*RAIS KIKWETE KIKWETE AWAAPISHA BALOZI NA WAJUMBE WA TUME YA OPERESHENI TOKOMEZA IKULU DAR

June 24, 2014


Balozi Joseph Edward Sokoine akila kiapo,kupokea miongozo ya kazi na kupongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha balozi mmoja pamoja na wajumbe wanne wa Tume ya Operesheni Tokomeza katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.

Balozi aliyeapishwa ni Joseph Edward Sokoine ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Wajumbe walioapishwa nia pamoja na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Hamisi Amiri Msumi, Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema,Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo pamoja na katibu wa tume hiyo Bwana Frederick Kapela.
 Wajumbe wa Tume ya operesheni Tokomeza wakiwakatika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal (Wanne Kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia) wajumbe hao kutoka kushoto ni Katibu wa Tume hiyo Bwana Frederick Kapela Manyanda, Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo(wapili kushoto), Jaji mstaafu Hamisi Amiri Msumi(Watatu kushoto), na Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema (kulia),Wasita kushoto ni  Balozi Joseph Edward Sokoine.
Picha ya pamoja na Balozi na Wajumbe wa Operesheni tokomeza. Picha na Freddy Maro

*CHINA NA TANZANIA ZAZINDUA UJENZI WA JENGO LA TAASISI YA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR

June 24, 2014


 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia) kwa pamoja wakizindua jiwe la msingi katika eneo litakapojengwa jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa pili kulia) kwa pamoja wakizindua wakimwaga mchanga kuashiria kuanza kwa ujenzi jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing.
 Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini Mkapa (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF).
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (wa pili kushoto) akisalimiana na Mama Maria Nyerere mara baada ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) jijini Dar es salaam wakishuhudiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
  Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ( kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Kulia) na Mama Maria Nyerere wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa Wawamu ya tatu, Benjamini Mkapa,Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WASICHANA WILAYA YA TANGA YAFANYIKA LEO,DIWANI WA VITI MAALUMU AWAFUNDA WASICHANA HAO

June 24, 2014
DIWANI WA VITI MAALUMU AMBAYE PIA NI MJUMBE WA BODI YA TAWODE AKIZUNGUMZA LEO WAKATI AKIFUNGUA MAFUNZO YA WASICHANA WA WILAYA YA TANGA KWENYE UKUMBI WA YDCP JIJINI TANGA,KUSHOTO NI BURHAN YAKUB MJUMBE WA TAWODE NA KULIA NI MKURUGENZI MTENDAJI WA TAWODE FATUMA MGANGA NA MAKAMU MWENYEKITI WA BODI ABDI MAKANGE AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA NA OFISA USTAWI WA JAMII WILAYA YA TANGA,

MKURUGENZI MTENDAJI WA TAWODE FATUMA MGANGA AKIZNGUMZA WAKATI WA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WASICHANA WILAYA YA TANGA YALIYOFANYIKA LEO KWENYE UKUMBI WA YDCP

MJUMBE WA BODI YA TAWODE,SAA MAMY MOHAMED AKIZUNGUMZA WAKATI WA UFUNGUZI WA MAFUNZO HAYO LEO

HAPA WAKIPIGA MAKOFI MARA BAADA YA MGENI RASMI DIWANI WA VITI MAALUMU NA MJUMBE WA BODI HIYO RUKIA MAPINDA KUMALIZA HOTUBA YAKE

BAADHI YA WASICHANA WALIOSHIRIKI KWENYE MAFUNZO HAYO WAKIPIGA MAKOFI KUPONGEZA HOTUBA YA MGENI RASMI.



HAPA BAADHI YA WASHIRIKI WAKIULIZA MASWALI.







MEZA KUU WAKIFUATILIA JAMBO WAKATI WA MAFUNZO HAYO LEO.




HAPA WASHIRIKI WAKIJITAMBULISHA MMOJA MMOJA.

      HAPA MGENI RASMI AKAPIGA PICHA MOJA NA WASHIRIKI WA MAFUNZ HAYO LEO