“Mwanamke wa Afrika bado anakabiliwa na changamoto” - Waziri Ummy Mwalimu

“Mwanamke wa Afrika bado anakabiliwa na changamoto” - Waziri Ummy Mwalimu

March 15, 2016
“Mwanamke wa Afrika bado anakabiliwa na changamoto” - Waziri Ummy Mwalimu
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ( Mb) ametoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Mkutano huu wa wiki mbili unawakusanya wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.
Wakati mamia ya wanawake kutoka serikalini na Asasi za Kiraia wakiwa wanakutana hapa Umoja wa Mataifa kwa mkutano wao unaojadili hali yao katika maeneo mbalimbali. Mamia mengine ya wanawake hususani wale wa Afrika wanaendelea kukumbana na changamoto lukuki zinazowarudisha nyuma kimaendeleo.
Ni wanawake hao wanaoishi katika nchi zenye migogoro, vita visivyokwisha, wenye kukabiliwa na uhaba na ukosefu mkubwa wa chakula, maji safi na salama, matatizo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ndio ambao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu(Mb) ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya ushirikiano ili malengo mapya ya maendeleo endelevu (Agenda 2030) yaweze kuwafikia.
Waziri Mwalimu ametoa wito huo jana jumatatu, wakati alipotoa hutuba kwa niaba ya nchi za Afrika katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya wanawake (CSW) ambao umeanza hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
08b03dc1-8077-433f-a8db-425449efcc49Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akitoa hotuba katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW).
Changamoto hizo pamoja na nyinginezo nyingi zikiwamo kutopata fursa ya huduma za afya ya uzazi salama, elimu na usawa wa kijinsia zinamfanya mwanamke wa Afrika ashindwe kushindana na wanawake wenzie hususani wale walioko katika mataifa yaliyoendelea.
Waziri Mwalimu ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu wa wiki mbili, alitoa hotuba hiyo kwa niaba ya nchi za Afrika kutokana na kwamba Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika kwa mwezi huu wa March.
Amewaeleza washiriki wa mkutano huo waliofurika katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwamba ingawa pamekuwapo na makubaliano na mapendekezo mengi kuanzia yale yaliyofikiwa huko Beijing, bado mwanamke anayeishi katika nchi zenye migogoro na vita barani Afrika ataendelea kuachwa nyuma na hivyo kukosa fursa ya kushinda na wenzie.
“ Ingawa vita, ukame wa kutisha, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji safi, ukichanganya na ukosefu wa fursa za kiuchumi, kijamii na kisiasa ni matatizo yanayowakabili watu maskini lakini mwanamke ndiye anayeathirika zaidi,” alieleza Waziri Mwalimu.
Na kuongeza kwamba Afrika inaendelea kutilia mkazo hoja ya kuwashirikisha wanawake katika majadiliano na utoaji wa maamuzi katika masuala yanayowagusa yakiwamo masuala yanayohusu mabadiliano ya tabia nchi na usuluhishi wa migogoro.
Alieleza kwamba, nchi zinazoendelea na zilizoendelea zinapashwa kuongeza kasi ya ushirikiano na ubia baina yao ili kufanikisha utekelezaji wa Agenda 2030), Makubaliano juu Mabadiliko ya Tabia nchi yaliyofikiwa huko Paris Ufaransa mwaka jana na makubaliano yaliyofikiwa na waafrika wenye kupitia Ajenda 2063 , ili katika umoja wake dunia basi iweze kumwondoa mwanamke na jamii nzima kutoka hapa ilipo na kufikia hali bora zaidi ya maisha.
Kama hiyo haitoshi Waziri alisema, Afrika inaamini pia katika uwezeshwaji wa Sekta binafsi, kupanua wigo wa ujasiliamali kama njia mojawapo ya kukuza uchumi endelevu , usawa wa kijamii, usawa wa jinsia, ulinzi wa mazingira na uwezeshaji wa mwanamke.
Mada kuu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake, ni “Uwezeshaji wa Wanawake na uhusiano wake na Ajenda 2030.
Awali akizungumza mwanzoni mwa mkutano huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amasema tangu alipoingia madarakani mwaka 2006 amejjitadi kuongeza nafasi za viongozi wanawake katika Idara za Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.
9222e2ae-9627-4a09-abd3-72692b57d550Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akiwa katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manong.
Akitilia msisitizo hoja na haja ya kupanua wigo wa wanawake kushika nafasi katika ngazi za juu za maamumizi, Ban Ki Moon amesema, ingawa nchi nyingi zimejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi bado kuna Nchi Tano ambazo hazina wanawake katika Mabunge yao ili hali Nchi nyingine 7 hazina mawaziri wanawake katika serikali zao.
Naye Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa Bw Monges Lykketoft, akizungumza wakati wa mkutano huo, pamoja na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Agenda 2030 ambayo ameitaja kuwa ni jumuishi ameendelea kupigia chapuo la kutaka Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa awe Mwanamke.
Na Mwandishi Maalum, New York

