STEVE NYERERE AMTANGAZIA NEEMA MZEE MAJUTO KWA MATIBABU NCHINI INDIA

April 26, 2018

Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ akimsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ akiongea machache mara baada ya kumtembelea Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam.

Mzee Majuto akitoa shukrani zake mara baada ya kutembelewa na kuonyeshwa mwanga wa matibabu zaidi nchini India.
Msanii Aunty Ezekiel akimsalimia Mzee Majuto.

Kicheko kidogo…
Mtoto wa Mzee Majuto, Hamza akitoa shukrani kwa wasanii waliofika kumsalimia baba yake.


Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ akiteta jambo na Mzee Majuto.



Na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG.

Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto anatarajia kupelekwa nchini India kwa matibabu kutokana na tatizo linalomkabili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutoka kumsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini, Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona mzee Majuto amekuwa akihangaika mara kwa mara kutafuta matibabu.

“Tumeona mzee wetu anahangaika na matibabu ya mara kwa mara ambayo hayakamiliki sasa tumekuja na wazo la kumpeleka nchini India ili akatibiwe tatizo lake liishe na huu ndiyo wakati mwafaka wa watu tujitoe si mpaka mtu ashindwe kuongea tuanze michango,” alisema nyerere.

“Jamani ifike wakati tujitoe kumsaidia mtu akiwa yupo hai na tusisubiri afariki ndiyo tuanze kuchanga, wakati ni sasa akiwa anaumwa tunamchangia anapatiwa matibabu na anaendelea na maisha,” amesema Nyerere.

Tunamshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuunga mkono kusaidia mwenzetu, pia Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taiga (NEC) Salim Asas ambaye yeye amesema atatusaidia kwa hali na mali na ameanza kutupa tiketi 2 za ndege.

Tunataka mwenzetu akatibiwe maradhi yake yaishe aendelee na majukumu yake ya kujenga nchi na familia yake kwa ujumla.

Nyerere amewaomba wadau mbali mbali akiwemo Azam, DSTV na wengine wote wenye mapenzi mema kumsaidia mzee Majuto ili apone na aendelee na shughuli.

Kwa Upande wa Mzee Majuto amewashukuru watu wote ambao wamekuwa wakijitokeza kumsalimia na waendelee kumuombea ili apone.

“Sina cha kuwapa zaidi ni kuwaombea muendelee na moyo mlionao, mimi sina pingamizi kwenda kutibiwa nchini India, nipo tayari kamilisheni mipango yote mje kunichukua,” amesema.

Ujumbe wa Steve Nyerere uliambatana na msanii mwenzake Aunty Ezekiel pia wakiwemo na waandishi wa habari wa mitandao ya jamii.

AfDB YARIIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA NISHATI YA UMEME INAYOFADHILIWA NA BENKI HIYO NCHINI

April 26, 2018

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha zuzu mkoani humo .
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdori Mpango ( Mb) akimuongoza Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha zuzu mkoani humo.
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akisalimiana na Mhandisi Peter Kigadi mara baada ya kuwasili mjini Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu mkoani humo
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akisisisitiza jinsi Benki hiyo inavyoridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa nishati hali itakayochochea maendeleo.
Mhandisi Mkuu wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Mkoani Dodoma Bw. Joseph Mongi akitoa maelezo kuhusu namna kituo hicho kinavyofanya kazi wakati wa ziara ya Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina katika kituo hicho.
Sehemu ya Miundombinu ya kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichoko mkoani Dodoma kama inavyoonekana.
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, wakimuongoza Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kukagua miundombinu ya Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, mjini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango)

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma


Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, amesema Benki hiyo imeridhishwa na utekelzaji wa miradi ya nishati hapa nchini kwani inachochea mageuzi katika maisha ya wananchi .

Akizungumza mara baada ya kuwasili Mkoani Dodoma na kutembelea kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, mkoani Dodoma, amesema kuwa benki hiyo inatambua na kupongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.

Dkt. Adesina ameeleza kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kupoza umeme ni mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa wananchi wake na umelenga pia kupunguza tatizo la upatikanaji wa umeme katika nchi jirani zinazopakana na Tanzania ikiwemo Burundi na Kenya.

Alisema kuwa katika kuhakikisha mpango huo wa kupeleka umeme huo na kuunganisha na nchi jirani, Benki yake imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 75 kufanikisha mradi huo wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 220.

