KAMPUNI YA TANZANIA MWANDI YAANZISHA MICHUANO YA AFRICAN YOUTH FOOTBALL TOURNAMENT
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam.
Kampuni ya Tanzania Mwandi kwa kutambua kuwa Tanzania na
Afrika nzima kuna vijana wengi ambao wana vipaji vya mpira wa miguu na hivyo
wanachohitaji ni kuonyeshwa tu jinsi ya kuufikia ‘Ulimwengu Halisi’ wa Mpira
duniani Tanzania Mwandi imeamua kuanzisha michuano ya African Youth Football Tournament
ambayo itawashirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 21.
Michuano hiyo itaambatana na mafunzo kwa siku tano ambapo
vijana hao watapata mafunzo ya mpira wa Miguu (elimu, ujuzi na hata mbinu za
uwanjani) kutoka kwa makocha wawili wa hapa nchini na watatu wa kimataifa
kutoka nje ya nchi, kuanzia tarehe 10/06/2013 hadi tarehe 14/06/2013 katika
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Aidha, mafunzo yatafanyika nyakati za asubuhi na jioni
wachezaji hao watashiriki Mashindano ya kucheza wao kwa wao ili kupata vijana
11 bora miongoni mwa wachezaji watakaoshiriki.
Wachezaji Bora 11 watakaopatikana watakuwa mabalozi wa
Mdhamini Mkuu wa Michuano ya African
Youth Football Tournament na watapata fursa ya kutangazwa zaidi kimataifa
na kutafutiwa vilabu vya kucheza soka Barani Ulaya katika nchi nane (Ufaransa,
Ureno, Uswis, Ubelgiji, Uholanzi, Norway, Sweden na Denmark pamoja na barani
Afrika na Asia.
Ili kupanua wigo wa kuwatangaza kimataifa wachezaji wengi
zaidi, Michuano hii pia itaalika skauti na mawakala wa soka wa kimataifa ili
kufuatilia uwezo wa wachezaji hao asubuhi katika mazoezi na jioni kwenye
michuano, kuwapata vijana bora ambao watapendelea kuwatafutia timu nje ya nchi
kukipiga huko kwa makubaliano ambayo pande hizo mbili (mchezaji na wakala)
zitaafikiana.
Miongoni mwa Mawakala ambao watakuwepo ni wakala wa
Kimataifa wa Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro, Phillip Mwakikosa (Sweden) na
wengine wengi.
Hata hivyo kutokana na gharama kubwa za uandaaji wa Michuano
hii, na ndio kwanza ikiwa inaanzishwa, Kampuni ya Tanzania Mwandi kwa kujali
mahitaji ya Kitanzania tumeweka kiingilio kwa mchezaji wa Tanzania kuwa
shilingi laki tatu (Tsh. 300, 000) na mchezaji wa nje ya Tanzania Dola 500 za Kimarekani
(USD 500).
Fedha hizo zitagharamia malazi, chakula na mahitaji mengine
yote kwa mchezaji pindi atakapokuwa kambini.
Hii ni fursa adimu kwa vijana wa Kitanzania kuonyesha uwezo
wao ili kutimiza ndoto za kucheza soka barani Ulaya, Asia na barani Afrika
katika vilabu vikubwa huku ikikumbukwa kuwa mnamo Mwaka 2012 ni wachezaji
wachache sana wa Kitanzania waliopata fursa ya kufanya majaribio ya kucheza
soka la kulipwa kutokana na uchache wa mawakala na gharama hivyo kuletwa
mawakala hao nyumbani Tanzania ni fursa pekee ya kufikia malengo.
Mpaka sasa tayari Kampuni ina majina takribani ya vijana 10
wa Nje ya nchi (Uganda, Nigeria na Ghana) ambao wameomba kushiriki hivyo
tunatoa wito kwa Watanzania kutoipoteza fursa ya kuletewa njia ya kuelekea kusakata
soka Barani Ulaya mlangoni mwao.
Lakini tunafahamu hali halisi ya maisha yetu kwahiyo nitoe
wito kwa Wadhamini mbalimbali ambao tumewaomba kutusaidia kufanikisha
Mashindano haya ambayo naamini yatalitangaza taifa letu na kulitangaza zaidi
soka letu kimataifa. Pia udhamini wao utatuwezesha kupunguza hizi gharama kwa
washiriki kutoka Tanzania na hivyo kuwachukua vijana wengi zaidi.
Kampuni ya Tanzania Mwandi ni Kampuni binafsi ambayo
imejikita katika kuendeleza sekta za utalii, michezo na burudani ndani na nje
ya nchi na hivyo kuiongezea kipato nchi moja kwa moja ama kupitia kuwawezesha
wananchi kama vile kuwatengenezea fursa za ajira vijana kupitia michezo.
Fomu za ushiriki Michuano hii zinapatikana kupitia www.tanzaniamwandi.co.tz
na www.blog.tanzaniamwandi.co.tz
“African Youth
Football Tournament; Live your Dream.”
Subscribe to:
Posts (Atom)