HAFLA YA MCHAPALO WA UZINDUZI WA INTANETI YA KASI YA TIGO 4G LTE JIJINI MWANZA YAFANA

March 15, 2016

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe  Joseph Mkirikiti(katikati),Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula(kulia),Mbunge wa Ilemela Angelina Mabula(wa pili kuhoto),Mkuu wa Kitengo cha Biashara Olivier Prentout(kushoto) na  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Ali Maswanya(wa pili kulia)wakipiga ngoma ikiwa ni ishara ya  uzinduzi wa mtandao wa tigo wa 4G jijini Mwanza
Wageni waalikwa wa uzinduzi wa mtandao wa tigo wa 4G jijini Mwanza,wakibadilisha line zao ili wapate zinazoweza kuendana na kasi hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe  Joseph Mkirikiti(kulia),Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula(katikati) na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Ali Maswanya,wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa mtandao wa tigo wa 4G jijini Mwanza.
Wageni waalikwa wa uzinduzi wa mtandao wa tigo wa 4G jijini Mwanza,wakinunua Modem  za 4G,ambapo ziliuzwa kwa punguzo la bei.

GESI YENYE UJAZO WA FUTI TIRIONI 2.17 YAGUNDULIKA BONDE LA RUVU MKOANI PWANI

March 15, 2016
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhomgo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kugundulika kwa futi za ujazo wa Gesi Tirioni 2.17 katika Bonde la Ruvu mkoani Pwani,  katika eneo la Mamba Kofi One ikiwa ni moja ya ugunduzi ulifanywa na Kampuni ya Dodsal ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli na Tanzania (TPDC). Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Justin Ntalikwa.
 Makamu wa Rais Uendeshaji na Meneja Mkuu wa  Kampuni ya Haydrocarbons and Power Limited (DODSAL), Tom Gray (kulia), akizungmza katika mkutano huo kuhusu kugundulika kwa gesi hiyo ambayo itachimbwa na kampuni yake hiyo. 
 Meneja Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Gesi Tanzania,  Venosa Ngowi (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Dk.Juliana Pallangyo wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

SERIKARI  imetangaza rasmi kugundulika kwa futi za ujazo wa Gesi Tirioni 2.17 katika Bonde la Ruvu mkoani Pwani,  katika eneo lijulikanalo kama Mamba Kofi One ikiwa ni moja ugunduzi ulifanywa na Kampuni ya Dodsal ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Akitoa tamko hilo mbele ya vyombo vya habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi, Waziri wa  Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa hadi kufikia Machi mwaka huu jumla ya gesi yote iliyogunduliwa nchini ni trioni 57.23.

"TPDC imerekebisha muundo wake tunataka iwe inajishughulisha  na utafutaji wa gesi ya mafuta hivyo kufuatana na sheria ya petroli ya mwaka jana kazi zote zitasimamiwa na TPDC na haitaendelea kusimamia makampuni mengine badala yake tuameazisha wakala wakusimamia kazi ," alisema Muhongo.

Akitolea ufafanuzi kuhusiana  na kugundulika kwa gesi hiyo asilia iliyopo nchi kavu imefikia futi za ujazo tirioni 10.17, na baharini katika kina kilefu cha futi za ujazo ni 47.08. 

Waziri Muhongo alisema ufumbuzi huo umefanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Haydrocarbons and Power Limited (DODSAL) hivyo wakiendelea na utafiti wataweza kuvuka hata futi 10 kama walivyo dai.

Alisema kuwa takribani futi za ujazo  elefu moja zina uwezo wakuzalisha jumla ya megawati za umeme zipatazo 5000 wakati huo bado wanaendelea na  utafiti wa gesi katika maeneo ya kusini mwa Tanzania ambapo kume gundulika kuwa na gesi nyingi .

"Nilazima taifa letu liwe na umeme mwingi, na umeme wa kutosha kwani tukifanya hivyo tunaweza kufikia kwenye bigawati kama nchi za kusini walivyoweza kupata umeme mwingi," alisema Muhongo.

Akijibu maswali kuhusiana  na kunufaika kwa wananchi na gesi hiyo alisema tayari wameaza kunufaika kwani kabla ya awamu ya tano ya Rais Dk. Jonh Magufuli,  jumla ya megawati 700 hadi 800 ndizo zilikuwa zikitumika katika matumizi ya umeme ambapo katika kipindi cha  awamu ya tano jumla megawati 1000 zinaendelea kutumika.

