Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

RAIS MSTAAFU AZINDUA KAMPENI ZA CCM ZA UBUNGE NA MADIWANI KATIKA JIMBO JIPYA LA KIVULE WILAYANAI ILALA, DAR ES SALAAM

September 10, 2025 Add Comment



Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete amezindua rasmi kampeni ya Ubunge na Udiwani ya CCM katika jimbo jipya la Kivule ambalo limemegwa kutoka jimbo la Ukonga wilayani Ilala jijini Dar es salaam siku ya Jumanne Septemba 9, 2025.


Huku akishangiliwa na nyomi ya watu Dkt Kikwete aliongea na wananchi na kisha kumtambulisha mgombea ubunge wa Kivue Bw. Ojambi Didas Msaburi na kumkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM.


Wanaogombea ubunge katika majimbo ya Ilala, Ukonga na Segerea, Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zungu Mhe Jerry Silaa na Mhe Bona Kamoli pamoja na aliyekuwa mbunge wa Ukonga Mhe Mwita Waitara waliongea pia kabla ya mgombea mwenyeji kumwaga cheche



















DKT.NCHIMBI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JUMUIYA YA MARIDHIANO NA AMANI MKOA WA KATAVI

September 10, 2025 Add Comment


MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya ya Mariadhiano na Amani Tanzania Mkoa wa Katavi (JMAT)  leo Jumatano Septemba 10,mjini Mpanda ,Katavi.


Mazungumzo yao yalijikita kuangalia jinsi gani ya kuendeleza amani na mshikamano wa wananchi wa mkoa wa Katavi hasa mnamo kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.


Balozi Dkt.Nchimbi yuko Mkoani Katavi akiendelea na Mikutano yake ya Kampeni ya kusaka kura za Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Pichani akiwa na viongozi hao mara baada ya kikao hicho kwenye ukumbi wa hotel ya Home Ground mjini Mpanda.

DKT.BITEKO AHIMIZA KURA ZA KUTOSHA BUSONZO

September 10, 2025 Add Comment


Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Dkt. Doto Biteko akisalimiana na wananchi wa Kata ya Busonzo alipofanya Mkutano wa kuomba kura kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, 2025. Kampeni hizo zimefanyika katika Kijiji cha Busonzo Kata ya Busonzo Wilaya ya Bukombe, Septemba 9, 2025.



📌 Wananchi wa Busonzo wanufaika na miradi ya uhakika ya umeme, maji, elimu


📌 CCM yaahidi maendeleo Busonzo


Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto  Mashaka Biteko amewahimiza wananchi wa Kata ya Busonzo wilayani Bukombe mkoani Geita kujitokeza kwa wingi na kuwapigia kura wagombea wa CCM ili kukipatia chama hicho ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu ujao Oktoba 29, mwaka huu.


Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 9, 2025 wakati akiendelea na kampeni katika Kata ya Busonzo wilayani Bukombe mkoani humo.


Amesema eneo la Idoselo katika Kata ya Busonzo lilikuwa na changamoto kadhaa ikiwemo barabara na shule.


Kufuatia hali hiyo, Rais Samia alielekeza wananchi wa eneo hilo wachongewe barabara, wajengewe shule na hospitali.


“ Hapa Idoselo tumejenga Kituo Kikubwa cha Kuzalisha umeme megawati 5 ili wananchi waweze kupata umeme, tunataka kuongeza upatikanaji wa maji na baada ya uchaguzi tutapanua chanzo cha maji ili kuhakikisha kunakuwa na maji ya uhakika,” amesema Dkt. Biteko.


Ametaja vipaumbele vya CCM ni kujenga shule nyingine ya sekondari  Idoselo ili kupunguza adha ya wanafunzi kwenda kusoma Busonzo.

Aidha, amewahimizi wananchi na wajumbe wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu na kumchagua mgombea wa Urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo pia amewaomba wananchi wamchague kwa nafasi ya Ubunge wa Bukombe pamoja na mgombea Udiwani Merikiori wa Busonzo.

Akimnadi mgombea udiwani wa Kata ya Busonzo, amesema mgombea huyo ni mchapakazi na anayetaka maendeleo hivyo, wananchi wamchague ifikapo Oktoba 29 huku akisisitiza kuwa ili CCM ishinde kwa kishindo wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura.

