NMB HAI WAIPIGA JEKI TIMU YA HALMASHAURI HIYO.

October 02, 2013
NA OMARY MLEKWA,HAI.

BENKI ya NMB  wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu ya mpira wa wavu ya Halmashauri ya Hai kwa ajili ya mashindano ya  timu ya Taifa  SHIMISHIMITA yanayotarajiwa kutimua vumbi  Oktoba 20 hadi Novemba 1   mwaka huu,  mkoani Dodoma.

Vifaa vilivyotolewa ni Jezi,bukta,Soks, Flana,na Traksuti vilikabidhiwa  kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ,kufuatia maombi maalumu yaliyotolewa na uongozi wa timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kufanikisha mpango wa mashindano hayo kwa timu hiyo .


Akikabidhi msaada huo ,Kwa Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo , Dkt Paul Chaote ,meneja wa  NMB Wilayani hapa Stella Tambikien  alisema kuwa ,NMB imetoa msaada huo kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa michezo nchini,na kwamba itaendelea kusaidia sekta hiyo ili kuboresha michezo nchini kwa kutenga sehemu ya faida inayoipata.

''NMB inaamini kwamba ili kupata wachezaji wazuri wa ngazi ya taifa ni lazima waanze kuandaliwa kwa ubora toka ngazi ya chini watakao iwakilisha taifa vyema kwenye michuano mbalimbali''alisema Tambikien

Aidha aliwaasa wachezaji hao kujituma kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanalete ushindi utakaoleta heshima kwa mkoa na kwa wale wote waliojitolea kusaidia kwa hali na mali.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi huyo pamoja na kuishukuru NMB kwa kuthamini na kuchangia michezo ,ameiomba benki hiyo kuendelea kutoa msaada , kadri inavyo pata faida ,na alitumia fulsa hiyo kuwahimiza wachezaji hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu wawapo katika mashindani hayo.

‘Michezo kwa sasa ni ajira kwa hiyo nawaombeni mkajitume muweze kuuletea heshima mkoa ,na mtambue kuwa mkicheza vizuri mtapata ajira na kuwa mabalozi wazuri sehemu muendako,alisema Tambieni

Tambikieni aliyataka mabenki mengine , taasisi za fedha na wadau wa michezo nchini kuiga mfano wa NMB katika kutambua umuhimu wa kuchangia michezo ili kujenga na kuimarisha afya za wachezaji hao sanjari na kupata wachezaji bora na wenye vipaji watakao weza kuliwakailisha taifa katika michezo mbalimbali.

Aidha aliwataka wafanyakazi maofisini kujenga utaratibu wa kushiriki michezo mbalimbali ,kwani hali hiyo itasaidia kujenga afya zao na kupunguza magonjwa ya ajabu ajabu yanayo wanyemelea baadhi ya wafanyakazi ambao wengi wao wamekuwa wakinenepeana kwa kula vyakula ovyo ,hali ambayo imekuwa ikiwasababishia kuugua kila mara .

Nahodha wa  timu hiyo, Ndeakifoo Shoo alisema  kutokana na msaada huo ambao umetolewa wakati maalum wachezaji watahakikisha wanakwenda kufanya vizuri na kurudi na vikombe kama msimu uliopita.

Hata halmashauri ya Wilaya hayo inaingia katika mashindano hayo ya SHIMISHIMITA Taifa  kama mabingwa watetezi ambapo pia mwaka jana walipata walipata kombe kwa timu yenye nidhamu
 

WATANZANIA WAASWA KUCHANGIA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA.

