Waziri Mpina aagiza mikataba ya wawekezaji wa vitalu vya ranchi ya taifa vyenye jumla ya hekta 68238 kuvunjwa mara moja.

November 30, 2017




Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) akiwa kwenye picha pamoja  na Viongozi wa Wilaya ya Mvomero na Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania  alipotembelea ranchi ya Dakawa jana



Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya  ya Mvomero, Muhamed Utaly  kulia  akitoa maelezo ya kuhusu eneo la hekta 20000 zilizoshindwa kuendelezwa na mwekezaji Mtibwa Sugar kwa lengo  la ufugaji. Kushoto ni Meneja Mkuu  wa Kampuni hiyo bwana Stan Rau hapo jana.


Meneja wa ranchi ya Mifugo  ya Mkata, Iddi Sadalah  akimuonyesha Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) banda  la Mbuzi  linalokadiriwa kuchukua mbuzi 800 kwa wakati mmoja katika ranchi ya Mkata jana.

Waziri wa  Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi za  Mifugo za Taifa, Profesa Philemoni Wambura kuvunja  mikataba ya wawekezaji wa vitalu vyenye jumla ya hekta 68,238 kwenye ranchi ya Mkata na Dakawa ndani ya mwezi  mmoja baada kushindwa kuviendeleza vitalu  vya ranchi na kushindwa kulipia kwa muda mrefu.
Mpina ameyasema hayo jana wakati alipotembelea katika ranchi ya Mkata na Dakawa kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika  katika ranchi hizo.
Amezitaja kampuni za wawekezaji  ambazo zilizomilikishwa  vitalu zinatakiwa kuvunja mkataba kwa kushindwa kuendeleza upande wa ranchi ya Mkata katika Wilaya ya Kilosa kuwa ni pamoja na Kadolo Farm Company Ltd  kitalu namba 418 yenye hekta 4005,Bagamoyo Farm kitalu namba 419 yenye hekta 3672.96, A to Z Animal Feeds Company Ltd kitalu namba 420 yenye hekta 3692.97 na Ereto Livestock Keepers kitalu namba 422 yenye hekta 4020.54.
Katika Wilaya ya Mvomero kampuni zilizoshindwa  kuendeleza vitalu ni pamoja na kampuni ya  Overland kitalu namba 415 yenye hekta19446.28, Katenda yenye hekta 2500, Mollel yenye  hekta 2500 na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa (Mtibwa Sugar) chenye hekta 20000 walizomilikishwa toka mwaka 1999 na kushindwa  kukiendeleza na kukilipia kwa miaka 18.
Mpina amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kumaliza  mara moja migogoro inayoendelea baina ya wakulima na wafugaji. Aidha Waziri Mpina amemtaka Diwani wa kata yaTwatwatwa, Katibu Tawala  wa Halimashauri ya Wilaya ya Kilosa pamoja na jamii ya wafugaji kumaliza migogoro inayowasumbua kwa muda mrefu kwa njia ya mazungumzo kabla ya kukimbilia muhimili wa mahakama bila sababu yoyote.
Mpina amesema kama  vyombo  vya Serikali vingetumika vizuri kuanzia ngazi ya kijiji kungepunguza  migogoro ya wakulima na wafugaji  katika wilaya  hiyo. Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Wilaya zinaongoza kwa  kuwa na migogoro mingi baina ya wakulima na wafugaji hapa nchini.
Kwa upande  mwingine, Waziri Mpina amezitaka Halimashauri zote nchini kutotunga sheria kandamizi  dhidi ya wafugaji. Akitolea mfano, wa sheria ndogo ya Halimashauri ya Mvomero ya kutoza faini ya shilingi 25, 000/=kwa kila mfugo kuingia  katika Wilaya hiyo bila kufuata taratibu  badala ya shilingi elfu kumi iliyoelekezwa katika Sheria ya Magonjwa ya  Wanyama namba 17 ya Mwaka 2003.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT)  Magembe Makoye amesema upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya wafugaji kutasaidia kuondoa migogoro  baina ya pande hizo na kuendelezwa kwa ranchi hizo za taifa  kutawasaidia wafugaji kupata shamba darasa litakalo wasaidia kufuga kwa kisasa  na kupata mbegu bora  za mifugo.

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) UTAENDELEA KUTOA FIDIA BORA – ERIC SHITINDI KATIBU MKUU – OWM

November 30, 2017
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba ya kufunga Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia kilele leo alasiri kwenye Kituo cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha Novemba 30, 2017.