Naye, Mgombea wa nafasi ya Udiwani  Kata ya Busonzo, John Merikiori amesema ni wajibu wa wananchi kupiga kura na kuchagua wagombea wa CCM ambao wakipata dhamana ya uongozi watahakikisha wanaleta maendeleo kwa wananchi. 


Mwisho.

DKT.NCHIMBI AWASILI SUMBAWANGA VIJIJINI

September 08, 2025 Add Comment

 


MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasili katika Uwanja wa Laela A,Sumbawanga Vijijini  kuwahutubia Wananchi  katika mkutano wa hadhara wa Kampeni  leo Jumatatu Septemba 8,2025.



Dk.Nchimbi ameingia Mkoani Rukwa leo kuendelea na mikutano yake ya kampeni ya kutafuta kura za kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.

MGOMBEA UBUNGE MAKUBELI ATAJA FLYOVERS TANGA

September 07, 2025 Add Comment



Na Oscar Assenga, TANGA


MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Kassim Makubeli amehaidi kwamba endapo atachaguliwa kuwatumikia wananchi atahakikisha anasimamia kwa karibu usanifu na ujenzi wa barabara za Juu (Flyovers) eneo la Kwaminchi kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na ujenzi wa madarasa.

Makubeli aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika eneo la uwanja wa Komesho Jijini Tanga ambapo alisema licha ya hivyo pia atahakikisha anasimamia miradi mingine ya maendeleo kama ilivyoelekezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ikiwemo ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma



Alisema eneo hilo kuna umuhimu mkubwa kuwa na barabara za juu ili kupunguza msongamano ambao unaweza kujitoeza hasa nyakati wa asubuhi na jioni ambapo wakati mwengine kumekuwa kukishuhudiwa foleni.

Aliwaomba wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupiga kura Octoba 29 kuwachagua kwa kumpa kura nyingi Rais Dkt Samia Suluhu na yeye kuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga ili aweze kuwapa maendeleo.

Awali akizungumza katika mkutano huo,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman aliwaomba wakazi wa Tanga kumchagua Kasim Amary Makubeli akieleza kwamba atakuwa kiendelezo wa kazi nzuri zilizofanywa na mtangulizi wake Ummy Mwalimu.

Alisema kwamba makubeli ni chaguo sahihi kwa sababu amepewa dhamana na chama kutekeleza ilani ya CCM ambayo msingi wake Mkuu ni amani,maendeleo na mshikamano wa Kitaifa.

Aidha alisema kwamba katika shughuli za maendeleo katika Jimbo hilo kuwa miradi mikubwa ya kimkakati imeanza kutekelezwa ikiwemo upanuzi na maboresho ya Bandari ya Tanga,Ujenzi wa viwanda pamoja na kuimarisha sekta ya elimu kwa kujengwa shule za Sekondari mpya ili kupunguza msongamano wa wanafunzi.

Rajabu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM alisema kwamba katika sekta ya afya ,Rais Dkt. Samia Suluhu ameendelea kupungumza kwa kiasi kikubwa changamoto zilizokuwepo awali kwa kujenga Vituo vya Afya,zahanati pamoja na kuboresha Hospitali za Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo.

Aliwataka wana CCM kuendelea kuendesha kampeni za Kistaarabu ili kuwaonyesha wapinzani kuwa CCM kina watu wema.

Naye kwa upande wake Mbunge aliyemaliza muda wake Ummy Mwalimu aliwataka wakazi wa Tanga kumchagua kwa kumpa kura nyingi Mgombea Urais wa CCM Dkt Samia Suluhu na mgombea Ubunge Kassim Makubeli na madiwani wa chama hicho ili kurahisisha maendeleo.

SIWEZI KUISUSA CCM,NITASHIRIKI KUTAFUTA KURA ZA WAGOMBEA -UMMY

September 07, 2025 Add Comment


Na MASHAKA MHANDO, Tanga

ALIYEKUWA mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, amesema hawezi kukisusa Chama Cha Mapinduzi (CCM) badala yake atahakikisha anashirikiana na walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili waweze kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni wa Chama hicho wa kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga, uliofanyika katika uwanja wa Vijana uliopo kata ya Duga, Ummy alisema CCM imemlea na kisha kumpa Uwaziri kwa miaka 14 hivyo, hawezi kuisusa wala kufanya nongwa.