October 02, 2013

NA OMARY MLEKWA,HAI
WATANZANIA wametakiwa kujitokeza katika kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa   kwa ajili ya watoto  wenye ulemavu ili kuwapatia fursa ya  kupata elimu sawa na watoto wasiokuwa na ulemavu badala ya kutegemea serikali pekee

Akizungumza katika ziara ya kutembelea watoto wenye ulemavu wa akili katika kata ya Machame Mashariki, katibu wa chama cha watu wenye ulemavu wa akili wilayani Hai, Anjella Mallya hali ya miuondo mbinu katika shule nyingi hapa nchini hairuhusu kuwapa fursa watoto wenye ulemavu

Alisema hali hiyo imesababishwa na jamii kuwatenga na kuwabagua wenye ulemavu katika suala nzima la kielimu kwa kutegemea serikali pekee katika kukabiliana na tatizo hilo jambo ambalo limekuwa likichangia zaidi watoto wengi kushindwa kupata haki zao za msingi katika elimu

“Ni  jukumu letu sote kuwatazama watu wenye walemavu kama watu wengine na tusiwachife watoto wenye ulemavu badala yake jamii ihakikishe inaboresha mangira ya watoto hao kwa kina kama ilivyo kwa watoto wengine ”alisema Mallya

“Tuwasaidie na kuwajali kwa kuhakikisha wanapata elimu katika
mazingira rafiki, ili waweze kuchagia maendeleo katika taifa kwani nao wana uwezo wa kujitegemea iwapo tutawaunga mkono, bila kusahau kuwa ulemavu hauombwi wala kununuliwa bali unakuja tu,” alisisitiza .

Alisema endapo jamii ikishirikiana na Serikali kuwa na majengo maalumu ya kwa ajili ya watoto wenye ulemavu itasaidia kuwavutia watoto hao kusoma kwani mazingira wanayosemea katika shule za kawaidia yamekuwa si rafiki nao
 

DC DENDEGO AWAFUNDA WANAFUNZI WA KIKE TANGA.

October 02, 2013
MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO KATIKATI KUSHOTO NI KATIBU WA CCM WILAYA YA TANGA,LUCIA MWIRU NA KULIA NI MWENYEKITI WA UWT WILAYA YA TANGA,MWANSHAMBA PASHUA WAKATI WA MAADHIMISHO YA UWT KIWILAYA AMBAYO YALIFANYIKA KATA YA PONGWE JIJINI TANGA.

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MKUU wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego amewataka wanafunzi wa kike katika shule za sekondari wilayani hapa kujitambua na kuacha kufikiria masuala ya mapenzi badala yake watilie mkazo elimu kwani ndio mkombozi wao wa maisha yao ya baadae na familia zao.

 

MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO AKIGAWA ZAWADI YA SABUNI KWA WAGONJWA KATIKA KITUO CHA AFYA PONGWE IKIWA NI WIKI YA MAADHIMISHO YA UWT AMBAPO KIWILAYA YALIYAFANYIKA KATA YA PONGWE.
Dendego alitoa kauli hiyo wakati akitoa somo maalumu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Pongwe ikiwa ni siku ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wilaya ya Tanga(UWT) ambazo kiwilaya zilifanyika kata ya Pongwe wilayani hapa.
MGANGA MFAWIDHI WA KITUO CHA AFYA PONGWE,DR.ALLY BUGHE AKIWA AMESHIKILIA ZAWADI YA SABUNI ALIZOPATIWA NA UWT WILAYA YA TANGA WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UMOJA HUO WILAYA AMBAPO YALIFANYIKA KWENYE KATA HIYO KUSHOTO KWAKE NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO ANAYEFUATIA NI MWENYEKITI WA UWT WILAYA YA TANGA,MWANSHAMBA PASHUA
Mkuu huyo wa wilaya aliweza kutoa somo la kuwakumbusha wanafunzi hao kuwa wazalendo wa kuipenda nchi yao ,kujitambua wao kama vijana wa kike wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupenda elimu na kuachana kufanya ngono zembe ambayo itaweza kuwapelekea kushindwa kutimiza malengo yao.

  



“Ukisoma utaheshimika na kuweza kufanya kazi yoyote kwa sababu una elimu ikiwemo kuweza kuendesha maisha yao hivyo nawasihii msome kwa bidii na mafanikio yake mtayaona “alisema DC Dendego.