"Ifahamike kuwa faida ya gesi kwa wananchi ni ya siku nyingi kwani viwanda takribani 37 vimekuwa vikitumika kwa matumizi ya gesi kikiwemo kiwanda cha Saruji " alisema.

Awali kabla ya uzinduzi huo Meneja Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Gesi (TPDC), Venosa Ngowi alisema wanatarajia kumpatia ripoti ya mapendekezo ya juu ya gharama za uuzaji wa gesi nchini ifikapo Aprili,20 mwaka huu.

Ngowi alisema zoezi linalofanyika ni mazungumzo ya wawekezaji na watalamu wa nchi husika kuweza kufanya uhakiki wa gharama wa bei za gesi nchini.


Alisema moja ya changamoto wanazokutanazo ni kuwepo kwa gharama nyingi  zinazo muhusu mwekezaji.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
LIGI KUU KUENDELEA JUMATANO

LIGI KUU KUENDELEA JUMATANO

March 15, 2016
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa mchezo mmoja, ambapo Azam FC watawakaribisha Stand United katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Ijumaa mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kambarage, wakata miwa wa Kagera Sugar watakua wenyeji wa ndugu zao kutoka wakata miwa Mtibwa Sugar kutoka Manungu Turiani.
Wikiendi Jumamosi na Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo mitano kuchezwa katikwa viwanja mbalimbali nchini, jijini Tanga wenyeji Coastal Union wakiwa wenyeji wa Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini humo.
Majimaji FC itakua nyumbani katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kucheza na Mbeya City, huku chama la wana Stand United wakiwakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Jumapili African Sports watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la magereza Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mkwakwani jijii Tanga, huku siku ya Jumatatu Mgambo Shooting wakicheza dhidi ya Toto Africans jijini Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.

TWIGA STARS KUWAFUATA ZIMBABWE IJUMAA

TWIGA STARS KUWAFUATA ZIMBABWE IJUMAA

March 15, 2016
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu “Twiga Stars” inatarajiwa kusafiri siku ya Ijumaa kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.
Kikosi cha Twiga Stars kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume chini ya kocha mkuu, Nasra Juma kujiandaa na mchezo huo muhimu ili kuweza kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Kuhusu maendeleo ya kambi, kocha Nasra Juma amesema vijana wake wanaendela vizuri, wamekua wakiendelea na mazoezi tangu baada ya mchezo wa awali na ana imani watafanya vizuri katika mchezo wa marudiano.
Twiga Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Jumapili, Machi 20 katika uwanja wa Rufalo uliopo jijini Harare ili kuweza kufuzu kwa hatua ya pili ya michuano hiyo.
TAARIFA MUHIMU KUTOKA TFF

TAARIFA MUHIMU KUTOKA TFF

March 15, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na taarifa za upotoshaji za chombo kimoja cha habari ambacho mmoja wa watendaji alipata fursa ya kuhudhuria mkutano mkuu kama mgeni mwalikwa uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Tanga.
Katika hali inayotia mashaka, siku mbili kabla ya mkutano huo, chombo hicho kiliripoti kuwa wajumbe walikuwa wanalalamika kwa kutopelekewa nyaraka zinazohusiana na mkutano, wakati ukweli ni kuwa nyaraka hizo zilitumwa tangu mwezi Novemba 2015 zikiwa ni sehemu ya barua ya mwaliko wa kikao. Hivyo isingewezekana mwaliko wa kikao ukapokelewa na nyaraka zisiwepo. TFF inao ushahidi wa nyaraka hizo kuwafikia wajumbe wa mkutano huo.
Katika toleo lake la leo chombo hicho kilidai TFF kupata hasara ya shilingi za kitanzania milioni 500.
TFF inaviomba vyombo vya habari kuacha kupotosha juu ya taarifa za mkutano mkuu kuwa shirikisho lilipata hasara (loss) , TFF haifanyi biashara yoyote mpaka kufikia kupata hasara, kilichotokea ni kuongezeka kwa nakisi (deficit) katika bajeti ya mwaka 2014.
Matumizi yaliongezeka kutokana na kulipa madeni ambayo uongozi wa sasa uliyakuta uliyosababisha hata basi la timu ya Taifa likamatwe, kuwepo kwa michezo mingi ya timu za Taifa (Taifa Stars, Twiga Stars, Serengeti Boys), gharama ambazo zilijumuisha kambi za maandalizi za timu pamoja na safari.
Kwa kuwa TFF haifanyi biashara yoyote, matumizi yaliongezeka zaidi ya bajeti iliyokuwa imeratajiwa na kufanya kuwepo na upungufu wa zaidi ya milioni 490.
Aidha TFF imesikitishwa na taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mwishoni mwa wiki iliyopita, kuhusiana na suala la tiketi za Elektroniki.
Ifahamike kwamba TFF ndiyo ilianzishwa matumumizi ya tiketi hizo kabla hazijasitishwa na Serikali mwaka jana kutokana na kubaini mapungufu katika utekelezaji.
TFF haijawahi kugomea kuwepo kwa mfumo huo wa ki elektorniki, na kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo wanaendelea na mazungumzo juu ya mfumo huo.
Vikao vinaendelea kati ya Wizara na TFF ili kuona njia gani itaweza kutumika katika uendeshaji wa kuingia viwanjani kw aka kutumia mfumo wa ki elektroniki na kesho kutakuwepo na kikao Wizarani kujadili mradi huo.
TFF inatafakari juu ya hatua za kuchukua dhidi ya wanaotoa taarifa za upotoshaji huo.
TZ MEETS NAIJA: BEN POL, VJ ADAMS & G NAKO TEAMS UP ON THIS MASSIVE PROJECT 'NINGEFANYAJE REMIX'

