RC PAUL MAKONDA ASEMA WANAWAKE NDIO CHANZO CHA UFISADI NCHINI

May 15, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua machinjio ya Vingunguti baada ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto.
Wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti wakiwa kwenye mkutano huo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani)
Makonda (kushoto), akisalimiana na wananchi na viongozi wakati akiwasili kwenye mkutano huo.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuzungumza na wananchi. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mnyamani, Shukuru Dege, RC. Makonda na Meneja wa Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB), Tawi la Ukonga, Das Ndazi.
Meneja wa Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB), Tawi la Ukonga, Das Ndazi (kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu suala zima la utoaji wa mikopo.
RC Makonda akizungumza na wananchi wa Vingunguti.
Wananchi wakimsikiliza RC Makonda.
Safari ya kwenda kukagua machinjia ya Vingunguti.
Sehemu ya machinjio ya Vingunguti.
RC Makonda akipatiwa maelezo kuhusu mitambo ya kuchinjia iliyopo kwenye machinjio hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi.

Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

" Ninyi wakina mama mmekuwa chanzo cha ufisadi kwa vile mmekuwa mkipokea fedha na zawadi mbalimbali kutoka kwa watoto wenu lakini mmekuwa hamuwahoji wanako zitoa fedha hizo kwani zingine zinakuwa za kifisadi" aliseama Makonda.

Makonda aliwaambia wanawake hao kuwa hata katika suala zima la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya wakina mama kwa watoto wao tangu wakiwa wadogo jambo ambalo lingesaidia kipindi hiki ambapo kunachangamoto kubwa ya kusafisha miji yetu.

Katika hatua nyingine Makonda alitoa pongezi kwa Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto kwa kuwa jirani na wananchi wa kata yake kwa kufanya maendeleo bila ya kujali itikadi za vyama hasa katika kujipatia mikopo kutoka katika Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

"Nimefurahishwa na diwani wenu Kumbilamoto kwa kushirikiana nanyi ili  kujiletea maendeleo ni jambo zuri na wakati huu ni wa kukutana kubuni na kuangalia jambo gani litawakwamua kiuchumi badala ya kuwaza maandamano yasiyo na tija" alisema Makonda.

AFRICAN ARTISTS ACADEMY BAND KUTUMBUIZA LEO JIJINI MWANZA.

May 15, 2016
Usikose leo jumapili Mei 15,2015 kuanzia saa 12 jioni ndani ya CHECK INN PUB Kilimahewa, Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA

May 15, 2016

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza  uliopo London wakati alipowasili ubalozini hapo  kuzungumza na watanzania  waishio  nchini humo Mei  14, 2016.. Kushoto  ni  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Msafiri Marwa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye ubalozi wa Tanzania  nchini Uingereza uliopo London kuzungumza na Watanzania Mei 14, 2016. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki , kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga na kushoto ni Jaji Mkuu wa Tamzania, Mohamed Othman.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania Waishio  nchini Uingereza  kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo London Mei 14, 2014.   Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga. Kushoto ni KaimuBalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Msafiri  Marwa .
Baadhi ya Watanzania waishio nchini Uingereza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ubalozi wa  Tanzania uliopo London   Mei 14,2016, 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza  uliopo London wakati alipowasili ubalozini hapo  kuzungumza na watanzania  waishio  nchini humo Mei  14, 2016.. Kushoto  ni  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Msafiri Marwa. 

(Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)

KIWANDA CHA BIA YA SERENGETI CHAPIGWA FAINI

May 15, 2016
Naibu Waziri Wa nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Afisa mazingira wa kiwanda cha serengeti Bw.Simon Peter mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo.

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina wa kwanza kushoto,katikati aliyevaa kanzu ni mbunge wa Temeke(CUF)Mh.Abdallah Mtolea wakitembezwa sehemu mbalimbali za kiwandani hapo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza.  
         Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipata maelezo jinsi gani kiwanda hicho kinavyochuja maji kwa njia ya kisasa kabisa kwaajiri ya matumizi na uzalishaji kiwandani hapo.
     
