RAIS DKT. MGUFULI APATA CHAKULA CHA MCHANA NA VIONGOZI WA DINI WA MKOA WA KILIMANJARO

RAIS DKT. MGUFULI APATA CHAKULA CHA MCHANA NA VIONGOZI WA DINI WA MKOA WA KILIMANJARO

April 30, 2017
MC1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya kupata nao chakula cha mchana katika Ikulu ndogo mjini Moshi leo Aprili 30, 2017
MC2
:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya kupata nao chakula cha mchana katika Ikulu ndogo mjini Moshi leo Aprili 30, 2017
MC3 MC4 MC5
Viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro  wakiwa  katika Ikulu ndogo mjini Moshi kupata chakula cha mchana walipata wasaa kueleza changamoto zao mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  leo Aprili 30, 2017
MC6
Viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro  wakiwa  katika Ikulu ndogo mjini Moshi kupata chakula cha mchana walipata wasaa kueleza changamoto zao mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  leo Aprili 30, 2017
MC7
Viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro  wakiwa  katika Ikulu ndogo mjini Moshi kupata chakula cha mchana walipata wasaa kueleza changamoto zao mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  leo Aprili 30, 2017

MKUU WA MKOA WA PWANI MHANDISI NDIKIRI AISHUKURU TANESCO KWA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI.

April 30, 2017
 Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiri, (kulia), akipeana mikono na Kaimu Meenja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi. Leila Muhaji, wakati akipokea msada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya kituo cha Afya Mkoani mjini Kibaha Aprili 29, 2017.
 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikiro, ameishukuru TANESCO kwa msaada wake wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya Kituo cha Afya Mkoani Mjini Kibaha.
Mhandisi Ndikiro alisema, hatua hiyo yaTANESCO ni ushahidi tosha wa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma afya katika mazingira ya usafi.
“Niseme tu mlichokifanya ni kitu kizuri sana, na ningeshauri taasisi nyingine za umma na binafsi, kutoa sehemu ya faida wanayopata kutokana na shughuli zao na kurudisha kwa umma kwa njia ya kusaidia shughuli za kijamii kama hii ya usafi.” Alisema.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi Leila Muhaji alisema, TANESCO  kama mtoa huduma ya umeme kwa Wananchi na ikitambua kuwa wananchi ndio wateja wake wakubwa, pia imeona ni busara kusaidia serikali katika kuhakikisha mazingira yanayowazunguka kama vile kituo hiki cha afya yanakuwa safi.” Alisema.
Bi. Leila pia alisema, TANESCO imetoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha umma kufanya usafi wa jumla kila mwisho wa wiki. “Tumeungana nanyi leo Jumamosi ambayo ni siku ya usafi, ili tufanye usafi pamoja kwenye kituo chetu hiki cha afya, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, napenda muwashukuru sana na mpokee msada wetu huu mdogo ambao nina hakika utasaidia kwa sehemu fulani katika kuweka mazingira ya hospitali yawe safi.” alsiema
Awali Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ndikiro, aliwaongoza watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Pwani na wachache kutoka makao makuu katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwa kufyeka nyasi kuzunguka mazingira ya kituo hicho cha afya.
 Mhandisi Ndikiro, akiwa na Mganga Mkuu wa Mji wa Kibaha, akitoa hotuba yake
 Bi leila Muhaji, (katikati), akitoa hotuba yake, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikiro, na Meneja Rasilimali watu TANESCO mkoa wa Pwani, Bi.Nisile Mwakalinga

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI

April 30, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitakiana amani na mmoja wa mapadre katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi Mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Ekaristi Takatifu toka kwa Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiungana na waumini  katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliposalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliposalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na watawa katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini baada ya  ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini baada ya  ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na waumini wengine wakimsikiliza Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI VYAIGIZA HASARA TANGA UWASA YA MILIONI 13 KWA SIKU.

