MKUU WA MKOA WA ARUSHA AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA DINI

August 31, 2016


Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo(katikati)akizungumza na Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto)  alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo nae akiwa ameambata na Mbunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki(Eala)Mheshimiwa Angela Kizigha.

Askofu wa Kanisa la Anglikan,Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia)  baada ya mazungumzo yao.
                             Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameendelea  na  ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa dini  ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi  baada ya kuteuliwa kushika  wadhifa huo hivi karibuni.
Mh.Gambo amekutana na  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Mchungaji  Solomon Masangwa , Askofu wa  Kanisa la Evangelistic Assemblies of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi  na Askofu  Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount  Kilimanjaro.
Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.
Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph  Magufuli kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani  halmashauri zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya  mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana wajasiriamali  zitakazowawezesha kufanya  shughuli za uzalishaji mali.
Amewataka  wawajulishe waumini wa dini zote na serikali iko tayari  kupanga utaratibu wa maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa  elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini hili iwe inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala kisiasa.
Askofu Stanley Hotay aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na kuomba vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye Mwenyekiti wake kukabiliana na changamoto za kiusalama na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Aidha alishauri  kutokana na idadi ya watu wanaotumia usafiri wa anga kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo  ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
Mh. Gambo amewahakikishia viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha mipango mbalimbali inayokusudia kuitekeleza ili  watoe mawazo yao katika kuiboresha na  kuifanya itekelezeke   kwa wepesi zaidi.

ALICHOKISEMA ALIYEKUWA KATIBU WA CHADEMA MKOANI MWANZA BAADA YA KUTIMKIA CCM

August 31, 2016
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia), akirejesha kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo katika ofisi za CCM hii leo.
Na BMG
Nzwalile ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema Taifa, Mjumbe Baraza Kuu Chadema Taifa, Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano Chadema Mkoa wa Mwanza, amefikia uamuzi huo baada ya jana kujivua vyeo hivyo.

Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na kwamba Chadema imepoteza mwelekeo kwani kimekuwa kikiibuka na oparesheni za kuichonganisha serikali na wananchi huku pia demokrasia ikikosekana ndani ya chama hicho.

"Kama ni udikiteta basi mimi niseme Chadema ndiko kuna udikiteta kwani zaidi ya mara tatu nimemsikia Lowasa (Edward Lowasa, aliyekuwa mgombea urais 2015) akisema yeye ndiye mgombea urais mwaka 2020, kwa kikao gani". Amesema Nzwalile na kuongeza kwamba yale mambo yote mabaya yaliyokuwa yakifanyika ndani ya CCM yamenyooshwa hivyo hakuna haja ya yeye kuendelea kukaa Chadema.

Amesema atazunguka Wilaya zote ili kuhakikisha anawarejesha wengine ndani ya CCM huku akiwa na jukumu moja la kuubomoa Ukuta unaoelezwa kujengwa na Chadema kwani ni ukuta wa tope hivyo atatumia tu maji kuubomoa.

Nzwalile amekaribishwa ndani ya CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo, ambaye pia amewakaribisha makada wengine wa upinzani kuhamia CCM akisema kwamba chama hicho kinaendesha mambo yake kidemokrasia.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akipokea kadi ya Chadema ya aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (katikati).
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia).
Soma HAPA Taarifa ya awali.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA TAASISI YA AFRICA MATTER LIMITED YA UINGEREZA MHE. LYNDA CHALKER

August 31, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa  Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31,
2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimkaribisha kuketi  Mwenyekiti wa  Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31,
2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa  Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31,
2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimsindikiza Mwenyekiti wa Taasisi
ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya  mzungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016
 “Hapa kazi tu…” anaonekana kusema Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya  mzungumzo yake na   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto M. James

