BRIGHTERMONDAY TANZANIA YATOA FURSA KWA WANAOTAFUTA AJIRA KUWATEMBELEA KWENYE MAONYESHO YA SABASABA

BRIGHTERMONDAY TANZANIA YATOA FURSA KWA WANAOTAFUTA AJIRA KUWATEMBELEA KWENYE MAONYESHO YA SABASABA

July 04, 2015
DSC_9352
Meneja Masoko wa kampuni ya Brightermonday Tanzania, Lugendo Khalfan ndani ya hema la banda la Jakaya Kikwete akiwa tayari kukuhudumia wewe mtanzania utakayetembelea banda lao katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, yanayoendelea kurindima kwenye viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.( Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Watafuta ajira kote nchini Tanzania wamehamasishwa kujisajili na tovuti ya Brighter monday ili wapate fursa ya kuunganishwa na watoa ajira.
Akifanya mahojiano na mtandao wa habari wa modewjiblog.com, Meneja Masoko wa Brighter monday Tanzania Khalfan Lugendo, amesema usajili huo mbao ni bure, utamwezesha mhusika kupata taarifa mbalimbali na kuweza kuomba nafasi tofauti za kazi ambazo zimewekwa katika tovuti hiyo.
Amesema Brightermonday inajivunia kuwa ndio tovuti namba moja ya ajira nchini Tanzania kwa kuwa idadi ya kazi wanazoziweka katika mtandao huo ni nyingi kuliko chanzo chochote kile cha ajira nchini Tanzania.
Bw. Lugendo ameongeza kuwa kwa mwaka jana 2014 waliweza kuweka nafa za ajira 30,000 na hivyo kuwarahisishia waajiri mchakato mzima wa kuajiri na kupata watu wenye viwango bora zaidi.
Aidha ametoa wito kwa watu wote wanaotembelea maonyesho ya mwaka huu ya kimataifa ya biashara Sabasaba, kutembelea banda lao lililopo katika hema la Jakaya Kikwete ambapo watapata maelekezo kuhusu namna ya kuweza kupata ajira kwa urahisi.
Ametaja namna ya kuwapata ni kupitia anuani ya tovuti ambayo ni www.brightermonday.co.tz au e-mail : info@brightermonday.co.tz,
Simu: +255688 333 334,
Katika mitandao ya kijamii wanapatikana kwa anuani zifuatazo
facebook: brightermondaytz,
Instagram: brightermondaytz pia katika Googleplus na Twitter.
DSC_0109
Key Account Manager wa Brightermonday Tanzania, Gloria Nyiti kwenye sehemu maalum ya kupokea wageni katika banda lao lililopo ndani ya hema la Jakaya Kikwete.
DSC_0310  
Wafanyakazi wa Brightermonday Tanzania wakitoa huduma kwa mmoja wa wateja aliyetembelea banda lao lilipo ndani ya hema la Jakaya Kikwete kwenye maonyesho sabasaba.
DSC_9343
Gloria Nyiti akiwahudumia watafuta ajira katika banda la Brightermonday lililopo ndani ya hema la Jakaya Kikwete.
IMG_6607
Gloria Nyiti akitoa maelekezo ya namna ya kujisajili kwenye mtandao wa Brightermonday kwa mmoja wa wateja aliyetembelea banda lao kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kupamba moto jijini Dar.
DSC_0318  
Timu ya wafanyakazi wa Brightermonday Tanzania wakiwa nadhifu katika banda lao tayari kuwahudumia wateja kwenye maonyesho ya Sabasaba.
UMOJA WA MATAIFA WAIBUKA KIDEDEA KATIKA UHABARISHAJI NA UTOAJI ELIMU KWENYE TUZO ZA MAONYESHO YA 39 YA SABASABA

UMOJA WA MATAIFA WAIBUKA KIDEDEA KATIKA UHABARISHAJI NA UTOAJI ELIMU KWENYE TUZO ZA MAONYESHO YA 39 YA SABASABA

July 04, 2015
  DSC_0178
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkadhi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) cheti na tuzo katika kipengele cha Uelimishaji bora kupitia Uandishi wa machapisho na mpangilio bora wa maonyesho, baada ya Umoja wa Mataifa kuibuka mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yalipozinduliwa rasmi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (kushoto) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt. Abdallah Kigoda (kulia).
DSC_0179 FullSizeRender_2
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaohudumia banda hilo kwenye maonyesho ya Sabasaba wakisheherekea mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
UN Tanzania inawakaribisha Watanzania wote wanaotembela maonyesho sabasaba kufika katika banda lao lililopo Karume Hall na kuweza kushiriki kutoka maoni ya juu ya utendaji wa kazi za Umoja wa Mataifa Tanzania kwa njia ya mtandao wa simu yako bila kutozwa malipo yoyote ukitumia huduma hiyo, kwa wateja wote mitandao ya Airtel, Tigo na Vodacom.
Jinsi ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Njia nyingine ya kuwasilisha maoni yako moja kwa moja kupitia mtandao (Online) bofya link hii http://gpl.cc/UN2
FullSizeRender  

STARS KUWAVAA THE CRANES LEO

July 04, 2015

Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager kesho jumamosi saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimba la Nakivubo kucheza na wenyeji Uganda.(The Cranes).

Mecho hiyo ya kesho ni mchez wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2016 zitakazofanyika mapema mwezi Januari nchini Rwanda, mgeni rasmi atakua Rais wa Uganda Yoweri Mseveni.

Kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa, kiliwasili jijini Kampala jana usiku na kimefikia katika hoteli ya Grand Global iliyopo jirani na chuo kikuu cha Uganda Makerere.

Taifa Stars imefanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Nakivubo yakiwa ni mazoezi mepesi na mwisho kuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe utakaofnayika kesho jioni.

Kocha Mkwasa akiongelea kuelekea mchezo huo amesema, anashukuru vijana wake wamefika salama wote, hali nzao ni nzuri, morali ni ya hali ya juu, kikubwa wanatambua wana deni kubwa kwa watanzania hivyo kesho watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Akiongelea hali ya hewa na mazingira ya timu ilipofikia, Mkwasa amesema hali ya hewa ni ya kawaida baridi na mvua kidogo haina tofauti sana na Tanzania, mazingira ya hoteli ni mazuri na kusema kikubwa kilichobaki ni kusaka ushindi katika mchezo huo na vijana wake wapo
 tayari. 


Wakati huo huo mashabiki zaidi ya 50 kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa kuwasili kesho jumamosi alfajiri wakitokea jijini Dar es salaam kuungana na watanzania wengine waishio nchini Uganda kuishangilia timu ya Tanzania itakapokuwa ikipimbana na Uganda katika uwanja wa Nakivubo.

Mawasiliano ya Afisa Habari wa TFF aliyepo Uganda ni +256 780 177008

NB: picha za mazoezi ya Taifa Stars Nakivubo leo zimeambatanishwa

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)