NA K-VIS BLOG
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Eric Shitindi amewahakikishia wadau wote wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kuwa Mfuko utaendelea kutoa mafao bora kwa wafanyakazi wote sekta binafsi na umma ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Hayo ameyasema leo Novemba 30, 2017 wakati alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Aidha, Bw. Shitindi amesisitiza ya kuwa suala la elimu ni la msingi sana na limejitokeza ambalo mfuko ni lazima uhakikishe umewafikia wadau wote ili wafanyakazi wote nchini waweze kujua kwa ufasaha haki zao ikiwemo kupata fidia pale watakapokuwa wanastahili, pia waajiri wao waweze kufuata matakwa ya kisheria ikiwemo kujisajili na kuwasilisha michango kama kwa wakati. Pamoja na mambo mengine Bw. Shitindi ameahidi kusimamia zoezi la utoaji elimu kwa wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ambavyo ilielekezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama  wakati akifungua Mkutano huo tarehe 29 novemba 2017.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira wakati akitoa salamu aliishukuru Bodi ya Wadhamini pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko kwa kumualika kushiriki katika Mkutano huo, pia amesema Mkoa wake unavyo viwanda vingi na mashamba mengi ambavyo vinapelekea kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyakazi ambao watahitaji huduma ya Mfuko.
“Nitawapeni ushirikiano wa kutosha kuhakikisha waajiri wote wa Mkoa wa Kilimanjaro wanajisajili katika Mfuko ili  wafanyakazi wasijekukosa Mafao endapo wataumia, kuugua au kufariki” alisema Bi. Nghwira
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Emmanuel Humba, amewashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kwa kutoa michango mingi ambayo imelenga kuboresha huduma za Mfuko.
Katika Mkutano huo uliobeba kauli mbiu ya "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”, umeshuhudia Mfuko ukitoa tuzo kwa waajiri waliofanya vizuri katika utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba ya kufunga Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia kilele leo alasiri kwenye Kituo cha Kimataifa cha AICC, jijini Arusha Novemba 30, 2017.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba wakati wa kufungwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Laure Kunenge, akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
  
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba wakati wa kufungwa kwa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Bw. Bernard Konga, (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF) Bwana Daud Msangi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) kwenye Kituo Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha Novemba 30, 2017.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Emmanuel Humba na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bi. Radhmina Mbilinyi, wakiongoza kikao.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi. Anna Mghwira, akihutubia Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), uliofikia kilele leo Novemba 30, 2017 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha.

 Viongozi wa vyama vya wafanyaakzi wakiteta jambo.


RC MGHWIRA-TUMIENI FURSA ZA UTALII KUONDOKANA NA UMASIKINI,WATANZANIA WASHAURIWA

November 30, 2017
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
WATANZANIA wametakiwa kuzitumia fursa zilizopo kwenye sekta  ya utalii ili kukuza kuongeza vipato na uchumi badala ya kuendelea kulalamika hali ngumu ya maisha.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira amesema wakati wa hafla ya kuwasindikiza mabalozi 9 wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali ulimwenguni wakiwemo na maafisa wa Bodi ya Utalii na Wizara ya Mambo ya Nje wakati wakipanda mlima Kilimanjaro mkoani hapa jana.
“Hatuna sababu ya kulalamika uchumi, utalii pekee laiti  tungeutangaza vizuri tutafika mbali. Sisi Watanzania hatuoni uzuri tulionao ukienda nchi nyingine ndio utaona, nashauri watu wengi zaidi wapande mlima huu tuliopewa bure na Mungu ili kuona uzuri uliokuwepo,” alisema Bi. Mghwira.
Akizungumza na mabalozi hao aliwashauri wakati mwingine wakifanya shughuli kubwa kama hiyo waje nchini na raia katika mataifa wanayowakisha ili kuongeza tija ya kujitangaza kimataifa.
“Leo wanapanda mabalozi wachache, lakini kama wangekuja na raia mbalimbali kutoka nchi wanazotuwakilisha tungeona zaidi ya watu 80 wanapanda mlima huu na ujumbe ungesambaa zaidi, hivyo nashauri tutumie nafasi hizi kujitangaza vizuri,” alisema Bi. Mghwira.
Aidha, alishauri watu wanaoishia katikati ya safari bila kufika kileleni wapewe vyeti kulingana na maeneo waliyofika kwa sababu kufika tu katika mlima huo ni historia tosha si lazima kufika kileleni ndipo upewe cheti cha utambulisho.

