BEI YA SAMAKI SOKO LA FERI JIJINI DAR ES SALAAM YASHUKA

September 11, 2016
 Wachuuzi wa Samaki wakisubiri kununua kitoweo hicho katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Bei ya samaki katika soko hilo imepungua kutokana kwa kupatikana kwa wingi kwa kitoweo hicho.
Mnada wa samaki ukiendelea

Na Dotto Mwaibalae

HALI ya bei ya samaki katika Soko la Kimataifa la Feri jijini Dar es alaam imeshuka kutokana na samaki kupatikana kwa wingi katika kipindi cha mwezi wa Septemba.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com jijini Dar es Salaam leo asubuhi mchuuzi wa samaki katika soko hilo Mohamed Hassan alisema katika kipindi cha wiki mbili bei ya samaki imeshuka ukilinganisha ni mwezi uliopita.

"Sasa hivi samaki aina ya King Fish, Changua wanauzwa kati ya sh.30,000 lakini kipindi ambacho wakiadimika ufikia hadi sh.35,000" alisema Hassan.

Mchuuzi mwingine wa samaki katika soko hilo Shabani Shamte alisema samaki aina ya kibua, ngisi wakati huu uuzwa kati ya sh. 23,000 hadi 25,000 ambapo wakiadimika ufikia hadi sh. 30,000.

Grace Tesha ambaye uuza samaki hao maeneo ya Mabibo Loyola alisema hata wao kipindi hiki biashara yao inakwenda vizuri kutokana na kuwepo kwa samaki wengi.

"Samaki wakiadimika huwa inatuwia vigumu mno kibiashara kwani wateja wetu wamekuwa wakilalamia kuwauzia kwa bei kubwa" alisema Tesha

MSIMU WA TIGO FIESTA WANOGESHWA NA BURUDANI YA KISHINDO MKOANI TABORA

September 11, 2016

Maua Sama na Nandy wakiimba kwa pamoja katika usiku wa Tigo Fiesta mkoani Tabora mwishoni wa wiki hii
Msanii wa Bongo fleva AMADAI akiimba kwa hisia katika jukwaa  la Tigo Fiesta Mkoani Tabora 


JUX na Benpol wakiimba wimbo wa pamoja "NAKUCHANA" katika jukwaa la Tigo Fiesta katika uwanja wa Ally Hassan  mkoani Tabora


Mkali wa HipHop Niki wa pili akishambulia jukwaaa la Tigo Fiesta mkoani Tabora mapema wiki hii katika uwanja wa Ally Hassan

Nuh Mziwanda akiimba kwa hisia nyimbo yake ya Jike shupa katika jukwaa la  Tigo Fiesta mkoani Tabora mapema ijumaa hii 


Young killer akiwakilisha vyema wana HIPHOP katika jukwaa la TIGO FIESTA mkoani Tabora
Msanii wa bongo fleva Shilole,akitumbuizakwenye tamasha la Tigo fiesta Mkoani Tabora katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi(usiku wa ijumaa)
Mashabiki na wapenzi wa burudani  wakiitikia kwa shangwe kibwagizo cha "IMOOOOOOOO " katika usiku wa TIGO FIESTA mkoani Tabora
Umati wa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia tamasha la Tigo Fiesta mkoani Tabora katika uwanja wa Ally Hassan  ijumaa hii

WAZIRI MBARAWA AZINDUA GATI JIPYA PANGANI MKOANI TANGA LILILOGHARIMU ZAIDI YA BILIONI 3

September 11, 2016
WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Karim Mattaka wakati alipofanya ziara ya kuzindua gati mpya wilaya ya Pangani Mkoani Tanga katikati ni Meneja wa Tanroad Mkoani Tanga,Mhandisi Alfred Ndumbaro
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa akizundua gati jipya la Bandari ya Pangani ambalo liligharimu zaidi ya bilioni 3 kulia ni Katibu  Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano wa mwisho kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA)Karim Mattaka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
 Kulia ni Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)Karim Mattaka wapili kutoka kulia wakati wa uzinduzi wa gati jipya wilayani Pangani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika akifuatilia mazungumzo hayo

Viongozi waliokaa meza mkuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Gati Jipya wilayani Pangani
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM),Jumaa Aweso wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Gati jipya wilayani Pangani
 Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani na mkoaani Tanga wakifuatilia uzinduzi wa Gati jipya

Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga wakifuatiliaa uzinduzi huo kutoka kulia ni PRO wa Mamlaka hiyo,Moni Jarufu kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Daudi Mayeji
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakifuatilia uzinduzi wa Gati hiyo


Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akisalimiana na wananchi wilayani Pangani mara baada ya kuzindua gati jipya

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffessa Makame Mbarawa akiwa na viongozi mbalimbali akisoma maelekezo yaliyoandikiwa kwenye jiwe la msingi mara baada ya kufanya  kuzindua gati jipya la Bandari wilayani Pangani kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Karim Mattaka kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella na PRO wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga,Moni Jarufu.

DC STAKI: APIGA MARUFUKU KUFANYA BIASHARA KWA KUJAZA RUMBESA

September 11, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akikagua magunia yaliyokutwa yakiwa yamejazwa Rumbesa
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akizungumzia unyonyaji wanaokumbana nao wananchi kutoka kwa wafanyabiashara wanaotaka magunia yaliyojazwa Rumbesa
Gari aina ya Fuso likiwa limekamatwa mara baada ya kubainika kuwa limebeba magunia ya vitunguu ambayo yamejazwa Rumbesa

MLIMBWENDE WA OZONA MISS LAKE ZONE 2016 APATIKANA

September 11, 2016
Jumamosi Septemba 10, 2016 kuamkia leo jumapili, kinyang'anyiro kikali cha kumsaka mlimbwende wa Kanda ya Ziwa, (OZONA MISS LAKE ZONE 2016), kimefanyika ambapo Mlimbwende, Eluminatha Dominick (pichani) kutoka mkoani Geita ameibuka mshindi miongoni mwa walimbwende 17 (baada ya mmoja kujitoa) waliokuwa wakiwania taji hilo.

Ushindi wa mlimbwende huyo ulionekana kuwafurahisha mamia ya watu waliohudhuria kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye Viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza, likiwa nimeandaliwa na kampuni ya Flora Talent Promotions chini ya Mkurugenzi wake, Flora Lauwo na kudhaminiwa na makampuni mbalimbali ikiwemo mdhamini mkuu, kampuni ya vipodozi ya OZONA pamoja na 102.5 Lake Fm Mwanza.

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Mhe.Jeseph Linzwa Kasheku Msukuma, alisema ni furaha kubwa mkoa wa Geita kunyakua taji la Ozona Miss Lake Zone 2016 na kwamba matarajio ni kujiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua taji la Miss Tanzania 2016 ikiwa ni sawa sawa na matarajio aliyoyaeleza mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016.
Na BMG
Mlimbwende, Eluminatha Dominick (pichani) kutoka mkoani Geita ameibuka mshindi wa Ozona Miss Lake Zone 2016, miongoni mwa walimbwende 17 waliokuwa wakiwania taji hilo.
Mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (katikati) kutoka mkoani Geita. Mshindi wa pili ni Mery Peter (Miss Mwanza 2016, kushoto) na Mshindi wa tatu ni Lucy Michael (Geita, kulia).
Mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (katikati) kutoka mkoani Geita. Mshindi wa pili ni Mery Peter (Miss Mwanza 2016, kushoto) na Mshindi wa tatu ni Lucy Michael (Geita, kulia).
Aliyekuwa akishikilia taji la Miss Lake Zone
Aliyekuwa Miss Lake Zone (kulia), akikabidhi taji la Miss Lake Zone mpya (kushoto)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaa ya Nyamagana, Mhe.Mary Tesha (kushoto) akimkabidhi mshindi wa Ozona Miss Lake Zone mfano wa ufunguo wa gari alilokabidhiwa kama zawadi. Mshindi wa Ozona Miss Lake Zone amewazadiwa gari lenye thamani ya shilingi Milioni 12 na kampuni ya Ozona.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, Mshindi wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick, Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ozona, Dr.Thobias Mkina, wakiwa katika picha ya pamoja.
Mshindi wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (kushoto) akiwa katika picha na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (kulia).
Washiriki walioingia nafasi tano bora ni, Eluminatha Dominick (wa pili kushoto kutoka Geita), Mery Peter (wa tatu kushoto kutoka Mwanza, Lucy Michael (wa kwanza kushoto kutoka Geita), Rose Masanja (wa pili kushoto kutoka Shinyanga) na Farida Hassan (wa kwanza kulia kutoka Mara).
Washiriki 17 wa Ozona Miss Lake Zone 2016
Ozona Miss Lake Zone akizungumza na Wanahabari baada ya kukabidhiwa gari
Mchekeshaji Eric Omond kutoka nchini Kenya akizungumza na Vesterjtz wa BMG baada ya show
Kushoto ni Christian Bella, akizungumza na Vesterjtz wa BMG baada ya kudondoka burudani kali
Katikati ni mbunge Joseph Msukuma akizungumza na BMG
Kulia ni mmoja wa wanakamati akihojiwa na BMG
George Binagi-GB Pazzo (ushoto) katika picha ya pamoja na Christian Bella (kulia) baada ya show
Mwanahabari Sadam Sadick (kulia) akishow love na Bella
Ozona Miss Lake Zone 2016 (kushoto) akiwa na Vesterjtz
Kijukuu kutoka RFA akiwa na Ozona Miss Lake Zone 2016
Mambo ya karanga fotooo na Ozona Miss Lake Zone 2016
Bonyeza HAPA Kwa Picha za Awali