Waziri wa habari Napa Nnauye akutana na balozi wa Norway nchini Tanzania

Waziri wa habari Napa Nnauye akutana na balozi wa Norway nchini Tanzania

January 06, 2016

nape1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kushoto akiongea na Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad wakati wa Kikao kilichofanyika Ofisini kwa Waziri,katika kikao hicho Norway iliahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya utamaduni, Sanaa na Michezo. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).
nape2
Mmoja wa Maofisa kutoka Ubalozi wa Norway nchini Tanzania kushoto akiongea na  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati wa wa Kikao kilichofanyika Ofisini kwa Waziri,katika kikao hicho Norway iliahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya utamaduni, Sanaa na Michezo. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).
nape3
Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad kulia akiongea na  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kushoto wakati wa Kikao kilichofanyika Ofisini kwa Waziri,katika kikao hicho Norway iliahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya utamaduni, Sanaa na Michezo. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).
Balozi wa Uturuki nchini amtembelea waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.

Balozi wa Uturuki nchini amtembelea waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.

January 06, 2016


utr1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Uturuki Bi.Yasemin ERALP.Balozi uyo alimtembelea Waziri Nape kwa ajili ya kuzungumzia ushirikiano wa Tanzania na Uturuki katika masuala mbalimbali ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
utr2
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kushoto) akizungumza jambo na Balozi wa Uturuki nchini Bi.Yasemin ERALP leo jijini Dar es salaam.Waziri Nape alimsihi Balozi uyo kuwekeza katika Nyanja mbalimbali za Filamu,Michezo na kubadilishana ujuzi katika sekta ya  Habari na kumwahidi ushirikiano ulio bora kati ya nchi izo mbili.
TRA YAVUKA LENGO YAKUSANYA TRILIONI 1.4 KWA MWEZI

TRA YAVUKA LENGO YAKUSANYA TRILIONI 1.4 KWA MWEZI

January 06, 2016

trk1
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Forodha Jocktan Kyamuhanga na kulia  ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu Salum .
trk2
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi
Picha Na raymond Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Dar es Salaam
 
Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.
Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi  bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.
Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.
Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.
Kidata amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.
 
Katika hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni 11.8zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.
Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao.

KICHUPA KIPYA : KITA- I WANNA FLY (OFFICIAL MUSIC VIDEO)

January 06, 2016

Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail info@tonemg.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.tonemg.com

Fastjet kuzindua safari kati ya Tanzania na Kenya

January 06, 2016

Shirika la ndege la bei nafuu lapanua wigo wa safari zake barani Afrika na kufungua safari ya kimataifa ya moja kwa moja kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam na Kilimanjaro.



 Januari 2016 – fastjet imetangaza safari yake mpya ya kimataifa ya kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi, Kenya kuwa itaanza rasmi mnamo tarehe 11 Januari 2016.

Fastjet imepewa ruhusa na serikali ya Kenya kufanya safari zake nchini humo kufuatia makubaliano ya pamoja na mashirika yanayotoa huduma za usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya, kama ilivyopitishwa na serikali ya Tanzania.

Vilevile Fastjet imetangaza kuwa inatarajia kuzindua safari zake za anga kati ya Zanzibar na Nairobi na pia kati ya Dar es Salaam na Mombasa ambapo uzinduzi huo utafanyika mapema mwaka huu 2016.

Tiketi za kurudi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kwenda uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na uwanja wa ndege wa Kilimanjaro zitakuwa za kila siku mara tu baada ya uzinduzi huo na wasafiri watasafiri na ndege ya kisasa aina ya  Airbus A319 ambayo hubeba abiria 156.

Kwa mujibu wa Fastjet, safari nyingine za ndege zinatarajia kuzinduliwa kufuatia kuongezaka kwa maombi ya wateja wake na hii ni kwa sababu ya unafuu wa bei zake sambamba na huduma bora.

Tiketi za safari hii mpya zimeanza kuuzwa, na nauli za Nairobi/Dar es Salaam zitatozwa kwa $50 kwa safari moja, na Dar es Salaam/ Nairobi zitatozwa kwa $80 kwa safari moja.

Nauli hizi ni pamoja na kodi ya serikali  ambayo itachajiwa. Kwa mantiki hiyo, Fastjet inawaomba abiria na wateja wake kwa ujumla kufanya booking mapema iwezekanavyo ili kufaidika na bei nafuu ambayo hutozwa kuliko ndege zote ambazo husafirisha abiria kati ya nchi hizi mbili.

“Usafiri wa anga katika uwanda wa Afrika mashariki umekuwa na ushindani mkubwa  kutokana na safari nyingi bado hutoza nauli kubwa jambo linalosababisha abiria wengi kushindwa kumudu safari hizo” alisema John Corse, Meneja Mkuu wa fastjet kanda ya Tanzania.

“Wasafiri wengi wanaosafiri kati ya miji hii miwili mikubwa yenye idadi ya watu wasiopungua milioni 8 hapa Afrika Mashariki wamekuwa wakipatwa na vikazo mbalimbali vinavyowarudisha nyuma kutokana na bei ya safari za ndege kuwa kubwa ambayo tunaamini imewakatisha tamaa wasafiri wengi”, alisema Corse.

Matarajio ya Fastjet kufanya safari zake nchini Kenya zitaleta matumaini mara tu baada ya shirika hilo kuzindua safari hizo ambazo bei zake zimepokelewa na wateja wengi wanaosafiri na ndege zingine hasa pale ambapo nauli za Fastjet zimepungua kwa asilimia 40 hivi.

“Jambo kuu la msingi ni kwamba ushindani ni muhimu kwa wateja, kwa kuwa inampa mteja nafasi ya kuchangua unafuu wa nauli atakayoimudu, na hali hii hufanya watalii na wajasiriamali na wageni wanaotembelea nchi hizi mbili kuwa huru kuamua kwa raha kati ya Tanzania na Kenya” Corse alisema.