TZ MEETS NAIJA: BEN POL, VJ ADAMS & G NAKO TEAMS UP ON THIS MASSIVE PROJECT 'NINGEFANYAJE REMIX'

March 15, 2016
Ben Pol
With ‘NINGEFANYAJE’ (What was I supposed to do?) video topping the Top 10 East and Africa Rox Countdown charts on SoundCity and making a splash on MTV Base Africa, it was only a matter of time before Ben Pol put a twist on his hit song to bring us the official...REMIX!
This New release (NINGEFANYAJE REMIX) brings together Tanzania's undisputed King of R&B Ben Pol, one of Naija's finest multi -talented artiste and media personality VJ Adams, and Tanzanian extraordinaire rapper G-Nako of the WEUSI Hip Hop group.
The song is now available on Tanzania's Music Selling platform MKITO and will soon be available itunes, Amazon, Spotify, Deezer and on all key music distribution channels.
Consume without moderation!
Be the first one to listen 'Press Play' and enjoy!
MO SPEAKS ABOUT BEING YOUNGEST BILLIONAIRES ON CNN MARKET PLACE IN AFRICA (VIDEO)

MO SPEAKS ABOUT BEING YOUNGEST BILLIONAIRES ON CNN MARKET PLACE IN AFRICA (VIDEO)

March 15, 2016
Mo on cnn marketplace Africa
In December 2015, Forbes Africa named Mohammed Dewji, CEO of MeTL Group, the continent's "Person of the Year". CNN's Eleni Giokos sat down with him to discuss what it's like being one of Africa's youngest billionaires.
WANAWAKE WASHIRIKISHWE ZAIDI KATIKA MABADILIKO YA TABIANCHI : WAZIRI UMMY MWALIMU

WANAWAKE WASHIRIKISHWE ZAIDI KATIKA MABADILIKO YA TABIANCHI : WAZIRI UMMY MWALIMU

March 15, 2016
ummm
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Masuala ya Wanawake, Wazee na Watoto wa Tanzania, Mh. Ummy Mwalimu akiwasilisha mada kuu ambapo aliwakilisha kundi la Afrika katika mkutano huo mkubwa unaoendelea nchini Marekani.
Bara la Afrika na hasa wanawake ndio wanaobeba mzigo zaidi wa madhara ya mabadiliko ya tabianchi, huku wakinyimwa fursa ya kushiriki katika kutafuta suluhu kwa tatizo hilo, ameeleza leo Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Masuala ya wanawake, wazee na watoto wa Tanzania.
Bi Mwalimu amesema hayo akihutubia kikao cha 60 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake, CSW60 kwa niaba ya kundi la nchi za Afrika, akisisitiza umuhimu wa kushirikisha zaidi wanawake katika uongozi wa kimataifa kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi.
"Wanawake wanapaswa kuweza kuongoza katika ngazi za kitaifa na serikali za mitaa. Ubunifu wao, ujuzi wa kiasili, matarajio yao yanaweza kusaidia katika kubuni na kushawishi suluhu kuhusu mabadiliko ya tabianchi.
Aidha amezungumzia suala la kilimo ambacho hushughulisha wanawake zaidi, akisema la msingi ni kusaidia sekta binafsi ili kukuza ukuaji wa uchumi katika sekta hiyo na hivyo kuwezesha wanawake.
ummBaadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanawake unaofanyika nchini Marekani ulioanza jana Machi 14-24, wakiwa nje ya jengo la Umoja wa Mataifa unapofanyika mkutano huo
unwomen
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano huo wa #CSW60
ummy