MATUKIO YA PICHA LEO WAKATI WA MAZISHI YA KOCHA WA MAKIPA SIMBA JAMES KISAKA

December 27, 2013

NDUGU WA MAREHEMU JAMES KISAKA WAKILIA KWA UCHUNGU LEO WAKATI MWILI WA NDUGU YAO UKISHUSHWA NYUMBANI KWAO LUSANGA LEO TAYARI KWA MAZIKO AMBAYO YALIFANYIKA KATIKA MAKABURI YA FAMILI KIJIJI HUMO.

MMOJA WA NDUGU WA JAMES KISAKA AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI MWILI WA NDUGU YAO ULIPOWASILI LEO

KISAKA APUMZISHWA NYUMBA YA MILELE

December 27, 2013
Imewekwa Desemba 27 Saa 5:51 Jioni.
 Kocha wa makipa wa klabu ya Simba,James Kisaka aliyefariki dunia juzi katika Hospitali ya Burhani Jijini Dar es salaam na mwili wake kusafirishwa kijijini kwake Lusanga Wilaya ya Muheza hatimaye alizikwa leo katika makaburi ya familia yake.

Misa ya mazishi ya Kocha huyo yaliyohudhuriwa na waombolezaji wengi iliendeshwa na Padri wa Kanisa Anglikana Lusanga,Aidano Kamote.