“Hali hii baadae italeta maendeleo ya pamoja kati ya nchi hizi mbili ambapo ukuwaji wa biashara zao za ndani na nje, vilevile pia utalii utaimarika kwa kiasi kikubwa na itakayo pelekea kukua kwa uchumi wa nchi hizi mbili”, aliongeza Corse.

Pia alisisitiza kuwa haileti maana halisi kwa mgeni ama mtalii kusafiri kwa zaidi ya masaa 12 kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi Kenya na kumfanya achoke kama ilivyo katika safari zingine. Na kwa kuwa sasa Fastjet imezindua safari mpya kama hii ya nchi na nchi, basi inategemea wasafiri wengi watafaidika na huduma za Fastjet.

Kwa kuunga mkono mategemeo haya hapo baadae, hii ni baada ya Fastjet kufanya utafiti wa kina na kubaini kuwa  abiria wake waliweza kumudu bei zao na kuzikubali moja kwa moja.

Safari za kila siku za fastjet kutoka Dar es Salaam zitaanza saa 3:50 asubuhi na kutua Nairobi-Kenya saa 5:10.

Safari za kurudi kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam zitaanza saa 8:10 na kutua saa 10 :05 kulingana na saa za Afrika mashariki.

Safari za kwenda Kilimanjaro kutoka Nairobi zitaanza saa 5:10 na kutua saa 6:40 na safari ya kurudi kutoka Kilimanjaro kwenda Nairobi zitaanza saa 7:10 na kutua saa 8: 40 kulingana na saa za Afrika mashariki.

Fastjet inatoza nauli iliyo nafuu kadri iwezekanavyo na kwa kutozingatia gharama za ushuru wa mizigo, vinywaji lakini vyote hivi vinapatikana kama msafiri atagharamia kwa hiari yake mwenyewe.

Ukatishaji tiketi mapema unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa kupitia tovuti ya festjet ambayo ni www.fastjet.com kupitia kwa mawakala wa shirika hili, ama mteja anaweza kupiga simu Namba 0784 108900. Malipo kwa ajili ya tiketi yanaweza kufanyika taslimu ama kwa kutumia benki ama kwa njia ya mitandao ya simu za mikononi.

Fastjet imepanua wigo wa ofisi zake na kwa sasa wanaendesha shughuli zao kimataifa kati ya Dar es Salaam ambako ndiyo ofisi kuu na kushirikiana na Johannesburg Afrika Kusini, Lusaka-Zambia, Entebbe - Uganda, Harare-Zimbabwe na Lilongwe nchini Malawi. fastjet pia hufanya safari zake kwenda Entebbe.

fastjet pia hufanya safari zake za ndani ya nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na pia kati ya Kilimanjaro na Mwanza. Safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar itaanza tarehe 11th Januari 2016.
photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"
DK. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA MUHIMBILI NA KUKAGUA MASHINE ZA CT-SCAN NA MRI, AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI

DK. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA MUHIMBILI NA KUKAGUA MASHINE ZA CT-SCAN NA MRI, AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI

