MWENYEKITI WA UVCCM AWAFUNDA WAZAZI MKOANI TANGA.

September 09, 2013
NA OSCAR ASSENGA,LUSHOTO.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga(UVCCM)Abdi Makange amewataka wazazi na walezi mkoani Tanga kuweka msukumo wa elimu kwa watoto wao ili iweze kuja kuwa mkombozi wao katika maisha yao ya baadae.

Makange alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa mahalafi ya kumi na moja kidato cha nne ya shule ya sekondari Mlongwema ambapo alimualikisha Mbunge wa Jimbo la Lushoto,Henry Shekifu na kueleza hakuna urithi muhimu hapa nchini zaidi ya elimu hivyo wazazi wanapaswa kulitilia mkazo suala hilo kwa umakini mkubwa.

Amesema endapo wanafunzi watasoma kwa bidii ikiwemo kuzingatia masomo itawasaidia kuweza kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho na hatimaye kuweza kupata kazi nzuri ambayo itakuwa dira katika kuendeleza maisha yao na jamii zao.

  "Ukisoma utakuwa na amani ya moyo kwani unaweza unaweza kumuabudu mungu kwa moyo mmoja bila kuweka mawazo ya wapi nitapata maisha mazuri,hivyo ndugu zao naombeni msome kwa bidii na matunda yake mtayaona "Amesema Makange.

Makange pia amewataka wazazi kuwa mstari wa mbele kutoa michango muhimu inayohitajika kwa watoto wao ili iweze kuchangia kasi ya maendeleo kwenye shule hiyo.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,John Tembo amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa vya sayansi na walimu kwani yupo mwalimu mmoja tu pamoja na uhaba wa nyumba wa walimu kwani zilizopo hazitoshelezi.

PICHA ZA MATUKIO YA MAHAFALI YA SHULE YA SEKONDARI MLONGWEMA ILIYOPO WILAYANI LUSHOTO

September 09, 2013
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE ALIYEVAA SHUTI KATIKATI ALIWASILI ENEO LA MAHAFALI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MLONGWEMA,
HAPA NI MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE AISAINI KITABU CHA WAGENI KATIKA SHULE HIYO.
AKIWA MEZA KUU WAKATI AKIFUATILIA MAHAFALI HAYO MWISHONI MWA WIKI.
HAPO AKITETA JAMBO NA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI MLONGWEMA,JOHN TEMBO.
HAPA WAKIIMBA WIMBO WA TAIFA KABLA YA KUANZA KUTOA HOTUBA YAKE.
WANAFUNZI WANAOMALIZA WAKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MGENI RASMI ABDI MAKANGE WAKATI AKITOA HOTUBA YAKE JANA.
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE AKIPOKEA HOTUBA YA SHULE HIYO KUTOKA KWA MKUU WA SHULE HIYO,JOHN TEMBO.

MAKANGALE STAR NA VUMAWIMBI BOYS WAMELIZA TOFAUTI ZAO.

September 09, 2013
Na Masanja Mabula -Pemba .
Mahasimu wa soka katika Wilaya ya Micheweni Timu ya Makangale Star na Vumawimbi Boys wameondoa tofauti zao na kuamua kuunganisha timu lengo ni kupata timu moja yenye nguvu na ambayo italeta ushindani kwenye michuano ya ligi daraja la pili Wilayani humo .

Taarifa ambazo zimepatikana kutoka kwa moja wa viongozi wa Timu hizo zenye maskani yake katika Shehia ya Makangale,   zinasema kwamba tayari makubaliano ya kuunganisha timu hizo yamefikiwa na kupewa baraka na chama cha soka Wilaya ya Micheweni .

Msemaji wa Klabu ya Makangale Star Rashid Ali Juma Sendeu amesema kuwa katika makubaliano hayo kila timu imetakiwa kutoa wachezaji kumi na tano ili kufanya idadi ya wachezaji thelesini wanaotakiwa kwenye fomu ya usajili .

Aidha amefahamisha kwamba timu ambayo imepatikana kutokana na muungano huo umesajiliwa kwa jina la Makangale United na inatarajia kushiriki ligi daraja la pili Wilaya hiyo na kwamba kwa sasa inaendelea na mazoezi katika kiwanja wa Skuli ya Makangale .

Na katika kuimarisha na kuleta mafaniko ya klabu , tayari umeundwa uongozi pamoja na kuanzisha kamati mbali mbali ambazo zitakuwa na jukumu la kusimamia maendeleo ya klabu hiyo .

Waliochaguliwa kuunda kamati hizo ni wazee wawili kutoka kila timu huku aliyekuwa kocha wa Klabu ya Makangale Star Juma Mbirimbi amepewa jukumu la kuinoa klabu hiyo akisaidiwa na Ali Mussa .

Mmoja wa washambuliaji wa kutegemewa wa klabu hiyo Mussa Ali Baby akizungumza na mwandishi wa habari hizi amekiri kuwepo na ushindani wa namba na kusema itakuwa vigumu mchezaji kujihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza .

Hata hivyo mpachika mabao huyo ameahidi kutumia uwezo na kujituma ili aweze kumshawishi kocha ili aweze kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza licha ya kwamba timu imesajili wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa .