti Maalum CUF aliipongeza Serikali kwa mchakato wake mzuri wa kuandaa Baraza la Vijana litakalo saidia vijana kujadili matatizo yao na kuyawasilisha Serikali kwa kupatiwa ufumbuzi kwa urahisi,pia ameishauri Serikali katika suala la wajumbe uwawakilishi waanze kuanzia ngazi ya Kata na Serikali pia iweke wazi ni kwa utaratibu gani wawakilishi hao watapatikana.
Naye Mhe.Magret Sitta Mbunge wa Viti Maalum CCM aliiomba Serikali kuandaa ziara kwenda kuangalia mabaraza ya Vijana katika nchi za wenzetu yanafanyaje kazi na kujifunza,pia aliendelea kuiomba Serikali itoe mafunzo mbalimbali ya ufundi kwa kushirikia na taasisi ya Veta na Vyuo vya Wananchi ilikuwapatia elimu itakayo wasaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kupunguza idadi ya vijana wa vijiweni.
Pamoja na hayo naye Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR) Mhe.Moses Machali alishauri Serikali Kuanzisha asasi moja ambayo vijana watakayo jiunga huko ili kudhibiti uanzishwaji wa asasi bandia kwa watu wenye nia ya kujinufaisha,pia aliipongeza Serikali kwa kuleta Muswada huo kwani unamanufaa Makubwa kwa vijana.
Aidha,mbali ya kuwepo na marekebisho mbalimbali ya Muswada huo Serikali iliyapokea maombi ya Suala la Baraza hilo kuanzia katika ngazi ya Kata ilikupata uwakilishi uliyowa uhakika na baraza likalete manufaa kwa kuanzia ngazi ya chini ambapo ndipo vijana wengi wanapatikana na jamii inawafahamu kwa usahihi zaidi.
Halikadhalika Serikali iliridhia kuanzishwa kwa uwakilishi wa vijana watano kutoka kundi maalum kwa maana ya wenye ulemavu na ili kuweka uwianao wa vijana hawa kuweza kuwasilisha maombi yao kwa Serikali kwa urahisi huku ikizingatia mahitaji yao maalum.
George Simbachawene akizungumzia kuhusu Ugunduzi wa nane wa gesi asilia

George Simbachawene akizungumzia kuhusu Ugunduzi wa nane wa gesi asilia

April 01, 2015

unnamed
Waziri wa Nishati na Madini (wa pili Kulia) Mhe.George Simbachawene akizungumza na waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu Ugunduzi wa nane wa gesi asilia uliyofanywa na Kampuni ya Statoil katika eneo la Bahari Kuu,(wa kwanza kulia) ni Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt Charles Mwijage,na (wa kwanza kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Nishati na Madini Mhe.Richard Ndassa (Mb) wa Sumve CCM.
Picha na Anitha Jonas – MAELEZO,Dodoma.

ZIARA YA KINANA MOSHI MJINI

April 01, 2015

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia vijana wa boda boda ,Stendi Kuu kata ya Mawenzi ambapo aliwaambia kuwa boda boda ni sehemu ya kupata kipato hivyo inabidi wafanye shughuli yao hiyo kwa umakini mkubwa ,ikiwa kudumisha umoja, kufuata sheria, kujisajili na kutambulika na mamlaka husika ,kuaminika ili waweze kukopesheka.
 Katibu wa Umoja wa Boda Boda Moshi mjini akisoma risala kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano uliofanyika ,Stendi Kuu kata ya Mawenzi Moshi mjini.
 Wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini wakiwa wamefunga njia kuzuia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana usipite mpaka wawasilishe kero yao ya kufungiwa soko kwa mwaka mzima na uongozi wa halmashauri ya mji kwa maelezo ya kupisha ukarabati ambao haujafanyika.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye mabango na wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma risala ya wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanya biashara ambao soko lao limefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuingia kwenye soko la kati, Moshi mjini mkoani Kilimanjaro ambalo lilifungwa kupisha ukarabati ambao mpaka sasa ni mwaka 1 hakuna kilichofanyika na wafanyabiashara wanaishi maisha magumu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa soko la kati ambalo limefungwa kwa mwaka mzima sasa.
 Ukuta wa soko la kati Moshi mjini ukiwa na matangazo yanayozuia kufanya biashara
 Katibu wa Vikoba kata ya Kongoroni Mariam Chawapoma akisoma risala ya kikundi chao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Wanachama wa Vikoba wakishangilia jambo wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wanachama wa Vikoba kata ya Makongoroni ambapo alishiriki kuzindua vikoba 11 vyenye wanachama 330,Kata ya Makongoroni,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali baada ya kutembelea kikundi Vijana cha Kata ya Miembeni
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa akina mama Lishe wa Njoro,Moshi mjini.
 Wajasiriamali na mama lishe wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kata yao ya Njoro.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajasiriamali pamoja na mama lishe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa Ndugu Idd Juma
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatiza kwenye maji wakati akielekea kwenye eneo la mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya Moshi mjini Ndugu Aggrey Marealle akihutubia wananchi wa Moshi mjini ambapo aliwaambia kuwa wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya kweli kwa kuchagua CCM kuongoza mji wa Moshi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Moshi mjini mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambie wastuke sasa wasiendelee kukandamizwa na viongozi wasiojali maendeleo yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Moshi mjini kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambia kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia picha ya gari alilotumia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kabala halijafanyiwa ukarabati na Chuo cha Ufundi Veta, Moshi mjini.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha gari alilotumia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kutafuta uhuru,kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenye gari alilotumia Baba wa Taifa wakati wa harakati za kutafuta uhuru.

