NAIBU WAZIRI MGALU AWASHA UMEME KATA ZA LUGOBA,MANDELA- PWANI

NAIBU WAZIRI MGALU AWASHA UMEME KATA ZA LUGOBA,MANDELA- PWANI

May 04, 2018

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati mstari wa kwanza) akiwasha rasmi umeme katika kijiji cha Hondogo Kata ya Mandela mkoani Pwani. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na wengine wanaoshuhudia ni Wataalam Waandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliyenyanyua mkono akishangilia baada ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji cha Hondogo Kata ya Mandela na mwenye shati la kijani ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete. Wengine ni Watumishi kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Uongozi wa Halmashauri ya Chalinze pamoja na Wananchi wa Kata hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akielekea katika eneo la tukio la uzinduzi rasmi wa kuwasha umeme katika kijiji cha Hondogo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete na wengine katika picha ni wananchi kutoka Kata ya Mandela.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi wa Kata ya Mandela pomoja na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha rasmi umeme katika kijiji cha Saleni kata ya Lugoba, wanaoshuhudia ni Watumishi kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO, REA, Uongozi wa Halmashauri ya Chalinze pamoja na Wananchi wa kata ya Lugoba.

……………….

Na Rhoda James, Pwani

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amezindua rasmi upatikanaji wa huduma ya umeme katika Kijiji cha Saleni Kata ya Lugoba na kijiji cha Hondogo Kata ya Mandela mkoa wa Pwani.

Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 3 Mei, 2018 katika vijiji hivyo wakati alipofanya ziara ya kukagua Mradi wa Ujazilizi (Densification) na miradi mengine ya umeme inayotekelezwa mkoani humo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Mgalu aliwaagiza watumishi wa TANESCO na REA kuhakikisha wanaunganishia wananchi wote umeme kwa wakati ili wananchi wafaidike nishati hiyo kwa maendeleo ya kiuchumi.

Pia aliwataka wananchi wa Pwani kuchangamkia fursa ya mradi huo pindi umeme unapofika katika kata zao.

“Fanyeni wiring haraka katika Zahanati na Mashuleni pia katika nyumba zenu ili muunganishiwe umeme wa REA kwa gharama ya shilingi 27,000 tu,” alisema Mgalu.

Mgalu alisema kuwa tayari Kaya 65 katika Kata ya Mandela zimeunganishwa na umeme na kaya nyingine 85 zimeongezwa kwa ajili ya utekelezaji.

Aliongeza kuwa, ifikapo mwaka 2021 vijiji vyote nchini vitakuwa vimepata umeme kwa kuwa tayari Wakandarasi wote wamekwisha idhinishiwa malipo yao na hivyo kuwataka ambao wameondoka katika maeneo yao kurudi haraka.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Lugoba Rehema Issa, alisema kuwa wananchi walichelewa wenyewe kufanya wiring kutokana na sababu mbalimbali lakini sasa watafanya haraka.

“Pia tulikuwa na tatizo la transforma lakini sasa tumewekewa na wananchi wangu watapata umeme,”alisema Issa.

Aidha, Diwani Issa alisema yapo baadhi ya maeneo ambayo hayajapata umeme hivyo alitumia fursa hiyo kumuomba Naibu Waziri Mgalu asaidie ili vijiji vipate umeme kwa wakati.

Kwa nyakati tofauti, Mbunge wa Jimbo la Chalize Riziwani Kikwete alimshukuru Naibu Waziri Mgalu kwa kutembelea jimbo lake na kwa kasi kubwa ya kuhakiksha wananchi wote wa Pwani wanapata umeme kwa wakati.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA KIDATU –IFAKARA YENYE KM 66.9 PAMOJA NA DARAJA LA MTO RUAHA KATIKA ENEO LA NYANDEO KIDATU

May 04, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy kushoto na Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer kulia kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kushoto pamoja viongozi mbalimbali na wabunge wa mkoa wa Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi pamoja na viongozi wengine wakiwemo Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy anayevuta utepe, Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer pamoja na wabunge mbalimbali wa mkoa wa Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la Ruaha lenye urefu wa mita 130.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kidatu kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la kidatu lenye urefu wa mita 130.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mkuu wa mkoa wa Morogoro Steven Kebwe kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la mto Ruaha lenye urefu wa mita 130.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kidatu kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la kidatu lenye urefu wa mita 130.


Mbunge wa Mikumi Joseph Haule akitumbuiza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la mto Ruaha lenye urefu wa mita 130.
Wananchi waliohudhuria katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la mto Ruaha lenye urefu wa mita 130.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwa njia ya simu ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kuhusu matatizo ya mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya Kidodi mkoani Morogoro.

- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kidodi wakati akielekea Kidatu mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzana wananchi wa Kidodi wakati akielekea Kidatu mkoani Morogoro.

JUMIA FOOD TANZANIA YASHUSHA GHARAMA YA KUAGIZA CHAKULA KWA 95%

May 04, 2018





KATIKA jitihada za kutoa huduma nafuu ya chakula mtandaoni, Jumia Food imeshusha kiwango cha chini cha kuagiza chakula kupitia mtandao wake mpaka kufikia shilingi 500!

