PICHA:TAZAMA BOTI TATU ZENYE MALI ZA MAGENDO ZILIVYOKAMATWA KIGOMBE,PANGANI

January 20, 2016

Jumuiya ya Veterani wa Umoja wa Vijana Zanzibar (Young Pioneers) yazinduliwa

January 20, 2016

Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Veterani wa Young Pioneers, Mhe. Khadija Hassan Aboud akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Mhe Asha Ali Abdalla akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya ya Veterani ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers, katika Ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee akiwahutubia Veterani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa ZSSFKiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. na kutangaza Fedha zilizopatika katika harambee aliyoiazisha kwa ajili ya kukuza Mfuko wa Jumuiya hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 9,724,000/= zimepatika ikiwa Fedha Taslimu Shs 3.874,500 na Ahadi Shs.5,850,000/=
Wanachama wa Jumuiya ya Veterani wa Young Pioneers wakimsikiliza mgeni rasmin akiwahutubia wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya yao.
Veterani wa Jumuiya ya Uomja wa Vijana wa Young Pioneers wakimsikiliza mgeni rasmin wakati akiwahutubia na kuwazindulia Jumuiya yao.
Wazee Maveterani wa Young Pioneers wakiwa meza kuu wakimsikiliza Mgeni rasmin Mhe Omar Yussuf Mzee akiwahutubia wakati wa uzinduzi huo wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. 
Maveterani wakichangia katika harambee hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo
Maveterani wakichangia katika harambee hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo
Veterani wa Umoja wa Vijana aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Tanzania Mhe Sukwa Said Sukwa akichangia katika harambee hiyo, ya Uzimguzi wa Jumuiya hiyo.
Veterani wa Young Pioneers Mhe. Aboud Talib Aboud akichangia wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo. baada ya kuitishwa upato wa maridadi na kupatikana shilingi milioni 9,724,000/= papo kwa papo wakati wa harambe hiyo ya Veterani wa Young Pioneers.
Veterani wa Young Pioneers Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis akichangia wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo. 
Mjumbe wa Kamati ya Jumuiya ya Veterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers Meja Generali Mstaaf Hassan Vuai Chema, akitowa neno la shukrani kwa Mgeni rasmin Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee baada ya kuwazinduliwa Jumuiya yao katika ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. 

Veterani wa Young Pioneers Makame Haji Makame (Cairo) akihamasisha kwa kuimbi wimba za Vijana za wakati huo wa kuhamasisha vijana katika kujenga taifa wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa uwanja wa watoto kariakoo Zanzibar, kabla ya kuaza kwa kongamano la Jumuiya hiyo
 Mwenyekiti wa Kongamano hilo la Veterani wa Young Pioneers Mhe Aboud Talib Aboud akiongoza kongamano hilo likizungumzia kumkomboa Kijana.katika kujiajiri na kujiengezea kipato.na kuwa na maadili mazuri.  
MTOA Mada katika Kongamano hilo la Uzinduzi wa Jumuiya ya Maveterani ya Young Pioneers Association Ndg Ali Khamis akitowa Mada kuhusu Wajibu kwa Kijana, kwa wajumbe wa mkutano huo wa uzinduzi uliofanyika ukumbi wa kiwanja cha watoto kariakoo Zanzibar
Veterani wa Young Pioneers wakimsikiliza Mtoa Mada juu ya Maendeleo ya Vijana katika kujikomboa Kiuchumi.
 
Maveterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakipiga makofi wakati wa kuingia mgeni rasmin Mhe Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya hiyo kuendeleza Vijana Zanzibar.
Maveterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakipiga makofi wakati wa kuingia mgeni rasmin Mhe Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya hiyo kuendeleza Vijana Zanzibar.
Ustadh akisoma Quran kabla ya Uzinduzi huo wa Jumuiya ya Veterani wa Umoha wa Vijana wa Young Pioneers uliofanyika katika ukumbi wa ZSSF kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Maveterani wa Young Poineers wa Umoja wa Vijna wakimsikiliza msoma quran wakati wa uzinduzi huo.

Katibu wa Veterani wa Young Pioneers Said Shaban akitowa maelezo ya Jumuiya hiyo ya Veterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakati wa Uzinduzi wake uliofanyika katika Ukumbi ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. 
Veterani wa Young Pioneers wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakato wa Kongamano.
Mgeni Rasmin Mhe Omar Yussuf Mzee akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Veterani wa Umoja wa Vijana  Young Pioneers wa wakati huo wa Umoja wa Vijana Zanzibar. Baada ya Kuizindua Jumuiya hiyo.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com.
DKT. KIGWANGALLA AUNDA KIKOSI KAZI KUBORESHA HUDUMA ZA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

