Khadija Kopa ataka wanawake wajikwamue kiuchumi

February 11, 2017




Baadhi ya nguo za maharusi zinavyoonekana katika duka la urembo na mitindo lililozinduliwa rasmi jana, huku mgeni rasmi akiwa ni mwimbaji wa muziki wa taarabu nchini Tanzania, Bi Khadija Kopa.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa taarab nchini Tanzania, Bi Khadija Kopa, amewataka wanawake kuendelea kujikwamua kiuchumi wao wenyewe bila kusubiri kuwezeshwa na wanaume.
Khadija aliyasema hayo katika ufunguzi wa duka kubwa la kisasa la urembo na nguo za wanawake linalojihusisha pia na kupamba maharusi, kukodisha na kuuza nguo za maharusi, linalojulikana kama Taiba Beauty, linalomilikiwa na mjasiriamali Twaiba Ahmed Ally.
Mwimbaji mkongwe wa muziki wa taarabu nchini, Bi Khadija Kopa, akizungumza na waandishi hawapo pichani katika uzinduzi wa duka la nguo za wanawake na za harusi linalomilikiwa na mwanamama Twaiba Ahmed Ally.

Alisema kwamba wapo wanawake wanaoamini kuwa hawawezi kuendelea hadi wawezeshwe, jambo linalohitaji kupingwa vikali ili wanawake waweze kupiga hatua kiuchumi na kujikomboa wao wenyewe.
Mmiliki wa duka la nguo za maharusi lililopo mtaa wa Livingstone na Mkunguni, Bi Twaiba Ahmed Ally, katikati akikata keki ya uzinduzi wa duka hilo jana. Kulia ni mwimbaji wa taarabu nchini, Khadija Kopa akilishwa keki kama mgeni rasmi. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi cha Ng'ari Ng'ari kutoka Clouds Tv, Sakina Lyoka.
Twaiba akimlisha keki Khadija Kopa katika tukio la uzinduzi huo jana.
Bi Twaiba akimlisha keki Sakina Lyoka jana.
Bi Sakika Lyoka akimlisha keki mmiliki wa duka hilo, bi Twaiba Ahmed. Kushoto ni Khadija Kopa.
Naomba wanawake tuache dhana kuwa hatuwezi kuendelea hadi tuwezeshwe na wanaume, ukizingatia kuwa Dunia imebadilika na wapo wenzetu wanaofanya kazi nzuri kiasi cha kutufanya tuige nyendo zao ili tusonge mbele, akiwamo Bi Twaiba Ahmed,” Alisema Kopa.
Akizungumzia hilo, Bi Twaiba alisema ni jukumu lao kuhakikisha kwamba wanawake wanasonga mbele kiuchumi, akisisitiza namna ya ujihusishaji na masuala yote ya ujasiriamali na kazi nyingine.

“Nashukuru kwa sapoti kubwa ninayoipata, akiwamo Bi Khadija Kopa, hivyo nitaendelea kufanya juhudi ili nizidi kupiga hatua kubwa kibiashara kwa kusimamia changamoto zote zinazonikabili. “Katika duka langu nafanya shughuli zote zinazomhusu mwanamke, wakiwamo wale wanaofunga ndoa kwa kuwapamba, kuwakodisha vifaa vya harusi bila kusahau wale wanaotaka kununua kwa fedha taslimu, ofisi yangu ikipatikana katika mtaa wa Mkunguni na Livingstone, Kariakoo, jijini Dar es Salaam,” Alisema.


Mbali na kuuza vifaa vya maharusi na nguo za kawaida za wanawake, pia Twaiba anajihusisha na ufundishaji wa upambaji kwa wanawake, shughuli inayomfanya aheshimiwe na wengi wanaojihusisha na sekta hiyo ya mitindo na urembo.

BODABODA YATAJWA KIKWAZO CHA BAADHI YA WANAFUNZI KUSHINDWA KUFIKIA MALENGO YAO

February 11, 2017
USAFIRI wa pikipiki maarufu kama bodaboda wilayani Mkinga mkoani Tanga umetajwa kuwa miongoni mwa vishawishi vikubwa vya kukwamisha juhudi za elimu kwa wanafunzi wa kike kutokufikia malengo yao .

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya shule nyingi kukosa mabweni ambayo
  yanaweza kuwasaidia wanafunzi hao kuepukana na vitendo vya namna hiyo ili waweze kufikia malengo yao ya kupata elimu bora.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu
  wilayani humo, Ajalii Marumwengu wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema hali hiyo inaatokana na shule nyingi kuwepo mbali na sehemu wanazoishi wanafunzi.

Alisema hali hiyo inatokana na mazingira ya umbali wanaotoka wanafunzi
  kuwa mbali na hivyo wengine kulazimika kutembelea umbali wa km 14 mpaka kufika maeneo ya shule.
 “Ukiangalia uhalisia wa mazingira ya shule za kata hasa zilizopo
maeneo ya vijijini ni mbali kwa zipo nyengine ambazo wanafunzi
wanatembea umbali kilomita 7 mpaka 14 hivyo wanapokutana na pikipiki maarufu kama bodaboda na kupewa lifti na baadae wanashawishika kuingia kwenye mahusiano”Alisema.

“Lakini njia sahihi ya kuhakikisha suala hilo linakwisha ni kuwekwa
  mazingira mazuri ya kuanzishwa bweni kwenye shule hizo ili wale wanaokaa mbali waweze kuishi humo ili kuepukana na vishawishi “Alisema.

Aidha alisema pia changamoto nyengine wanao kabiliana nazo ni

kutokuwepo kwa nyumba za walimu na hivyo walimu hao kulazimika kukaa umbali mrefu na maeneo wanayofundishia.
 “Zipo shule nyingi hapa mkinga walimu wanafundisha lakini hawana nyumba za kuishi na hivyo kujikuta wakitembea umbali mrefu kwenda kufundisha hivyo tunaomba hilo nalo liangaliwe kwa jicho la kipekee”Alisema.