January 06, 2016
IMG_0833
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Januari 4, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi.
Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na Kitengo cha dharura, Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU), wodi ya Mwaisela, duka la dawa la MSD na kukagua ufanyaji wa kazi wa mashine ya CT-Scan na MRI.
Akizungumzia ziara hiyo mara baada ya kutembelea Hospitalini hapo, Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa ili kuweza kuona hali ya utendaji wa kazi iliyopo katika hospitali hiyo ya taifa tangu ambapo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza na kutokuridhishwa na utendaji kazi wa hospitali hiyo hali iliyopelekea kuivunja bodi iliyokuwa ikisimamia hospitali.
Dk. Kingwangalla alisema amefurahishwa na utoaji wa huduma katika upimaji kwa kutumia mashine ya CT-Scan na MRI ambazo awali wakati wanaingia madarakani hazikuwa katika hali nzuri ya ufanyaji wa kazi na kuwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuifanya hospitali hiyo kuonekana yenye hadhi ya kuwa hospitali ya taifa.
Alisema limekuwa jambo ambalo linasikitisha kuona huduma zinazopatikana katika hospitali ya taifa zinashindwa na huduma zinazotolewa katika hospitali za watu binafsi na akilinganisha huduma za kulipia vitanda zinazotolewa Muhimbili kuwa hazina viwango vya juu ambavyo vinaweza kuwashawishi wananchi wenye uwezo kuacha kwenda hospitali binafsi na kwenda hospitalini hapo.
“Ni jambo la kushangaza hospitali za watu binafsi zinakuwa na watu wengi kuliko hapa na wakati sisi tuna madaktari bingwa zaidi ya 500 hapa Muhimbili lakini hizo hospitali zao hazina hata daktari mmoja bingwa lakini na huduma zinazopatikana katika madaraja ya juu zinatakiwa kuboreshwa,
“Kama tunaweza kuwa na huduma nzuri katika first class (daraja la kwanza) tunaweza kuwavuta wananchi wengi waje hapa na waache kwenda hospitali binafsi, wanatakiwa kutengwa madaraja ya juu ambayo huduma zake zinakuwa zimeboreshwa sio mtu anakuwa daraja la kwanza alafu bado anachangia choo na wengine au anaelala nae hapewi kitanda,” alisema Mhe. Kingwangalla.
Aidha Mhe. Dkt.Kingwangalla aliwatupia lawama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa jinsi wanavyopanga madaraja ya hospitali na kuilinganisha Muhimbili na hospitali zingine za watu binafsi kuwa jambo hilo siyo sahihi kwa kuiweka hospitali ya taifa sawa na hospitali za watu binafsi.
“NHIF wanaweka sehemu moja hospitali ya taifa na hospitali binafsi hili haliwezekani walinganishe huduma zilizopo hospitali ya taifa na zile zingine, nina mpango wa kuwatembelea hivi karibuni nitazungumza nao,” alisema Kingwangalla.
Aidha Mhe. Naibu Waziri aliupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuongeza vitanda katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo awali ilikuwa na vitanda sita hali ambayo ilikuwa ikiwashangaza wananchi wengi kutokana na kuwepo kwa vitanda zaidi ya 1350 katika hospitali hiyo na hivyo kuongezeka kwa vitanda katika wodi hiyo kutasaidia upatikanaji wa wa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.
Awali akitoa taarifa mbele ya Mhe. Dkt. Kingwangalla, Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo, Dkt. Flora Rwakatare alisema tangu kuanza kwa kutumika kwa mashine ya MRI mwishoni kwa mwezi Novemba mwaka jana jumla ya wagonjwa 560 wamefanyiwa vipimo katika mashine hiyo na ndani ya siku tatu amabazo wamefunga mashine mpya ya CT-Scan wameshawapima wagonjwa 26.
Alisema kufungwa kwa mashine ya CT-Scan kunaonekana kuwepo kwa matumaini mapya kwa watanzania kutokana na kasi ya ufanyaji kazi kwa mashine hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya Siemens ambayo inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde 6.
“Mashine ya CT-Scan ambayo imefungwa ina ubora mkubwa na ni ya pili kwa ukubwa Afrika Mashariki na kwasasa tunategemea kufanya kazi kwa ubora zaidi kutokana na ukubwa iliyonayo na inaweza kufanya kazi kwa kasi tofauti na ile iliyokuwa ikitumika awali,” alisema Dkt. Flora.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru alisema awali hawakuwa wakifanya visingizo ili wasifanye kazi lakini ni hali halisi iliyokuwepo kuwa mashine iliyokuwepo awali ilikuwa na matatizo lakini kufanikisha kufungwa kwa mashine mpya ambayo imeigharimu serikali Dola za Kimarekani Milioni 1.7 ambapo ni zaidi ya Milioni 400 za kitanzania kutawapa wao motisha ya kufanya kazi kwa kutumia kifaa cha kisasa na chenye kufanya kazi kwa haraka.
IMG_0836
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akitoka katika ofisi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.
IMG_0857
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto). Katikati ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
IMG_0861
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga (kulia) kuelekea kwenye chumba cha vipimo vya CT Scan pamoja na MRI alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.
IMG_0873
Baadhi ya watumishi katika kitengo cha vipimo cha MRI wakiandaa kitanda kwa ajili ya kumpokea mgonjwa wa kipimo cha MRI (hayupo pichani) kama walivyokutwa na mpiga picha wa wetu.
IMG_0876
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata taarifa ya idadi ya wagonjwa waliofanyiwa vipimo tangu mashine hiyo ipone kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare (kulia).
IMG_0886
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare akizungumza jambo na waandishi wa habari katika chumba cha vipimo vya MRI wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla, Januari 4, 2016.
IMG_0891
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya chumba cha vipimo vya MRI katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016.
IMG_0900
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata maelezo ya mashine mpya ya CT Scan iliyonunuliwa hivi karibu na Serikali kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
IMG_0903
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) akitoa maelezo ya uwezo mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibuni ambayo hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na muda wa siku tatu tangu kuanza kutumika hospitalini hapo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.
IMG_0910
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru baada ya kuona mabadiliko makubwa katika hospitali hiyo tangu alipokaimu kiti hicho wakati wa zaiara ya kushtukiza katika chumba kilichofungwa mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibu na inauwezo mkubwa wa kufanya kipimo kwa sekunde 6 na kutoa majibu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare.
IMG_0924
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa kwenye dirisha la malipo ya matibabu hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya, Januari 4, 2016.
IMG_0930
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla aliyetembelea kitengo chake, Januari 4, 2016. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
IMG_0932
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akiendelea kupewa maelezo ya namna wananchi wanavyohudumiwa katika kitengo hicho na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
IMG_0935
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinangaakitoa maelezo ya ubao maalum unaowaongoza madaktari na wagonjwa wanaohudumiwa katika kitengo hicho kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla.
IMG_0950
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akikagua wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru akimtembeza Mh. Naibu Waziri kwenye wodi hiyo.
IMG_0951

RAIA WAAMIRIFU WASAIDIA VIONGOZI MBALIMBALI WA VIJIJI KUCHUKUA HATUA NA KUJUA WAJIBU WAO WA KAZI.

January 06, 2016

Mraghbishi Zaituni Rashida toka wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga

Katika vijiji vya mikoa ya Geita, Simiyu, Shinyanga na Arusha, wananchi wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanajisimamia wao wenyewe na viongozi wao ili kufanikisha shughuli za maendeleo. Hata hivyo, si wote wanaofanya hivyo. Wale walio mstari wa mbele tunawaita waraghbishi na kile wanachofanya ni uraghbishi.Hawa ni wale wanaochukua hatua kustawisha au kulinda haki za binadamu na maslahi ya jamii kwa ujumla wake; kiuchumi, kisiasa au kijamii. Watu hawa wapo kwenye makundi tofauti tofauti wakiwamo wenyeviti wa vijiji, madiwani, wakulima, wafugaji, viongozi wa kidini, sungusungu, na walimu. Watu hawa wamechukua hatua mbalimbali ikiwamo kuwashawishi na kuwawezesha wanavijiji wenzao kuwa waraghbishi. Uraghbishi wao kwa wenzao unafanyika kwa njia mbalimbali; iwe kwa kukutana kwenye vijiwe vya kahawa, mashambani, kwenye visima vya kuchotea maji, shuleni ama popote pale wanapopata nafasi zikiwamo sehemu za ibada.

Harakati hizi zimewawezesha kujisimamia kwa kutambua wajibu na haki zao wanazostahili kuzidai kutoka, aidha kwa viongozi wao waliowachagua ama wale waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali kwa niaba yao. Mifano ipo mingi kuanzia kudai taarifa na mapato na matumizi, kudai huduma bora za kijamii kama upatikanaji wa dawa kwenye zahanati, huduma za maji na elimu n.k.Pamoja na mafanikio hayo, bado ni jukumu la uraghbishi si rahisi. Ni gumu na linalokatisha tamaa. Waraghbishi hawalipwi malipo yoyote zaidi ya kutumia zaidi walichonacho, kubwa zaidi likiwa ni muda wao. Ni shughuli ambayo wakati mwingine yaweza kukutia matatizoni.


Hakuna mtu anayependa kufuatiliwa mambo yake, hasa yanapokuwa na matatizo; yawe ya kujisababishia au ya bahati mbaya. Uraghbishi ni pamoja na kumulika mambo ambayo yanawahusu watu wengi. Akieleza changamoto ya kufanya uraghbishi, Melina Ndumuzi, toka wilayani Mbogwe mkoani Geita anasema: “Yataka moyo wa ujasiri sana kufanya uraghbishi vinginevyo unaweza ukaogopa kuthubutu. kwa sababu ya mtazamo wa jamii kuhusu watu waraghibishaji.” Kwa upande wake Epifania Mwenda toka kijiji cha Tanga, kata ya Katente wilayani Bukombe anasema: “Maisha ya uraghbishi ni ya kujitolea zaidi, si rahisi ni kazi sana, njia pekee ni kupenda kufanya unachofanya. Matokeo ya kile unachofanya ndio utaona mwisho wa siku wengine wanavutika kuraghbisha. Ila ni kazi nzito na kama una moyo mdogo huwezi kuifanya.”
 

Zaituni Rashid anayefanya uraghbishi katika kijiji cha Mhunze, kata ya Kishapu, mkoa wa Shinyanga anataja changamoto ya kukimbiwa na wale anao waraghbisha, “Huku kwa ujumla tunajitolea, inafika mahali wenzako wanakukimbia kila mmoja ana sababu zake, yaani shidaa!” Ugumu unakuja hasa pale unapokuwa ni mwajiriwa wa serikali na wakati huo huo unafanya uraghbishi. Kwa mfano mraghbishi ambaye ni mwalimu na kwa upande mmoja anawaunga mkono wale wanaopingana na mwenendo wa mkurugezi wa wilaya, ambaye ndiye mwajiri wake. “Ebu fikiria unamuona mwenzako anatafutwa na mwajiri wako, na wewe upo upande wa mraghbishi. Ni changamoto sana,” anaeleza mraghbishi William Msangi toka kijiji cha Buluhu kilichopo kata ya Ipoja wilayani Mbogwe. 


Akiunga mkono changamoto hiyo ya kimaslahi Zaituni Rashida anasema, “Sisi huku ni shida, mapato yanaliwa na wakuu wako. Unaanzaje kuwasonga? Na ukiwahoji viongozi wa chini wanakueleza kwenda kwa mkurugenzi wako,” Said Simoni toka kijiji cha Mheza, yeye kwa upande wake anaanza kwa kuuliza waraghbishi wenzake toka vijiji vya wilaya yao Bukombe kuhusu uragbishi wao katika vijiji vyao. Swali hili anawauliza baada ya kukutana na wenzake“Vipi vikao vya wazazi mashuleni vimefanyika nyie huko kwenu.?”Swali hili anauliza akilinganisha na changamoto zinazokabili uraghbishi katika eneo hilo na kamati za shule za vijijni. Kamati hizi zinaundwa na watu 9; Diwani (1), walimu (3) na wazazi (5). Mwenyekiti wa kijiji anakuwa kama mgeni mwalikwa.

 

Mraghbishi William Msangi toka kijiji cha Iponya, wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita

Akiongelea changamoto anazokumbana nazo hasa linapokuja suala la kusimamia kamati za shule, Simon anasema:“Yaani hadi mtu anafikia mahala anasema unataka uchukue cheo chake, kisa nimeuliza maswali yanahusu mapato na matumizi ya shule. Ni ngumu sana kwa sababu wabadhirifu hawapendi sana kufuatwafuatwa. Hivyo, muda mwingine unajikuta upo kwenye mtafaruku usioutarajia.”Hofu hii ya wananchi kuuliza maswali kwa viongozi waliowachagua ni chagamoto. Simon anaongeza kwa kusema: “Elimu inahitajika mno ili watu waweze kujiamini kwani kuna watu wanawasujudia madiwani kama miungu watu wakati wao ndio waliomweka madarakani. Hali hii ya kuwaogopa viongozi ni tatizo kubwa.”

Na hapo ndipo wanapokiri kuna umuhimu wa kuwa na mbinu mbadala ya kufanya uraghbishi, vinginevyo waraghbishi na wale raia waamilifu ambao ni waajiriwa na muda huo huo ni wananchi hujikuta katika mazingira hatarishi. Na hawa viongozi wa chini wanahitaji kupatiwa mbinu za uraghbishi. Kwa nini? Kwa sababu kuna baadhi yao wana hofu na woga kwa wakubwa zao.


Hatua mbalimbali wanazochukua zinatokana na uamilifu wao; yaani uwezo wa kujitambua na kusimamia kile ambacho wanaamini sahihi. Kwa kufanya hivyo wanakuwa si tu waraghbishi bali pia raia waamilifu. Pamoja na changamoto hizo, na nyingine nyingi kama za kutishiwa kufungwa au kudhuriwa, bado raia hawa waaminifu wameendelea na uamilifu wao. Akifafanua nini hasa kinachowasukuma kufanya uraghbishi, Gabriel Jonathan toka kijiji cha Lugunga anasema: “Watu hawa ni wa muhimu na mafanikio ya uraghbishi ni kuungwa mkono na watu wengi. Hapa changamoto lazima iwe inahusisha watu wengi, hiyo ndio tunaiita changamoto.” Ili mtu aweze kuchukua hatua ni lazima awe na sababu inayomgusa.  Mraghbishi unapoibua jambo ni lazima uwe umelifanyia tathmini ya kutosha na kujiridhisha kwamba unachowaambia watu ni sahihi. 
 