Kabla ya punguzo hilo, kiwango cha chini cha kuagiza chakula kilikuwa ni kati ya shilingi 7000 mpaka 10000, kutegemeana na utaratibu wa mgahawa pamoja na umbali alipo mteja. Maboresho haya yanalenga kuwapatia wateja machaguo mengi zaidi na unafuu kwa wateja kuweza kuagiza vyakula wavipendavyo kwa gharama ndogo.

Meneja Mkazi wa Jumia Food Tanzania, Xavier Gerniers amebainisha kuwa lengo kuu ni kufafanua zaidi juu ya dhana kwamba huduma ya chakula kupitia mtandaoni ni ghali na inawalenga watu wenye vipato vya juu.
“Kwa kufanya hivi, tunawahakikishia wateja wetu kwamba sasa wanaweza kuagiza na kufurahia chakula bila ya hofu ya
bajeti waliyonayo,” alisema Gerniers na kuongezea kuwa kushuka kwa bei pia kutaiwezesha kampuni kugusa mahitaji na matakwa ya wateja tofauti.

“Lakini cha muhimu zaidi, ni kuwahamasisha Watanzania kuchangamkia fursa ya huduma ya chakula kwa njia ya mtandao ili kurahisisha shughuli zao za kila siku. Unaweza kupata huduma ya chakula kutoka kwenye migahawa mbalimbali kupitia Jumia Food kwa kutumia simu yako ya mkononi na kufaidika na ofa hizi lukuki kutoka Jumia Food,” aliongezea Meneja Uhusiano wa Umma, Kijanga Geofrey.

Huduma za chakula kwa njia ya mtandaoni ni maarufu kwenye miji tofauti duniani kwa sababu husaidia kuokoa muda na gharama kwa wateja. Kwa kuongezea, huongeza thamani kwa wamiliki wa migahawa kupitia fursa ya bure ya kufanyiwa shughuli za kimasoko hivyo kujiongezea idadi ya wateja wa mtandaoni waliopo katika maeneo tofauti. Kwa upande mwingine, wateja nao hunufaika kwa kupata huduma ya chakula kutoka kwenye migahawa wanayoipenda bila ya kuitembelea moja kwa moja.

Mapema mwaka huu, Jumia Food ilizindua programu yake ya simu ya mkononi iliyofanyiwa maboresho zaidi. Kwa mfano, kupitia maboresho hayo mteja ana uwezo wa kupata orodha ya migahawa iliyo karibu yake yenye huduma ya chakula anachotaka kuagiza.

Kuhusu Jumia Food

Jumia Food Tanzania ni mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma ya chakula kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam. Jumia Food ipo kwenye nchi 11 barani Afrika zikiwemo Kenya, Nigeria, Morocco na Uganda. Huduma hii huwawezesha wateja kwa kupata huduma ndani ya wakati, huongeza wateja, kusaidia uendeshaji na njia za masoko.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA ILULA, RUAHA MBUYUNI NA RUAHA DARAJANI WAKATI AKIWA NJIANI KUELEKEA MKOANI MOROGORO

May 04, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ilula mkoani Iringa wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ruaha mbuyuni mkoani Iringa wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ruaha darajani mara bada ya kuingia mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ruaha darajani mara bada ya kuingia mkoani Morogoro.

MENEJA MAWASILIANO WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) PASCA SHELUTETE AWAFUNDA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA ,SEMINARI YA AGAPE .

May 04, 2018


Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akielekezwa jambo na Mkuu wa Shule ya sekondari ya Seminari Ndogo ya Agape Mch,Godrick Lyimo alipoalikwa kama mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania.

Mkuu wa Shule ya sekondari ya Seminari Ndogo ya Agape,Mch,Godrick Lyimo akitoa maelezo juu ya shule hiyo kwa Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania ambaye pia ni Meneja Maawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete.

Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania ambaye pia ni Meneja Maawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akioneshwa maeneo mbalimbali ya Shule ya Sekondari ya Seminari Ndogo ya Agape .


Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania ambaye pia ni Meneja Maawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiotesha mti wa kumbukumbu katika moja ya maeneo ya shule hiyo.

Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania ambaye pia ni Meneja Maawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwafunda wanafunzi wa kidato cha sita wanaohitimu katika shule ya sekondari ya Seminari Ndogo ya Agape.
Wahitimu wa Kidato cha Sita katika shule ya Sekondari ya Seminari Ndogo ya Agape wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi katika mahafali hayo ambaye pia ni Meneja Maawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete( hayupo pichani ) wakati akizungumza


Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania ambaye pia ni Meneja Maawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitunuku vyeti kwa Wahitimu hao.
Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania ambaye pia ni Meneja Maawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Seminari Ndogo ya Agape ,Mch ,Godrick Lyimo .
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Seminari Ndogo ya Agape,Mch Godrick Lyimo akikabidhi zawadi kwa Mgeni Rasmi ,Pascal Shelutete.
Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ya Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania ambaye pia ni Meneja Maawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu .


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .