RHINO RANGERS,COASTAL UNION HAKUNA MBABE,ZATOKA SARE YA BAO 1-1

September 18, 2013
MBUNGE WA JIMBO LA TANGA,OMARI NUNDU AKISALIMIA NA MCHEZAJI WA COASTAL UNION YA TANGA SULEIMAN KASSIM SELEMBE LEO KABLA YA KUANZA MECHI YAO YA LIGI KUU DHIDI YAO NA RHINO RANGERS YA TABORA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI.

HAPA AKISALIMIANA NA WAAMUZI ANAYEFUATIA MWENYE TISHETI YA MISTARI NI MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION  YA TANGA,HEMED AURORA.

HAPA MBUNGE WA JIMBO LA TANGA,OMARI NUNDU AKISALIMIA NA WACHEZAJI WA TIMU YA RHINO RANGERS YA TABORA KALBA YA KUANZA MECHI HIYO.

KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOCHEZA LEO.

WA KWANZA KUSHOTO NI MBUNGE WA JIMBO LA TANGA,OMARI NUNDU ANAYEFUATIA NI KATIBU WA KLABU YA COASTAL UNION ,KASSIM EL SIAGI NA MWENYE TISHTI YA MISTARI NYEUSI NI KATIBU WA UVCCM MKOA WA TANGA,ACHENI MAULID.


MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF,KHALID ABDALLAH AKIBADILISHANA AKITETA JAMBO NA MBUNGE WA JIMBO LA TANGA,OMARI NUNDU LEO KABLA YA KUANZA MCHEZO HUO ULIMALIZIKA KWA SARE YA BAO 1-1.
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga leo imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Rhino Rangers ya Tabora ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Ligi kuu Tanzani bara mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Mchezo huo ulikuwa mkali na wenye upinzani wa hali ya juu kutokana na timu zote kushambuliana kwa zamu na kuonyesha kandanda nzuri na la kuvutia ambapo mpaka timu hiyo zikienda mapumziko,Rhino Rangers ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 bao lililofungwa na Salim Majid dakika 26.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Coastal Union union waliwatoa Suleiman Kassim Selembe,Yayo Lutimba,Keneth Masumbuko na kuwaingiza Razack Khalfani,Pius Kisambale na Danny Lyanga ambao waliweza kuubadilisha mchezo huo.

Baada ya kuingia wachezaji hao Coastal Union waliweza kucharuka kwa kucheza pasi fupi fupi na ndefu kitendo ambacho kilipeleka kuweza kufanya mashambulzi mfululizo langoni mwa Rhino Rangers ya Tabora bila mafanikio.

Kwa upande wao Rhino Rangers walionekana kuukamia mchezo huo kwa kucheza kwa umakini mkubwa na ucheza pasi ndefu hali ambayo iliwapeleka kupata  nafasi nyingi za wazi na kushindwa kuzifanyia kazi ipasavyo.

Wakionekana kucharuka na kujipanga Coastal Union waliweza kucheza vema katika kipindi pili na kutua baada ya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao na kufanikiwa kuandika bao lao la kusawadhisha dakika ya 81 kupitia Jerry Santo kwa njia ya penati iliyotokana na mchezaji wa Rhino Rangers,Saad Kipanga kuunawa mpira eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo,Jacob Zakaria kuamuru ipigwe penati iliyopigwa kiufundi na Santo na kutinga wavuni.

Katika mchezo wa leo Coastal Union iliwakilishwa na Shaban Kado,Hamad Hamis,Abdi banda,Juma Nyoso,Marcus Ndeheli,Jerry Santo,Suleiman Kassim Selembe,Haruna Moshi Boban,Yayo Lutimba,Keneth Masumbuko na Uhuru Suleiman Mwambugu.

Huku Rhino Rangers ikiwachezesha Abdulkarim Mtumwa,Ally Mwanyiro,Hussein Abdallah,Laban Kambole,Ladslausi Mbogo, Hamisi Msafiri,Nurdin Bakari,Salum Majid,Gidion Brown,Saad Kipanga na Kamana Salum.

WAZAZI VUNJENI MAKUNDI-DR.MNDOLWA.

September 18, 2013
MWENYEKITI WA JUMUIYA WA WAZAZI CCM MKOA WA TANGA,DR.EDMUND MNDOLWA AKISISITIZA JAMBO WAKATI AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA JUMUIYA WA WAZAZI LUSHOTO.
KATIBU WA WAZAZI MKOA WA TANGA.
MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA LUSHOTO,LOTTI AKIZUNGUMZA KWENYE KIKAO HICHO.
MJUMBE WA HALMASHAURI WA KAMATI YA UTEKELEZAJI WAZAZI MKOA NA MWENYEKITI YA HALMSHAURI YA KOROGWE VIJIJINI,SADICK KALLAGE NAYE AKIZUNGUMZA JAMBO KWENYE MKUTANO HUO
NA OSCAR ASSENGA,LUSHOTO.
MWENYEKITI wa Jumiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga,Dr.Edmund Mndolwa amewataka makatibu wa Jumuiya hiyo ngazi ya kata kuvunja makundi na kutokukubali kugawanywa kwa sababu hali hiyo itapeleka mpasuko ndani yao badala yake wawe mstari wa mbele kukilinda chama hicho.

Mndolwa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na makatibu wa wazazi wilaya ya Lushoto ambapo madhumuni makubwa ilikuwa ni kutoa shukrani kwao kwa kumchagua ikiwemo kuzungumzia ujio wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho,Abdallah Bulembo ambaye atafanya ziara yake mkoani Tanga kutembelea shughuli mbalimbali za jumuiya hiyo.

Aidha aliwataka makatibu hao kutokukubali kugawanywa na viongozi wasioitakia mema jumuiya kwani kufanya hivyo kutapeleka wao kushindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa pamoja na kuchangia kuzoofisha maendeleo yao ya kiutendaji kila siku.
  
"Tusikubali kugawanywa gawanywa kama mahindi au bidhaa sokoni wadhulumu wenu wataadhibiwa wakati wa uchaguzi "Alisema Mndolwa.

Aidha aliwataka kuitunza elimu ikiwemo kuipa kipaumbele na wakubali kuwa elimu ni kitu cha muhimu sana na kuelezea katika shule za wazazi zinahitaji mafanikio makubwa ili ziweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.

Mwenyekiti huyo alisema kwenye  shule zao wanahitaji ufanisi mkubwa sana hivyo alimuagiza katibu wake na atailalalisha kwenye kamati ya utekelezaji inayokuja na watatangaza kuwa na sanduku la maoni ambalo litakuwa kwa ajili ya kuwekwa maoni kuhusu ufanisi wa shule za wazazi mkoani hapa.

Alisema aliamua kuweka hivyo kutokana na kuwa wakati mwengine walimu wanaofundisha shule hizo hushindwa kufundisha vema pindi waingiapo darasani na kutomaliza silabasi hali ambayo huchangia kurudisha nyuma maendeleo yao pamoja na wanafunzi wanaofundisha.