Watu ni changamoto ambayo inaendana na muda. Waraghbishi wengi ni watu ambao wana shughuli zao. Na shughuli hizi ndizo zile zinazowaingizia kipato wanachotumia na familia zao. Akifafanua changamoto hii baba wa watoto wanne na mke, Gabriel Jonathan anasema:

“Ili waweze kuchukua hatua ama kufanya kitu fulani, wanahitaji uwepo wako. Wasipokuona kwenye vikao hivyo huwa inawakatisha tamaa, hivyo inakulazimu kufunga biashara na kuja kujumuika na watu. Hii ni changamoto kubwa.”Unahitajika ubunifu mpya wa kuwawezesha waraghbishi kukabiliana na changamoto hizi. Njia mojawapo ni kutengeneza urafiki na wale ambao tunahitaji kuwabadilisha. Njia hii ni muhimu katika kushawishi wale ambao kwa njia moja ama nyingine wanaoneka kwenda kinyume na maadili ya uongozi. Kwa kufanya hivi inasaidia kupunguza uhasama na kuonana kama maadui.  Akisisitiza umuhimu wa dhana ya nguvu, Richard Mabala anasema waraghbishi wakumbuke daima kwamba nguvu yao hutokana na nguvu ya watu na si mapambano binafsi. Na hii ndio siri ya mafanikio ya waraghbishi ama raia waamilifu. Kwa kawaida wajumbe wengi wa halmashauri ya serikali ya kijiji hutegemea posho za vikao kama njia mojawapo wa kujikimu. Hawa hawana mshahara na ni watu kutoka kwenye jamii ile ile ya wale waliowachagua. Ni mara chache sana wanaunga mkono hoja ya kutolipwa kwenye vikao.


Kutokana na uraghbishi, wajumbe wa kijiji cha Buluhe kilichopo kata ya Iponya walikubaliana kutopokea fedha za posho na badala yake zitumike katika shughuli nyingine. Akielezea jinsi alivyowabadilisha wajumbe wa halmashauri ya kijiji kuwa raia waamilifu, katika maana ya kujitambua, William Msangi toka anasema: “Baada ya kuwaraghbisha wajumbe wa halmashauri ya serikali ya kijiji kuhusu dhamana yao kwa wananchi kwa kuacha kujitazama wao wenyewe zaidi, walikubali kutopokea posho. Kwa siku hiyo tuliweza kuokoa kiasi cha shilingi laki tatu na elfu sabini na tano,” Baada ya fedha hizo kukusanywa zilikabidhiwa kwa mwenyekiti wa kamati ya mipango na fedha ikiwa kama ni sehemu ya uraghbishi kwani hapo mwanzo fedha alikuwa anakaa nazo mtendaji wa kijiji, jambo ambalo halikuwa sahihi. Kwa hiyo ili uamilifu na uraghbishi uwe wa kweli inabidi liwe ni suala la watu na si la mtu mmoja mmoja ili nguvu za pamoja zifanye kazi. Na hapo ndipo ujenzi wa taifa unapoonekana moja kwa moja kwa sababu ni chetu si sote. Pamoja na changamoto zote bado raia hawa waamilifu wamendelea na harakati za ujenzi wa taifa pasipo kukata tamaa na badala yake wanaendelea kuhamasishana wao kwa wao.  
Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail info@tonemg.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.tonemg.com
WATUMISHI WA KADA ZA AFYA NCHINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA MAADILI NA VIAPO VYA TAALUMA ZAO

WATUMISHI WA KADA ZA AFYA NCHINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA MAADILI NA VIAPO VYA TAALUMA ZAO

January 06, 2016
IMG-20160105-WA0026
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi hospitali teule ya rufaa ya mkoa wa Geita.(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA).
IMG-20160105-WA0030
Wauguzi wa wodi ya akinamama katika hospitali teule ya mkoa wa Geita.
IMG-20160105-WA0029
Tabibu wa kituo cha afya Nyankumbu, Abdallah Kiroboto akimsikiliza Waziri Ummy mara alipoingia kwenye chumba cha kutolea huduma, pembeni ni mama aliyefika kituoni hapo na watoto wake kupata matibabu.
IMG-20160105-WA0031
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwlimu akisalimiana na wagonjwa kwenye kituo cha afya Nyankumbu mkoani Geita alipotembelea kituo hicho.
IMG-20160105-WA0028
Wagonjwa waliofika hospitalini hapo wakisubiri huduma kwenye hospitali hiyo.
IMG-20160105-WA0027
Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea hospitali hiyo.

WANASIASA WAKWAMISHA SHUGHULI ZA URAGHABISHI WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI

January 06, 2016
Mchungaji wa kanisa la Umoja wa Makanisa ya Ubatizo  Lucas Machibya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu baadhi ya shughuli za uraghabishi katika kijiji cha Pandagichiza



Na Krantz Mwantepele ,Shinyanga


Si mara nyingi viongozi wa kidini hujihusisha moja kwa moja na harakati za kisiasa ila wamekuwa mstari wa mbele kukemea matendo yanayofanywa na wanasiasa. Hawafanyi hivyo kwa bahati mbaya ila kutokana na nafasi yao katika jamii, hususani kuwaongoza waumini wao kwenda mbinguni.

Hata hivyo, hii haimaanishi hakuna kabisa viongozi wa dini waioamua kujiingiza katika harakati za siasa ili kuleta maendeleo ya watu kwa haraka na ufanisi. Mchungaji Lucas Machibya ni mmoja kati ya viongozi wachache wa dini wanaoingia katika siasa.


Huyu ni mchungaji wa kanisa la Umoja wa Makanisa ya Ubatizo lililopo katika kijiji cha Pandagichiza chenye wakazi wanaokadiriwa 2,481, idadi kubwa ikiwa ni ya wanawake wanaokadiriwa kufikia 1,476. Hiki ni moja ya vijiji vilivyopo wilaya ya Shinyanga Vijijini, jimbo la Solwa.