VODACOM YAWALETEA WATEJA WAKE PROMOSHENI YA"JIONGEZE NA M-PAWA

August 31, 2016


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni ya ‘Jiongeze na M-Pawa’ inayoendeshwa na kampuni yake ikishirikiana na Benki ya CBA, kwenye hafla iliyofanyika leo Mlimani City jijini Dar es Salaam.Ili kushiriki kwenye promosheni hiyo, mteja wa Vodacom Tanzania anatakiwa kujiwekea akiba katika akaunti yake ya M-Pawa kwenye simu yake katika kipindi cha promosheni.Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100.Washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja.Promosheni hiyo ambayo imeanza leo itadumu kwa kipindi cha wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao (wa tatu kushoto) akiwa na maofisa waandamizi wa kampuni hiyo, wakionyesha mabango kwenye uzinduzi wa promosheni ya ‘Jiongeze na M-Pawa’ inayoendeshwa na kampuni yake ikishirikiana na Benki ya CBA, kwenye hafla iliyofanyika leo Mlimani City jijini Dar es Salaam.Ili kushiriki kwenye promosheni hiyo, mteja wa Vodacom Tanzania anatakiwa kujiwekea akiba katika akaunti yake ya M-Pawa kwenye simu yake katika kipindi cha promosheni.Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100.Washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja.Promosheni hiyo ambayo imeanza leo itadumu kwa kipindi cha wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao (kulia) na Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo, Hassan Saleh (kushoto) wakizindua rasmi msafari wa magari kwenda mikoa mbalimbali nchini kutoa elimu juu ya promosheni ya ‘Jiongeze na M-Pawa’ inayoendeshwa na kampuni yake ikishirikiana na Benki ya CBA, kwenye hafla iliyofanyika leo Mlimani City jijini Dar es Salaam.Ili kushiriki kwenye promosheni hiyo, mteja wa Vodacom Tanzania anatakiwa kujiwekea akiba katika akaunti yake ya M-Pawa kwenye simu yake katika kipindi cha promosheni.Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100.Washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja.Promosheni hiyo ambayo imeanza leo itadumu kwa kipindi cha wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2016.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakihudhuria uzinduzi wa promosheni ya ‘Jiongeze na M-Pawa’ inayoendeshwa na kampuni hiyo ikishirikiana na Benki ya CBA, kwenye hafla iliyofanyika leo Mlimani City jijini Dar es Salaam.Ili kushiriki kwenye promosheni hiyo, mteja wa Vodacom Tanzania anatakiwa kujiwekea akiba katika akaunti yake ya M-Pawa kwenye simu yake katika kipindi cha promosheni.Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100.Washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja.Promosheni hiyo ambayo imeanza leo itadumu kwa kipindi cha wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2016.

Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushiriana na benki ya CBA imezindua promosheni kubwa ambayo itawawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pawa kujishindia fedha taslimu kutoka kwenye kitita cha milioni 300 zilizotengwa kwa ajili ya promosheni hii na mshindi mmoja wa zawadi kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100.Promosheni hii inayojulikana kama ‘Jiongeze na M-Pawa’ itatoa washindi wa siku wa shilingi milioni 1/- kila mmoja,washindi wa wiki  shilingi milioni 20/- kila mmoja na wateja wapatao 200 wataongezewa mara mbili ya akiba zao walizojiwekea kwenye akaunti zao za M-Pawa kila siku.

Promosheni hii ambayo imeanza leo Agosti 31 itadumu kwa kipindi cha wiki 6 na itafikia mwishoni mwezi Oktoba ambapo itafanyika droo ya kumpata mshindi wa zawadi kubwa.Katika kipindi chote cha promosheni mabalozi wa bidhaa za Vodacom na maofisa wa kampuni watatembelea sehemu mbalimbali za Tanzania kwa ajili ya kuwaelimisha  faida za kujiwekea akiba kupitia huduma hii hususani wanaoishi maeneo ya vijijini.

Ili kushiriki kwenye promosheni anachotakiwa kufanya mteja ni kujiwekea akiba kwenye akaunti yake ya M-Pawa kwenye simu yake katika kipindi cha promosheni.Kwa kujiwekea akiba mojamoja kutawawezesha wateja kujipatia pointi za kuingia kwenye promosheni na kuwa na uwezekano wa kujishindia fedha taslimu kila siku,kila wiki na zawadi kubwa ya promosheni.Kadri mteja anavyojiwekea akiba kwenye akaunti yake ya M-Pawa ndivyo anakuwa na nafasi kubwa ya kushinda. 

Kwa mfano kwa kujiwekea akiba kati ya shilingi 1,000/-mpaka 19,000/-mteja anajipatia pointi 20,wakati akijiwekea  akiba kati ya shilingi 20,000/-mpaka shilingi 99,999/-mteja anajipatia pointi 40 na kadri anavyoweka akiba ndivyo pointi zinaongezeka  zaidi na  kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.

Kuweka akiba kwenye akaunti ya M-Pawa na kuwa kwenye  nafasi ya kushinda mteja anaweza kupiga  *150* 00#  kisha kwenda kwenye menu ya  M- Pawa, chagua Weka  kwenye M-pawa, weka kiasi cha fedha kisha weka namba yako ya siri ya  M-Pesa  .

Wateja watakaojishindia shilingi milioni 1/-na wale  watakaoongezewa fedha zaidi ya mara mbili ya akiba zao fedha zao zitaingizwa kwenye akaunti zao za M-Pawa moja kwa moja ambapo watafahamishwa kuwa wameshinda kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS).Washindi wa wiki wa shilingi milioni 20/- na mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni watakabidhiwa zawadi zao  na maofisa wa Vodacom watakaochaguliwa kufanya kazi hiyo kulingana na mikoa watakayotokea washindi.

Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwahamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba na kunufaika kwa mikopo yenye riba nafuu ya kati ya asilimia 2% hadi 5% kulingana na akiba ya mteja aliyojiwekea.”Promosheni inawakumbusha watanzania kuwa kuweka akiba kwenye M-Pawa ni chaguo la busara hususani kwa wajasiriamali kwa kuwa inawezesha kupata mikopo nafuu yenye riba ndogo”.amesema Ian Ferrao,Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania .

“Huduma ya M-Pawa ni akaunti ya benki kwenye ncha ya kidole chako ambayo imebuniwa kuboresha maisha ya wateja!Zaidi ya watanzania milioni 4.8 wanaendelea kufurahia huduma hii na natoa wito kwa watanzania wengi wajiunge zaidi na kufurahia huduma hii ya M-Pawa.Unavyojiwekea akiba zaidi ndivyo kiwango cha kukopa kinavyoongezeka”.Alisisitiza Ferrao.

CHUO CHA UDEREVA CHA NYATO'S CHAWATUNUKU VYETI MADEREVA WALEMAVU 19

August 31, 2016
 Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kulia), akimkabidhi cheti, Mpoki Mwasunga, baada ya kuhitimu mafunzo ya udereva ya mwezi mmoja katika chuo cha udereva cha Nyato's kilichopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo. Wahitimu 19 ambao ni walemavu walihitimu mafunzo hayo.
 Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga, akiangalia  alama ya usalama barabarani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
 Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mshairi, Kiiza Amani akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (katikati), akihutubia kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero, akitoa neno kwenye mkutano huo.



H
 Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kushoto), akimkabidhi cheti, mhitimu, Subira Semsimbazi.
Hapa James Hizza akipokea cheti chake.
Sikujua Mbwembwe, akikabidhiwa cheti chake.
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
Stafu Sajeni, Enock Machunde akitoa darasa kwa hitimu hao kuhusu sheria za usalama barabarani.
Koplo, Faustina Ndunguru, akizungumza kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

WATU Jamii ya walemavu ambao ni maderava wa vyombo vya moto wametakiwa kujitokeza kwenye shule mbalimbali za udereva ili kupata mafunzo ya udereva ikiwa pamoja na kupata leseni kabla ya kutumia vyombo hivyo.

Wito huo umetolewa Dar es Salaam leo na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi wa Ilala,Peter Mashishanga wakati akiwatunuku vyeti walemavu 19 ambao wa mefunzo ya mwenzi mmoja katika shule ya udereva ya Nyato's iliyopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala.

Alisema kuwa ipo haja ya walemavu ambao wanamiliki vyombo vya moto na kuendesha vyombo hivyo kabla hawajaingia barabarani ni vema wakapata mafunzo ya kujuwa alama,kanuni na sheria za usalama barabarani.

"Ni muhimu kwa kundi hili ambalo leo mmepata vyeti vya kuhitimu mafunzo ya udereva kwenda kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajapata fursa ya kupata mafunzo kama  nyie kwenda  kuwahamasisha ili wajiunge katika vyuo vya udereva ikiwamo chuo hiki cha Nyato's ambacho kimeaza mpango wa kutoa mafunzo haya kwa nchi nzima kwa kushirikiana Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu."alisema Mashishanga

Aidha aliwaeleza wahitimu hao kuwa wahakikishe  wanakwenda kupata majaribio kwa wa kufunzi wa kikosi cha Usalama barabarani ili wapate leseni zitakazo wafanya waweze kuendesha vyombo vya vya moto.

Kwaupande wake Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero alisema kuwa ni muhimu kwa wahitimu hao kwenda kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa pamoja na kuvaa kofia ngumu,na kutozidisha abiria.

Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato alishukuru kwa ushirikiano uliopo kati ya   Jeshi hilo na taasisi yake ambapo pia ametoa  ofa ya kusoma bure kwa mlemavu Thomas Kone ambaye hivi karibuni alipata msaada wa bajaji kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli.

Nyato alisema kuwa kimeazisha mpango wa kutoa mafunzo  ya udereva kwa kushirikiana na kamati ya  Taifa ya usalama kwa watu wenye ulemavu kwa lengo la kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Click here to Reply, Reply to all, or

MASAUNI AZINDUA PROGRAMU YA “TUNZA AMANI IKUTUNZE” JIJINI DAR ES SALAAM

August 31, 2016



Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO) , Kulia ni Mkurugenzi wa shirika hilo, Askofu Nason Ngoy Ngoy. Hafla hiyo imefanyika leo Agosti 31, 2016katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam .
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”,

Mkurugenzi wa Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania (PSEDO). Askofu Nason Ngoy Ngoy, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania (PSEDO). Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
Washiriki wa uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha UDP, Goodluck Ole Medeye, mara baada ya kumaliza uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”.Hafla hiyo imefanyika leo.
 