DKT. KIGWANGALLA AUNDA KIKOSI KAZI KUBORESHA HUDUMA ZA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

January 20, 2016
IMG_0652
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameanzisha kikosi kazi cha watu 24 ambacho kitakuwa na kazi ya kutengeneza mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Katika taarifa ambayo imetolewa na Dkt. Kigwangala imeeleza kuwa kazi ya kuanzisha kikosi kazi hicho ni agizo kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ambaye alimtaka aanzishe kikosi hicho ili washirikiane kuanzisha mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii.
“Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu alinipa kazi ya kuunda kikosi kazi maalum na kushirikiana nacho kutengeneza mpango mkakati wa kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),” alisema Dkt. Kigwangalla.
Dkt. Kigwangalla amewataja wajumbe wa kikosi kazi hicho kuwa ni Prof. Angwara Kiwara, Prof. Phares Mujinja, Dkt. Francis Frederick, Dkt. Heri Marwa, Dkt. Deogratius Pisa, Dkt. Amos Kahwa, Irenei Kiria, Semkae Kilonzo, Gemini Mtei, Dkt. Jehovaness Aikaeli na Obey Assey.
Wengine ni Mathias Kabunduguru, Dkt. Dereck Chitama, Prof. Flora Kessy, Florence Mwanri, Athuman Rehani, Maximillian Mapunda, Bedason Shallanda, Daniel Ngowi, Beng' Issa, Edwin Mikongoti, Hussein Sengu, Dkt. Beatus Leon na Dkt. Pastory Sekule.
Aidha Dkt. Kigwangalla amewashukuru wajumbe hao kwa kukubali kufanya kazi na wizara ya afya kupitia mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii bila malipo yoyote.
Hata hivyo mara baada ya kuwachagua wajumbe wa kikosi kazi hicho tayari kimependekeza mapendekezo yao jinsi ya kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii ambayo ni kuipa nguvu kadi ya CHF ili itumike kwenye mfumo wa Afya mpaka ngazi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa na vituo vya Jirani na kupandisha kiwango cha kuchangia CHF mpaka 30,000.
Mapendekezo mengine ni kuweka bei za kukatisha tamaa watumiaji wa huduma za Afya bila kadi ya Bima ya Afya ama ya CHF na kuwahamasisha waamue kujiunga kuliko kulipa gharama za kila huduma watakayotumia, kuhamisha Mfuko wa fedha za CHF kutoka Halmashauri na kuupeleka NHIF ngazi ya mkoa lengo likiwa kumtenganisha mtoa huduma na mteja na kuweka 10,000 kuwa kiwango cha chini kwa bei za huduma za afya sehemu yoyote nchini kwa mtu asiye na kadi.
Aidha mapendekezo yao yatatumika kama serikali itayaridhia na wao wametoa mapendekezo hayo kutokana na kutambua kuwa Watanzania wapo tayari kulipia huduma za afya kwa bima ilimradi wawe wanapatiwa huduma bora ambazo zitawaridhisha.

BALOZI WA NORWAY HAPA NCHINI AWATUNUKU WAHITIMU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

January 20, 2016
Balozi wa Norway nchini Tanzania,Hanne -Marie Kaarstad ambaye alikua mgeni rasmi katika Mahafali ya Saba ya Chuo chaUfundi Arusha(ATC)akiwatunuku Vyeti,Stashahada na Shahada wahitimu katika fani za Uandisi Umwagiliaji,Umeme,Ujenzi,Mawasiliano Anga ,Mitambo na Kompyuta Januari 16,2016.

Baadhi ya wahitimu wa fani ya Uandisi Mitambo wakifurahia mara baada ya kutunukiwa Stashahada zao

Wahitimu wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali

Balozi wa Norway nchini Tanzania,Hanne -Marie Kaarstad ambaye alikua mgeni rasmi katika Mahafali ya Saba ya Chuo chaUfundi Arusha(ATC) akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wanaobaki.

Balozi wa Norway nchini Tanzania,Hanne -Marie Kaarstad (kulia)akipokea zawadi kutoka idara ya Uandisi Madini .

Balozi  Hanne -Marie Kaarstad akifurahia kazi za wanachuo alipotembelea maonesho yaliyoandaliwa kwaajili yake.

Wanachuo wanaobaki walionegesha mahafari hayo kwa bendera za kuvutia

Balozi Hanne -Marie Kaarstad  na Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Massika aliyevaa tai nyekundu wakipata maelezo kwenye idara ya Umwagiliaji .

Furaha ya kuhitimu ilitawala 


Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Massika(kulia)akifafanua jambo kwa mgeni rasmi.
Balozi wa Norway ,Hanne -Marie Kaarstad (wa pili kushoto mbele)akiwa na wageni mbalimbali na Wakuu wa Idara mbalimbali za Chuo katika picha ya pamoja.

Burudani kwa wahitimu ilikuwepo kunogesha mahafali hayo

Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com 0713 821586,Arusha.

KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI YARINDIMA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA.

January 20, 2016
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza leo imeahirisha Kesi ya Kupinga Matokeo ya Ubunge katika Uchaguzi Mkuu Uliofanyika Novemba 25,2015 Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na Christopher Ryoba Kangoye ambae alikuwa Mgombea ubunge kupitia CCM katika Jimbo hilo.

Pichani ni Wakili Tundu Lisu (Katikati) ambae ni Wakili upande wa mjibu maombi wa kwanza ambae ni Mbunge wa Jimbo hilo John Heche akizungumza juu ya kesi hiyo baada ya kuahirishwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi January 27,2015 itakaposikilizwa tena.
Wakili Tundu Lisu (Katikati) ambae ni Wakili upande wa mjibu maombi ambae ni Mbunge wa Jimbo hilo John Heche akizungumza juu ya kesi hiyo baada ya kuahirishwa. Lisu aliiomba Mahakama kuifuta kesi hiyo kutokana na makosa mbalimbali ambayo ni pamoja na mleta maombi kushindwa kuainisha amefungua kesi kupitia sheria ipi ambayo inaitaka mahakama kufuta kesi ya uchaguzi.
Wakili Constatine Mutalemwa (Mwenye Miwani) anaetetea kesi hiyo kwa upande wa Mleta Maombi ambae anaiomba Mahakama hiyo kufuta matokeo ya Uchaguzi katika Jimbo la Tarime Vijijini kutokana na sababu mbalimbali ambazo ni pamoja kuhesabiwa kwa kura zisizo halali ambazo zilimpa ushindi Mhe.Heche.
(Picha kutoka Maktaba)
John Heche ambae ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini kupitia Chadema (Wa pili kushoto) akiwa na wenzie nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza
Na:Binagi Media Group