Machibya ni mmoja wa wachungaji waraghbishi toka mkoa wa Shinyanga ambao uraghbishi wao umepelekea wananchi kumchagua kuwa mwenyekiti wa kijiji. Kujibainisha kwake kama mtu mwenye uwezo wa kusimamia anachokiamini na kushawishi wananchi kutambua majukumu na haki zao na jinsi ya kuzidai vimekuwa nguzo yake kubwa ya kukubalika.
Kama walivyo wananchi wengi wa kijiji chake, yeye ni mkulima mdogo ambaye pia ni mwanachama wa Mtandao wa Wakulima Wadogo Tanzania (MVIWATA). Kupitia mwaliko wa mkulima mwenzake, Elizabeth Edward, Machibya amefanikiwa kupata maarifa ya uraghbishi na jinsi ya kufanya uraghbishi; uwezo wa kuwashawishi na kuwahusisha ama kuwachokoza watu ili waweze kujitambua na kutojiona wao ni wa jamii ya chini.
Sifa iliyomfanya aalikwe kwenye mafunzo ya uraghbishi ni uwezo wake wa kuhoji mambo mbalimbali pasipo kukata tamaa kama anavyosema mwenyewe:
“Mimi ni mtu wa kuhoji vitu na si mtu wa kuridhika ama kukaa kimya n’napoona kuna jambo sijalielewa. Kwa kweli yale mafunzo yalinifanya kujiona mtu tofauti sana nikijilinganisha na nilivyokuwa awali. Nilijihisi tayari nimekuwa mtaalamu wa masuala ya uwajibikaji na utawala bora.”
Kwa kuwa wao ni wakulima, walianza uraghbishi wao kwa kutaka kujua nini kinaendelea kuhusu bei ya pamba. mchungaji Machibya anaeleza ilivyokuwa:
“Kule tulifundishwa jinsi ya kuuliza maswali. Na cha kwanza tulichotaka kujua ni kwa nini bei ya zao letu la pamba imeshuka sana. Hili tuliliuliza sisi sote, mimi na waraghbishi wengine.”
Hawakuishia hapo tu bali wakaanza pia kufuatilia mapato na matumizi ya fedha za kijiji toka kwa viongozi wao. Walifanya hivyo kwa kuwatembelea ofisini na kuomba kupatiwa taarifa hizo na pia walitaka kufanyika mikutano ya hadhara. Baada ya harakati hizo kushika kasi, iliwabidi waongeze watu wengine zaidi kwa kuwatembelea majumbani kwao na kuwaraghbisha.


“Mchungaji aliomba kunitembelea nyumbani na alipofika alinipatia elimu. Kimsingi, alitaka nijitambue kwa kujua wajibu na haki zangu. Alinitaka nisiogope kuuliza maswali kwenye mikutano kwa kuwa tuna uhuru wa kufanya hivyo. Nikajua kuwa nina wajibu kuuliza na kujua mapato ya fedha za kijiji na na matumizi yake kuwa hiyo ni haki yangu,” anaeleza Bw. Daudi Denis toka kijiji cha Pandagichiza.


Baadhi ya waraghabishi wa kijiji cha Pandagichiza wakiwa na waandishi wa habari za mtandaoni katika moja ya jengo la jiko  la shule ya msingi Pandagichiza ambalo limetoakana na juhudi zao za uraghabishi 



Kufanikisha haya yote kumewajengea uaminifu mkubwa sana waraghbishi na baadhi yao wamekuwa wakishirikishwa katika vikao muhimu vya maendeleo na serikali yao ya kijiji. Baadhi yao wametokea kuaminika zaidi na jamii kiasi cha kuombwa wagombee nyadhifa mbalimbali za uongozi wa serikali na ndani ya vyama vya siasa kama ilivyokuwa kwa mchungaji Machibya.


Hivyo basi, waraghbishi wengi wanaojihusisha na siasa wamejikuta wakinasa katika mtego huu wa migogoro ya kimaslahi kati ya shughuli zao za uraghbishi na zile za kisiasa kwa kuchukiwa na baadhi ya watu wanaotofautiana kimlengo wa kisiasa na kuonekana wasaliti na watu wasiokuwa na misimamo.

Wakati mwingine wanachukiwa ikidhaniwa kuhoji kwao mara kwa mara ni njia ya kujitafutia mtaji wa kisiasa na si kuwatumikia wananchi na kuibua maovu kwa maslahi ya jamii nzima na kwamba uraghbishi unawanufaisha wao binafsi na vyama vyao tu.
Uraghbishi ulimuingiza mchungaji Machibya kwenye mgogoro mkubwa na walinzi wa jadi, Sungusungu. Katika maeneo mengi ya Kanda ya Ziwa walinzi hawa wamekuwa na nguvu kubwa na wakati mwingine wanaweza kutoa adhabu kali kwa yeyote anayebainika kutenda kosa.
Tofauti hiyo na Sungusungu ilisababisha yeye na waraghbishi wengine sita kukamatwa na kutozwa faini ya shilingi laki tano na elfu sitini (560,000/=) kwa mpigo kwa kisingizio cha kuvuruga amani katika kijiji hicho. Hii ni kwa sababu tu walikuwa wanauliza maswali kuhusu mapato yanayotokana na faini na michango mingine toka kwa wanakijiji.
Vitisho na maonyo ya uongozi viliwapunguza kasi baadhi ya waraghbishi na kuingiwa hofu kiwa wangefikishwa pabaya zaidi ya hapo. Ila mchungaji Machibya hakuishia hapo bali aliendelea na shughuli hizo kama kawaida. Baadaye aliteuliwa kuwa katibu wa mtandao wa waraghbishi na huko ndiko alikojizolea uaminifu na umaarufu zaidi baada ya kuanza kujihusisha na kuhoji mambo makubwa ya kiutawala na utendaji kijijini hapo.
Hiyo ilimwongezea hamasa ya kuendelea kuwatumikia watu kwa kuongeza juhudi katika shughuli za uraghbishaji na kufikia hatua ya kuombwa na wananchi kugombea wadhifa kichama (siasa) na uongozi katika serikali ya kijiji.


Na mwaka 2014 wakati wa mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ukiendele, ndipo yeye alijikita kwa dhati kuomba nafasi ya kugombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanikiwa kuteuliwa kugombea. Akielezea ilivyokuwa, mchungaji Machibya anasema:
“Wapinzani wangu walipojua kwamba mimi ndio nimepitishwa waliamua kujitoa katika vyama vyao na kuniunga mkono. Hii kwa sababu hawakuona sababu ya kupingana nami kwa kuwa wanafahamu uwezo na umakini wangu kiutendaji na kiuwajibikaji.”