 
MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO KULIA AKIMKABIDHI MGANGA MKUU WA KITUO CHAAFYA PONGWE DR.ALLY BUGHE WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UWT AMBAPO KIWILAYA YALIADHIMISHWA KATA YA PONGWE WILAYANI HAPA

MWENYEKITI WA UVCCM WILAYA YA TANGA,SALIMU PEREMBO KULIA MWANZO MEZA KUU AKIFUATILIA KWA UMAKINI VIKUNDI MBALIMBALI VYA NGOMA WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UWT WILAYA AMBAYO ILIFANYIKA KATA YA PONGWE JIJINI TANGA.
 Alisema endapo watasoma kwa bidii kwa kuzingatia yale yote watakayofundishwa darasani watapata uelewa mzuri wa kufanya vizuri katika mitihani yao na hatimaye kuweza kupata kazi nzuri ili kuweza kuzisaidia jamii zao kwa ujumla.

"Nimeunda kikosi kazi cha kuwatafuta wanafunzi wanaotoroka shuleni muda wa masomo ili kuweza kutokomeza vitendo vya wanafunzi kutoroka na hii nadhani itachochea wanafunzi kupenda masoma na kuongeza kasi ya ufaulu miongoni mwao "Alisema DC Dendego.

Aidha katika hatua nyengine mkuu huyo wa wilaya aliwataka wakina mama kujitambua kwa kuongeza jitihada zao katika shughuli za maendeleo kwani wanawake wakiwezeshwa wanaweza hivyo wahakikisha wanakuwa mstari kwa kuungana pamoja ili waweze kusonga mbele.

    “Wakina mama tupendane,tuheshimiane na tuache kukosoana badala yake tukimuona mwanamke mwenzio anakosea kaa naye umuelekeze kuliko kukosoana “Alisema DC Dendego na kusisitiza upendo kati yao.

Awali akizungumza wakati akitoa somo katika maadhimisho hayo,Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Tanga, Mwanshamba Pashua aliwataka vijana wa kike wahakikishe wanatimiza ndoto zao kwa kusoma kwa bidii na kufanya kazi ili iweza kuwa msingi bora wa maisha yao.

Maadhimisho hayo yakikwenda sambamba na shughuli mbalimbali za kijamii ambapo Mkuu wa wilaya Dendego  na Katibu wa CCM wilaya ya Tanga,Lucia Mwiru na viongozi wa UWT wilaya na  Kata hiyo walitembelea kituo cha Afya Pongwe kutoa zawadi kwa wakina mama wajawazito na kuwafariji wagonjwa.

MSHAMBULIAJI WA MAKANGALE KIDS TORRES ARIPOTI KAMBINI NA KUONGEZA NGUVU KWENYE KIKOSI HICHO.

October 02, 2013

NA MASANJA MABULA -PEMBA .
KOCHA MKUU WA KIKOSI CHA MAKANGALE KIDS , STANSLAUSI MARKUS (MORINHO) AMESEMA KUWA KURIPOTI KATIKA MAZOEZI YA TIMU HIYO MSHAMBULIAJI OTHMAN SAID (TORRES) KUMEZIDI KUKIONGEZEA NGUVU KIKOSI CHAKE AMBACHO KINAJIWINDA NA MICHUANO YA JUNIOR KWA VIJANA WALIOCHINI YA UMRI WA MIAKA 15 KATIKA  WILAYA YA MICHEWENI .

AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA BLOG HII KISIWANI PEMBA , MORINHO AMESEMA KUWA,  MSHAMBULIAJI HUYO ALIWASILI KATIKA KAMBI YA MAZOEZI YA TIMU HIYO JANA AKITOKEA NDAGONI  KUJUMUIKA NA WENZAKE KWENYE MAZOEZI YANAYOFANYIKA KATIKA KIWANJA CHA KIJIJINI MAKANGALE .

AMESEMA KUWA MCHEZAJI HUYO ATAIMARISHA SAFU YAKE YA USHAMBULIAJI AMBAPO ATAONGOZA MASHAMBULIZI KWENYE LIGI HIYO AMBAYO INATARAJIA KUANZA MWEZI UJAO .

AMEAHIDI KUWA TIMU YAKE ITAFANYA VYEMA KATIKA LIGI HIYO NA HIVYO KUWEZA KUIBUKA BINGWA NA KUZITAKA TIMU PINZANI KUTOTEGEMEA MTEREMKO WAKATI WATAKAPO KUTANA .