WCF YAPATA HATI SAFI KATIKA UKAGUZI WA TAARIFA YA FEDHA ULIOFANYWA NA CAG

November 30, 2017
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akifafanua baadhi ya mambo wakati viongozi wa Mfuko walipokuwa wakiwasilisha taarifa za utendaji wake kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, jijini Arusha leo Novemba 30, 2017.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) umepata hati safi katika taarifa ya hesabu zake za fedha katika kipinmdi cha mwaka 2015-2016 ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.

Katika taarifa hiyo mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016 (mwaka wa kwanza tangu kuaza kufanya kazi zake), thamani ya Mfuko ilifikia shilingi bilioni 65.68 na mfanikio haya yaliweza kufikiwa kutokana na ubunifu na ushirikiano mkubwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Mfuko na Bodi ya Udhamini, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Mfuko huo, Bw.Bezil Kwala, aliwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wadau wa Mfuko huo unaoingia siku yake ya pili nay a mwisho kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC jijini Arusha, wakati akiwasilisha taarifa hiyo ya fedha leo Novemba 30, 2017.
Amesema Mfuko umekuwa ukiaandaa hesabu zake kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uaandaji wa hesabu za fedha na kwa mujibu wa sheria CAG ndiye mwenye mamlaka ya kufanya ukaguzi na Hati Safi ni uthibitisho wa taarifa ya fedha za Mfuko kuonyesha hali halisi na kutokuwa na dosari ya aina yoyote.
Amesema katika ukaguzi huo, CAG alishirikiana na kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC). Mwakilishi wa kutoka Ofisi ya CAG, Bw…….. amethibitishia wajumbe usahihi wa taarifa hiyo ya fedha ya WCF.
Mkutanmo huo ambao umeanza Novemba 29, 2017 na kubeba kauli mbiu isemayo, "Mafao ya Fidia: Haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza uchumi wa viwanda”, pia ulipokea taarifa ya mipango ya uwekezaji ambapo Bw. Kwala aliwaambia wajumbe kuwa, katika kipindi kati ya mwaka 2017/18 – 2021/22, Mfuko umepanga kuwekeza kwenye miradi mbalimbali itakayoleta faida kwa mujibu wa tathmimi za kitaalamu zitakazofanyika.
“Maeneo tuliyoyaanisha katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda ni pamoja na kiwanda cha Grape Processing Factory kwa ushirikiano kati ya  GEPF na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, kiwanda cha Madawa mkoani Simiyu kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Kiwanda cha Morogoro Canvas Mills kwa kushirikiana na mifuko ya WCF, NSSF, PSPF, GEPF, na LAPF”. Alifafanua.
Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa Mfuko kuwekeza, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba alisema, fedha zitokanazo na michango ya Wanachama ni kidogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya ulipaji Mafao ya fidia na kwa hali hiyo, ni muhimu Mfuko kuwekeza ili kupanua wigo wa kuongeza mapato na hivyo kuendelea kutoa Mafao ya Fidia bila ya shaka yoyote.
 Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa WCF wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, akizungumza
 Mkurugenzi wa Fedha WA WCF, Bw.Bezil Kwala, akiwasilisha ripoti ya fedha ya Mfuko kwa mwaka wa 2015-2016.
 Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Ofisi ya Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Johanes Joel Kisiri, akisikiliza uwasilishaji wa taarifa hiyo ya fedha.
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria cha WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu Sheria juu ya kuanzishwa kwa Mfuko na jinsi unavyofanya kazi zake. Pamoja na mambo mengine Bw. Siyovelwa aliwaambia wajumbe kuwa,   Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoazishwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura Na. 263 (Marejeo ya 2015) na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai 2015. Lengo la kuazishwa kwa Mfuko ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi waliopo katika sekta rasmi (Binafsi na Umma) Tanzania bara ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter, akiwasilisha taarifa ya uendeshaji ya Mfuko katika kipindi cha uahai wake, ambapo alisema Mfuko umekuwa ukifanya vizuri ikiwa ni pamoja na usajili wa wanachama " katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015-2017 jumla ya Waajiri 5,178 walisajiliwa ikiwa ni asilimia 71.92 ya lengo la kusajili waajiri 7,200