Matokeo ya harakati hizo ni kwamba Mchungaji Machibya alichaguliwa kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa kijiji na baadaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa wilaya nzima. Sanjari na nafasi mwenyekiti wa kijiji, aliendelea pia kushika nyadhifa nyingine ikiwamo kuwa mraghbishi kiongozi na mchungaji.
Hizi ni nyadhifa nyingi zinazoambatana na majukumu mengi kwa mchungaji Machibya hivyo kujikuta kwenye mazingira magumu sana ya kutumikia nyadhifa zote. Lakini pia alipata upinzani mkali sana kutoka kwa viongozi wengine na hata wakati mwingine kushindwa kusimamia kwa pamoja majukumu yote.

Huku ni mraghbishi na huku ni mwenyekiti wa kijiji. Hii haikuwa changamoto ndogo kwake. Akifafanua hilo, mchungaji Machibya anasema:
“Kwa sababu nilikuwa kiongozi wa waragbishi ilikuwa ni kama nayajua maswali kabla ya mtihani na wenzangu walikuwa wanashindwa kuhoji vizuri kwa kuwa mie ni kiongozi wao. Ndipo nikaamua kujitoa uongozi na kuwa mraghbishi wa kawaida, lakini sikuishia hapo nikajivua na majukumu ya uchungaji wa kanisa japo ni shughuli niliyoipenda sana na kuwa mzee wa kanisa kawaida.”


Kwa haraka haraka, unaweza kusema shughuli ya kuhoji mwenzio inafanana na kuhojiwa wewe binafsi. Mwanzoni alipata ugumu kidogo kwa sababu kila mwananchi alikuwa anategemea mabadiliko ya haraka wakati vitu vingine vilikuwa kimfumo zaidi. Hiyo ilimfanya achelewe kutoa majibu ya haraka. Na ili asiangukie kwenye dimbwi la lawama, alihakikisha anakuwa muwazi kwa wananchi na viongozi wake wa karibu katika kila jambo.
Kuna mbinu kadhaa alizotumia ikiwa ni pamoja na kuteua viongozi wa halmashauli ya kijiji wanaoendana na falsafa yake ya uwazi na uwajibikaji na pia aliendelea kuwatumia waragbishi wenzake katika kuibua mambo pale alipohisi yanakwama. Mchungaji Machibya anafahamu kwamba yeye kama kiongozi ana wajibu wa kuwa na uelewa wa mambo mbalimbali ikiwemo sheria na sera za nchi. Kwa kuelewa hilo, alipoanza kutafuta fursa za mafunzo ya uongozi na kukutana na mashirika mbalimbali yaliomwezesha kupata elimu.
Hakuishia hapo bali aliendelea kujenga mizizi ya waraghbishi wengi zaidi na mpaka sasa amefanikiwa kuwajengea uwezo wenyeviti wenzake 40 kati ya 126 wa wilaya nzima, na bado anaendelea kutafuta maarifa mengine ili awape wenzake.

Kwa nafasi yake, anatafuta wadau na mashirika yenye ujuzi huo ili awezeshe wenyeviti wote kupata mafunzo kwani wengi wao wanatawala wananchi kimazoea tu. Hawana ufahamu wa namna nzuri ya kutekeleza majukumu yao.
Kwa misingi hiyo, mchungaji Machibya ameamua kutumia uraghbishi kama nyenzo ya kumuongezea ufanisi katika majukumu yake na si kutengeneza uadui na waragbishi kama ilivyo kwa viongozi wengi wa vyama na serikali. Kwa mfano huu, tunapata picha halisi ni kwa namna gani uragbishi ukichukuliwa kwa mtazamo chanya unakuwa nyenzo muhimu ya kuongeza chachu ya utawala bora katika serikali zetu za mitaa, kijiji na taifa kwa ujumla. Na kwa sasa, anapambana na mambo makuu matano ikiwa ni pamoja na mradi wa maji utakaomwezesha kukusanya kiasi cha shilingi 500,000.

Pamoja na mapato mengine yanayokusanywa na Sungusungu pamoja na kuhamasisha kusomeshwaji kwa wingi kwa watoto wa kike. Na tayari hatua za makusudi za kuhakikisha kwamba malengo ya kuongeza mapato na hivyo kulipia watoto wa kike kuhudhuria shuleni zimeshachukuliwa.

Hii ikiwa ni pamoja kupunguza adhabu kali za viboko, kuunda upya uongozi wa Sungusungu. Kwa upande wa mapato, wameweka mikakati ya wazi ya kuhakikisha mapato yanayopatikana yanasomwa mbele ya wananchi. Kwa upande wa shule, kila mzazi na jamii nzima imeandaliwa mikakati ya makusudi kuwawajibisha wale wote wanaoshindwa kuwapeleka watoto wa kike. Waraghbishi wamekuwa chachu kubwa katika uvumbuaji wa taarifa pamoja na uelimishaji pia.

Jambo la kwanza kwa kiongozi yeyote anayetaka mafanikio katika uongozi wake ni kutanguliza maslahi ya wananchi kwanza kabla ya maslahi binafsi au ya chama chake. Kinyume na hivyo anaweza kutia doa hata huo uraghbishi wake. Utu wa mtu hupimwa kwa matendo yake na hata mtazamo wa watu anaowaongoza.
Viongozi wengi wanatumia uraghbishi kama nyenzo ya kujijengea umaarufu wakati wenyewe ni kama hulka ama tabia ya mtu kupenda haki na mambo yakiwa yanasonga. Kwa hiyo unaweza kukuta waraghbishi wengi sana kama matendo yako yatalenga kukomboa watu na si maslahi binafsi.

Jambo lingine ambalo alisisitiza ni kwamba hawa viongozi wawe na utamaduni wa kutafuta maarifa na si kusubiri fursa za kuletewa tu na wahisani. Kiongozi bora ni lazima aendane na mabadiliko ya kila siku na si kuongoza watu kwa mazoea. Binadamu wanabadilika kila siku, hivyo kuna umuhimu wa kuonesha tofauti kati ya kiongozi mraghbishi na wa kawaida. Hiyo itaibua mwamko mkubwa wa viongozi wengi kuwa waraghbishi.
Kiongozi asiyejua sheria na sera za nchi ni sawa na kipofu. Siri ya elimu na ufahamu ipo kwenye maandishi, mafunzoni na kwenye semina elekezi kwani bila kufanya hivyo utauchukia uraghbishi.
photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"
WATANZANIA MSIKUBALI KUTOZWA RUSHWA KWA AJILI YA DAMU, TOA TAARIFA KWA NESI, DAKTARI ATAKAYETOZA DAMU!- DK. KIGANGWALLA

WATANZANIA MSIKUBALI KUTOZWA RUSHWA KWA AJILI YA DAMU, TOA TAARIFA KWA NESI, DAKTARI ATAKAYETOZA DAMU!- DK. KIGANGWALLA

January 06, 2016
IMG_0681
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Modewjiblog, Team.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo watamchukulia hatua kali.
Kauli hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dares Salaam.
Dk. Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.
“Kwa watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!. Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.
Mtu atakayekutoza damu, wewe tuambie, huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja, hatuwezi kuendekeza watu wa namna hii... Serikali inaingia gharama kubwa kukusanya damu kwa watu, Kuna watu wanajitolea damu zao bure. Leo wewe nesi ama mganga ukauze damu, hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa hiyo natoa rai kwa watanzaia hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali kuuziwa damu hata kidogo.” Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.
Awali katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kazi wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha Halmshauri katika ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti viwango vya damu ya matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo kutoa maelekezo ya kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu salama ambapo kwa wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.
“Motisha sio soda na maji kwa wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa kwamba damu yake imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa anaumwa ugonjwa fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama soda ama maji yanayotolewa anapochangia damu..
Lakini kama imeshajitokeza mtu kuwa na tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa kumpoteza, maana yake kuna uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia damu, mtu huyu ni lazima kuwe na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa kumtakia salamu, taarifa na anakuwa kwenye database yenu.
“Mnatakiwa muwe na mfumo wa kumpa taarifa pindi damu yake imetumika, ikiwemo kumueleza kuwa damu yako imemsaidia Mama mjamzito aliyejifungua na kutokwa damu nyingi, na mtu huyo akipata taarifa hiyo ni motisha tosha hivyo ni lazima muwe na huo mfumo kutoa motisha zaidi.
IMG_0689
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla na msafara wake wakishuka ngazi kuelekea kukagua idara mbalimbali katika ofisi hizo, Januari 4, 2016
Awali akielezwa na Meneja wa kanda ya Mashariki katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo, Kwa hatua hiyo, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmshauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti za kutosha ilikusapoti mpango wa damu salama.
Katika hilo Dk. Kigwangalla ameapa kuwashughulikia wale wote watakaozembea na kuwachukulia hatua kali Ma DMO, Wakurugenzi na kushtakiwa kwa mamlaka zilizopo na kufukuzwa kazi.
“Naziagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinatenga bajeti za kusapoti mpango wa ukusanyaji damu salama. Na Halmashauri zitakazoshindwa, DMO na Mkurugenzi wake tutahakikisha tunawashtaki kwa mamlaka zilizowateua ili uteuzi wao ukome mara moja. Maana hatuwezi kuacha akinamama wajawazito wapoteze damu wakati wa kujifungua, watu wanaopata ajali wapoteze maisha kwa sababu ya watu hawataki kutimiza wajibu wao.
Hilo haliwezi kukubalika, Mfumo wa hali ya damu kwa Tanzania kwa sasa unatisha. Kwa sasa nchi inakiwango cha chini mno, tokea wafadhili wajiondoe katika hili. Ni lazima tuwe makini sana maana leo mzima kesho umepata ajali, umepasuka mfupa wa kwenye paja damu nyingi zimemwagika unahitaji damu!!
Kwa upande wa watu wote wanaopata damu salama nchini, huduma hiyo wanazipata bure kwani damu hizo ni za Serikali, Hata hivyo mifuko na vitu vinavyotumika kuhifadhia damu hiyo vina gharama kubwa.
“Damu inatolewa bure na serikali. Mtambue kuwa, vifaa vya kutunzia damu hii ni gharama kubwa. Hivyo mifuko mashirika ya Bima, na mashirika mengine kuanzia leo kutazama namna ya kulipa gharama za vifaa vya utunziaji damu hizo. Damu ni bure, lakini mfuko ule wa kutunzia ile damu ni gharama kubwa sana na hata vifaa vya kupimia damu ile nayo ni gharama kubwa hivyo walipie kwa kila damu watakayochukua.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
IMG_0703
Meneja wa kanda ya Mashariki Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa (mwenye miwani) akielezea utaratibu wa ukusanyaji wa damu unavyofanyika kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016 jijini Dar.
IMG_0690
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla (aliyeipa mgongo kamera) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma ya namna wanavyopokea watu wanaofikia kuchangia damu kwa hiari na kuhifadhiwa kwenye benki hiyo yaTaifa ya Damu Salama, alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016 katika ofisi hizo.
IMG_0725
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akitoa mkono wa pongezi kwa wananchi walioonyesha uzalendo kwa kufika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Januari 4, 2016 na kuchangia damu kwa hiari yao ambapo mmoja kati yao alisema hii ni mara yake ya nne na ni utararibu aliojiwekea.
IMG_0729
IMG_0743
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisalimiana na kumpongeza mmoja wa wananchi (jina lake halikuweza kupatikana) aliyefika kuchangia damu kwa hiari, Januari 4, 2016 katika makao makuu ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
IMG_0764
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi hizo, Januari 4, 2015 jijini Dar es Salaam.
IMG_0770
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.
IMG_0760
Mmoja wa watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama (ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.
IMG_0774
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisaini vitabu vya wageni nje ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Januari 4, 2016 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo.
IMG_0826
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kuzungikia vitengo mbalimbali katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama jijini Dar es Salaam.