DKT.NCHIMBI AWASILI MKOANI GEITA

September 05, 2025 Add Comment


Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Balozi. Dkt. Emmanuel Nchimbi akiteta jambo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Shule ya Msingi  Masumbwe, Wilayani Mbogwe, Mkoa wa Geita leo Septemba 5, 2025.



NCHIMBI ATINGA GEITA ,APOKELEWA KWA KISHINDO MBOGWE

September 05, 2025 Add Comment

 


Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi  akiwahutubia Wananchi wa kata ya Masumbwe,katika Viwanja vya Shule ya Msingi  Masumbwe, leo Ijumaa Septemba 5,2025 Wilayani Mbogwe, Mkoa wa Geita .

Dkt Nchimbi ameingia mkoani Geita leo kuendelea na Mikutano yake ya Kampeni ya kusaka kura za ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),akitokea mkoani Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbongwe,Fagasoni Aron Nkingwa pamoja na Madiwani.

Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Geita ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.





NIKIWA RAIS UBUNGE ITAKUWA NAFASI YA WITO- DOYO

September 04, 2025 Add Comment


Na Paskal Mbunga,TANGA


MGOMBEA Urais kupitia Chama cha NLD Doyo Hassani Doyo amesema kwamba akipata ridhaa ya kuwa Rais Ubunge itakuwa ni nafasi ya wito na ndani ya miaka mitano hivyo mtu akipelekewa fomu ya ubunge atatimua mbio kwa sababu hakutakuwa na maslahi.

Doyo aliyasema hayo leo wakati alipozindua Kampeni za chama hicho Taifa zilizofanyika eneo la Komesho Jijini Tanga ambapo alisema kwa sababu atakwenda kushusha maslahi ya wabunge ili kusiwe na fujo kwenye vyama vya siasa kwa kushusha kiwango cha mshahara wao kwa mwezi

Alisema kwamba kwa sasa mbunge analipwa milioni 12 kila mwezi wakati daktari bingwa analipwa Milioni 1.8 hivyo iwapo akipata ridhaa ya kuwa Rais atashusha viwango hivyo kwa wabunge ili walipwe madaktari bingwa kutokana na kazi kubwa wanayoifanya kuwahudumia watanzania

“Niwaambie hapa kwamba nikiwa Rais Ubunge itakuwa nafasi ya wito na ndani ya miaka mitano mtu akipelekewa fomu ya ubunge atatimua mbio kwa sababu hakuna pesa na nitakwenda kushusha maslahi ya wabunge ili kusiwe fujo kwenye vyama vya siasa mbunge analipwa milioni 12 uzalendo uko wapo wakati daktari bingwa analipwa milioni 1.8 lakini mwana sasia analipwa milioni 12 kwa mwezi nikiwa rais mbunge atalipwa mlioni 1.5 na  Daktari Bingwa atalipwa milioni 12”Alisema Doyo
 

“Hatutaki mchezo ni nchi hii viongozi wa Serikali wamekuwa wakitunga kanuni kwa ajili ya faida ya maisha yao wakati mama mjamzito anatozwa fedha kwa ajili ya kujifungua laki moja mbunge analipwa milioni 12 kwa mwezi na sitingi allowance lakini mtanzania maskini anakwenda kulipishwa laki moja mama yake akijifungua mdogo wake"Alisema

Hata hivyo alisema kwamba hilo haliwezekani ndio maana aliwaeleza kwamba akiingia madarakani ndani ya siku 100 za kwanza atapiga marufuku wakina mama wakienda kujifungua kutozwa gharama zozote ndio maana amekuja Tanga kuomba kura ili awe Rais wa nchi ili aondoe kero zinazowakabili.


Ajira kwa vijana



Alisema kwamba Serikali ya NLD itahakikisha inaboresha ajira kwa vijana ikiwemo kuimarisha uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo ya chakula na kuhakiksha wazee wanapata matibabu bora.