April 30, 2017

 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na mikakati waliochukua kukabiliana na kuondoa tatizo la maji machafu yanayotoka jijini Tanga ili kuhakikisha maji yanarudi kwenye hali yake ya kawaida  lakini kulia ni Meneja wa Ufundi wa Mamlaka hiyo,Farles Aram
 Kushoto mwenye tisheti ya njano ni Mwandishi wa Gazeti la Majira Mkoani Tanga,Mashaka Mhando akiuliza swali katikati ni Joachim Kapembe kutoka Shirika la Utangazaji la TBC na kulia ni Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani Tanga,Wiliam Mngazija.
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Citizeni Mkoani Tanga, George Sembony kulia akiuliza swali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwandishi Zawadi Kika wa Clous TV
 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo  katikati akisisitiza jambo kulia ni Mwandishi wa Gazeti la Citizeni George Sembony

Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akizungumza jambo kwenye mkutano huo
 Baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari leo
 Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakichukua habari
 Joachim Kapembe kutoka Shirika la Utangazaji la TBCkushoto akiwa sambamba na mtumishi wa mamlaka ya Maji Tanga Uwasa wakiingia kwenye kituo cha kusafishia Maji cha Moye
 Waandishi wa habari wakitazama namna maji yaliyohifadhiwa kwenye kituo cha kusafishia maji cha Mowe kabla ya kufika kwa walaji wa kwanza ni Sophia Wakati wa Gazeti la Uhuru wa pili ni Mbaruku Yusuph wa gazeti la Tanzania Daima
 Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania,Sussan Uhinga naye akiangalia namna maji yanavyosafishwa kabla ya kuwafikia walaji
 Waandishi wa Habari wakiongozwa na Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania wakitembelea eneo la kusafishia maji kabla ya kufika kwa watumiaji la



 Eneo la Mowe ambalo maji huchujwa kabla ya kuwafikia walaji
 Mwandishi wa gazeti la Mtanzania,Sussan Uhinga na Frank wa TK wakiwa kwenye eneo hilo kujionea
 Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akizungumza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu dawa ambazo zinatumika kuwekwa kwenye maji
 Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akiwaonyesha mitambo iliyopo kwenye kituo hicho wakati walipoitembelea kujionea

 Waandishi wakitoka kulia ni Mashaka Mhando wa gazeti la Majira Mkoani Tanga kushoto ni William Mngazija wa ITV na Radio One Mkoani Tanga 


 William Mngazija wa ITV na Radio One Mkoani Tanga akiwa ongoza waandishi wengine kuingia kwenye vyanzo vya maji kuona namna hali ilivyo

JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOSOMA BEIJING WAADHIMISHA MIAKA 53 YA MUUNGANO

April 30, 2017
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania wanaosoma  Beijing Nchini  Husein Mtoro ( katikati)   aliyemwakilisha Balozi,aliambatana na Viongozi wote Wakuu akiwemo Makam Mwenyekiti Khamis Ngwali,Katibu Mkuu Ndugu Remidius Emmanuel,Naibu Katibu Mkuu Ndugu Alinanuswe Mwakiluma na Mweka Hazina Ndugu Kulwa Gamba.Pamoja nao,Viongozi waasisi wa Umoja huo Ndugu Suleiman Serera na Irenius Kagashe nao walishiriki sambamba na Viongozi wastaafu wengine akiwemo Makam Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Kassim Jape,Katibu Mkuu Mstaafu Angelina Makoye,Mtunza Hazina Mstaafu Lusekelo Gwassa katika maadhimisho  ya  muungano yaliyofanyika mapema wiki hii kwa kushriki maonesho ya utalii na utamaduni.
Baadhi ya watanzania wanaosoma katika chuo cha Beijing nchini China wakiwa katika maonesho ya utamaduni na utalii kama moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano  wa Tanzania mapema wiki hii.


Wadau wakipozi kwa picha 


Maonesho ya utalii na utamaduni  yakiendelea Jijini Beijing






Mmoja wa watanzania anayesoma Beijing akipamba maonesho hayo kwa bendera ya Tanzania wakati wa maonesho ya utalii na utamaduni ikiwa ni maadhimisho ya miaka 53 ya Mungano Hafla hizo zilifanyika mapemaa wiki  hii.


Picha ya pamoja 

Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania wanaosoma nchini China,wameadhimisha kumbukumbu ya Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kushiriki MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NA UTAMADUNI katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Biashara na Uchumi jijini Beijing.Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa Tanzania nchini China Balozi MBELWA KAIRUKI,Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,ndugu HUSSEIN MTORO  aliwaasa Watanzania hao kudumisha Amani,Mshikamano na kushiriki katika ajenda muhimu za Taifa ikiwemo,kushiriki katika kukuza soko la Utalii kwa kutangaza Vivutio vya asili vya nchi yetu,kuhamasisha Watalii wengi wa kimataifa kutembelea vivutio mbali mbali vilivyopo Tanzania.Pia Mwenyekiti alifikisha salam za Balozi Mbelwa za kuwatakia kila la heri Wanafunzi wote walio katika hatua mbalimbali za kukamilisha Tafiti zao kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.