Wananchi wakiuaga msfara wa  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya mkutano kumalizika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mandela,Bomambuzi, Moshi Mjini.
 MSHINDI WA MWISHO WA”MTOKO WA MBUGANI” WA KAMPENI YA TUTOKE NA SERENGETI AFURAHIA MTOKO WAKE WA SIKU TATU NDANI YA HIFADHI YA SERENGETI

MSHINDI WA MWISHO WA”MTOKO WA MBUGANI” WA KAMPENI YA TUTOKE NA SERENGETI AFURAHIA MTOKO WAKE WA SIKU TATU NDANI YA HIFADHI YA SERENGETI

April 01, 2015
1
Mshindi wa mwisho wa shindano la “Tutoke na Serengeti” Bw.Gabriel Robert Moriale (Kulia) akiwa na kaka yake Bw.Joshua Robert Moriale (Kushoto) walipowasili mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro jijini Arusha tayari kwa kuanza safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kukamilisha mtoko wao wa siku tatu ndani ya hifadhi hiyo. Robert aliibuka mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa mbugani” baada ya kushiriki kwenye kampeni ya “Tutoke na Serengeti” iliyoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa ushirikiano na BPESA kwa takriban miezi(4) ambapo washindi walijinyakulia zawadi nyingine kama Limo Bajaj, fedha taslim, Bia za bure sambamba na punguzo la Tsh.300 kwenye bia ya Serengeti Premium.
9
Mshindi wa mwisho wa shindano la “Tutoke na Serengeti” Bw. Robert Gabriel Moriale wa pili (Kushoto) aliyeongozana na mdogo wake Bw. Joshua Robert (Wa kwanza kulia) wakitalii ndani ya Ngorongoro na kupata maelekezo kutoka kwa mwelekezi (Tour guide) kabla ya kuanza safari ya kwenda Serengeti national park. Bw. Robert aliibuka mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa mbugani” baada ya kushiriki kwenye kampeni ya “Tutoke na Serengeti” iliyokua ikiendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa ushirikiano na BPESA kwa takriban miezi(4) ambapo washindi walijinyakulia zawadi nyingine kama Limo Bajaj, fedha taslim, Bia za bure sambamba na punguzo la Tsh.300 kwenye bia ya Serengeti Premium.
2
Ndugu wa mshindi wa “Mtoko wa Mbugani” ajulikanaye kwa jina la Joshua Robert akimpiga picha simba ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwenye mtoko wao wa siku tatu ndani ya hifadhi hiyo.Joshua alimsindikiza kaka yake Bw.Gabriel Robert aliyeibuka mshindi wa mwisho wa mwisho wa “Mtoko wa mbugani” baada ya kushiriki kwenye kampeni ya “Tutoke na Serengeti” iliyokua ikiendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa ushirikiano na BPESA kwa takriban miezi(4) ambapo washindi walijinyakulia zawadi nyingine kama Limo Bajaj, fedha taslim, Bia za bure sambamba na punguzo la Tsh.300 kwenye bia ya Serengeti Premium.
8
Mshindi wa mwisho wa shindano la “Tutoke na Serengeti” Bw.Gabriel Robert Moriale akiangalia kundi kubwa la wanyama aina ya pundamilia katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa kukamilisha mtoko wao wa siku tatu ndani ya hifadhi hiyo. Robert aliibuka mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa mbugani” baada ya kushiriki kwenye kampeni ya “Tutoke na Serengeti” iliyokua ikiendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa ushirikiano na BPESA kwa takriban miezi(4) ambapo washindi walijinyakulia zawadi nyingine kama Limo Bajaj, fedha taslim, Bia za bure sambamba na punguzo la Tsh.300 kwenye bia ya Serengeti Premium.
7
Mshindi wa mwisho wa shindano la “Tutoke na Serengeti” Bw. Robert Gabriel Moriale (Kulia) aliyeongozana na mdogo wake Bw. Joshua Robert (Kushoto) wakifuruahia bia ya Serengeti Premium wakati wakitalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa kukamilisha mtoko wa siku tatu ndani ya hifadhi hiyo. Bw. Robert aliibuka mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa mbugani” baada ya kushiriki kwenye kampeni ya “Tutoke na Serengeti” iliyokua ikiendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa ushirikiano na BPESA kwa takriban miezi(4) ambapo washindi walijinyakulia zawadi nyingine kama Limo Bajaj, fedha taslim, Bia za bure sambamba na punguzo la Tsh.300 kwenye bia ya Serengeti Premium.