 Kiwanda cha bia aina ya serengeti kilichopo chang'ombe wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kimepigwa faini ya shillingi za kitanzania millioni kumi na sita(16)na Baraza la usimamizi wa mazingira Nchini(NEMC)baada ya kutokutimiza masharti ya sheria ya mazingira ya mwaka(2004)na kanuni zake.   
       
Uamuzi huo umefikiwa baada ya  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina kupata malalamiko kutoka kwa wanainchi wanaozunguka maeneo ya kiwanda hicho na kuainisha uchafuzi wa mazingira yanayowazunguka wananchi hao na kuhatarisha  usalama wa afya zao,ambapo ilimlazimu naibu waziri kufanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo,huku akiambatana na Wakurugenzi kutoka Baraza la usimamizi wa mazingira nchini(NEMC)na kujionea uharibifu huo.     
              
Mh.Mpina ameagiza kiwanda hicho kulipa faini hiyo na kurekebisha miundo mbinu hiyo ndani ya siku arobaini na tano kusiwepo tena na utiririshaji maji machafu na yenye kemikali kali za sumu ambayo yanatoa harufu mbaya inayohatarisha afya  za wakazi wa chang'ombe wilaya ya temeke. 
              
Pia mkurugenzi wa mazingira Bw. Boniventure Baya ametoa siku saba kwa kiwanda hicho kiwe kimelipa faini hiyo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kutokana na kwamba wamekua wakikaidi maagizo yanayotolewa na Baraza hilo la mazingira nchini(NEMC)na kuwataka kufanya hivyo haraka iwezekanavyo baada ya kukiuka sheria ya utunzaji mazingira ya mwaka(2004) na kutokutimiza masharti waliyopewa takribani miaka miwili iliyopita.    
       
Naye mbunge wa Temeke(CUF) Mh.Abdallah Mtolea alisema kiwanda hicho kimekua na mahusiano mabaya na wananchi wanaozunguka maeneo jirani na kiwanda hicho hivyo kupelekea kuwa na mgogoro wa muda mrefu na uongozi kiwandani hapo na kumuomba Naibu waziri kutatua tatizo hilo ambalo limekua likifanywa kwa makusudi na na uongozi wa kiwanda hicho ilihali wanajua madhara ya wanayoyapata wananchi.                                                         
Aidha kwa upande wake afisa mazingira wa kiwanda hicho Bw.Simon Peter alipinga vikali tuhuma hizo ambazo zimeelekezwa katika kiwanda hicho na kusema uongozi wa kiwanda hicho unafanya kila jitihada ili kuweza kutatua kero hiyo na si kweli kwamba hawashughulikii tatizo hilo la mazingira jirani na wakazi hao.    
           
Kwa upande wao wananchi kupitia kwa Bi.Emanuela Peter,walisema hiyo ni kero kubwa sana kwao ambapo imekuwa ikiwalazimu kuyahama makazi yao hasa wakati wa kipindi cha masika ambapo maji ya mvua na yale ya kiwanda huchanganyikana na kujaza uchafu wote majumbani mwao kutoka kiwandani na kuhatarisha afya zao hivyo kuhamia kwenye nyumba za kulala wageni kwa muda,hivyo wameiomba serikali kuangalia kwa makini na kuweza kulipatia ufumbuzi.     
               
Vilevile Mh.Luhaga alifanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha Cement Wazo kilichopo Tegeta wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam,hata hivyo hakuweza kukutana na kiongozi yeyote wa kiwanda hicho kwa madai kua walikua nje ya mkoa wa Dar es salaam,aidha Mh.Mpina alitoa tamko la serikali kuwa,serikali ya awamu ya tano haina uadui na wafanyabiashara pamoja na wawekezaji kama inavyozaniwa na watu wengine,bali inachotaka ni kufuatwa kwa Sheria,taratibu na kanuni kama inavyostahili.