"Umeme ni jambo muhimu sana katika maendeleo ni sawa na damu katika mwili wa binadamu, ukiwa na damu mwilini unakuwa na hai kama huna unakufa! kwa hiyo uchumi bila umeme wa uhakika hauwezi kushamiri" alisisitiza Dkt. Adesina

Aliahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza maendeleo ambapo hivi sasa Benki yake iko katika mazungumzo na Serikali ili mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 165 uweze kupatikana kwa ajili ya kujenga mradi wa nishati ya umeme katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa nchi.

"Vile vile tutawasilisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Benki yetu ili kiasi cha dola za Marekani milioni 45 kinachoombwa na Serikali kwa ajili ya kujenga mradi wa umeme unaotokana na joto ardhi uweze kupatikana ili kuboresha na kuwa na umeme wa uhakika nchini kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya viwanda nchini" alisema Dkt. Adesina

Alisema kuwa kwa ujumla Benki yake katika kipindi cha miaka miwili ijayo (2018/2019 na 2019/2020) Benki yake itatoa kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.5 katika sekta ya umeme na kueleza matumaini yake kwamba hatua hiyo itawawezesha wazalishaji mali wadogo, wa kati na wakubwa kuzalisha bidhaa na mali mbalimbali na hivyo kukuza uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.

Kituo cha kupoza umeme zuzu ni sehemu ya mradi wa umeme unaonufaisha mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga ambapo vijiji zaidi ya 121 vimeshanufaika na maradi huo wa uzalishaji na usambazaji wa umeme kwa mikoa husika.

Alisema kuwa miradi inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki yake imefikia thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa Serikali ya Tanzania inashukuru kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni mshirika mkubwa wa Maendeleo wa Tanzania kutokana na kusaidia Serikali katika uwekezaji mkubwa unaogusa nyanja mbalimbali ikiwemo nishati na miundo mbinu mingine kama barabara.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli kwa kuwa hiyo ndio dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amesema kuwa Benki hiyo ni mshirika wa kweli katika sekta ya nishati na imewezesha kufanikiwa kwa miradi mbalimbali ya umeme ukiwemo ule unaoinifaisha mikoa ya Iringa, Singida, Dodoma, Shinyanga na Dodoma.

Miradi inayotekelezwa hapa nchini kwa sasa kupitia ufadhili wa Benki ya AfDB imefikia zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.

Ushirikiano wa AfDB na Tanzania ulianza tangu mwaka 1971 na mpaka sasa benki hiyo imeipatia Tanzania kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.6, karibu shilingi trilioni 8 za Tanzania.

Rais wa AfDB yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA AfDB MJINI DODOMA

April 26, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini Dodoma kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika mjini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina ambaye aliambatana na ujumbe wake mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina ambaye alihudhuria maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF

April 26, 2018

TANGA: INAVYOKUA KIVUTIO CHA UTALII NCHINI TANZANIA

April 26, 2018
Na Jumia Travel Tanzania
Miongoni mwa mikoa maarufu nchini Tanzania ni pamoja na Tanga. Ukiachana na ukaribu wake na jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Tanga una utajiri wa utamaduni wa Waswahili wanaopatikana katika pwani ya bahari ya Hindi, makumbusho ya kihistoria, shughuli za uchumi na kibiashara, pamoja na wanasiasa na wanasanaa mbalimbali mashuhuri wanaolipeperusha vema jina la mkoa huu.

Hivi karibuni mkoa wa Tanga umekuwa ni eneo mojawapo la kitalii linalokua kwa kasi na kuwavutia watalii wengi ndani na nje ya Tanzania. Watalii wengi kupendelea kwenda Tanga kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa zikiwemo miongoni mwao tayari wamekwishatembelea sehemu zingine, kupata simulizi kutoka kwa watu wao wa karibu pamoja na vivutio vingine ambavyo havipatikani sehemu zingine isipokuwa Tanga.

Jumia Travel imekukusanyia baadhi ya sababu ambazo zimepelekea watu wengi kupendelea kwenda kutalii mkoa wa Tanga:
Jiografia. Asilimia kubwa ya watalii hupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo katika jiji la Dar es Salaam. Umbali uliopo kati ya jiji hili na mkoa wa Tanga sio mkubwa, huchukua muda wa takribani masaa 6 kitu ambacho watalii wengi huweza kumudu. Hii imerahisisha shughuli za kitalii kwa urahisi kwa sababu watalii wanaweza kwenda na kurudi kwa urahisi.