 (PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI) 

MAMA WA MITINDO NA YASIN KAPUYA KUIWAKILISHA TANZANIA MAREKANI

August 31, 2016
Taarifa mpya kwa wadau wa mitindo na fashion + vyombo vya habari inasema hivi, Mama wa mitindo maarufu kama Asya  Idarous Khamsin kutoka Tanzania anategemea kuiwakilisha Tanzania kwa kuonesha mitindo yake katika jukwaa kubwa la biashara nchini Marekani katika mji mkuu wa California, Sacramento.

Show hiyo inatambulika kama 'The African Trader Show',  Tamasha litafanyika siku 3 kuanzia Tarehe 2 mwezi wa 9/2016 - 4/9/2016. Mbali na Asya pia Mr. Yasin Kapuya atawakilisha Tanzania kwa kutoa mada na kuonesha ufundi wa kazi zake katika onesho hilo. Hivyo ndugu jamaa na marafiki + Watanzania kwa ujumla tunapaswa kutoa ushirikiano wadhati kwa Wanzanzania hao. Asanteni.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA

August 31, 2016

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd, Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipeana mkono wa shukurani na Nd,Hassan Khatib Hassan,baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha ACP Sida Mohamed Himid kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshughulikia Idara Maalum za SMZ,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitia saini hati ya kiapo ya ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ walihudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi, walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Baadhi ya Mawaziri wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi katika taasisi mbali mbali walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo. Picha na Ikulu ya Zanzibar.

CHRISTIAN BELLA KUWASHA MOTO SHINDANO LA MISS KINONDONI 2016, KESHO KUTWA UKUMBI WA DENFRANCES SINZA JIJINI DAR ES SALAAM

August 31, 2016

Washiriki wa shindano la  Lete Raha Miss Kinondoni 2016 wakishuka kwenye gari Dar es Salaam jana walipofanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Mdhamini wao Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd Mikocheni.
Wanyange hao 20 wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya 
gari la kampuni hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Mr Rutha akizungumza na wanyange hao walipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo Mikochezni Dar es Salaam jana.
Warembo hao wakiwa mbele ya ghala zinamo hifadhiwa bia za Windhoek wakati wa ziara hiyo.
Warembo hao wakisubiri mkutano na wanahabari baada ya ziara hiyo.

Mshauri wa Miss Kinondoni, Boy George (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya shindano hilo. Kutoka kulia ni Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo,Constantine Mwafulilwa, Andrea Missana, Mratibu wa Shindani la Miss Kinondoni Rhamat George na Mwalimu wa warembo hao, Neema Chaky.
Maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa katika pozi. Kutoka kushoto ni, Mr Jerome, Ismail Mzava na Mr Rutha.
Mwalimu wa Wanyange hao, Neema Chaky (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanyange hao katika tabasamu.
Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Viongozim meza kuu na wanyange hao wakionesha bia ya windhoek.


Na Dotto Mwaibale

Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi hapa nchini Cristian Bella anatarajiwa kuwasha moto katika shindano la kumsaka Malkia wa Ulimbwende
Kanda ya Kinondoni linatarajiwa kufanyika kesho kutwa Ijumaaya katika Ukumbi wa Denfrances Sinza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwa kutanisha warembo hao  na wadhamini washindano hilo ambao ni Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambao ni wasambaji wa kinywaji cha Windhoek Dar es Salaam jana, Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo, Andrea Misama alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendalea vizuri ambapo aliwashukuru warembo wote waliojitokeza kwenye shindano hilo kwa mwaka huu na kuwa mwanamuziki huyo akishirikiana na kundi la sanaa la kampuni hiyo watapamba jukwaa kwa kutoa burudani la kukata na shoka.

"Mwaka huu washiriki waliojitokeza ni wengi ukulinganisha na mwaka jana, hivyo tunatoa pongezi kwa wazazi waliowaruhusu watoto wao kushiriki, malengo yetu ni kukuza vipaji na kutoa ajira kwa wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao”,  alisema.


Kwa pande wao warembo watakaoshiriki shindano hilo wameahidi kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuwaomba wadau na mashabiki waurembo kujitokeza kwa wingi siku ya shindano ili wawezekusapoti Miss Kinondoni.


Shindano hilo linashirikisha warembo 20 kutoka vitongoji mbalimbali vya Kanda ya Kinondoni ambapo kiingilio kitakuwa sh 10,000 na 20,000 kwa VIP huku shindano hilo likipambwa kwa burudani kutoka kwa mkali wa masauti Christian Bella.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)