Vivutio vya kitalii. Mkoa wa Tanga umebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali ambavyo haviwezi kupatikana sehemu nyingine. Tanga inazo mbuga kama vile Saadani, Mkomazi, na Jozani ambazo unaweza kujionea wanyama, ndege na mimea ya aina mbalimbali lakini pia ina maeneo kama vile mapango ya Amboni na makumbusho ya kale ambayo yamebeba historia na urithi wa mkoa huo tangu enzi za wakoloni.
Hali ya hewa. Miongoni mwa mji mashuhuri kwa shughuli za kitalii hivi sasa mkoani Tanga na Tanzania kwa ujumla ni Lushoto. Hali ya hewa nzuri, mandhari ya kuvutia na hoteli za kitalii katika eneo hili zimekuwa ni hamasa kubwa kwa wasafiri wengi. Eneo la Lushoto ambalo linapatikana kwenye safu ya milima ya Usambara limejizolea umaarufu kutokana na shughuli tofauti za kitalii kama vile matembezi na kupanda milima, shughuli za uvuvi, kuendesha baiskeli, kutembelea makumbusho ya kale, nakadhalika. Na kwa kuongezea eneo hili limewekezwa kwa hoteli za kisasa za kitalii.

Hoteli za kitalii. Kutokana na kuwepo kwa shughuli nyingi za kitalii, kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika huduma ya malazi. Miongoni mwa changamoto kubwa inayoikumba sekta ya utalii nchini na duniani kote ni huduma ya malazi. Malazi ni huduma ambayo huwa ghali ukilinganisha na huduma nyingine kama vile usafiri wa kwenda na kurudi, viingilio na makato mengineyo.

Mkoa wa Tanga umejitahidi kwa hilo, wafanyabiashara wengi wamejenga hoteli ili kuweza kukidhi haja ya kila aina ya mtalii. Si jambo la kushangaza kukuta hoteli za kitalii karibu na vivutio vya kitalii.
Gharama nafuu. Miundombinu kama vile barabara imewavutia watu wengi kwenda kwa urahisi kutalii vivutio vya mkoa wa Tanga kwani imerahisisha gharama za usafiri. Ukiachana na usafiri wa mabasi yanayokwenda na kurudi kila siku, watu wengi siku za hivi karibuni wamekuwa wakitumia usafiri wao binafsi. Unafuu pia upo kwenye huduma ya malazi ambayo kila mtu anaweza kumudu pamoja na gharama za kuishi kwenye jiji hilo kwa ujumla.

Ukarimu wa watu wake. Watu wa Tanga wanasifika kuwa na haiba ya ukarimu kama walivyo watanzania wengi nchini. Hiki nacho kimekuwa ni kivutio kingine kwa watalii wengi kutembelea eneo hilo. Ukarimu huwavuta watalii wengi, kuwajengea hali ya usalama na kujifunza mengi kutoka kwa wenyeji wao. Wakazi wa Tanga wanatoa mchango mkubwa katika kulitangaza jiji lao kitalii kwa kuwapokea wageni na kuwafunza mambo yanayopatikana mkoani mwao.

Kama ulikuwa unafikiria sehemu ya kwenda kutalii tofauti na sehemu ulizozizoea, Tanga itakuwa ni chaguo sahihi kwa hivi sasa. Ni miongoni mwa sehemu zinazofikika kwa urahisi na unaweza kufanya shughuli nyingi ndani ya muda mfupi na kurejea kwenye majukumu yako ya kawaida.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWAONGOZA MAELFU YA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZILIZOFANYIKA MKOANI DODOMA

April 26, 2018

Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kwenda kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshma katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma

Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika jukwa kuu kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Vikosi mbalimbali vya Jeshi la Wananchi, Magereza na Polisi vikipita kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma




Mmoja wa Makomando wa JWTZ akitoa Heshma kwa kupiga Saluti wakati akipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Mmoja wa Makomando wa JWTZ akitoa Heshma kwa kupiga Saluti wakati akipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani DodomaKikosi cha Makomando wa (JWTZ) kikipita na kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa Pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, wakati kikundi cha Halaiki kilipokuwa kikipita mbele kutoa heshma katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Askari wa Jeshi la Magereza wakionesha umahiri wa kupambana na vikwazo mbalimbali katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.




Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU